Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

WEMA SEPETU AMLIZA MAMA KANUMBA

$
0
0

BAADA ya mama Kanumba Bi. Flora Mtegoa kutunzwa kitita cha sh. laki tano na msanii wa filamu nchini Wema Sepetu, kitendo hicho kilimtoa machozi mama huyo na kudai kuwa kila anapokutana na baadhi ya wasanii anajikuta kumkumbuka mtoto wake.

Kitendo hiko kilitokea mwishoni mwa wiki katika uzinduzi wa Filamu ya Elizabeth Michael iliyopewa jina la Foolish Age katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo mama Kanumba alijikuta akitokwa na machozi mfululizo mara baada ya kukutana na msanii huyo.

Mama huyo ambaye alijikuta akivutiwa na uchezaji wa Wema ukumbini hapo wakati bendi ya Machozi ikitumbuiza aliamua kumfuata na kutaka kumtunza kutokana na uchezaji wake.

Wema alishindwa kupokea hela hiyo aliyotunzwa na mama huyo na badala yake alianza kumtunza yeye hela hali ambayo ilimtoa machozi.

Wema alimpigia magoti mama huyo kwa ishara ya kuonyesha kuwa anamuheshimu, na kumpenda huku akizingatia alishawahi kuwa mama mkwe wake.

Akizungumza mara baada ya kutunza kitita cha fedha hizo mama huyo aliweka wazi kuwa kila anapokutana na wasanii ambao walikuwa wanaukalibi na mtoto wake huyo anajikuta anamkumbuka mwanaye.


MSHINDI MISS REDD'S PHOTOGENTICS 2013 APATIKANA

$
0
0

 Mshindi wa Miss Redd's Photogentics (katikati) akiwa amepozi na washiriki waliofanikiwa kuingia tano bora ya miss Photogenitics. Kinyanganyiro hicho kilifanyika juzi katika hoteli ya Giraff Dar es Salaam.

BREAKING NEWS: MICROSOFT YAINUNUA NOKIA

$
0
0
Kampuni ya Microsoft imeingia makubaliano ya kununua kampuni ya simu za mkononi ya Nokia kwa kiasi cha shilingi trilioni 11.5 (uro bilioni 5.4 au dola bilioni 7.2).

Nokia pia itatoa leseni zake za hati miliki pamoja na ramani za huduma zake kwa kampuni ya Bill Gates ya Microsoft.
Kwa mujibu wa mitandao mbali mbali duniani ikiwa ni pamoja na BBC, Sky News, CNN, USA Today, Makampuni hayo kwa pamoja yalinukuliwa mbele ya waandishi wa habari kuwa makubaliano hayo yatakamilika mwanzo ni mwa mwaka 2014, wakati ambao kiasi cha wafanyakazi 32,000 wa Nokia watahamishiwa kwenye kampuni ya Microsoft. Wakati Nokia ikikumbwa na ushindani mkali kutoka kwa washindani wake Samsung na Apple, Microsoft imekuwa ikikosolewa kwa kutokuwa na kasi ya kutosha kwenye soko la simu za mikononi.

“Ni hatua kubwa kwa siku zijazo – ambapo ni mafanikio makubwa kwa wafanyakazi, wanahisa na wateja wa makampuni yote mawili” alisema Steve Ballmer, Mtendaji Mkuu wa Microsoft

Makubaliano hayo yanasubiri baraka za wanahisa na wadhibiti.

MOHAMMED ENTERPRISES YASHINDA KESI DHIDI YA BAKHRESA

$
0
0
Kundi la makampuni ya MeTL imeshinda kesi dhidi ya matumizi ya haki miliki zake dhidi ya makampuni ya Bakhressa. Bakresa sasa itatakiwa kuilipa METL Group kiasi cha shilingi milioni 732 pamoja na riba.

taarifa hiyo iliwekwa hatharani katika mtandao wa Twitter na mmiliki na Mkurugenzi wa makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL), Mohammed Dewji MO (pichani chini) muda si mrefu kama msisitizo wa Twitt nyingine iliyowekwa na kampnuni hiyo jana.


MWANAMKE AMEZA SIMU

$
0
0
WIVU wa kimapenzi umemuweka matatani msichana anayeishi nchini Brazil, Adriana Andrade baada ya kuamua kumeza simu yake ya mkononi ili kumzuia mpenzi wake asisome 'message' katika simu yake.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19 amejikuta akilazimika kuumeza simu hiyo baada ya kugundua alikuwa na message za ajabu ambazo zingezua utata pindi mpenzi wake angezisoma.


