Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

VIDEO: NUMBER 1 REMIX YA DIAMOND HII HAPA


IGP MPYA AKUTANA NA KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI

$
0
0



Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu (kushoto) akimfafanulia jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) kuhusiana na masuala mbalimbali ya uboreshaji wa jeshi hilo. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi na Naibu Inspekta Generali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki. IGP Mangu pamoja na Naibu wake walikutana na Katibu Mkuu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo.






KULIA:Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kulia) akiagana na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Ernest Mangu baada ya mazungumzo yao kuhusiana na masuala mbalimbali ya uboreshaji wa jeshi hilo. Wapili kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mwamini Malemi na Naibu Inspekta Generali wa Polisi, Abdulrahman Kaniki. IGP Mangu pamoja na Naibu wake walikutana na Katibu Mkuu ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo.

VIDEO : MAKOMANDO - KIBABABABA

BANGI NOMA: 37 WAPOTEZA MAISHA SIKU MOJA TU BAADA YA KUHALALISHWA

$
0
0
Imebidi serikali ifikirie upya uamuzi wake wa kuhalalisha uvutaji bangi baada ya watumiaji kuzidisha kiwango cha matumizi mpaka kusababisha vifo, kwa mujibu wa mtandao wa daily currant.

Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya Rocky Mountain, watu wapatao 37 walikufa siku ya mwaka mpya, siku moja tu baada ya kuhalalisha ununuzi wa bangi kwa watu wazima huko Colorado, Washington, Marekani. Wakati huo huo baadhi wakiwa wamelazwa hospitali bila matumaini yoyote ya kuishi.

“Imekuwa balaa” anasema Dr. Jack Shepard, mganga mkuu wa upasuaji katika hospitali ya St.Luke Medical Center huko Denver

“nimesha hifadhi miili mitano ya wanafunzi wa vyuo tokea asubuhi na wengine wanaendelea kuongezeka kila dakika.”

Alidai kuwa tatizo kubwa ni mshtuko wa moyo na maradhi mengine yanayo husiana hayo pamoja na baadhi ya viungo vya mwili kushindwa kufanya kazi.



“Mpaka kufikia wiki ijayo, vifo vitakuwa vimefika mpaka 200 au labda 300. Panahitajika kusimamisha hichi kichaa. Mungu wangu kwanini tumehalalisha bangi? Tunafikiria nini?” aliongea Dkt Shepard kwa masikitiko

ZITTO KACHAFUA MAGAZETI LEO, HEBU ONA

MKONO: GARI NILITOA NDIO, KWA ZITTO NA MBOWE

$
0
0
Mbunge wa Musoma Vijijini (CCM), Nimrod Mkono (Kushoto Pichani) ametoa ufafanuzi juu ya uhusiano wake na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe.

Hatua hiyo ya Mkono imekuja baada ya Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kumtuhumu kuwa aliwahi kumpa Zitto magari mawili.

Katika taarifa yake aliyoitoa jana, Mkono alisema kuna magari mawili yanayohusishwa na Zitto na kuyataja kuwa ni Toyota Land Cruiser na Nissan Patrol.

“Sijawahi kumpatia Zitto magari, isipokuwa kuhusu hiyo Land Cruiser, nilitoa msaada wa kuwanusuru Zitto na Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe), kule Tarime kwenye msiba wa marehemu Chacha Wangwe (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti Chadema), kwani walikuwa wakitishiwa kupigwa.”

Alisema alitoa gari hilo lililokuwa na Bendera ya Bunge liwachukue Mbowe na Zitto na kuwapeleka Mwanza... “Walipofika Mwanza, Zitto aliwasiliana na mimi kuhusu ununuzi wa gari hilo na kupitia wakala wangu nilimuuzia,” alisema Mkono.

Kuhusu Nissan Patrol, Mkono alisema lilikodishwa kwa Zitto na mpaka sasa bado analipa gharama za kulikodisha...

“Hata nyaraka za umiliki wa gari hili ninazo mimi mwenyewe kama mmiliki halali. Ninamiliki magari mengi tu hata wewe mwandishi ukitaka Vogue (aina ya gari) nitakukodisha tu,” alisema Mkono.

Alisema wanafahamiana kwa siku nyingi hata kabla ya Zitto kuwa mbunge na kwamba aliwahi kufanya mazoezi kwa vitendo katika ofisi yake (Mkono), alipokuwa mwanafunzi.

