Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

DIAMOND ABARIKI MAPENZI YA NEY WA MITEGO

$
0
0


MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini Naseeb Abdul 'Diamond' amebariki mahusiano ya msanii mwenzie Ney wa Mitego  ambayo yeye mwenyewe bado hajataka kuyaweka wazi.

Diamond ameonekana kuvutiwa na mahusiano hayo yaliyopo kati ya msanii huyo pamoja na mwanamke ambaye Ney hakuliweka wazi jina lake, kwa kuwakutanisha wawili hao kukumbatiana ikiwa ni ishara ya mapenzi yao.


Akizungumza wakati anafanya kitendo hiko Diamond alizungumza maneno ya utani kwa Ney kuwa ampige busu msichana huyo bila ya kuwa na uoga .

"Wewe ebu mpige busu mwenzio Hip Hop hadi kwenye mapenzi acha hizo Ney haya msogelee mwenzio" alisema Diamond huku akicheka

Kwa upande wake Ney wa Mitego 'alimtonya' mwandishi wa habari hii ampige picha ya 'Xcrusive' akiwa na mpenzi wake huyo ambaye hakumuweka wazi jina lake

"Njoo unipige picha ya ukweli na mama kijacho wangu hapa huyu ndiye mke wangu " alisema Ney wa Mitego

Hayo yote yalitokea mwishoni mwa wiki siku ambapo wasanii hao walikuwa wanazindua video yao mpya inayojulikana kwa jina na 'Muziki Gani' iliyofanyika Dar Live jijini Dar es Salaam





Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

Trending Articles