Habari zilizoripotiwa na mtandao wa Hispania Yipeta zilieleza kuwa msichana huyo aliamua kumeza simu yake ya mkononi baada ya mpenzi wake kutaka kusoma message zilizomo katika simu hiyo.

Mtandao huo uliendelea kuripoti kuwa baada ya tukio hilo msichana huyo alilazimika kufanyiwa upasuaji ili kutolewa simu hiyo tumboni mwake.

MWANAUME ADHANIWA KUAMBUKIZA VVU

$
0
0
MWANAMUME Richard Thomas ambaye amefungwa gerezani kwa kumbaka mwanamke anasubiri matokeo ya vipimo vyake kama ameambikizwa virusi vya Ukimwi kutoka kwa mwanamke huyo.

Bw. Thomas alihukumiwa kifungo cha miaka mitano na miezi minne gerezani baada ya kukiri kumbaka mwanamke huyo nyumbani kwake mjini Leigh, Greater Manchester.

Mbakaji huyo alifahamu kuwa mwanamke huyo ni mgonjwa lakini hakuweza kujua kama mhanga wake ana VVU na alizimia wakati polisi walipomjulisha, Mahakama ya Liverpool Crown ilizikiliza.

Kwa mujibu wa BBC, Bw. Thomas, 27, kutoka mtaa wa Sandringham Drive, Leigh, alimbaka mwanamke huyo wakati alipokuwa amekunywa kidonge cha usingizi.


KOSA LAKE

Alisema alikuwa amekunywa pombe kupita kiasi na kutumia dawa za kulevya, na alishindwa kukumbuka shambulizi lake, lakini alimuamini mwanamke huyo, Mahakama hiyo ilisikiliza.

Bw. Thomas aliingia ndani ya nyumba ya mwanamke huyo usiku wa manane bila ya kualikwa na muathirika huyo, ambaye alikuwa ameuchapa usingizi na aliposhituka alimuona Bw. Thomas akimbaka.

Harry Pepper, akiendesha mashitaka, alisema: "Mwanamke huyo alishikwa na mshangao kuwa na hakukuwepo na matamshi baina yao. Bw. Thomas alichukua nguo zake na kuondoka."

Kwa mujibu wa BBC, hakimu Mark Brown aliuelezea ualkifu huo kama wa "kutisha".

Mwanasheria wa Bw. Thomas, Virginia Hayton, alisema: "Ni kosa lake mwenyewe huyo mwanamume, kama asingefanya kosa hili asingejiweka katika sehemu hii.".

FEDHA YAMJERUHI MWANAMKE

$
0
0
Mwanamke wa kimarekani amelazwa hospitali baada ya kuumia kooni na tumboni wakati akijaribu kutoa kiasi kikubwa cha fedha alizozimeza kwa kutumia ufagio wa kusafisha choo.

Christie Black 43 mkazi wa Bulls Gap, katika jimbo la Tennessee, alipata majeraha hayo baada ya kushindwa kutoa dola za Marekani 5000 alizomuibia mpenzi wake ambaye ni Bobby Gulley.

Kwa mujibu wa taalifa ya polisi wa jimbo hilo, Christie, alichukua maamuzi hayo ili kukwepa kugawana fedha hizo na mpenzi wake huyo baada ya kutengana.

Taarifa hiyo iliweka wazi kuwa mara baada ya kujiingiza fagio hilo tumboni kupitia mdomoni, mwanamke huyo alisikia maumivu makali kutokana na michubuko iliyomfanya atokwe na damu mfululizo.

Hali ya mwanamke huyo inaendelea vizuri baada ya kuwahishwa hospitali alikopewa matibabu kwa haraka.

Taarifa hiyo ya polisi iliweka bayana kuwa walipata taarifa ya tukio hilo kutokana na mpenzi wake huyo aliyekwenda kushitaki kuibiwa fedha hizo na kwamba baada ya upelelezi ndipo walipombaini mwanamke huyo akiwa taabani.

Alipohojiwa mwanamke huyo juu ya uamuzi wa kumeza kiasi kikubwa cha fedha alisema alikuwa anataka zikamsaidia kujiendeleza kimaisha baada ya kupata taalifa kuwa mpenzi wake anapanga kumuacha.

MAHAKAMA YASITISHA KUFUKUZWA KWA WANAFUNZI WAJAWAZITO

$
0
0

Hukumu ya hivi karibuni ya mahakama ya kikatiba imethibitisha kwamba shule haziwezi kuwafukuza wanafunzi kwa kupata uja uzito.Lakini Afrika Kusini bado inang'ang'ana kukabliana na suala hilo linalowaathiri wasichana 180,000 kila mwaka.

