Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

WATANZANIA WAPEWA SOMO KUHUSU DIPLOMASIA YA UCHUM (ECONOMIC DIPLOMACY)

$
0
0
Kutoka kushoto ni Balozi mstaafu Ahmed Kiwanuka,Nduwayo Mzonya,Hussein Melele,na Rashid Njenga wakiwasikiliza wachangaji mbalimbali katka kongamano hilo lijulikanalo Epowerment of Economic Diplomacy in Tanzania .

Balozi mstafu wa Tanzania Nchini India ambaye pia ni mwalimu katika chuo cha diplomasia Balozi Ahmed Kiwanuka akitoa mhuadhara elo kuhusu namna Tanzania inavyoweza kutekeleza diplomasia ya uchumi kupitia ekta mbalimbali na kwa kutumia makundi mbalimbali

Allan Kasamala(mwenye shati ya bluu) akiwa na Baadhi ya washiriki walioshiriki kongamano hilo ambalo limeandaliwa na Wanafunzi,wahitimu na marafiki wa chuo cha diplomasia leo katka ukumbi wa chuo hicho  kilichopo kurasini jijini Dar es Salaam ambapo kongamano hilo limeandaliwa na uongozi wa serikali ya wanafunzi wakishirikiana na wahitimu wa Kozi mbalimbali za mwaka wa masomo 2014/2015 wakiongozwa na Simalenga Simon amaye amemaliza PGD MFR 2014/2015.
Washiriki wa kongamano hilo.


BRAND NEW RELEASE: JOH MAKINI - DON'T BOTHER FT. AKA OFFICIAL VIDEO

MWANAMKE AUA MJAMZITO KISHA AMPASUA NA KUTOA MTOTO

$
0
0
Mwanamke mmoja amekamatwa na polisi nchini Mexico, baada ya kumshawishi mwanamke mjamzito kwenda nyumbani kwake kabla ya kumuua na kumpasua kisha kutoa mtoto ndani ya tumbo lake.

Nancy Carrasco (PICHANI KULIA), 34, ambaye pia alikuwa mjamzito na kisha mimba yake kuharibika miezi mitatu kabla ya kujifungua, lakini badala ya kuitaarifu familia yake, alidanganya kuwa bado ni mjamzito, linaarifu gazeti la Daily Mirror.

Licha ya uongo wake aliendelea kuhudhuria kliniki ya wajawazito kama kawaida na ndipo alikutana na mjamzito mwingine, Luviniydi Yasmin Velazques Thomas mwenye umri wa miaka 23, na kuanza urafiki naye.

SOMA ZAIDI. . .


Baada ya urafiki wao kupamba moto, Nancy alimualika Yasmin nyumbani kwake huko Tijuana, eneo la Mexico lililoko karibu na mpaka wa Marekani, ambapo alimuua na kumpasua kisha kumtoa mtoto.

Kwa mujibu wa poilisi, Nancy akijitahidi kumwokoa mtoto asife, alikimbia katika hospitali ya kujifungua ya IMSS na kudai kuwa mtoto ni wa kwake.
Hata hivyo madaktari wanadai hakuwa na dalili zozote za kutoka kujifungua, hivyo waliwasiliana na familia yake wakidai mfuko wa uzazi (placenta) upelekwe hospitali hapo.  Ndugu hao walipofika nyumbani kwake, walishtuka kukuta mwili wa mwanamke na ndipo walipotoa taarifa polisi.

Nancy alipobanwa na kuhojiwa kuhusu mwili huo, polisi wanasema alikubali na kusema “nimemtoa mtoto wake na kumuua. Nilimkaba kwa nyuma kwa kutumia mtandio wake. Kisha nikatumia kisu kumpasua tumbo lake na kisha kumuibia mwanae.”

Alidai sababu ya kufanya yote hayo ni hofu kuwa mumewe angemuacha kama angegundua kuwa mimba yake iliharibika.





BREAKING NEWS: RAIS AMTEUA DK TULIA ACKSON KUWA MBUNGE

BREAKING NEWS: MAKOPO YA BIA 48,000 ZA PEPSI ZAKAMATWA

$
0
0
Jamaa mmoja amenaswa nchini Saudi Arabia, wakati akijaribu kuingiza nchini humo zaidi ya makopo 48,000 ya bia aina ya Heineken, yaliyozibwa na kufanana na soda aina ya Pepsi (PICHANI KULIA), katika taifa hilo la kiislam lililoko Umoja wa Nchi za Falme za Kiarabu.

