Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

TAARIFA : MAULID JUMATATU(13/01/14), SIKUKUU JUMANNE(14/01/2014)

$
0
0
Maulid ya kuadhimisha mazazi ya Mtume ( S.A.W) yatafanyika Jumatatu usiku -BAKWATA

MAULID ya kuadhimisha mazazi ya Mtume(S.A.W) yanatarajiwa kusomwa usiku wa Jumatatu tarehe 13.1.2014.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) kitaifa  maulid itasomwa Kigoma Mjini baada ya Swala ya I’sha.


Taarifa hiyo imeongeza kuwa baraza la maulid litafanyika saa tisa alasiri (9.00) mjini Kigoma siku ya Jumanne ya tarehe 14.1.2014  ambapo pia itakuwa siku ya mapumziko(Public Holiday)

ZITTO HUYO: CHADEMA YASIMAMISHA KIONGOZI WAKE

$
0
0
Lindi. 

Kamati ya utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, imemsimamisha Katibu wake, Jordan Membe, kwa madai ya kwenda kinyume na katiba ya Chama.

Habari kutoka wilayani humo zilizothibitishwa na uongozi wa chama hicho, ngazi ya wilaya na ile ya mkoa, zinaeleza Membe amesimamishwa kutokana na kukiuka maadili ya uongozi, ikiwa ni pamoja na kujihusisha na masuala ya kuleta na kusababisha vurugu ndani ya chama.

Baadhi ya wajumbe waliohudhuria kikao hicho, kilichofanyika makao makuu ya ofisi ya chama hicho, wilayani Nachingwea, ambao hawakupenda majina yao kuandikwa kwenye vyombo vya habari kwa madai sio wasemaji wa Chama, wameeleza kuwa Membe anadaiwa kusambaza waraka unaopinga kuondolewa kwa aliyekuwa Naibu Katibu mkuu, Zitto Zuberi Kabwe na wenzake.

SOMA ZAIDI...

Walisema kikao hicho kilichokuwa chini ya  mwenyekiti wa chama Wilaya ya Nachingwea, Hassani Likolovera na mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Mtwara, Kassimu Ahamadi Bingwe, zinaeleza kuwa Kamati imeamua kumsimamisha uongozi katibu wake kwa kukiuka kwa baadhi ya vifungu vilivyopo ndani ya katiba ya chama chao.

Aidha, wajumbe hao, walidai katika kikao hicho, kilikuwa na mvutano mkubwa, kwani wajumbe tisa kati ya 13 waliokuwepo katika kikao hicho, walipinga kitendo cha kusimamishwa Membe, huku wanne waliobaki wakipendekeza asimamishwe.

Pia,walisema wajumbe tisa walipinga hatua hiyo kwa madai hawajaona kasoro katika utendaji wake wa kutimiza majukumu yake ya kukitumikia chama hicho.
“Baadhi yetu wamepinga hatua hiyo, lakini wenzetu walisema asimamishwe, hivyo hali ndio ipo hivyo” alieleza mjumbe mmoja aliyehudhuria kikao hicho.


Katibu huyo alitafutwa lakini hakuweza kupatikana mara moja.

UJUMBE WA LEO: WANAGU SOMENI, HAMUONI MIMI NAUMIA

$
0
0
Pikipiki maarufu kama Bodaboda yenye namba za usajili T671BFS, ikiwa imebeba abiria na ujumbe wa maandishi yanayosomeka "WANANGU SOMENI HAMUONI MIMI NAUMIA" yakiambatana na picha inayoonesha mzazi akiwa na mzigo mzito na watoto wakiwa wamevaa sare ya shule, kama walivyokutwa jana jioni, eneo la Mwenge, Dar es Salaam.

MAZITO YAZIDI KUIBUKA : SAMAKI AZIDI KUMTESA MTOTO, SOMA HAPA

$
0
0

Mkuu wa Polisi Wilaya ya Bunda, Mika Nyange, ameagiza askari wake kufanyia uchunguzi taarifa za tukio la samaki aina ya sato kuruka na kuingia sehemu za siri na kisha kukimbilia tumboni mwa mtoto wa kike wenye umri wa miaka 12 (jina tunalo).