Daktari Jay-Anne Devjee ambaye ni mkuu wa afya ya akina mama katika hospitali ya King Dinuzulu anasema kwa mara nyingi hulazimika kuwazalisha wasichana kwa njia ya upasuaji, jambo linaloongeza hatari ya kuvuja damu na kuhatarisha maisha ya wazazi hao.

Phumla Tshabalala, mwenye umri wa miaka 16, anamshikilia mwanawe mchanga aliye na umri wa siku moja.Hii ni mara yake ya kwanza kujifungua na anasema ana wasiwasi kuhusu uwezekano wa kumlea mwanawe peke yake.Msichana mwenye umri mdogo zaidi hapa ana umri wa miaka 14 na anaonekana kuzidiwa na uchungu wa uzazi kiasi cha hata kushindwa kuongea.

Anaeleza hajamuona mpenzi wake kwa muda mrefu na licha ya kumuarifu kwamba amejifungua, hakuna mtu kutoka familia ya mpenzi wake aliyekuja kumjulia hali. Anatoka katika familia maskini, Babake ndiye anayeilisha familia. Yeye ni binti wa mwisho kati ya mabinti watatu na wa kwanza aliyejifungua mtoto, jambo ambalo familia yake bado haijalipokea vyema.

Inakisiwa kuwa kila mwaka wasichana zaidi ya laki moja na themanini nchini Afrika Kusini hushika ujauzito. 180 kati ya wengine 1000, hupata kuwa wajawazito. 36% ya wasichana wenye mimba hufariki kila mwaka kulingana na takwimu za nchi hiyo wakati wanapojifungua.

Mifuko yao ya uzazi huwa bado haijakuwa vyema kiasi cha kubeba mimba na wengi huwa na wakati mgumu sana wanapojifungua , kulingana na daktari Jay-Anne Devjee.

Phumla anapanga kurudi shuleni kwa wakati muafaka ili aweze kufanya mtihani wa mwisho wa mwaka , lakini ana wasiwasi kuhusu vipi atakavyoweza kutimiza majukumu yote mawili ya kuwa mwanafunzi na mzazi pia.

BUNGE LAGEUKA UWANJA WA NGUMI LEO

$
0
0
UKUMBI wa Bunge leo uligeuka kuwa ulingo wa ngumi baada ya wabunge wa kambi ya upinzani kutunishiana  misuri na askari wa bunge hilo ambapo  Kiongozi mkuu wa kambi ya upinzani Freeman Mbowe alipoamliwa kutoka nje na Naibu Spika Job Ndugai.

Hatua hiyo ilitokana  baada ya wabunge hao kupiga kura za kukubali au kukataa kuhusu kupitishwa kwa kujadili Mswaada wa Katiba uliopelekwa Bungeni hapo na Serikali ili kuweza kujadiliwa na bunge hilo.

Wabunge hao wa kambi ya upinzani wakiongozwa na Freeman Mbowe walipinga matokeo hayo na kuamua kusimama na wakati huo huo Spika Ndugai aliwataka kukaa chini ili kuendelea na kuchangia hoja za msingi za kujadili mswaada huo.

Ndugai aliwataka wabunge hao kukubaliana na matokeo yaliyotokea na kwa pamoja waweze kujadili mswaada huo ambao ni faida kwa taifa lakini mbali na ombi hilo kambi ya upinzani walikaidi ndipo Spika alitoa dakika tano kwa za kiongozi huyo kutoka ili bunge liendelee,ambapo hata hivyo kiongozi huyo alikaidi amri hiyo.


Baada ya mabishano hayo ndipo Spika alipotumia kiti chake na kuwataka askari wamtoe kwa nguvu nje ya ukumbi wa bunge ,amri ambayo ilizua taflani na hekeheka kupelekea wabunge wa kambi ya wapinzani kuungana na kuwatunishia misuri askari hao wakimkingia kiongozi huyo kutolewa nje.

Tukio hilo lililochukua dakika zaidi ya 30 lilipelekea Bw. Job Ndugai kuwatolea macho askari hao akiwaamuru kutumia mabavu ili kuweza kumtoa nje ya ukumbi Bw. Mbowe.

Sakata hilo lilifanikiwa baada ya askari hao kutii amri ya Naibu Spika huo kwa kutumia mabavu kumtoa nje kiongozi wa kambi ya upinzani ambapo aliungwa mkono na wabunge  kutoka nje ya ukumbi na kususia kikao hicho.