Pamoja na kuwa adhabu za makosa kama hayo hutofautiana ni kinyume cha sheria kukutwa na pombe katika Ufalme wa Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa Mtandao wa LBC America, maafisa ushuru katika mpaka wa Al Batha walikamata shehena hiyo ilipokuwa ikijaribu kupenya na kuingia nchini humo.


“Gari lililobeba iliyodhaniwa kuwa na shehena ya vinywaji vya Pepsi lilisimamishwa na baada ya utaratibu wa kawaida wa kukagua bidhaa hiyo ilibainika kuwa ni pombe iliyovalishwa stika ya ilizibwa na karatasi ya Pepsi” alikaririwa akisema Meneja Mkuu wa mpaka wa Al Batha, Abdulrahman al-Mahna

Afisa huyo pia alikaririwa akisema kuwa pamoja na jitihada, ubunifu na ujanja wa kuingiza bidhaa nyingi zilizopigwa marufuku, askari doria wake “siku zote wako tayari kukamata bidhaa hizo”

Hata hivyo haijajulikana bado mtuhumiwa huyo atachukuliwa hatua gani kwa kitendo hicho.


AFYA BORA INAANZA NA KIFUNGUA KINYWA BORA - SIKU YA KISUKARI DUNIANI

$
0
0
Dk. Bhuvaneshwari Shankar, Mkuu wa idara ya lishe kutoka hospitali za Apollo. (KUSHOTO
 PICHANI)

Na Mwandishi Wetu,
Novemba 14 kila mwaka tunaadhimisha siku ya kisukari duniani ili kuongeza uelewa kuhusu madhara ya kisukari, matatizo yanayoletwa na huu ugonjwa na taarifa muhimu kuhusu kisukari.

Siku hii inabeba ujumbe mahususi kwa watu wote ulimwenguni. Kauli mbiu katika siku hii tokea 2014 hadi 2016 ni maisha bora na kisukari(healthy living and diabetes) na mwaka huu kuna mtazamo zaidi katika kuzingatia mlo kamili na kuanza kila siku na kifungua kinywa bora.

Kutoka katika shirika la kisukari Africa, Tanzania ni kati ya nchi 32 katika shirikisho hilo kwa viwango vya nchi zenye viwango vya kisukari duniani. Kulikuwepo na zaidi ya kesi milioni 1.7 za kisukari hapa Tanzania kwa mwaka 2014. Shirika la afya duniani (WHO) linakadiria zaidi ya watu milioni 180 ulimwenguni wana kisukari, na hiyo takwimu inatarajiwa kuongezeka ifikapo mwaka 2030 kama hamna hatua yoyote itakayochukuliwa.
Kifungua kinywa bora na sahihi kitasaidia sana kiwango cha sukari mwilini kutokuwa juu sana wala chini sana na kukuweka vizuri kutokea asubuhi.

Katika maadhimisho ya siku ya kisukari dunia, kliniki ya sukari kutoka hospitai za Apollo imeandaa siku 2 za kupima na kuhamasisha katika kambi iliyopo hospitali za Apollo kuwaasa watu kuhusu mifumo na staili za maisha yao ili kujikinga na kisukari. Kambi hiyo itakuwa na; vipimo vya sukari katika damu, mchanganuo wa mafuta mwilini, na namna ya kuepuka kisukari ambapo hospitali za Apollo zitatoa somo kuhusu milo kamili kutoka kwenye timu yao ya wataalam wa milo. Wataalam hao watafundisha namna ya kujikinga na kisukari kwa kuzingatia milo bora, namna ya kudhibiti kiwango cha sukari mwilini na namna ya kupambana na kisukari kwa ujumla.

Kwa kuona umuhimu wa kutoa huduma hiyo ya kisukari kupitia elimu ya mlo, Dk. Bhuvaneshwari Shankar Mkuu wa idara ya lishe kutoka hospitali za Apollo, ana lengo la kuwaelimisha watanzania kuhusu mambo muhimu wanapaswa kuyajua kuhusu kisukari na mlo kamili katika siku hii ya kisukari duniani.

