Quantcast
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

MENDE MILIONI 1 WATOROKA

Image may be NSFW.
Clik here to view.

Imeripotiwa kuwa mende zaidi ya milioni moja wametoroka kutoka kwa shamba walimokuwa wakifugwa nchini China ili kuweza kutumika kwa dawa za kienyeji.

Mende hao walitoroka katika shamba eneo la Dafeng, mashariki mwa Jiangsu, na kuelekea katika mashamba ya mahindi yaliyopo karibu na eneo hilo. tukio hilo lilitokea mapema mwezi huu baada ya mtu asiyejulikana kuharibu sehemu ambayo walikuwa wanafugwa, gazeti la Modern Express lilisema.

Wakuu wa kudhibiti maradhi wametuma wapelelezi watano katika eneo hilo kutoa mpango wa kuwaondoa.

Mmiliki wa shamba hilo Wang Pengsheng aliwekeza zaidi ya Sh1.3 milioni katika kilo 102 za mayai ya Periplaneta americana baada ya kuunda mpango wa biashara wa miezi sita, ripoti ilisema.

Mende kwa kawaida huchukuliwa kama mdudu lakini wanaoamini dawa za kienyeji za Wachina hutumia mimea na pia wanyama ambao ni pamoja na viumbe vilivyopo hatarini wakisema kuwa vinaweza kutibu kansa, kupunguza uvimnbe na kumarisha kinga maradhi.

Kufikia wakati ambapo kinyumba cha plastiki ambapo walikuwa wakifugiwa kiliharibiwa, kulikuwa na kombamwiko zaidi ya 1.5 milioni waliokuwa wameanguliwa na walikuwa wakilishwa chakula ambacho ni pamoja na “matunda na biskuti” kila siku, Wang alinukuliwa kusema.

Bw Wang alisema kuwa alikuwa ametarajia kutengeza zaidi ya Sh14,000 kama faida kwa kila kilo ya mende ambayo angeuza, lakini sasa anakabiliwa na hasara kubwa.

KENYA BALAA:NDOA YA WATU 3, MKE NI MMOJA WANAUME WAWILI

Wanaume wawili Wakenya wamesaini makubaliano ya kumoa mwanamke mmoja, imeripotiwa.

Mwanamke huyo amekuwa na mahusiano na wanaume hao wawili kwa kipindi kisichopungua miaka mine na kukataa kuchagua kubakia na mmoja kati yao.

Makubaliano hayo yaliwahalalisha Sylvester Mwendwa(kushoto Pichani) na Elijah Kimani kuishi na katika nyumba ya mwanamke huyo na kukubaliana kulea watoto watakao zaliwa na mwanamke huyo.

Mwanasheria alidai kuwa ndoa yao itatambulika kisheria kama watatoa ushahidi kwamba ndoa ya aina hiyo ni sehemu ya utamaduni wao.
SOMA ZAIDI...

Wivu 

Bw. Mwendwa na Bw Kimani waliandaa mkataba baada ya kugundua kuwa wote wawili walikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanamke mmoja huko Mobasa kwa zaidi ya miaka mine, iliripotiwa na gazeti la Daily Nation la nchini Kenya.

Afisa wa mambo ya jamii Adhalah Abdulrahman aliwashawishi wanaume hao kwa pamoja kumuoa mwanamke huyo baada ya kuona jinsi wanavyomgomania mwanamke huyo.

"Tumekubaliana kuanzia leo hatutogombana wala kutishiana au kuoneana wivu kwa sababu ya mke wetu, ambaye amesema hayuko tayari kuachana na hata mmoja kati yetu” makubaliano hayo yalieeleza alisema mtangazaji wa televisheni ya Kenya ya NTV.

“kila mmoja ataheshimu siku yake aliyopangiwa. Tunakubali kupendana na kuishi kwa amani. Hakuna aliyetulazimisha kufanya makubaliano haya.” Kiliongeza kipengele hicho

Bw. Mwenda alisema wazazi wake wamempa Baraka zote, wakati anajiandaa kutoa mahari.