Tukio hilo linadaiwa kutokea Januari Mosi, mwaka huu wakati mtoto huyo akichota maji katika Ziwa Victoria ili aweze kumwagilia bustani. 
Akiwa amechuchumaa ndipo samaki huyo anayedaiwa kuwa mwenye ukubwa inchi nne aliruka kutoka majini na kuingia sehemu zake za siri na kukimbilia tumboni.

SOMA ZAIDI...

Baba mdogo wa mtoto huyo, Lenatus Mtani, alidai baada ya kumfikisha Hospitali ya Wilaya Ukerewe, alipimwa lakini samaki huyo hakuonekana tumboni. 
"Hospitali baada ya kumpima walisema hawaoni kitu, lakini anapoenda kujisaidia haja ndogo mkia wa samaki unaonekana," alisema Mtani. 


Alisema wameamua kumrudisha mtoto huyo kwa waganga wa kienyeji ambapo hali inazidi kuwa mbaya kwani ameanza kutoa harufu mbaya sehemu za siri. 
Kuonekana kwa mkia wa samaki huyo kumethibitishwa na bibi yake, Imaculate Mtani (64) na Monica Faustine, ambao ndiyo wanaomhudumia.

Akizungumzia tukio hilo kwa njia ya simu jana, OCD huyo wa Wilaya ya Bunda, alikiri kupata taarifa zisizo rasmi za tukio hilo kutoka kwa bwana mmoja ambaye hakumtaja jina. 


"Ndiyo nimepata taarifa zisizo rasmi za tukio hilo na nimeagiza askari wangu walifuatilie," alisema Nyange na kuongeza kwamba amepata taarifa kuwa mtoto huyo alipelekwa Hospitali ya Wilaya Ukerewe, lakini hawakupata msaada mzuri hivyo ikabidi wampeleke kwa waganga wa kienyeji. 


Aliongeza kuwa; "Nimeagiza askari wawafuate ndugu zake ili wampeleke hospitali kubwa." Pia alisema ameagiza Diwani wa Kata ya Napindi, Elias Magoti, kushirikiana na Polisi ili kufuatilia tukio hilo. 


Mganga Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Dkt. Hassan Mataka, alipoulizwa kama anafahamu tukio hilo, alisema halifahamu na kwamba kama kukitokea matukio ya ajabu huwa wanatoa taarifa. 
"Nimempigia Mganga Mfawidhi yeye ameniambia tukio hilo wamelisikia, lakini watu hao hawajafika hospitalini hapo," alisema Dkt.Mataka. Akizungumza na gazeti hili jana.

MASTAA WETU: DIAMOND AMFANYIA KWELI WEMA

$
0
0
Msanii wa musiki wa kizazi kipya Nasibu ‘Diamond’ Abdul inasemekana yuko anafanya mpango wa kumnunulia nyumba ya kifahari anayedaiwa kuwa mpenzi wake, Wema Sepetu.

Kwa mujibu wa gazeti moja jijini, “Diamond ameamua kuingia kwenye kujikamua huko kufuatia taarifa kwamba, mmiliki wa nyumba anayoishi Wema kwa sasa (jina lipo), Kijitonyama, Dar es Salaam amemwamuru mlimbwende huyo kuhama kwenye mjengo wake mara baada ya kumaliza mkataba mwezi Juni, mwaka huu. Awali mjengo huo aliutangaza ni wake”.

Imedaiwa kuwa mwenye nyumba huyo ameamua kuto kusaini upya mkataba wake na Wema ili mrembo huyo asiendelee kuishi hapo.