Katika tukio hilo Mwenyekiti wa vyama vyenye wabunge wengi bungeni na Mbunge wa Jimbo la Vunjo Mkoani Kilimanjari Agustino Mrema alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wabunge wezake si cha kungwa na na kinaleta fedheha kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Alisema yeye kutokutoka kwake nje haimaanishi kuwa ni kibaraka wa CCM na  si ndicho alichotumwa kufanya na wananchi wake,hivyo haungi mkono hata kidogo na haeleweke hivyo kuhusu msimamo wake.

"Hatoki mtu hapa nitakaa ndani ya bunge mpaka kieleweke na mnielewe kwamba mimi ndiye kiongozi wao vyama vyote tisa,hivyo nastahili kuheshimiwa na sikubaki humu ndani kwa sababu mimi ni kibaraka wa CCM bali  kinachopiganiwa ni maslahi ya taifa na ndicho nilichotumwa na wananchi wangu sikutumwa nije kutoka nje au kususia bunge."alisema Mrema.

Naye, Mbunge wa Same Mashariki na Bi Anne Kilango Malecella aliitaka Serikali kusimama imara na isiogope vitisho vinavyotolewa na wasioitakiwa mema nchi katika kupigania maslahi ya taifa.

Alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wapinzani bungeni hakina nia njema katika kupata katiba mpya na wajumbe 156 waliopiga kura wanavigenzo vya kuweza kuchangia Mswaada huo kujadiliwa.

Vurugu za bunge hilo ziliaza toka awali katika kipindi cha muongozo wa Spika ambapo vijembe,kashifa kwa wabunge kuzungumza bila kufuata utaratibu ilimradhimu Naibu Spika Job Ndugai kusimama mara kwa mara kujaribu kurejesha utulivu katika matukio yaliyotawala Ukumbini humo.

Mara baada ya kutolewa mwongozo ulioombwa na wabunge juzi wakidai Muswada wa Mabadiliko ya rasimu ya katiba umeingizwa vipengele kinyemele, na Zanzibar kutoshirikishwa kikamilifu, wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni na wale wa CCM walikuwa wakituhumiana kusema uongo kuhusiana na hatua hiyo ya uandaaji wa mchakato wa Rasimu wa Katiba mpya.

Hali hiyo ilipekea wabunge hao kuchambua vipengelee mbali mbali vya sheria vya kutafasili kanuni za bunge kwa wabunge ambao wanasema uongo bungeni ambapo msemaji wa Kambi ya upinzani bungeni Tundu Lissu alisema Kanuni ya 61 A inawataka wabunge kutotoa taarifa zisizo na ukweli bungeni huku kipengele 63 (3)kinamtaka mbunge mwingine anayeweza kusimama nakusema mbunge aliyesema kabla yake alisema uongo hivyo Tundu Lissu alisema mwenyekiti wa Katiba juzi alisema uongo kuwa wazanzibar wametoa maoni katika kamati ya katiba.

Lissu alisema yeye akiwa ni mmoja wa wanakamati waliambiwa kamati haiwezi kwenda zanzibar kwa sababu za kiusalama hivyo mwenyekiti huo amelidanganya bunge.

Muongozo huo ulipelekea Waziri Nchi Ofisi ya Rais Uratibu na Sera wa shughuli za Bunge William Lukuvi kutaka kiti cha Spika kichukue hatu zidi ya wanaotumia bunge ambalo ni chombo cha sheria kudanganya na fitirisha pamoja na kutumia jina la rais kwa dhihaka.

Alisema kuwa msemaji huyo wa kambi ya upinzani bungeni Tundu Lissu ameshawishi wabunge na wananchi kuamini uongo kuwa uteuzi wa rais katika uundwaji wa kamati ya maoni ya katiba amelenga watu anao wafahamu kwa maslahi yake na si kwa maslahi ya watanzania.

Lukuvi alifafanua kuwa uteuzi wa rais katika uundwaji wa tume hiyo umezingatia matakwa ya sheria kwa kushirikisha mapendekezo ya kila Sekta ikiwemo vyama vya hiari,walemavu,taasisi za dini,vyama vya maendeleo ya Jamii na vyama vya Siasa kikiwemo Chadema ambapo kati ya majina yaliyopendekezwa ni pamoja Tundu Lissu hakuchaguliwa kwa sababu hakuwa na sifa ya kumzidi Professa Baregu kati ya majina yaliyopendekwaza na Chama hicho.