Mwanamke huyo mjane mwenye watoto wawili hakutaka kutajwa jina lake.
Mwanasheria wa mambo ya familia, Judy Thogori aliliambia gazeti la Daily Nation kuwa sheria haizuii kitendo hicho cha mwanamke kuwa na waume zaidi ya mmoja.

“sharia haiongelei suala hilo lakini ili ndoa hiyo itambulike hapa Kenya, itabidi iwepo kwenye sharia au sharia za kijamii za ndoa”

UGONJWA WA KUDUMAA WAMTESA MTOTO WA MIAKA 14 AONEKANE MZEE WA MIAKA 110


MTOTO wa miaka 14 anasumbuliwa na ugonjwa wa kuduma 'progeria', hali inayopelekea mwili wake kuonekana kama mzee wa miaka 110. Mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Ali Hussain, anayeishi nchini India anaonekana kama mzee wa miaka 110 kutokana na tatizo hilo linalomfanya akue kwa haraka kuliko kawaida.

Ugonjwa huo unaonekana kuitesa zaidi familia yake ambapo hadi sasa mtoto huyo ameshuhudia dada zake pamoja na kaka zake watatu wamefariki kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa huo.

Imeripotiwa kuwa watu wanaosumbuliwa na ugonjwa huo hawawezi kuishi zaidi ya miaka 14 huku wakiwa wanasumbuliwa na tatizo la macho pamoja na moyo Hussain  bado kwa upande wake hajakata tamaa ya kuishi.


"Ninamatumaini ipo dawa ya tatizo langu na ninatamani sana kuishi siogopi kifo lakini wazazi wangu wanateseka sana juu yangu naumia kwani sitaki kuwabebesha mzigo wa maumivu wazazi wangu"

Tatizo hilo linaonekana ni la kurithi ndani ya familia yao ambapo baba mzazi wa mtoto huyo Nabi Hussain Khan (50) aliweka wazi kuwa kama wangeambiwa mapema na daktari juu ya ugonjwa huo wasingeendelea kuzaa.

Ripoti hiyo imedai kuwa waliendelea kuzaa kwa matumaini kuwa wangepata mtoto asiye na tatizo na ndipo walipompata Sanjeeda.

FAT JOE AANZA KUTUMIKIA KIFUNGO

Rapper Fat Joe ameanza kutumikia kifungo chake cha miezi minne alichohukumiwa baada ya kukutwa na hatia ya kushindwa kulipa kodi. Joe aliamua kuwaaga mashabiki wake kwa kutumia ukurasa wake wa Twitter, ikionyesha kuwa ameamua kwenda  kuripoti mwenyewe jela ya Federal Detention Center, Miami nchini Marekani.


June 24 Joe alihukumiwa kifungo cha miezi 4 jela kwa kushindwa kulipa deni la kodi zaidi ya dola milioni 1 kwa kipindi cha miaka miwili 2007 na 2008, ambapo kifungo hicho kinaambatana na faini ya dola 15,000 pamoja na usimamizi maalum wa mwaka mmoja baada ya kutoka jela

WAKAZI WA MIVINJENI WASHINIKIZA SERIKALI KUWALIPA HUNDI ZAO

WAKAZI wa Mivinjeni Kurasini wanaotakiwa kuhama kupisha mradi wa  uwekezaji wa EPZ wamefunga barabara kuishinikiza Serikali kuwalipa hundi zao na si viwanja.

Hali hiyo ilijitokeza jana Dar es Salaam Majira ya Saa tano asubuhi ambapo wananchi walijipanga barabarani na kuzuia magari kupita kuishinikiza serikali kuwalipa fidia ili waweze kuondoka katika eneo hilo.

Akizungumza na gazeti hili Katibu anayefutilia malipo ya wakazi hao Judith George alisema kuwa  wakazi hao wamelala  barabarani kutokana na serikali kuwapiga dana dana kulipwa hundi za nyumba zao ili waweze kuhama.


Alisema kuwa Viongozi wa Serikali pamoja na Mwekezaji  (EPZ) walifika katika eneo hilo March 13 mwaka huu na kufanya mkutano na wananchi kuhusu  uwekezaji katika eneo hilo.