Mkataba wa Wema unaotakiwa kuisha mwezi juni, mwaka huu ulisainiwa kwa kipindi cha miaka mitano na kwamba Diamond aliposikia hilo akamwambia Wema isiwe tabu huku akimuahidi kumnunulia nyumba yenye thamani ya shilingi milioni 125

Kwa mujibu wa gazeti hilo, nymba hiyo iko maeneo ya Mwananyamala, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

BREAKING NEWS: PICHA BASI LA MTEI LAUA, LACHOMWA MOTO LEO SINGIDA

$
0
0

Taarifa zilizotufikia mapema leo zimesema ajali imetokea Mkoani Singida iliyohusisha basi la abiria la Mtei na pikipiki iliyokuwa imebeba wanafamilia watatu katika mtindo wa mshkaki na kusababisha kifo cha wawili katika eneo la ajali na mwingine kufia njiani wakati anakimbizwa hospitali.

Ajali hiyo iliyotokea saa mbili na nusu asubuhi katika eneo la minara ya Posta na TBC mkoani Singida, ilisababishwa na dereva wa pikipiki alipokuwa akitaka kukata kona bila kuonyesha ishara ya taa wakati basi la Mtei likiwa lina ovateki.


Basi la Mtei lililokuwa limebeba abiria wakati limeanza safari ya kuelekea Arusha, ililazimu abiria wote kushuka wao na mali zao wakati wananchi wenye hasira kali walipoamua kujichukulia sharia mkononi kwa kulichoma basi hilo kama linavyoonekana pichani (chini).

MAGAZETI YA TANZANIA LEO 10/01/2014 LEO YANATOFAUTI

HII IMEKAAJE : NUSURA AUWAWE NA MUMEWE KISA SOMA HAPA

$
0
0
Shinyanga

Mwanamke mwingine mkazi wa Lubaga Manispaa ya Shinyanga amenusurika kifo kutokana na kipigo alichokipata kutoka mumewe akimtuhumu kutopokea simu haraka. Kipigo hicho kilisababisha mwanamke huyo kulazwa hospitali akiwa mahututi mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo (jina limehifadhiwa) ambaye hivi sasa amelazwa katika hospitali ya serikali mkoani Shinyanga akipatiwa matibabu chanzo cha yeye kupokea kipigo kutoka kwa mumewe ni kuchelewa kupokea simu aliyokuwa amempigia.

Mwanamke huyo amemtaja mumewe kuwa ni Daniel Daud na kwamba tukio hilo lilitokea wiki iliyopita baada ya kushindwa kupokea simu aliyopigiwa na mumewe kutokana na wakati huo alikuwa akivuka barabara na hivyo kuhofia kugongwa na gari.

Alisema mara ya kufika nyumbani mumewe alianza kumfokea na kuhoji kwa nini alichelewa kupokea simu aliyokuwa amempigia na kudai huenda alikuwa na mwanamume mwingine na ghafla alianza kumshambulia kwa kipigo sehemu mbalimbali za mwili wake.

“Nilijaribu kumuelewesha mume wangu kwamba wakati akipiga simu nilikuwa navuka barabara hivyo nisingeweza kupokea simu wakati huo nikihofia kugongwa magari, na kwamba hata angemuuliza dada yake mdogo mwenye umri wa miaka saba tuliyekuwa pamoja angemthibitishia ukweli,”

“Pamoja na maelezo yangu hakunielewa, hata dada yake alipojaribu kunitetea na kueleza ukweli bado aliendelea kunifokea na kudai mimi ni mwanamke malaya na hivyo alianza kunipiga ngumi sehemu mbalimbali za mwili na kunisababishia maumivu makali mwilini,” alieleza.

Hata hivyo alisema pamoja na juhudi za wifi yake kutaka kuamua ugomvi huo hakufanikiwa kutokana na kuwa mdogo kiumri ambapo baada ya kipigo alichukua uamuzi wa kumfungia chumbani na kisha yeye mwenyewe aliondoka nyumbani na kutokomea kusikojulikana.

Alisema alikaa ndani bila ya matibabu yoyote na kusababisha sehemu zilizokuwa na majeraha kuanza kutoka usaha huku akihisi maumivu makali na kwamba aliokolewa katika hali hiyo na jirani yake aliyekwenda kumuangalia baada ya kutomuona akitoka nje kwa siku mbili.