Akiomba ufafanuzi muwasilisha wa mjadala huo bungeni Ally Hamisi Seif aliomba hoja ya kuondolewa kwa msaada huo wa sheria kwakua hakuna ushirikishwaji wa kutosha kwa wazanzibar katika mchakato wa kuandaa rasmu ya Katiba mpya kutokana na kamati kutokupokea maoni ya wananchi wa zanzibar.

Akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Freem Mbowe lililohoji kuwa msaada huo una maeneo makubwa yatakayoleta ufa nchini , hivyo yakafanyiwe malekebisho kabla ya mswaada wake kujadiliwa bungeni.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mizengo Pinda akijibu swali hilo alisema  kuwa hakuna haja ya mswaada huo kuondolewa kwani kabla ya  kuletwa bungeni kulikuwa kunafursa kwenye kamati mbalimbali,na tofauti zilizopo zinazungumzika ili uweze kujadiliwa.

Naye, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi James Mbatia alishauri Serikali umuhimu wa majadiliano hayo kufanyika kwa uwazi kabla ya kisheria ili kusaidia maana halisi ya kuunda dola kwani kura ya maoni ya zanzibar inaeleza wazi mgogoro wa kikatiba uliopo ambapo ulipelekea hata mamlaka ya kugawa ardhi aliyonayo rais wa Tanzania hufanywa na rais wa zanzibar katika ardhi ya zanzibar.

Akijibu swali hilo  Pinda alisema hana tatizo na ushauri wa Mbatia ila ungekuwa na nafasi endapo katiba mpya isingekuwepo kwani ndiyo itakayofuta tofauti zilizopo.

Hata hivyo Sakata hilo liliaza Juzi jioni  wakati wabunge wa Chadema na Cuf kuwa kitu kimoja na kuamua kutoka nje baada ya Tundu Lissu kuwsiliha maoni ya kambi hiyo huku akieleza kuwa wananchi wazanzibar hawakushirikishwa kwenye maoni ya rasmi ya katiba mpya.

AUNT EZEKIEL KUKATWA MKONO

$
0
0
MSANII wa filamu za bongo , Grayson Gwantwa Aunt Ezekiel yupo hatarini kukatwa mkono kutokana na
jeraha la kupigwa chupa lililotokea Agosti 26 mwaka huu Dar es SalaamTukio la Aunt kupigwa chupa na mwanamke aliyetajwa kwa jina moja la Yvonne nje ya Club Bilicanas, Posta jijini Dar, lilitokea  wakati staa huyo alipokwenda kujiachia na mshosti zake.


Baada ya kupigwa chupa siku hiyo, Aunt alikimbizwa katika Hospitali ya Aga Khan lakini bahati mbaya alikosa daktari wa kumtibu hivyo akalazimika kwenda kutibiwa katika Hospitali ya Dk. Mvungi, Kinondoni ambapo alishonwa nyuzi sita pamoja na dawa za kukausha kidonda.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Aunt ni muoga wa dawa na wakati kidonda kikiwa bado hakijapona vizuri aliacha kumeza dawa alizopewa.

Chanzo hicho kilisema tatizo la staa huyo kukatisha dozi lilisababisha kidonda kishindwe kupona na badala yake kikaanza kutengeneza usaha na taratibu mkono ukaanza kuoza.“Mkono ulifikia hatua ukaanza kuoza kwani licha ya kushonwa lakini kilibadilika rangi ndipo alirudi hospitali." kilieleza chanzo hicho.

Imeelezwa kuwa mapema wiki hii, Aunt alirudi tena katika Hospitali ya Dk. Mvungi na kusafishwa upya kidonda baada ya madaktari kugundua tatizo lilizidi kuongezeka.

Kwa mujibu wa nesi wa hospitali hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, hali ya Aunt ilimshtua daktari, akamwambia aombe Mungu kwani kidonda kilichimbika sana na tatizo kama hilo huweza kusababisha mtu kukatwa mkono.

“Iligundulika mkono ulikuwa unaoza, daktari alimwambia amuombe Mungu kwani hatua iliyokuwa imefikia ni mbaya hivyo asipokuwa makini tatizo hilo litamfanya akatwe mkono,” alisema nesi huyo.Aunt alipigwa chupa akigombania penzi la mwanaume na Yvone .

JAYDEE KUFANYA COLLAB NA KHADIJA KOPA?

