Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

SHOO YA JAYDEE YAUNDIWA ZENGWE

$
0
0


KUNATETESI kuwa mwanamuziki nguli wa miondoko ya bongo fleva Judith Wambura 'Lady Jay Dee' a.k.a Anaconda kuundiwa zengwe ili kukwamishwa shoo yake  ambayo inatarajia kufanyika Mei 31 mwaka huu.

Tetesi hizo zimeibuka baada ya msanii wa bongo fleva nchini Khalid Mohamed 'Tid' kuandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii 'Facebook' kujitoa kwenye shoo ya msanii huyo.


Habari zilizoibuka hivi karibuni kwenye chanzo cha karibu cha msanii huyo kilisema kwamba Tid amepokea kitita cha hela ili asishiriki kwenye shoo hiyo ambayo teyari ameshapokea malipo ya awali.

Chanzo hicho kiliendelea kueleza kuwa hapo mwanzo msanii huyo alikuwa na nia ya dhati kuungana na Jay Dee katika shoo hiyo lakini baada ya kupokea kitita hicho alijikuta akiamua kubadili mawazo bila hata kuomba ushauri kwa marafiki zake.

"Tid alikuwa kama kakurupuka hivi hajamwambia mtu yeyote yule akaamua kuandika ujumbe huo kwenye ukurasa wake wa facebook, ameikacha shoo ya Jaydee kisa hela yaani hadi mashabiki zake wanamshangaa maana matangazo yalikuwa yamesharuka yanayoonyesha kuwa Tid atakuwepo kwenye shoo hiyo" kilibainisha chanzo hicho

Mwandishi wa habari hii aliamua kumtafuta Tid ili aweze kuelezea ukweli wa jambo hili.

Akizungumza kwa njia ya simu Tid alisema kuwa hayupo teyari kuzungumzia jambo lolote lile linalohusu ujumbe alioutuma kwenye ukurasa wake wa Facebook

"Sipoteyari sasa kuzungumzia jambo lolote leo hata linalohusu mimi kukaribia kuoa pia siko teyari kuzungumzia kwa sasa" alisema Tid

Kwa upande wake Meneja wa msanii Jay Dee anayejulikana kwa jina la Gadna G. Habashi alisema kuwa hakupokea taarifa yoyote rasmi kutoka kwa Tid kuhusu kujitoa kwenye shoo hiyo, zaidi ya kupokea taarifa kupitia facebook.

Alisema kuwa baada ya kuusoma ujumbe huo kwenye mtandao huo alimpigia simu Tid ili kujua msimamo wake wa kwenye shoo hiyo ambapo msanii huyo alimwambia kuwa hatoshiriki shoo hiyo.

"Baada ya kuniambia kuwa hatoshiriki nikaamua kumwambia anirudishie hela ambayo tulimlipa ili zitumike sehemu nyingine yeye alijibu kuwa 'kama upepo' neno hilo bado sijalielewa mpaka sasa lilikuwa na maana gani" alisema Gadna

Alisema mbali kutokea na kitendo hiko kwa upande wao hawana tatizo lolote lile na msanii yoyote kwani wanaamini kuwa kila msanii anakuwa na maamuzi yake .






Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

Latest Images

Trending Articles