“Rafiki yangu mmoja alikuja nyumbani wakati mume wangu hayupo nilimweleza hali yangu kuwa si nzuri kutokana na kipigo nilichokipata, alisikitika sana na kuchukua uamuzi wa kuniiba ambapo alitafuta gari na kunikimbiza hapa hospitali ili niweze kutibiwa baada ya kupata fomu namba tatu kutoka polisi,” alieleza.

Kwa upande wake mganga mfawidhi katika hospitali ya serikali mkoani Shinyanga, Dkt. Fredrikck Mlekwa alithibitisha kupokelewa kwa mgonjwa huyo hospitalini hapo na kwamba hivi sasa amelazwa wodi namba saba ambayo ni ya majeruhi akiendelea kutibiwa majeraha aliyoyapata kutokana na kipigo cha mumewe.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala amekiri kutokea kwa tukio hilo na kwamba hivi sasa polisi inaendelea na msako wa kumtafuta mtuhumiwa huyo ili aweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani kujibu shitaka la shambulio la kudhuru mwili alilomtendea mkewe.



Tukio hili ni la pili kutokea mjini Shinyanga ndani ya wiki moja likihusiana na vitendo vya kikatili vinavyofanywa na baadhi ya wanaume dhidi ya wake zao ambapo tukio la awali lilitokea huko katika Mtaa wa Katunda baada ya mwanamke mmoja aliyedai talaka kupokea kipigo kikali kutoka kwa mumewe.

ACHA TU:JAMANI SHINYANGA NI BALAA…ONA HII

$
0
0
Shinyanga

Mkazi wa kijiji cha Ibelansuha kata ya ushetu wilayani Kahama mkoa wa Shinyanga amekufa papo hapo baada ya mdeni wake aliyekuwa akimdai kiasi cha shilingi 3,000 kumpiga na mpini wa jembe sehemu za ubavuni.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala amemtaja aliyekufa kuwa ni Magulu Mhangwa (35) na kwamba tukio hilo limetokea Januari 5, mwaka huu saa 2.00 asubuhi huko kijijini Ibelansuha wilayani Kahama.

Akifafanua kamanda Mangala alisema siku hiyo ya tukio Mhangwa alimfuata mtu mmoja aliyetambuliwa kwa jina moja la Majaliwa kwa ajili ya kudai fedha alizokuwa amemkopesha kiasi cha shilingi 3,000 ambapo baada kudaiwa fedha hizo alichukua uamuzi wa kumshambulia mdai wake.

SOMA ZAIDI...

“Mhangwa siku hiyo alimfuata huyo mtu aliyekuwa amemkopesha fedha zake na kumuomba amlipe deni hilo, lakini jambo la kusikitisha, mdaiwa alishikwa na hasira za kudaiwa ndipo alipookota mpini wa jembe na kumpiga nao mdai wake sehemu za ubavuni na kusababisha kifo chake papo hapo,” alieleza Mangala.

Kamanda Mangala alisema mara baada ya mtuhumiwa huyo kubaini Mhangwa amekufa alitoroka na kwenda kusikojulikana ambapo hivi sasa polisi inaendelea na msako wa kumtafuta ili aweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Katika tukio lingine mwanafunzi mwenye umri wa miaka minane aliyekuwa akisoma darasa la kwanza katika shule ya msingi Buchambi wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, Paschal Mahembo amekufa papo hapo baada ya kugongwa na gari lililokuwa katika mwendo kasi.

Kamanda Mangala alisema ajali hiyo ilitokea juzi saa 5.45 asubuhi huko katika barabara ya Shinyanga kuelekea Mwanza eneo la kijiji cha Buchambi wilayani Kishapu wakati mwanafunzi huyo alipokuwa akikatisha barabara.

Alilitaja gari lililosababisha kifo hicho kuwa ni lenye namba za usajili T. 398 BKA Toyota Land cruiser mali ya kampuni ya Salum Transport Ltd. ya wilayani Nzega mkoa wa Tabora likiendeshwa na dereva aliyetajwa kwa jina la Paulo Michael (30).

Kamanda Mangala alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa gari hilo alipokuwa akitokea wilayani Bariadi mkoa wa Simiyu akielekea Nzega na kwamba uchunguzi wa kina unaendelea.