UTAUMIZA MOYO VIDEO - Tr@st KForce

AZONTO LIVE IN DAR, FUSE APAGAWISHA MASHABIKI WAKE

$
0
0








 Msanii Snura akicheza sambamba na wacheza shoo wake wakati wa ufunguzi wa shoo ya Azointo live in Dar jana katika viwanja vya Ustawi wa Jamii
 Msanii H.Baba akitumbuiza jukwaani hapo
 Kundi la Tip Top connection wakitumbuiza jukwaani hapo akiwa Madee pamoja na Tunda Man


 MSANII wa Ghana mwenye maskani nchini Uingereza Fuse ODG, juzi alifanikiwa kuwateka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwa kufanya shoo ya kihistoria, huku akipandisha mzuka kwa mashabiki waliohudhuria shoo hiyo iliyofanyika katika viwanja vya Ustawi wa Jamii.

Msanii huyo anayetamba na kibao cha Azonto pamoja na Antenna aliweza kuwateka mashabiki wake baada ya kupanda jukwaani hapo na kucheza pamoja na mashabiki miondoko hiyo.

Kwa kumuunga mkono msanii huyo baadhi ya mashabiki waliohudhuria shoo hiyo walipanda jukwaani hapo na kuanza kucheza naye pamoja na kumfundisha msanii huyo miondoko ya Kiduku ambayo umezoeleka kuchezwa hapa bongo.

Msanii huyo alionekana kumudu kucheza kiduku ambapo aliungana na baadhi ya mashabiki wake waliopanda jukwaani hapo.

Shoo hiyo imeonyesha kufanikiwa kwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi ambapo baadhi ya wasanii kutoka nyumbani walitumbuiza huku msanii Hamis Ramadhan 'H.Baba' alionyesha mashabiki wake kuwa yeye ndiye mkali wa miondoko ya Bongo Bolingo Fleva.

Shoo hiyo pia iliweza kunogeshwa na baadhi ya wasanii akiwemo Banana Zoro, kundi la Tip Top Conection akiongozwa na Madee pamoja na Tundaman ambapo walipanda jukwaani hapo pamoja na msanii wa hip hop Chid Benz.

A

MWANAUME KUFUNGA NDOA NA MBUZI

$
0
0
Mwanaume mmoja nchini Brazil anatarajia kufunga ndoa na mbuzi wake ingawa aliahidi kutoikamilisha ndoa hiyo kwa ngono. Bw. Aparecido Castaldo, (74) anatarajia kuoana na kipenzi wake mbuzi aitwaye Camelita ifikapo Oktoba 13 mwaka huu, baada ya kuamua kutaka kumaliza siku zake za kuishi akiwa na mbuzi wake.

Kwa mujibu wa gazeti la Red Pepper la nchini Uganda, habari hiyo ambayo watu wengi wameiita ya mzaha inaripotiwa kuamsha hasira katika mji wa Jundiai jimbo la Sao Paulo anakoishi Castaldo.

Mwanaume huyo amekuwa katika mapenzi na mbuzi huyo kwa miaka miwili sasa na amesema mbuzi huyo anafaida nyingi zinazotokana na mwenza wake binadamu.

WANAWAKE ZAIDI YA 26 WAPOTEZA MAISHA KILA SIKU

$
0
0
TWAKIMU za hivi karibuni zinaonesha kuwa Tanzania ni kati ya nchi zinazoongoza kwa idadi kubwa ya vifo votokanavyo na uzazi huku wanawake 26 hupoteza maisha kila siku ambapo vifo hivyo asilimia 19 vinachangiwa na utoaji wa mimba usio salama.

Takwimu hizo ziimetolewa na shirika lisilo la kiserikali Marie Stopes (MST) ambapo iliweka wazi kuwa asilimia 16 tu ya vijana ndio walio katika umri wa uzazi wanatumia njia za kisasa za uzazi wa mpango


Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa shirika hilo Bw. Johnbosco Baso alisema takwimu zinaonesha vijana 8000 waliacha shule kwa sababu ya mimba za utotoni kwa mwaka 2010,hali inayopelekea kijana kupoteza dira ya maendeleo.

Alisema kuwa inatakiwa kuwaelimisha vijana  kuwa na matumizi sahihi ya uzazi wa mpango ili kuepuka mimba katika umri mdogo ambapo itawasaidia kutimiza malengo na ndoto zao za baadae.

Baso alisema mimba za utotoni zimechangia kwa kiasi kikubwa utoaji wa mimba usio salama unaopelekea vijana wengi kupoteza maisha .