Kula kwa afya ni silaha bora kujikinga na kisukari. Mazoezi ya mara kwa mara na mlo kamili vinasaidia sana. Hamna chakula mahususi au mfumo mgumu wa lishe unaohitajika.

Dk Bhuvaneshwari Shankar anatutia moyo kula milo mitatu kama inavyostahili kitu ambacho watanzania wengi hatufanyi hivyo. “muda mrefu bila chakula kunafanya sukari kushuka, na utajikuta unakula chakula kingi ambacho kitapelekea sukari katika damu kutokuwa sawa. Alisisitiza

Ratiba nzuri ya chakula cha mtu wa kisukari kinatakiwa kiwe na mafuta kidogo, mboga mboga, katika siku ni muhimu. chakula kingi kinanafanya sukari ya mwili kutokuwa sawa. Angalizo linahitajika katika uchaguzi sahihi wa vyakula.

Katika chaguo sahihi la vyakula “Dk Shankar wa hospitali ya Apollo anasisitiza umuhimu wa watanzania kudhibiti kiwango cha sukari katika damu kwa kufuata mlo sahihi.

”chagua vyakula vyenye nyuzinyuzi, na kabohaidreti ndogo ni muhimu. Epuka bidhaa nyingi zilizochujwa nyuzi zake, ila chagua unga. Unga ulio na virutubisho vyote ni wa muhimu. Dhibiti kiwango cha mafuta kuingia mwilini, na epuka mafuta yaliyotengenezwa.

Ule milo 3 kwa siku na vitafunwa hapo katikakati. Chagua milo yenye nyuzinyuzi sana zaidi ya ile yenye kabohaidrates, mbogamboga zenye stachi Epuka chokleti, barafu tamu zenye mafuta na sukari nyingi. Chagua samaki wazuri na kuku wakuchemsha sio kukaangwa na mafuta. Chagua maziwa yenye mafuta kidogo.

Dumisha uzito unaopaswa kwa kufanya mazoezi kwa kutembea na kula katika muda muafaka, alisisitiza Dk. Shankar.

Kisukari ni ugonjwa unaoathiri watu katika umri wowote ambapo mwili unashindwa kutengenzea sukari ya kutosha au kushindwa kutumia inslulini iliyotengezwa hivyo kupelekea kiwango cha sukari mwlini kutodhibitiwa. Mwili wa mwanadamu unapata sukari kutoka kwenye sehemu kuu mbili; kwanza kutoka kwenye vyakula tunavyokula, pili kutoka kwenye ini linalotengeneza pindi unapokuwa hujala chakula. Mwili unabadilisha hii sukari na wanga kwenda na kuwa nguvu kwa kutoa homoni zinazoitwa insulin zinazotengenezwa na kongosho.


Kuhusu Hospitali za Apollo
Hospitali ya Apollo ilifunguliwa mnamo mwaka 1983, na kutoka kipindi hicho imekuwa ikiendeshwa kwa kauli mbiu isemayo "Dhamira yetu ni kuleta huduma ya kisasa karibu kabisa na walengwa. Tunajitolea kutoa huduma bora na mafanikio katika elimu na utafiti kwa ajili ya jamii ya kibinadamu".Katika miaka 30 tokea kuanzishwa kwake, hospitali ya Apollo imeandika historia kubwa kupata kuonekana nchini India. Ni moja ya kampuni kubwa ya Afya katika bara la Asia, na pia imeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya afya nchini india.

Katika safari yake, imeweza kuboresha maisha ya watu wapatao milioni 39 kutoka nchi 120.Inatoa huduma maalum 52 na vitanda vya upasuaji 710.Imefanya upasuaji wa moyo wenye kufikia idadi ya watu 152,000 na panuzi 125, 000 za mishipa myembamba.Imefanya upasuaji wa wa viungo unaopita kiasi cha idadi ya watu 10,000, upasuaji wa uvimbe wa ubongo, uti wa mgongo na zaidi.Taasisi ya Apollo ni moja ya taasisi zinazoongoza nchini india, zikiwa na teknolojia za kisasa kama Novalis TX, PET MRI na Upasuaji unaotumia mashine za kiroboti.