NEWS: ABIRIA 1600 WAANDAMANA KUSHINIKIZA USAFIRI

$
0
0
Dodoma.

Zaidi ya abiria 1600 waliokuwa wakisafiri kwa kutumia reli ya kati kutoka mkoani Kigoma kwenda mikoa ya Morogoro na Dar es Salaam juzi waliandamana kuelekea katika ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakipinga safari yao kusitishwa na Shirika la reli Tanzania(TRL) kutokana na kuharibika kwa reli eneo la Gulwe na Godegode wilayani Mpwapwa.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake mbele ya mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt, Rehema Nchimbi mmoja wa abiria hao aliyejitambulisha kwa jina la Alphonce Evarist alisema kuwa wameshakaa njiani kwa muda wa siku nane tangu watoke Kigoma kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya reli ya Dodoma kuharibika kwa kusombwa na maji yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

“Tukiwa Kigoma tuliahirishiwa safari kwa madai kuwa reli ya hapa Dodoma imeharibika kwa kusombwa na maji ya mvua sasa na tulipofika hapa tukaambiwa kuwa bado wanatengeneza reli sasa ni reli gani hiyo ambayo inatengenezwa kwa muda wa siku saba?”alihoji Evaristi.

Aliongeza kuwa abiria wengi wamepoteza mali zao ikiwemo mizigo na pesa hata kukosa chakula pamoja na kuuza baadhi ya vitu vyao ili kununua jambo ambalo limekuwa kikwazo kwao kutokana na kuishiwa na pesa pamoja na vitu vya kuuza ili kuweza kujikimu kwa chakula.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt, Rehema Nchimbi alikiri kuwepo kwa tatizo la kuharibika kwa reli hiyo katika eneo la Gulwe na Godegode lililoko katika Wilaya ya Mpwapwa na kusema kuwa hici karibuni reli hiyo ilitengenezwa na treni kuendelea na safari lakini kumetokea na uharibifu huo kwa mara nyingine ambapo wahusika wanalishughulikia tatizo hilo.

“Kipande cha reli katika eneo la Gulwe na Godegode ni moja kati ya eneo korofi sana kwakuwa mara nyingi huwa hukumbwa na mafuriko na ni kweli walishatengeneza hivi karibuni na baada ya matengenezo yalitokea mafuriko mengine na kusomba reli hiyo kwa mara nyingine tena,” alisema Dkt, Nchimbi.

Hata hivyo aliiagiza kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Dodoma mjini kwa kushirikiana na uongozi wa TRL kuhakikisha zinaangalia usalama wa abiria hao kwa kipindi chote watakapokuwa mkoani hapa hadi usafiri wao utakapopatikana mara baada ya TRL kukamilisha matengenezo yao.

Aidha aliuagiza uongozi wa TRL kuhakikisha abiria wote wanapata huduma zote mihumu bure ikiwemo ya chakula na maliwato hadi hapo watakapo anza safari yao kwakuwa kwa wakati huo hapakuwa na usafiri wa magari ya kuwafikisha wanapokwenda kutokana na magari yote kuondoka hivyo hapakuwa na magari ya kutosha kuwarejesha makwao na kuwataka wavumilie hadi huo muda waliopewa na TRL.



Kwa upande wake Mhandisi Mitambo kutoka TRL mkoa wa Dodoma John Mandalu aliahidi kuwasaidia abiria hao huduma za chakula hadi safari yao itakapokuwa tayari kuanza na kuahidi hadi kufika saa 11 jioni ya jana tayari safari yao itaanza.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI 11/01/2014

ONA HII: INADAIWA MWIGULU,RIDHWANI&KAPUYA MARUFUKU KUINGIA MAREKANI

WEMA AWEKA VIDEO AKIWA KITANDANI NA DIAMOND, ANGALIA ...