Alisema kuwa Mwekezaji huyo alipozungumza nao walikubali kuhama kupisha ujenzi wa kiwanda katika eneo hilo la Mivinjeni na aliahidi kuwalipa fedha zao ili waweze kutafuta sehemu nyingine.

Aliongeza kuwa  mwekezaji huo alifuatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka na kuahidi wakazi hao kuwapatia  Viwanja mbadala katika eneo la Kigamboni Uvumba Kibanda.

Alisema kuwa  baada ya hapo serikali ilishirikiana na Wilaya ya Temeke kufanya tathimini April mwaka huu ya nyumba zote za wakazi hao na kuweka x.

"Baada ya tathimini Mkuu wa Wilaya ya Temeke kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali wa serikali kwa na mwekezaji walifanya tena tatahimini na kubaini kuna nyumba 60 zina matatizo  eneo la Shimo la Udongo Kurasini na kufanikiwa kuokoa sh Bilioni 1.4zilikuwa za usanii.

Aliongezea kuwa baada ya kufanyiwa tathimini walitangaziwa kwamba Agosti 26 mwaka huu wafike wilayani kwa jili ya kuchukua Hundi zao, lakini walipofika waliambiwa  zoezi la utoaji hundi limesitishwa.

Hata hivyo alisema kama zoezi la ulipaji wa fidia  limesitishwa kwa nini hawakutangaziwa kama walivyofanya mikutano mara ya kwanza ya kuambiwa eneo hilo linahitajika na mwekezaji.

Naye Mkazi Mwingine wa eneo hilo Mgeni Juma alisema  serikali imejaa usanii tu kutokana na mwekezaji kutoa fedha za kulipwa lakini wao wanasitisha bila kutoa taarifa kwa wananchi.

Alisema  kuwa kama serikali hiyo ikicheza 2015 hawaweze kupiga kura kutokana na kudanganya wananchi, tusije tukafanyiwa kama wakazi wa Kipawa walivyokuwa wanadanganywa mpaka leo.

Naye Rodi Panjo mkazi wa kurasini alisema  walipotangaziwa hundi zitaanza kutolewa  August 26 alisafiri kutoka Mbeya kuja kuchukua hundi yake lakini alipofika zoezi limesitishwa na ukizangatia nalala nyumba za wageni fedha ya kulipa nitapata wapi.

Mkazi mwingine Gerad Mahinya alisema  biashara zao zimefungwa kutokana na nyumba hizo kuwekwa alama ya x hali ambayo hawajui hatma ya maisha yao.

"Wakazi wengi wameshahama kutoka maeneo hayo na wengin walikopa kutoka  benki mbalimbali na kutafuta maeneo mengine ya kukaa huku wakitegemea kupata fedha zao ili kulipa  madeni ,"alisema.

Naye Kamanda wa Polisi Mkoa wa kipolisi Temeke  Engelbert Kiondo aliwataka wakazi hao kuwa na subira na kufika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya saa nane ili kupata majibu ni lini watapewa  hundi zao.

Hata hivyo aliwataka wakazi hao kuwa wavumilivu na kuachia magari yaweze kupita ili alhamisi atawasilina na Waziri wa Ardhi aweze kwenda kuzungumza nao katika ofisi za serikali za mtaa wa kurasini.
 





MASKINI AUNTY EZEKIEL, ALA KICHAPO AKIJIRUSHA

Image may be NSFW.
Clik here to view.
Msanii wa filamu za Bongo, maarufu kama Aunt Ezekiel amepigwa na kuumizwa katika mkono wake wa kushoto alipokuwa Club Bilicanas katika utambulisho wa wasanii wa Bongo Fleva waliokuwa wakitambulishwa na Wema Sepetu.
Image may be NSFW.
Clik here to view.

Wema Sepetu ambaye pia ni msanii maarufu kati ya watu maarufu katika uwanja wa sanaa nchini Tanzania alitambulisha wasanii wapya wa muziki wa kizazi kipya katika ukumbi mkongwe na maarufu wa Bilicanas jijini Dar es Salaam siku ya jumapili.
Image may be NSFW.
Clik here to view.