MKUTANO WA UMEME AFRIKA KUFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
Mkutano wa mwaka maarufu kama POWERING AFRICA: Tanzania Investment Conference (www.PoweringAfrica-Tanzania.com) unatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam, katika hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro Hotel kwa siku mbili kuanzia tarehe 3 mwezi Disemba 2015.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kusambazwa na mtandao wa African Press Organisation mapema leo, mkutano huo utaangazia masuala ya umeme wa Tanzania baada ya uchaguzi, fursa za uwekezaji pamoja na kujenga mahusiano baina ya serikali na sekta binafsi katika soko la umeme.
Akidhibitisha taarifa hizo, January Makamba ambaye ni Mbunge Mteule wa Bumbuli, na mwakilishi kutoka tume maalumu ya Rais (President’s Delivery Bureau –PDB ), Wizara ya Nishati na Madini na Kampuni ya Usambazaji Gesi (GASCO), walionesha dhamira ya serikali katika kukuza sekta ya nishati kama uti wa mgongo wa maendeleo nchini.

Mpaka sasa kuna makampuni 37 kutoka sekta binafsi nchini ambayo yamedhibitisha kushiriki ambayo ni pamoja na Tanzania Investment Bank, Standard Chartered Bank, Mitsubishi Corporation, Citibank Tanzania Limited, BVI Consulting, Liquefied NG Tanzania Limited, Statoil na Sunfunder.

Ajenda kuu ya mkutano huo itahusisha pamoja na dhamira ya Tanzania katika mageuzi ya nishati, kukua kwa sekta ya nishati, maendeleo ya gesi nchini, mikakati ya manunuzi ya serikali na umuhimu wa umeme katika sekta ya kilimo.

Kufuatia msaada uliotolewa na IFC ili kuwezesha utekelezaji wa maendeleo ya nishati nchini, ratiba hiyo itahusisha uwezekano wa nishati mbadala ikiwa ni pamoja na umeme utokanao na nguvu za jua, upepo, jotoardhi, na maji.



KIPINDUPINDU CHANYEMELEA JIJI LA MBEYA

$
0
0

Na Mwandishi wetu,Mbeya

Halmashauri ya jiji la Mbeya limewataka wafanyabiashara ndogondogo hususani wa chakula kujijengea tabia ya kuchoma taka nyakati za jioni mara wamalizapo kuuza biashara zao na si kusubili gari ya taka kuja kuzoa.

Aidha imewataka wakazi hao kuondokana na fikra duni ya kuamini kuwa kazi ya uzoaji wa taka na kusafisha mazingira ni ya halmashauri ya Jiji na sio mali ya mtu.
( Picha Kushoto:Wafanyabiashara ndogo ndogo katika eneo la Makunguru jijini Mbeya wakiendelea na shughuli zao kama kawaida . )

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Mbeya, Dkt. Samweli Lazaro, amesema, wananchi wanatakiwa kujenga tabia ya usafi na sio kusubili kupigizana kelele na serikali kwa kuwahimiza kufanya usafi kwani adui mkubwa wa afya ni uchafu hivyo kila mmoja anapaswa kuwa mlinzi wa mwezake katika kutunza mazingira.


Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa malimbikizo mengi ya taka kwenye sehemu zisizorasmi ndani ya JIji la Mbeya na kupelekea jiji hilo kuwa chafu hususani katika maeneo ya sokoni.
Amesema, hivi sasa halmashauri ilianzisha mpango wa uzoaji wa taka barabarani ambapo mpango huo umeonekana kupokelewa na wananchi kwa asilimia 100 changamoto inakuja kwa upande wa halmashauri kuonekana kuzidiwa kutokana na ukosefu wa vitendea kazi.

“Halmashauri ilianzisha zoezi la kupitia taka zinazozalishwa na wananchi ambazo huziweka barabarani na magari yanapitia lakini mapango huu umeonekana kuzaa matunda kwa jamii kuupokea lakini tatizo ni uhaba wa vitendea kazi,”alisema.

Alisema, ili zoezi hilo lifanikiwe halmashauri inahitaji zaidi ya gari saba za ubebaji taka na kontena 80 lakini mpaka sasa magari yaliyopo ni manne na kontena 30 .