TULIPOFIKA SASA BASI: MKE AUA MUME, KISA 25,000/-

$
0
0
Singida

Mkazi moja wa Kijiji cha Ntewa Kata ya Ntuntu wilayani Ikungi Mkoa wa Singida Juma Abdalah (44) amefariki dunia baada ya kupigwa kwa kipande cha mti usoni na mke wake baada ya kumtuhumu kumwibia sh. 25,000/.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Geofrey Kamwela, tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 2 mwezi huu saa 7.00 mchana, ambapo mtuhumiwa Veronika Hamisi (25) ambaye ni mke wa marehemu anadaiwa kufanya kitendo hicho.

Katika taarifa yake iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana mjini Singida, Kamwela alieleza kuwa siku hiyo marehemu pamoja na mkewe walikuwa wametoka kilabu cha pombe ya kienyeji, na walipofika nyumbani marehemu alichukua sh. 25,000/= zilizokuwa zimehifadhiwa katika pochi.

“Fedha hiyo ambayo inadaiwa ilikuwa ni mali ya mwanamke huyo, alidai arudishiwe kiasi hicho na mme wake, lakini jambo hilo halikuwezekana” alisema Kamanda Kamwela.

Alibaini kuwa baada ya juhudi za kumnyan’ganya fedha hiyo marehemu kutofanikiwa ndipo Veronika Hamisi alipoita wanaume wengine wawili ambao bado hawajajulikana na kushirikiana naye ili iweze kurudishwa.

Alisema kuwa katika purukushani hizo ndipo mtuhumiwa alipopata nafasi ya kuchukua kipande cha mti na kumpiga mme wake kichwani sehemu ya paji la uso na kufariki papo hapo, wakati wanaume hao wawili walikimbia kusiko kujulikana.

“Uchunguzi wa kina wa tukio hilo la aina yake katika mwanzo wa mwaka unaendelea ikiwa ni pamoja na kuwakamata watuhumiwa wengine wawili wanaosadikiwa kushirikiana na mke wa marehemu kufanya kitendo hicho”. Alisema Kamanda huyo.

Aliongeza kuwa mke wa marehemu amekamantwa na jeshi la polisi kuhusiana na tukio hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili mara uchunguzi huo utakapokamilika.


HAPA WANANCHI HAWAJAIELEWA EWURA

$
0
0
 Moshi

Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mjini Moshi (MUWSA), imeiangukia Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ili kurejesha tozo ya huduma ya majitaka kwa wananchi baada ya kubaini wananchi kufurahia hatua hiyo na kuanza kutupa taka ngumu zinazoharibu mtandao huo.

Imebainika kwamba wananchi hutupa taka ngumu zinazoziba mtandao huo na kuipa kazi ya ziada MUWSA kuizibua huku baadhi ya mitaa majitaka yakianza kutiririka na kuchafua mandhari ya manispaa ya Moshi.

Akizungumza mbele ya waziri wa maji, Profesa Jumanne Maghembe, mkurugenzi wa mamlaka hiyo mhandisi Cyprian Luhemeja alisema tayari ofisi yake imewasiliana na EWURA ili irejeshe tozo hizo ili kujenga nidhamu ya wananchi katika kutumia mtandao huo.

“EWURA imeondoa tozo hili katika agizo lake namba 13-03 la kubadili bei za huduma za majisafi na majitaka za mamlaka lililotolewa Julai 2013 na kuanza kutumika mwezi Agosti 2013” alisema.

Mbali na tozo hiyo, Luhemeja alisema katika siku 180 walizokuwa wamemuahidi waziri, wanatarajia kuongeza makusanyo ya maji kutoka Sh mil 302 ya Juni 2013 hadi sh mil 821 Juni mwaka 2014.

Mipango mingine iliyopo katika utekelezaji ni kupanua mtandao wa maji kwa kuongeza wateja 21,000 hadi wateja 35,000 ifikapo Juni mwaka 2014.

Awali waziri Maghembe,pamoja na kuipongeza MUWSA kwa kuongeza vyanzo vya maji vya Coffee Curing na tankila maji la Kilimanjaro vitavyomaliza tatizo la maji mjini humo,alitaka mgawo wa maji kutorejea mjini humo.

“Mara kadhaa nilikuwa nikisikia kuhusu mgawo wa maji,naomba muhakikishie mgawo wa maji mjini humo uliokuwa ukiripotiwa awali haurejei tena”alisema.

HII KIBOKO: BIRTHDAY YA MICHELLE OBAMA, KULA KABISA KABLA,HAKUNA MSOSI

$
0
0
Washington, USA.