WEMA ALIVYOANDIKA AKIWA NA DIAMOND KITANDANI

$
0
0
Hapa alikuwa anaandika nyombi wakati Wema anamrekodi kwa simu yake, comment inaonyesha maelezo zaidi

WAZIRI MKUU AFARIKI, ALILAZWA KWA MIAKA 8 AKIWA HAJITAMBU

$
0
0
Aliyekuwa kiongozi wa Israel Ariel Sharon (kulia), amefariki akiwa na umri wa miaka 85. Alipatwa na Kiharusi Januari mwaka 2006 na tangu hapo akawa anatumia mashine kupumua. Hatimaye viungo vya mwili wa Sharon vimekuwa vikiathirika kutokana na hali yake mahututi.

Sharon alizaliwa katika eneo la Palestina mwaka 1928. Alipigana katika vita kati ya waarabu na wapalestina kati ya mwaka 1948-49 na kuongoza majeshi ya Israel mapema miaka ya hamsini
Mwaka 1971, Sharon aliamuru kuharibiwa kwa nyumba 2,000 za wapalestina katika juhudi zake za kukabiliana na wapiganaji wa kipalestina waliokuwa wanapigania uhuru wa Palestina

Mwaka 1973, Sharon alihudumu katika jeshi wakati wa vita vya Mashariki ya Kati. Kama waziri wa kilimo chini ya utawala wa Menachem Begin, aliunga mkono sera ya kujenga makazi ya walowezi katika eneo la Palestina

Kama waziri wa ulinzi Sharon alioongoza uvamizi dhidi ya Lebanon mwaka 1982. Alifanya hivyo ili kuwezesha wanajeshi wakristo wa Phalangist kuingia katika kambi za Sabra na Shatila kuwasaka wapiganaji wa PLA.

Maelfu ya watu walifariki katika vita hivyo, na kupelekea wapalestina kumuita Sharon muuaji. Waisraeli, 400,000 waliandamana kupinga matamshi hayo. Sharon aliungwa mkono na mkewe wa pili Lili na wanawe Omri na Gilad. Mkewe wa kwanza Margalit alifariki katika ajali ya barabarani, mwaka 1962. Mwanawe Margalit alifariki mwaka 1967 katika tukio la ufyatulianaji risasi. Naye Lili alifariki mwaka 2000

Sharon alijiondoa katika siasa na wala hakuonekana sana hadharani akitoa matamshi ya kisiasa baada ya kustaafu. Lakini mapema miaka ya 1990, nyota yake ilianza tena kung'aa na mwaka 1999 alichaguliwa kama kiongozi wa chama cha Likud.

Sharon alianza kuwaondoa walowezi kutoka katika ukanda wa Gaza na maeneo machache ya Ukingo wa magharibi mwaka 2005. Kitendo chake hicho kiliwaghadhabisha baadhi ya wafuasi wake na kumlazimisha kudhibiti usalama zaidi

Mnamo mwezi Septemba mwaka 2000, huku hali ya taharuki ikishuhudiwa, ziara ya Sharon katika Hekallu la Mount/Dome eneo takatifu kwa wakristo na waisilamu, ilizua utata na kuchochea harakati za waplestina dhidi ya Israel.

Mwaka 2001, Sharon alishinda uchaguzi mkuu baada ya kuwaahidi waisraeli kuwa angekabiliana vilivyo na mashambulizi yoyote kutoka kwa waplestina. Lakini uhasama ulikithiri na Sharon akachoka kuwa mvumilivu kwa wapalestina

TAARIFA HII NI KWA MUJIBU WA MTANDAO WA BBC

LIVE BEYONCE AKIRI KUABUDU DINI YA MASHETANI..! SOMA HII

$
0
0

Hivi karibuni katika kipindi cha mahojiano Beyonce (Bey) akihojiwa na mwana mama tajiri na ntangazaji maarufu Oprah aliyefanikiwa pengine kuliko wanawake wote duniani, hatimaye alikubali kuwa ni mmoja wa kundi la wanaojiita New World Order ambao pia wanajulikana kama Illuminati.

Beyonce ambaye ni msanii maarufu wa muziki na mke wa msanii Jay Z ambao kwa pamoja waliwahi kutembelea Tanzania miaka ya hivi karibuni amedaiwa kuhusishwa na kundi hilo linalo abudu mashetani huku Tanzania maarufu na huusishwa na freemasons, ni kundi maarufu sana lililoibuka huko Marekani.