Inadaiwa kuwa Aunt Ezekiel alipigwa chupa katika mkono wake na mtu asiyejulikana na kitendo hicho kuhusishwa na ugomvi wa mapenzi uliotokea siku za nyuma. Bi Ezekiel ameumiza vibaya katika mkono wake kwa kuchimbwa na kitu chenye ncha kali na kusababisha kidonda kikubwa kilichochimbika.

Kwasasa bi Ezekiel amelazwa akiuguza jeraha hilo.


PICHA ZOTE KWA HISANI YA MTANDAO

POLENI WALA SAMAKI JIJINI DAR ES SALAAM

SAKATA LA SILAHA ZA SUMU, SYRIA KUSHAMBULIWA

Wasiwasi wa muungano wa mataifa ya Magharibi kuishambulia Syria umenukia, kufuatia Marekani, Uingereza na Ufaransa kusema kuwa itatoa adhabu kwa taifa hilo la kiarabu kwa kutumia silaha za kemikali katika mapigano dhidi ya waasi nchini humo juma lililopita.

Mataifa ya Magharibi, yakiongozwa na Marekani yanaunga mkono hatua ya kijeshi dhidi ya Syria huku mataifa ya Mashariki na Asia yakiongozwa na Urusi yakipinga.

Wachanganuzi wa maswala ya Mashariki ya Kati walianza kuona dalili za mataifa ya magharibi kujiingiza kijeshi nchini Syria kufuatia matumizi ya silaha za kemikali katika eneo lililo kaliwa na waasi majuma machache yaliyopita, ambapo watu kadhaa walifariki kikatili.

Katika shambulio hilo, ilikuwa dhahiri kuwa silaha hizo za kemikali zilitumiwa lakini kila upande katika mzozo huo ukilaumu mwenzake kwa kufanya hivyo.

Hapa uamuzi ulifanywa, kupitia Umoja wa Mataifa, kuwa wataalamu wa silaha za kemikali wa Umoja huo, wasafiri hadi Syria ili kuchunguza ukweli. Baada ya kushawishi Serikali ya Rais Assad kwa muda, idhini ilitolewa na pia wanajeshi wa Syria wakaahidi kuwa siku hiyo ya kuchunguza mapigano kati ya Serikali na waasi wanaoungwa na mataifa ya Magharibi watasitisha mapigano.

Juma lililopita wachunguzi hao walishambuliwa na wadenguaji mara mbili wakielekea kwenye eneo la kuchunguza, na isitoshe muda mfupi baadaye shambulio kubwa zaidi la silaha za kemikali likafanywa katika makaazi wa waasi, karibu sana na jiji la Damascus.

Kufuatia shambulio la pili ilikuwa wazi sasa kuwa Marekani, Uingereza na Ufaransa ziko tayari kushambulia.Suala la pekee ambalo hadi dakika hii watu wanajiuliza ni, lini?Image may be NSFW.
Clik here to view.

ARSENAL YAFANYA KWELI


Image may be NSFW.
Clik here to view.

Aaron Ramsey alifunga mabao mawili na kuipa klabu yake Arsenal ushindi wa wazi bila upinzani mkali dhidi ya Fenerbahce ya Uturuki.

Katika mechi iliyochezwa hapo jana kwenye uwanja wa Emirates, Arsenal imefuzu kwa Ligi ya Mabingwa kwa mwaka wa kumi na sita mfululizo.

Wageni Fenerbahce walibaki nyuma tangu mechi ya awamu ya kwanza walipofungwa mabao matatu kwa bila na Arsenal. 


Adhabu hiyo kwa Fenerbahce imerahisisha kazi ya shirika la kandanda la Uropa, UEFA, kwani sasa haitajishughulisha kuizuia klabu hiyo kutoshiriki mechi ya ligi za mabingwa, hii inafuatia marufuku ya miaka miwili ambayo inafaa kutolewa kwa Fenerbahce baada ya kushtumiwa na hatia ya kupanga mechi.