Wageni wote watakao hudhuria hafla ya kusherehekea miaka 50 ya kuzaliwa ya mke wa raisi wa Marekani, Michelle Obama katika Ikulu ya Marekani (White House) hawatokula chakula cha jioni.

Kwa mujibu wa mtandao wa gazeti la Washington Post, baadaye mwezi huu First Lady Michelle atatimiza miaka 50 ambapo mwaliko kwa wageni wote uliwashauri kula kabisa kabla hawajaja kwenye tafrija ya kuzaliwa kwake.
Katika halfa hiyo ya kukata na shoka inayosubiriwa kwa hamu, wageni wametakiwa kujiandaa ipasavyo, viatu visafi kwaajili ya kusakata rumba la ukweli.
Hata hivyo huo umekuwa ni mtihani mkubwa kwa waandaaji wa shughuli hiyo huku wakikuna vichwa jinsi shughuli hiyo itakavyokuwa.
Watu mbali mbali hawakusita kuonyesha hisia zao kutokana na tukio hilo.

“Sidhani kama kuna ubaya, lakini pia ni tofauti kidogo na jinsi watu walivyozoea” alisema Lizzie Post, mjukuu wa mwandishi maarufu wa kitabu cha masuala ya hafla za nyumbani.
Naye rafiki wa karibu wa Oprah Winfrey, Colin Cowie alitoa hisia zake “kuwaambia watu wale kabla hawajaja sivyo ambavyo ningefanya, mara nyingi nafikiri chakula ndio kinawafurahisha watu ikifuatiwa na muziki, bar iliyopendeza na huwezi kuvitenganisha”

Bi Obama alisikika akiwaambia watoto wa shule hivi karibuni kuwa anakaribia kufikia miaka 50 na kwamba atasherehekea ki-namna yake mwenyewe. Na kuamini kwamba jinsi unavyozidi kukua, ndiyo unavyozidi kuwa huru kusema unachotaka

ONA HII: RAISI WA TFF AMUUNGA MKONO WAZIRI MEMBE

M/KTI CHADEMA APIGWA, ATOLEWA KUCHA KISHA KUTUPWA

$
0
0
(Via Milladayo.com) Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Temeke Joseph Yona amepigwa na watu wasiojulikana na kisha kutupwa kwenye eneo la Ununio kwenye Magorofa ya Wasomali Kawe Dar es salaam. 

Shuhuda Abdul Ally ambae ni mkuu wa nyumba zilizokaribu na alikopigwa Mwenyekiti huyu, anasema walisikia kelele za huyu mtu kupigwa saa tisa usiku na walipomsogelea walimkuta peke yake.

‘Niliomba wasiniue, wamenipiga sana… wamenichukua saa tano nyumbani kwangu Kwa Aziz Ally, wao walikua na gari kama ya Polisi lakini inaonekana sio ya polisi wakasema tunakupeleka Central, tulikua wanne na hawakuhangaika na mtu wakanichukua mimi moja kwa moja.. tulipopanda kwenye gari wakachukua nguo yangu wakanifunga uso, wakaanza kunipiga wakisema nisiwajibu na hawakuniambia chochote’

Unaweza kusikiliza maelezo yake mengine akihojiwa kwa kubonyeza play hapa chini.




CHADEMA YAONGELEA SUALA LA M/KITI KUTEKWA, KUPIGWA NA KUTUPWA

DUH: AUAWA BAADA YA KUFUMANIWA NA MKE WA MTU

$
0
0

Mbeya

Watu wawili wamefariki dunia Mkoani Mbeya likiwemo la mkazi wa kijiji cha Igundu Kata ya Sangambi Tarafa ya Kiwanja Wilayani Chunya, Paul Mwashemele(57) kuwawa kwa kuchomwa kisu tumboni baada ya kufumaniwa na Mke wa mtu.

Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya Kamashna msaidizi mwandamizi wa polisi, Ahmed Msangi alisema kuwa tukio la kwanza limetokea Januari 6 mwaka huu majira ya saa 00.30 usiku katika kijiji cha Igundu.

Msangi alisema kuwa mauti hayo yalimkuta marehemu baada ya kukutwa na mke wa mtu katika nyumba ya mgoni wake wakifanya mapenzi.

Aidha Msangi alisema licha ya marehemu kuchomwa kisu na mgoni wake pia mke wa mgoni huyo alijeruhiwa vibaya na kwamba marehemu alichukuliwa na ndugu zake huku akiendelea kuvuja damu nyingi tumboni ambapo hawakuweza kumpeleka hospitali hivyo kuendelea kuguulia nyumbani kwa matibabu.