Hata hivyo kutokana na changamoto hiyo, Lazaro anawasihi wananchi kujenga tabia ya kuweka mazingira safi hasa kipindi hiki cha mvua kwani ndipo magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu yanapoibuka na kusababisha vifo vya watu.
(Kwa hisanna ya JAMIIMOJABLOG MBEYA)

MAMA ADAI MZIMU WA MICHAEL JACKSON UMEMPA MIMBA, AFUNGUA KESI

$
0
0
Mwanamke mmoja ameibuka na madai kuwa amejifungua mtoto wa mzimu wa Michael Jackson. Mwanamke huyo amefungua kesi kuishitaki wamiliki wa mali za mkongwe huyo wa muziki wa Pop ili kupata fidia ya matunzo ya mtoto.

Kwa mujibu wa chaneli ya televisheni ya shirika la Now8News nchini Marekani, Kiera Johnson (Pichani Kushoto) alidai kuwa wakati anaangalia dvd ya saa mbili ya toleo maalumu la miaka 30 ya Michael Jackson (Michael Jackson 30 Year Anniversary Special), lipofikia sehemu ya muziki wa Thriller, macho yake yakawa mazito akasinzia. Na ndio hapo sasa maajabu yalipotokea…


Kiera, 32, anaeleza “ghafla, niliamshwa na mkono uliokuwa unanipapasa usoni wakati nilikuwa ndani peke yangu, mume wangu akiwa kazini. Kilichofuata nilikuwa nalazimishwa kufanya mapenzi na Michael Jackson.

Hata hivyo hakuwa Michael Jackson mweupe, alikuwa mweusi na amevalia kama ametoka kwenye video ya nyimbo hiyo. Nilijaribu kumzuia na kumwambia ‘stop’ lakini hakusikiliza.”

Kiera alidharau tukio hilo kwa madai kuwa ilikuwa ni ndoto tu. Hata hivyo tarehe 25 septemba, 2015 yeye na mumewe (wote wazungu) walipata mtoto wa tatu wa kiume.

“Kila kitu kimeenda vizuri” alisema mume wa Kiera, Ken. “lakini nilipomuona mtoto wangu kuwa ni mweusi, nikasema ‘ni kitu gani hiki!’ nilikumbwa na mshtuko mkubwa. Na ndipo Kiera aliponieleza kuhusu ndoto yake ya ajabu.

“nafikiri si sahihi, ndio maana tunashitaki wamiliki wa mali za Michael Jackson. Tunachotaka ni fedha za kutosha kusaidia malezi ya mtoto wake” alieleza baba huyo.

Kiera amedai hakuwahi kuchepuka hata siku moja toka awe na Ken, wachilia mbali na mtu mwenye utaifa mwingine. Nae Ken anaemtambulisha Kiera kama “Malkia” wake anasema anamuamini sana mkewe.

Familia hiyo inasema ikotayari kumalizana nje ya mahakama na wameipa familia ya Michael Jackson mpaka tarehe mosi januari 2016 kutoa jibu. Familia ya Jackson haijasema chochote hadharani kufuatia tuhuma hizo.




HAPA KAZI TU: KAMA ULINUNUA KIWANDA NA MASHIRIKA YA SERIKALI HII INAKUHUSU

$
0
0

http://www.tro.go.tz//docstation/com_content.article/119/press_release___kurejeshwa_kwa_viwanda_vilivyokiuka_masharti_ya_mikataba.pdf

HANDING OVER OF EQUIPMENT’S TO THE TANZANIAN POLICE FORCE (TPF)

$
0
0
Speech by the German Ambassador to Tanzania Honorable Egon Kochanke
Handing over of Equipment’s from German Bundeskriminalamt (BKA) to the Tanzanian Police Force (TPF) on 18.11.2015


Honorable Inspector General of Police Mr. Mangu,
Deputy Commissioner of Police Ally Lugendo,
Detective Chief Superintendant Sven Radke,
Detective Chief Inspector Rainer Harms,
Distinguished Participants of the Police Academy Dar es Salaam,

It is my privilege and great pleasure to address you today on the occasion of this handing-over ceremony of equipment from the German Bundeskriminalamt to the Tanzania Police Force.

Germany and Tanzania are good development partners. Germany is one of the top donors. Sometimes we forget some of the other areas where we work together – be it TPDF or the police.

The BKA and the TPF can look back on a successful cooperation of Police Training Assistance in East Africa over the past 10 years. East Africa is a focal point for our Africa policy – we support the EAC as Regional Organization in this area. Main focus lies on “train the trainer” in the fields of crime scene work and criminal police investigation. In the last year, organized crime linked to drug trafficking became a major problem. Also in this field, BKA and TPF are strengthening their cooperation.