UN YAISHANGAA TANZANIA KUWAFUKUZA WAKIMBIZI

$
0
0
Umoja wa Mataifa umesema kuwa takriban wakimbizi elfu 25 kutoka Burundi wameondoshwa Tanzania kwa nguvu katika mwezi mmoja uliopita.

Afisa wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi UNHCR amesema malori yanayowasafirisha warundi yamekuwa yakivuka mpaka kila siku , huku wahamiaji haramu wengi wakikosa mahitaji muhimu kama vile maji na chakula

Katika wiki za hivi karibuni, Tanzania imekuwa ikiwarejesha makwao kwa nguvu wale walioelezwa wahamiaji haramu kutoka Burundi, Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.



Kwa miaka mingi Tanzania iliwahifadhi mamilioni ya wakimbizi waliokuwa wakiyakimbia mapigano katika nchi jirani . Tanzania kwa upande wake inasema watu hao ni wahamiaji haramu wala sio wakimbizi.

Takriban watu milioni moja walitoroka kutoka Burundi na kuingia Tanzania wakati wa mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe wakati vita vilipozuka mwaka 1993. Wengi walirejea kwa hiari wakati amani ilipopatikana mwaka 2006.

Nchi hiyo imekuwa makao kwa mamilioni ya wakimbizi katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi iliyopita kutokana na migogoro katika eneo la maziwa makuu.

Maafisa wa Tanzania sasa wameanza kutekeleza amri ya kuwaondoa kwa nguvu wale wanaodaiwa kuwa wahamiaji haramu kutoka Burundi, Rwanda, na Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Shughuli hii imetokea wakati mmoja na mgogoro wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda ambayo imekuwa ikikanusha madai ya kuchochea vurugu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mgogoro ndani ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo nao unaendelea kuchochea idadi ya wakimbizi wanaotoroka vita na kuingia katika nchi jirani.

SUALA LA MAPADRI KUOA LAJADILIWA VARTICAN

$
0
0
Suala la mapadri wa Kanisa Katoliki kuoa au la, limeibuka upya na tayari limeanza kuzua mijadala mikali duniani. Mjadala wa sasa umeibuliwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Vatican, Askofu Mkuu Pietro Parolin ambaye aliteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo aliposema useja, yaani maisha ya utumishi ndani ya kanisa bila ndoa siyo imani, bali utamaduni na mazoea.

Akizungumzia kauli hiyo, Msemaji wa Vatican, Federico Lombardi alisema kauli ya Askofu Parolin haipingani na mafundisho ya kanisa.

Askofu Mkuu Parolin ambaye aliteuliwa karibuni na Papa Francis kushika wadhifa huo kutoka kwa Kardinali Tarcisio Bertone amenukuliwa na Gazeti la El Universal la Venezuela, Amerika ya Kati akieleza kuwa suala hilo linaweza kujadiliwa.


Hata hivyo, msimamo huo unaweza kupingwa na waumini wengi wenye misimamo mikali ndani ya kanisa hilo ambao bado wanaamini kuwa kuishi useja ndiyo mfumo na utamaduni unaofaa ndani ya kanisa hilo.

Kwa upande wake, Papa Francis mwaka jana hata kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, alizungumzia suala hilo kwa maneno mafupi kuwa angependa kuona mfumo huo ukibaki kama ulivyo.

Msimamo huo wa Askofu Mkuu Parolin unamaanisha kuwa kuna haja ya kanisa hilo kufanya mabadiliko makubwa kwenye kanuni ngumu ya useja kwa mapadri wake.

“Useja si suala la kitaasisi, lakini linaonekana kuwa kweli, linaaminika. Ni suala gumu ambalo linaweza kujadiliwa kwani si imani ya kanisa (dogma), halihusu imani ya kanisa,” alisema Askofu Mkuu Parolin.

Askofu huyo alisema kwa kuwa siyo suala la kiimani, useja katika kanisa hilo limezama zaidi kwenye utamaduni.

'CHANGUDOA' , OMBAOMBA WAKAMATWA

$
0
0
Ombaomba zaidi ya 200 na wasichana wanaofanya biashara ya ngono maarufu kama ‘dada poa’  usiku wa kuamkia jana walikamatwa kwenye operesheni maalumu ya kuwaondoa katika maeneo mbalimbali ya jiji,iliyofanywa kwa ushirikiano wa Polisi na askari wa jiji.

Ombaomba na kinadada hao walikamatwa kwenye Manispaa ya Kinondoni na Ilala ambapo baadaye walihifadhiwa kwenye Viwanja vya Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa(Sabasaba) kabla ya kufikishwa kwenye Mahakama ya Jiji kwa makosa ya uzurulaji.