Uvumi ulizuka kuwa Beyonce ni Illuminati na kwamba kwanini Oprah akumuuliza swali kuhusina na uzushi ulioenea kuhusu mahusiano yake na illuminati na kudaiwa kuwa ni sababu pia yeye mwenyewe (Oprah) anajihusisha na shughuli za illuminati.

SOMA ZAIDI…

Kwa muda usiozidi sekunde 3 Oprah alimgeukia Beyonce na kumwambia “unajua nini, ntakwambia…illuminati” baada ya hapo Beyonce akaanza kufanya mambo ya kiiluminati.

Kwa mujibu wa mtandao wa Huffington Post, imedaiwa kuwa umaarufu mkubwa wa Bey na mafanikio yake hayo ni kutokana na msaada mkubwa wa kundi hilo la Illuminati.

Inadaiwa Bey aliamua kufunguka na kuweka wazi shukrani zake kutokana na mafanikio yake na kuwashukuru waliko nyuma yake kwa msaada wao mkubwa waliompa.

Alisema “watu wanajiuliza siri ya uzuri na muonekano wangu usiozeeka wa usiozeeka, ni ksababu ya hizo damu nazokunywa katika sadaka na matoleo”

ANGALIA ZAIDI KWENYE http://www.huffingtonpost.com/reductress/beyonce-illuminati_b_4470601.html?utm_hp_ref=email_share

MAJANGA: LIVE MAKALIO YA KUONGEZA YAMUUMBUA SUPERSTAR JUKWAANI

$
0
0
Mwanadada mwanamuziki maarufu K’Mitchelle(Pichani Kulia), anayekuja juu kwa kasi ya ajabu nchini Marekani alikumbwa na mkasa ambao sidhani kama atausahau kwenye maisha yake.

Taarifa zilizo enea katika vyombo vya habari na kuchapishwa katika mtandao wa beforeitsnews nchini Marekani, zilimkariri msemaji wake jana akisema “K’Mitchel alienda ku-twerk (style mpya ya kucheza muziki ya kutingisha makalio), makalio yake yakagoma kutoa ushirikiano na ndipo tulihisi kuna tatizo pale”

Msemaji wake alidai kuwa walihisi tatizo ni kubwa kupindukia pale walipoona makalio ya mwanadada huyo hayatingishiki kama ilivyo kawida yake akianza kucheza mtindo huo. Iliwalazimu kupiga simu kitengo cha dharura 911 ili kupata huduma ya kwanza kwa msaada zaidi.

SOMA ZAIDI...

Katika msimu huu wa majira ya baridi kali nchini Marekani, inadaiwa makalio ya mwanadada huyo ambayo ni ya kuongeza kwa kwa upasuaji hospitali (Implant) yalizidiwa na baridi iliyopita kiwango kinachostahili.

Huku baridi ikizidi kuwa kali na joto kushuka kufikia digiree 0, ilibidi K’Mitchel alazwe hospitali mapema asubuhi jana jijini New York baada ya kugundua kuwa makalio yake hayatingishiki hata akijaribu vipi.

Bi dada K’Mitchelle anajulikana kwa makalio yake yalivyo makubwa na mwonekano nzuri, “la sivyo angekuwa demu wa kawaida tu kama waimbaji wengine” alidai mmoja wa mashabiki wake akimaanisha kuwa makalio yake yanamsaidia kumuinua na kumuongezea mashabiki na umaarufu.

Shabiki huyo aliyekuja hospitali kumtia moyo mwanadada huyo, aliongeza “hebu pata picha ya lile tako kwa karibu”

Hata hivyo madaktari walifanikiwa kuondoa kipandikizi kilichokuwa kinampa shida mwanadada huyo na kukipasha joto mpaka kilipokuwa tayari kurudishiwa katika makalio yake tena.

LIVE JINSI WAUMINI WALIVYOSHAWISHIWA KULA MAJANI KANISANI

$
0
0


Muhubiri wa kikristo amekuwa akiwahamuru waumini wake kula majani ili kuwa ‘karibu ni Mungu’ kabla ya kuanza kuwaombea kama wanavyoonekana pichani.