Ikiwa klabu hiyo ingefaulu kushiriki Ligi ya Mabingwa basi kingekuwa kibarua kigumu kwa UEFA kutekeleza sheria na adhabu ipasavyo.

Hii leo jumatano, mahakama ya rufaa itasikiliza kesi hiyo.

Arsenal imewahi kushindwa na timu za Uropa mara mbili tu katika muda wa miaka hamsini, huku klabu hiyo ya Uturuki imepata kufunga mabao mara tatu tu katika ziara zake nane za England.

MDINGI JELA KWA CHABO, ALIJIFICHA KWENYE SHIMO LA MAJITAKA

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 52 amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na faini ya takribani shilingi milioni 8 (karibu sawa na dola za kimarekani 5000) baada ya kupatikana na kosa la kupiga chabo.

Image may be NSFW.
Clik here to view.
Bw. Keneth Enlow(Pichani Kulia) alikamatwa mwezi wa saba baada ya mwanamke mmoja na mwanae wa miaka 7 kumshtukia baada ya kusikia kitu kinasogea kwenye shimo la choo walichokuwa wanakitumia eneo la White Water huko Sand Springs, Oklahoma Marekani.

Mama huyo, Ambra Reynolds(Juu Pichani akiwa na mwanae) alipoangalia kwa karibu akamuona Bw.Enlow akimchungulia chooni kutokea kwenye shimo hilo la maji machafu. “sio jambo la kwaida unapokuwa unajisaidia” alisema Bi. Reynolds.



“nilipiga mayowe, nikamchukua mwanangu, njiani nikambeba na mwanangu wa kiume aliyekuwa anatusubiri na kutoka nje nikiwa na wasiwasi mkubwa” alisema mama huyo.


Kundi la waokoaji walikuja na kumuibua Bw. Enlow akiwa ametapakaa vinyesi mwili mzima na kumsafisha kwa kutumia mpira wa maji.

Alikubali kosa katika mahakama ya Tulsa la kupiga chabo wiki iliyopita na kuhukumiwa.

MSHINDI WA AIRTEL YATOSHA

Mmoja wa wafanyakazi wa Airtel, Jackline Kaaya akikabidhi shilingi milioni moja kwa mshindi, Michael Joseph mkazi wa Mwanza, baada ya kushinda katika shindano la Airtel linalojulikana kama 'Airtel yatosha shinda nyumba 3', inayowawezesha wateja kote nchini kujishindia shilingi milioni moja kila siku. Tukio hilo fupi la Kukabidhi zawadi hiyo lilifanyika katika ofisi za Airtel Mwanza leo.

WASHIRIKI RED'S MISS TANZANIA WAKIWA KAMBINI

 Washiriki wa shindano la kumtafuta Red's miss Tanzania wakiwa katika pozi la pamoja na wadhamini washindano hilo pamoja na uongozi Giraf Hotely jijini Dar es Salaam ikiwa katika maadhimisho ya siku ya waandishi wa habari
 Baadhi ya warembo wa shindano hilo wakitoka kuzungumza na wadhamini wa shindano hilo
Mshiriki kutoka Kanda ya juu akiwa katika pozi na mshiriki mwenzie kambini

WATOTO WANANYANYASWA MIGODINI

Maelfu ya watoto wanaofanya kazi katika machimbo ya madini nchini Tanzania wanakabiliwa na tishio kubwa la kupata magonjwa na hatimaye kufa.


Shirika la kutetea haki za kibinadam la Human Rights Watch, limefichua ushahidi zaidi kuhusu unyanyazaji wa watoto nchini Tanzania, baadhi yao wenye umri wa miaka minane ambao wanafanya kazi kwa zamu, katika migodi ya madini iliyoko chini ya ardhi, kwa saa ishirini na nne.

Shirika hilo limesema watoto hao wanakabiliwa na tishio la kuvuta hewa ya sumu inayotokana na uchimbaji wa madini ya dhahabu na wakati mwingine kuuawa wakati migodi hiyo, inapoporomoka nyingi zikiwa hazina leseni.