Ombaomba hao baada ya kufikishwa mahakamani hapo  walitakiwa kurudi katika makazi yao kuanzia leo  ili wasichukuliwe hatua za kisheria.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick alipohojiwa alisema,operesheni hiyo,imebaini zaidi ya asilimia 70 wanatoka mikoani .

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova alithibitisha kukamatwa kwa ombaomba hao na kueleza kuwa zoezi hilo ni endelevu.

YANGA YAWASILISHA RUFAA YAKE

$
0
0
Klabu ya Yanga tayari imewasilisha rufaa yake kwa shirikisho la soka nchini TFF juu ya kucheza mchezo wake katika hali isiyokuwa na usalama na kuomba mchezo huo urudiwe katika uwanja wa ugenini kwa timu zote.

Mchezo hu ambao ulitawaliwa na vurugu kutoka kwa washabiki wa Mbeya City ulichezeshwa na mwamuzi Andrew Shamba kutoka mkoani Pwani ambaye pia hakutoka maamuzi sahihi kwa kukataa bao halali la mshambuliaji Didier Kavumbagu dakika ya 70 ya mchezo.


Mashabiki wa Mbeya City walirusha chupa za bia na mawe kwenye bus la timu ya Yanga na kuvunja kioo cha bus kubwa upande wa dereva na kumjeruhi mkononi hali iliyoplekea wachezaji wa Yanga kucheza kwa hofu katika mchezo huo wakihofia usalama wao.


Afisa habari wa Yanga Baraka Kizuguto aliwasilisha taarifa hizo kwa kamisaa wa mchezo juu ya matukio hayo na ushahidi wa kipande cha chupa kilichorushwa na kumjeruhi dereva baada ya kupasua kioo.


Tukio hilo la kabla ya mchezo lilipelekea timu ya Yanga kucheza kwa woga na wasiwasi juu ya usalama wao(under protest) kitu ambacho kikanuni kinairuhusu timu iliyokutwa na matatizo hayo kuka rufaa kuhusiana na hali ya usalama iliyojitokeza.


Aidha klabu ya Yanga pia inaomba kuhakikishwa usalama na shirikisho la soka nchini (TFF) katka mchezo wa siku ya jumatano dhidi ya timu ya Prisons vinginevyo inaomba mchezo huo pia uhamishiwe katika uwanja wa ugenini kutokana na kutokua na uhakika wa usalama.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara ulimalizika kwa sare ya bao 1-1, mchezo uliofanyika katika dimba la uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

WALIMU WAANZA MGOMO UGANDA

$
0
0
Walimu wa shule za msingi na sekondari nchini Uganda wamegoma hii leo ikiwa siku ya kwanza ya muhula wa tatu na wa mwisho mwaka huu kwa wanafumzi.
Hii ni baada ya matakwa yao ya kutaka wizara ya elimu kuwalipa mshahara zaidi kugonga mwamba.

Walimu hao wanataka nyongeza ya asilimia ishirini pamoja na kuitaka serikali kuboresha mazingira ya kazi.
Mwalimu wa shule nchini Uganda hulipwa dola 98 kwa mwezi wakati mwalimu wa sekondari anapokea dola 176 kila mwezi.

Duru zinasema kuwa walimu waliamua kuwa watafika madarasnai ingawa hawatawafundisha wanafunzi. Hii ni kutokana na madai kuwa serikali inawatisha kuwafuta kazi walimu watakaoshiriki mgomo huo.


Walimu hao inasemekana walitoa onyo la siku 90 kwa serikali lakini kwa sababu wanahisi kuwa serikali iliwapuuza ndio maana wakaamua kugoma.

Serikali kwa muda mrefu imekuwa ikiahidi kuwaongeza mishahara walimu hao ambao ni baadhi ya wafanyakazi wa umma wanaopokea mishahara duni katika taifa hilo la Afrika Mashariki.

Changamoto kwa Uganda imekuwa gharama ya matumizi serikalini hasa tangu wahisani kusitisha msaada kwa taifa hilo kutokana na utumizi mbaya wa pesa za umma na ufisadi.

Maafisa wa chama cha walimu wamesema kuwa takriban walimu 159,000 hawatafunza kuanzia leo hadi serikali itakapotimiza matakwa yao.

Kumekuwa madai ya maafisa wa usalama kuwatisha walimu wanaogoma , ingawa serikali imeyakanusha madai hayo.
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live