In 2014 and 2015 alone, the German government provide for all participating countries in East Africa an amount of up to more than 800.000.- Euros for this assistance. These are funds from the German tax payers channeled through the Ministry of Interior and Foreign Affairs.

Today, the Police Academy Dar es Salaam will receive classroom and computer equipment and tables and chairs for the Officers Mess. The Anti Terror Unit Dar Es Salaam will be equipped with five brand-new motorcycles, the same as CID Zanzibar and CID Arusha - altogether worth about 80.000.- Euros.

On this occasion I would like to thank you Mr. Radke and you Mr. Harms. Mr. Radke is the Head of Police Development Assistance Unit in BKA Berlin and Mr. Harms is the Advisor for Police Development Assistance of BKA in East Africa. Both have lobbied for East Africa and particularly for Tanzania. During their previous visits they have informed me about the Trainer – to –Trainer concept. For both and my colleagues of the Embassy Tanzania became an important and reliable partner.

I hope that the German contribution will help to continue to keeping up the good work of the Tanzanian Police Force and strengthen our bilateral cooperation.



Drive safely!

KILIMANJARO MARATHON 2016 YAPIGWA TAFU ZAIDI YA MILIONI 200

$
0
0



Meneja Mawasiliano ya Umma wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, John Wanyancha akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) katika hafla ya kuzindua msimu mpya wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2016, ambapo Tigo wametoa zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya mbio hizo. Hafla hiyo imefanyika leo asubuhi jijini Dar es Salaam.




Wadhamini wa mbio za Marathon msimu wa 2016 wakiwa katika picha ya pamoja.



Mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi msaidizi wa Michezo tokaWizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Alex Nkenyenge akizungumza na wageni waalikwa pamoja na wanahabari. Kushoto kwake ni Meneja Mawasiliano ya Umma wa kampuni ya simu za mkononi ya Tigo, John Wanyancha.








Wadhamini wa mbio za marathon msimu wa 2016, wakilipua baruti za makaratasi kuashiria kuzinduliwa kwa udhamini huo jijini Dar es Salaam leo asubuhi.



Wana habari wakiwa katika uchukuaji wa tukio hilo ili kuipasha jamii.


Wadau wa masuala ya riadha pamoja na wana habari mabalimbali wakifuatilia kwa karibu uzinduzi wa msimu wa mbio za marathoni za Kilimanjaro msimu wa 2016.

BREAKING NEWS: NAFASI YA KUTEULIWA WAZIRI MKUU NI KASSIM MAJALIWA

$
0
0

Jina la Ukoo:     Majaliwa
Jina la Kwanza:     Kassim
Jina la Kati:     Majaliwa
Tarehe ya Kuzaliwa:     1960-12-22
Mahali Alipozaliwa:
Hali ya Ndoa:     Nimeoa
Kundi:     Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano
Jinsia:     M
Simu ya Ofisi:     -
Simu ya mkononi:     0785205910
Barua pepe:     majaliwa.kasimu@yahoo.com
Anuani: P.O.Box 51,Ruangwa


Elimu
Toka    Hadi    Jina la Shule/Chuo    Cheti

1970     1976    Mnacho Primary School     cheti cha Elimu ya Msingi
1977     1980    Kigonsera Secondary School     CSEE
1991     1993    Mtwara Teachers College     -
1994     1998    University of Dar es Salaam     Bachelor Degree
1999     1999    Storckolm University     PGDP

Mafunzo Mengineyo
Uzoefu
Toka    Hadi    Jina la Mwajiri    Ngazi/Wazifa

2010     2014    -     MB
2006     2010    PM     Mkuu wa Wilaya
2001     2006    PS-CWJ     Katibu Mkoa
2001     2001    PS-CWJ     Katibu Wilaya
1988     2000    PS-Moec     Mkufunzi
1984     1986    TD-Lindi Council     Mwalimu