Hata hivyo Kamanda msangi alisema kuwa chanzo cha mauji hayo ni baada ya marehemu kukutwa nyumbani kwa Mgoni wake akiwa na Mke  wa Mlalamikaji  ,Nganga Nyapini(48)wakiwa wanafanya mapenzi.

Msangi alisema kuwa Mtuhumiwa Nyapini alikamatwa na polisi na kufikishwa mahakamani hata hivyo Kamanda Msangi ametoa kwa jamii kuachana na tamaa za kimwili kwani zina madhara makubwa na badala yake watafute mpenzi mmoja wa kuishi nae.

Wakati huo huo  Mkazi wa Kijiji cha Nsungwi Juu Wilaya ya Mbeya Mjini Stephen Philipo (28) ameuwawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kaka yake baada ya kutokea ugomvi wa kugombea mashamba.

Msangi alisema kuwa tukio hilo limetokea Januari 6 mwaka huu majira ya saa 6.00 mchana huko Nsungwi juu Kata ya Tembela.

Alisema kuwa marehemu alipigwa na kitu kizito kichwani wakati wakigombea mashamba na kaka yake aitwaye Lucas Philipo (25) baada ya kutokea ugomvi wa wanandugu uliosababishwa na mashamba.

Aidha Kamanda Msangi alisema kuwa mtuhumiwa amekamatwa  na atafikishwa mahakamani  kujibu shitaka hilo dhidi yake aidha Msangi ametoa wito jamii kutatua migogoro yao ya kifamilia kwa njia ya amani kwa kukaa meza moja ya mazungumzo ili kufikia muafaka.

Mwisho

MAGAZETI YA LEO 08/01/2014 NI ZITTO TENA

AJALI ZITATUMALIZA, HII MBAYA IMETOKEA HIVI KARIBUNI

$
0
0

Hivi karibuni imetokea ajali mbaya katika eneo la KINGOLUWIRA MADAFU kilometa 11 kutoka Morogoro kuelekea Dar es salaam majeruhi wawili, dereva mmoja wa lori amekufa hapo,



Juu lori lilobeba mbao baada ya kugongana na lori la mafuta, chini ni lori la mbao lilivyo haribika





 Juu ni jinsi ajali hiyo inavyoonekana, chini ni picha ya dereva aliyepoteza maisha



HII INATISHA: SAMAKI AINGIA TUMBONI MWA MTOTO WA MIAKA 12

$
0
0
Bunda


MAISHA ya mtoto mwenye umri wa miaka 12, mwanafunzi wa darasa la tano, shule ya msingi Bwanza (jina tunalo), wilaya ya Bunda mkoani Mara yako hatarini baada ya samaki aina ya sato kumrukia na kuingia tumboni mwake kwa kupitia sehemu yake ya siri.

Tukio hilo la aina yake,  lililowashangaza wengi kijijini hapo na maeneo mengine jirani, lilimtokea mtoto huyo Januari mosi, mwaka huu, saa 11 alfajiri alipokuwa amechuchumaa akiteka maji ndani ya ziwa Victoria kwa lengo la kumwagilia bustani yao ya nyanya na vitunguu waliyoilima kandokando ya ziwa hilo.

SOMA ZAIDI



Akiwa amechuchumaa akiteka maji, samaki huyo anayedaiwa kuwa mwenye ukubwa wa nchi nne, aliruka kutoka majini na kumuingia sehemu yake ya siri na kuzama kabisa tumboni mwa mtoto huyo ambaye, jitihada zake za kumvuta  ili asizame tumboni hazikufua dafu kwani aliambulia maumivu makali na kutokwa na damu nyingi sehemu yake ya siri kwa kuparazwa na  miiba ya mgongoni ya samaki huyo.

Baada ya tukio hilo, alirudi nyumbani kwa shida, akijivuta na kuugulia maumivu makali na kumweleza mama na ndugu zake mkasa uliomkuta ambao,  walimchunguza na kujaribu kuingiza mkono sehemu yake ya siri wakidhani watampata samaki huyo lakini hawakufanikiwa.

Kaka wa mtoto huyo, Lenatus Mtani (31) alisema, walipompeleka katika zahanati iliyopo kijijini hapo, hali yake ilizidi kuwa mbaya, akilalamika maumivu makali tumboni, ndipo familia akalihusisha tukio hilo na imani za kishirikina na kuamua kumtoa katika zahanati hiyo na kijijini hapo, na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji katika kijiji cha Amuyebe, wilayani Ukerewe.