Katika mahubiri ya Mchungaji(Pastor) Lesego Daniel (Pichani kushoto) wa Rabboni Center Ministries, kundi la wa waumini walianguka chini na kuanza kula majani katika huduma yake huko Garankuwa, kaskazini mwa jiji la Pretoria nchini Afrika Kusini baada ya kuambiwa ‘mtakuwa karibu zaidi na Mungu’.

kwa mujibu wa mtandao wa The Daily Mail wa nchini Uingereza, mwenendo wake huo wa ajabu umekosolewa na maelfu ya watu pamoja na kwamba waumini wake wameapa maisha yao kuendana na mtazamo wa Pastor Lesego

Mchungaji huyo anadaiwa kutamka kuwa mwanadamu anaweza kula chochote na kuishi kwa chochote atakachokula.

“Ndio tunakula majani na tunajiskia fahari kubwa kwani huo ndio uwezo na nguvu za Mungu, na kwa nguvu hiyo tunaweza kufanya lolote” alisema mmoja wa waumini wa kanisa hilo Rosemary Phetha akiongea na Time Live, televisheni ya Afrika Kusini.

Rosemary ambaye ni msichana wa miaka 21 amekuwa akipatashida kumeza huku akisumbuliwa na  koo kwa zaidi ya mwaka lakini aliponywa baada ya kuanza kula majani.

 ANGALIA MAPICHA ZAIDI...








HAPPY MAULID: KESHO SIO SIKU KUU, NI JUMANNE

$
0
0


Maulid ya kuadhimisha mazazi ya Mtume ( S.A.W) yatafanyika Jumatatu usiku -BAKWATA

MAULID ya kuadhimisha mazazi ya Mtume(S.A.W) yanatarajiwa kusomwa usiku wa Jumatatu tarehe 13.1.2014.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (BAKWATA) kitaifa maulid itasomwa Kigoma Mjini baada ya Swala ya I’sha.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa baraza la maulid litafanyika saa tisa alasiri (9.00) mjini Kigoma siku ya Jumanne ya tarehe 14.1.2014 ambapo pia itakuwa siku ya mapumziko(Public Holiday)

SURPRISE: MTOTO WA NDAUKA APEWA ZAWADI YA AJABU…SOMA HAPA

$
0
0
Msanii wa filamu Tanzania Rose Ndauka aambaye alipata mtoto hivi karibu akiwa salama kabisa yeye na mwanae wamepata zawadi ambayo hawakutegemea kutoka kwa baba wa mtoto hivi karibu.

Maliki Bandawe(pichani akiwa na Rose Ndauka) ambaye pia ni msanii wa musiki wa kizazi kipya alimzawadia mtoto wake nyimbo maalum aliyoitunga na kuingia studio kwaajili hiyo tu.

Kama Jay Z na Beyonce, Malik aliamua kutunga nyimbo maalumu kwaajili ya mwanae wa kike ambaye mpaka tunakwenda mitamboni nyimbo hiyo imeshaanza kuingia sokoni.

SOMA ZAIDI...

Habari kutoka kwa watu walioko karibu na Rose zinasema, Rose alijifungua salama mtoto wa kike tarehe 27 mwezi disemba katika hospitali ya Muhimbili kwa njia ya upasuaji.

Mtoto huyo ambaye amepea jina la Naveen anaendelea kukua na afya njema. Mashabiki na wapenzi wa msanii huyo wa filamu wanamsubiri kwa hamu kubwa Rose ambaye imekuwa ni vigumu sana kuonekana.

Jitihada za kumpata Rose ili kuzungumzia hali yake ziligonga mwamba na hatimae kumpata superstaa aliyekwenda kumjulia hali na kumtakia afya njema katika mafanikio yake na kupokea mtoto wa kike.


Inadaiwa Malik alipatwa na furaha ya ajabu alipo pata taarifa ya kufunga mwaka salama kwa kupata taarifa hizo njema.
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live