BURDEN : Soccer

MSAADA WA WASAMARIA WEMA WA MATIBABU UNAHITAJIKA KWA DADA HUYU

$
0
0

Ndugu Wasamaria wema
Napenda kutumia fursa hii kukushirikisha habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye, na migu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na mwanaye mwenye umri wa miaka 4.
Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo haikusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa  Mbeya ambako inasemekana alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,  hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa Mbeya baada ya kukosa shilingi 550,000/- za vipimo na matibabu.
Hadi nakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake (pichani kushoto) ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wote wawili kufariki dunia. 
Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye na bibi yake. Inasikitisha.
Hivyo nimejitahidi kufuatialia ili kujua mahitaji halisi lakini sikufanikiwa kumpata daktari bingwa wa mifupa . Ili kumsaidia Joyce inatakiwa aanze process upya za matibabu kuanzia hapa Mbeya referral Hospital  hadi Muhimbili jijini Dar es salaam.
Gharama za matibabu ni kama ifuatavyo:
1. shilingi 300,000/- za kupima CT-SCAN
2. Shilingi 250,000/- za MRI
3. Usafiri wa kutoka Mbeya-Dar kwa gari maalum la kukodi 700,000/-
4. Gharama za msaidizi ambaye ni rafiki yake 300,000/-
5. Chakula 450,000/- (Endapo watakaa hospitali mwezi mzima)
6. Gharama za matibabu (CT-SCAN&MRI ni vipimo tu) 500,000/-
7. Na mahitaji mengineyo wakiendelea kupata tiba 500,000/-

Hivyo kwa kuanzia kiasi cha shilingi 3,000,000/- (milioni tatu) kinahitajika kumpunguzia mateso dada yetu huyu. Asante sana kwa moyo wako wa kujitoa na Mungu atakubariki.

Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema
+255769 512 420

Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal amejitolea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba +255 754 271266 kwa jina la Ankal.

LOADING. . . KITI CHA NAIBU SPIKA KINAPIGIWA KURA SASA

$
0
0
DKT. TULIA ACKSON (CCM)                                    MAGDALENA SAKAYA (CUF)



TOA MAONI YAKO SASA HAPA CHINI 

BREAKING NEWS: WAZIRI MKUU RASMI NI KASSIM MAJALIWA, ASHINDA KWA 73.5%

$
0
0
Mh. Nassim Majaliwa
Matokeo ya zoezi la kura za Waziri Mkuu
Idadi ya wabunge ni 394 
Waliopiga kura ni 351 
Zilizoharibika ni kura 2 sawa na 0.06%,
Kura za Hapana ni 91 sawa na 25.9%
Kura za Ndio ni 248 sawa na 73.5%

Waziri Mkuu ametangazwa na kudhibitishwa rasmi na Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai na kuita ni ushindi wa Kimbunga.

Ataapishwa kesho tarehe 20/11/2015, katika Ikulu ndogo ya Chamwino, jijini Dodoma

KINYANG'ANYIRO CHA UNAIBU SPIKA, DK TULIA ACKSON APITA KWA KISHINDO

$
0
0
Dkt TULIA ACKSON MWANSASU

Matokeo ya zoezi la kura za Naibu Spika
Idadi ya wabunge halali kikatiba ni 394 
Webunge waliosajiliwa ni webbing 369
Akidhi ni 184

Waliopiga kura ni Wabunge 351, hakuna kura zilizoharibika 
Mh. Magdalena Sakaya amepata kura 101 sawa na 28.8%
Mh. Dk. Tulia Ackson Mwansasu amepata kura 250 sawa na 71.2%

Naibu Spika ametangazwa na kudhibitishwa rasmi na Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai. 

Dkt Tulia Ackson apishwa rasmi kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

RIHANNA KUFUNGUA BIASHARA YA BANGI, KUITWA "MaRihanna"

$
0
0
Mwanamuziki maarufu wa kimataifa wa nchini Marekani, Rihanna anajiandaa kuzindua biashara ya Bangi itakayoitwa “MaRihanna”

Kwa mujibu wa mtandao wa Celeb Stoner wa nchini humo, Rihanna atazindua biashara yake mpya itakayojulikana kama MaRihanna. 

Imeripotiwa kuwa Rihanna ametangaza jijini Jamaica pamoja na kwamba hapajakuwa na taarfa rasmi kutoka katika kambi yake.

Rihanna alisikika akisema “MaRihanna ya Rihanna kwa kweli itakuwa ni kanabis mpya duniani na ni fahari kubwa kuwa mkongwe. MaRihanna inakuja kuliwasha soko”




ISIS YATOA PICHA YA BOMU LILILOLIPUA NDEGE YA URUSI NA KUUA ABIRIA 224

$
0
0
Kundi la kigaidi la Kiislam, maarufu kama ISIS limetoa picha ya bomu na kudai ndilo lililotumika kulipua ndege ya Urusi katika anga ya Misri eneo la rasi ya Sinai mwezi uliopita na kuua abiria 224 waliokuwemo ndani ya ndege hiyo.