"Mdogo wangu amechezewa kamchezo, katika hali ya kaawaida samaki hawezi kumrukia mtu sehemu yake ya siri na kuzama tumboni, huu ni ushirikina, tumempeleka kwa mtaalamu lakini bado hali yake inazidi kuwa mbaya" alisema Bw. Mtani

Alisema hata baba yao alifariki katika mazingira ya utatanishi mwaka 2003, kisha kaka zake watatu nao wakafariki kwa mfululizo mwaka 2004, 2005, 2006 wote hao vifo vyao vikigubikwa na utata akidai ni kutokana na ugomvi wa shamba uliopo kati ya familia yao na mkazi mmoja wa kijijini hapo.

Mwenyekiti wa kitongoji cha Alwego anakoishi mtoto huyo, Bi. Reticia Bituro alithibitisha kutokea kwa tukio hilo alilodai limemshutua na kumshangaza sana kwani, hajawahi kushuhudia tukio la namna hiyo tangu azaliwe na kuahidi serikali yake kulifanyia uchunguzi wa kina ili kubaini kama ni mapenzi ya Mungu au kuna mkono wa mtu.

Naye diwani wa eneo hilo la kata ya Napindi Bw. Elias Magoti ambaye yuko safari kuhudhuria kikao cha baraza la madiwani Bunda mjini alikili kupokea taarifa za tukio hilo kwa mshangao mkubwa na kudai atalifuatilia kwa karibu atakaporudi kijijini kwa kufanya uchunguzi kubaini kilichotokea kwani hajawahi kusikia tukio la namna hiyo katika umri wake wote.

Taarifa zilizopatikana kutoka ukerewe anakotibiwa mtoto huyo, zilisema hali yake inazidi kuwa mbaya, hawezi kuzungumza na anazidi kulalamika maumivu makali tumboni ikielezwa kwamba, samaki huyo bado yumo tumboni mwa mtoto huyo.

KUFURU: AMBAKA DADA YAKE, AUWAWA NA MWANAYE

$
0
0
Nachingwea

Mkazi wa mmoja wa kijiji cha Nang’ondo, Wilaya ya Nachingwea,  anashikiliwa na jeshi la polisi baada ya kumuua baba yake mzazi katika harakati ya kumwokoa shangazi yake aliye alikuwa anabakwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, George Mwakajinga, alisema tukio hilo limetokea siku ya mkesha wa mwaka mpya saa 4 usiku ambapo Bw. Jemsi Leslie (20) akiwa njiani kuelekea nyumbani alisikia kilio cha mtu kichakani kando ya njia akiomba msaada na aliposogea akakuta baba yake, Leslie Amuri (45) akimbaka huku amemkaba shingoni dada yake (Esha Amuri (68)



Mwakanjinga alisema, Jemsi alijaribu kumtoa mikono baba yake ili asiendelee kumkaba shagazi yake lakini hakufanikiwa,  akihofia maisha ya shangazi yake, alianza kumpiga baba yake  mikononi ili amuachie lakini kutokana na giza akampiga kichwani na ndipo alipofariki kwenye eneo la tukio.

“Mtuhumiwa alikuwa anatoka kwenye sherehe za mwaka mpya usiku na ndipo aliposikia sauti ya mtu akigumia kichakani kando ya njia aliyokuwa anapitia na ndipo kwa lengo la kumwokoa shangazi yake alijaribu kumgandua baba yake lakini alishindwa hivyo akalazimika kutumia magongo ambayo alimpiga kichwani na kumsababishia maumivu makali na kumuua baba yake papo hapo”alisema Mwakanjinga.

Kamanda huyo alisema kuwa jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa Jemsi Leslie na kuwa linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

WAKOLA AKAMATIWA SINGIDA NA RUNDO LA HELA FEKI

$
0
0
Singida.

Jeshi la Polisi mkoani Singida linamshikilia mtu moja Toyi Wagela maarufu kama Wakola kwa tuhuma za kupatikana na noti bandia 409 zenye thamani ya zaidi ya sh. 3/=.

Kamanda Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Geofrey Kamwela amebainisha kuwa mtu huyo ambaye ni mkazi wa mkoani Kigoma, alikamatwa na noti hizo akiwa katika Hotel ya Afro Petrol eneo la Chipondoda mjini Manyoni.