Picha hiyo (KULIA) ilichapishwa katika jarida lenye msimamo mkali la kiingereza likionesha neno “EXCLUSIVE - picha ya IED iliyotumika kushusha ndege ya shirika la Urusi” 

Picha hiyo ilionesha kikopo cha kinywaji cha soda aina ya Schweppes Gold na kuambatanishwa na vitu ambayvo ni sehemu ya vilipuzi.

Taarifa hiyo iliandika “ Tarehe 30, Septemba, 2015, baada ya kuunga mkono Nusayrī tāghūt kwa miaka mingi katika vita dhidi ya Uislamu wa Shām, Urusi imeamua kushiriki moja kwa moja kwa kutumia ndege zao katika vita hiyo.
Ilikuwa ni uamuzi wa haraka usio na busara wa Urusi, kana kwamba vita kupinga Uislam wa Qawqāz halikuwa kosa la kutosha.

Baada ya kupata njia za kiusalama za Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Sharm el-Sheikh za kushusha ndege ya taifa linaloshirikiana mataifa yanayoongozwa na Marekani dhidi ya vita na taifa la Kiislamu, lengo likabadilika na kuwa ni ndege ya Urusi.

Bomu liliingizwa kinyemela katika ndege hiyo, na kusababisha vifo vya raia wa Urusi 269 na wengine 5 ikiwa ni miezi michache baada ya uamuzi wa Urusi” 

Hata hivyo Urusi imesema bomu lilitumika kuangusha ndege hiyo iliyokuwa imebeba abiria ambao wengi walikuwa ni watyalii wa Kirusi.



BUSU LA SINEMA MPYA YA JAMES BOND LAZUA UTATA NCHINI INDIA

$
0
0
Bodi ya Filamu nchini India imeficha baadhi ya vipande vya filamu mpya ya James Bond “007” ijulikanayo kama “SPECTRE” vinavyoonesha akipiga mabusu, hatua hiyo ni kuendana na maadili na kulinda tamaduni na mila za nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN, Kiongozi wa Bodi hiyo, Pahlaj Nihalani ameliambia shirika la habari kuwa wamepunguza sehemu mbili zinazoonesha Daniel Craig(007) akimbusu Monica Bellucci pamoja na Lea Seydoux

“Kazi yetu ni kuziba maeneo yasiyofaa kutokana na daraja la sinema, kwa hiyo tumetekeleza hilo” Nihalani aliiambia AFP. Matusi mawili pia yameondolewa.

Hata hiyvo wakihojiwa na CNN, baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo walikosoa hatua hiyo. Ashok Pandit aliandika katika ukurasa wake wa Tweeter, “kimekuwa kituko cha uhuru wa watengeneza filamu.”

India ni nchi inayoficha matukio mbalimbali. Ni nchi yenye demokrasia kubwa kuliko nchi nyingi duniani, utamaduni wenye mijadala ya kisiasa ya kina pamoja na vyombo vingi vya habari.

Nchi hiyo imekuwa na historia ya kuzuia vitabu, filamu, miziki na hata ramani. Mapema mwaka huu mahakama moja nchini humo ilizuia filamu ya makala ya BBC “India’s Daughter”. Makala hiyo inaonesha mwenendo wa kesi ya ubakaji na mauaji.

Filamu nyingine ya vichekesho iliondolewa katika mtandao wa internet mwezi januari baada ya wazalishaji wa filamu hiyo kutishiwa kushtakiwa. Filamu nyingine ya "Fifty Shades of Grey" ilizuiwa kuingia katika nyumba za sinema nchini humo kutokana na picha za mapenzi.

Matukio yote hayo huusishwa na tamaduni na imani za dini. Katiba ya nchi hiyo inalinda uhuru wa kujieleza lakini kwa wale wanaonesha dharau kwa imani za dini wanaweza kuishia jela.
Uamuzi wa kuondoa vipande vya mabusu katika filamu ya Bond umeshambuliwa sana katika mitandao ya kijamii, ambapo kampeni mbalimbali zimeanzishwa.
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live