Akizungumza na wandishi wa Habari ofisini kwake jana Kamanda huyo alifafanua kuwa noti hizo ni pamoja na 200 za sh. 10,000/= na 209 za sh. 500/= ambazo zilipatikana baada ya kupekuliwa kutokana na mtu huyo kutoa noti moja y ash. 5,000/= kwa mhudumu huyo wakati alipokuwa anataka kulipia huduma ya chakula alichopata.

“Mtuhumiwa Tayi Wagela ambaye alikuwa mteja aliyekwenda katika hotel hiyo, ndipo aliposhtukiwa na mhudumu huyo na taarifa kupelekwa Kituo cha Polisi cha mjini Manyoni, ambapo askari wa jeshi hilo walikwenda huko na kumnasa akiwa na noti hizo". Alisema Kamanda Kamwela.

Jeshi hilo linaendelea kumuhoji mtu huyo ili kujua undani wa jambo hilo ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa kina katika kubaini mahali zilipotengenezewa, watu wengine walioshiriki katika uhalifu huo wa utengeneza wa fedha bandia, na mtandao mzima unaotumika katika shughuli hiyo isiyo halali.

Kamanda alieleza kuwa mtu huyo atafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika na kuwatahadharisha wananchi kuwa makini na noti za bandia ambazo zinawezi kuwa katika mzunguko wa biashara mbalimbali mkoani Singida pamoja na kutoa taarifa ili hatua za kudhibiti ziweze kuchukuliwa na serikali kwa mujibu wa sheria.

MAGAZETI YA LEO 09/01/2014: BADO NI CHADEMA NA ZITTO

NJEMBA YAKAMATWA NA BUNDUKI NA NDEGE

$
0
0
Singida

Afisa Wanyamapori wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Agustino Lorry (43) amekamatwa na Jeshi la Polisi baada ya kupatikana na Bunduki mbili na ndege hai 12 aina ya Flamingo vyote vikiwa nyumbani kwake.

Bunduki hizo mbili moja aina ya Riffle V. 15152 na Shotgun No. 729 na Nyaraka hizo za serikali vilipatikana nyumbani kwake katika maeneo ya Sabasaba Kata ya Mandewa mjini Singida.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi Mwandamizi Geofrey Kamwela , siku ya tukio Jeshi hilo lilipata taarifa za siri kutoka kwa raia mwema kuhusu mtuhumiwa kujihusisha na vitendo vya usafirishaji wa ndege.

Akizungumza na waandishi wa Habari juzi Kamanda Kamwela alisema kuwa taarifa hizo pia zilibainisha kuwa Agustino Lorry alikuwa na ndege wengine nyumbani kwake wa aina ya Flamingo.

“Askari Polisi walimpekuwa nyumbani kwake, na kukutwa akiwa na silaha hizo mbili pamoja na Risasi tatu mbili za shortgun na moja ya Riftle, vyote vikiwa vimefichwa chumbani kwake chini ya godoro la litanda chake” alisema Kamwela.

Alieleza kuwa hata hivyo upekuzi huo ulipokuwa unaendelea katika mazingira ya nyumba ya mtuhumiwa ndege hao walikutwa wamefichwa katika chumba kimoja cha uani.

“Uchunguzi wa awali ulionesha kuwa ndege hao waliletwa kwa Lorry na mtu mwingine anayedaiwa amekuwa akishirikiana naye na ndiye mtegaji na ukamataji wa Nyara hizo za Serikali.” Alisema Kamanda huyo.

Aliongeza kuwa Jeshi hilo lilishirikiana na Idara ya wanyama pori Mkoani hapa kufuatilia tukio hilo na kufanikiwa kumkamata mtu mwingine Hamza Ally(40) Mkazi wa Mtaa wa Majengo mjini Singida.

“Alikutwa katika Ziwa Singidani lililopo mjini hapa akiwa katika harakati za kutega na kukamata ndege wengine kwa lengo la kusafirishwa”.alisema Kamanda huyo.

Alieleza kuwa uchunguzi zaidi unaendelea ikiwa ni pamoja na kujua wamiliki halali wa Bunduki hizo, na jinsi zilivyofika kwa mtuhumiwa Agustino Lorry ambaye ni mfanyakazi wa Serikali.

Jeshi la Polisi Mkoani Singida limetoa tahadhari kuwa litashirikiana na Idara hiyo pamoja na wananchi ili kudhibiti vitendo vya ujangiri ambavyo vimekuwa vikitishia kumalizika kwa wanayama pori na ndege hapa Tanzania
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live