Tanzania ina sheria kali inayozuia watoto kufanya kazi katika machimbo ya madini lakini shirika hilo limesema, serikali ya rais Jakaya Kikwete ni sharti iimarishe juhudi zake za kuhakikisha sheria hizo zimetekelezwa.

TAARIFA HII NI KWA MUJIBU WA SHIRIKA LA UTANGAZAJI LA UINGEREZA  BBC

KOCHA WA NIGERIA APATA KASHFA


Shirikisho la mchezo wa soka duniani FIFA, limethibitisha kuwa limepokea malalamishi kutoka kwa shirikisho la mchezo wa soka nchini Malawi FAM, kuhusiana na matamshi yaliyotolewa na kocha wa Nigeria, Stephen Keshi (Pichani).

Hata hivyo shirikisho hilo la FIFA limesema kuwa kwa sasa haliwezi kusema lolote kuhusu suala hilo, hadi uchunguzi utakapo kamilika. FAM limedai kuwa Keshi alitoa matamshi ya ubaguzi dhidi ya kocha wake Tom Sainfiet raia wa Ubelgiji.

Katibu mkuu wa FAM, Suzgo Nyirenda ameiambia BBC, kuwa matamshi hayo ya ubaguzi hayafai kuwepo katika michezo katika dunia ya sasa. ''Tunahisi na shambulio dhidi ya kocha wetu na tutamtetea kwa hali na mali, bila kuzingatia uraia wake na rangi ya ngozi yake'' Alisema Nyirenda.

''Tumetuma ushahidi wa yale Keshi aliyoyasema na tunatarajia kuwa FIFA itachukua hatua kali dhidi ya kocha huyo wa Nigeria Stephen Keshi'' aliongeza Nyirenda.

Kesi hiyo inahusiana na matamshi ambayo Keshi aliyatoa kufuatua wito wa Malawi wa kuhamisha mechi yao ya kufuzu kwa kombe la dunia mwaka wa 2014, kutoka mji wa Calabar kutokana na sababu za kiusalama. Katika mahojiano na runinga moja ya Uingereza, Keshi alisema ''Nafikiria kuwa kocha huyo wa Malawi ni wazimu''.
SOMA ZAIDI...

''Ikiwa anataka kuongea na FIFA, basi ni lazima arejea kwao nchini Ubelgiji. Yeye sio mtu wa Afrika, ni mzungu mweupe, ni lazima arudi kwao Ubelgiji'' Alisema Keshi katika mahojiano hayo. Maafisa wakuu wa shirikisho la mchezo wa soka nchini Nigeria pamoja na kocha huyo hawajasema lolote kuhusiana na madai hayo ya kocha wa Malawi Saintfiet na FAM.

Mechi hiyo kati ya Malawi na Nigeria mjini Calabar itaamua nani atafuzu kwa raundi ya mwisho ya mechi ya kufuzu kwa fainali hiyo barani Afrika. Mabingwa hao wa Afrika wanahitaji kutoka sare ya aina yoyote ili kufuzu ili hali Malawi inahitaji ushindi ili isonge mbele.

URUSI YAPINGA UVAMIZI SYRIA

Marekani imeachana na jitihada za kutafuta uungwaji mkono wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuichukulia hatua Syria kwa utumiaji silaha za kemikali.

Hii ni kufuatia kukataa Urusi kwa rasimu ya maazimio yaliowasilishwa kwenye mkutano wa wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo la usalama.

Akilaumu Urusi kwa kile alisema msimamo wake wa kutobadili maoni kwa chochote, Msemaji wa wizara ya mashauri ya kigeni, Maria Harf amsema kuwa Marekani haitaruhusu alichotaja kama uzembe wa kidiplomasia kutumiwa kama ngao ya kutetea Serikali ya Syria. Azimio lilioandikwa na Uingereza lingaliruhusu hatua za kuwalinda raia wa Syria lakini likapingwa na Urusi katika kikao cha wanachama watano wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Urusi, ambayo hutoa silaha kwa Serikali ya Syria na pia mshirika wake mkuu kimataifa, ilisema kuwa kura ya azimio hilo inapaswa kuahirishwa hadi tume maalumu ya umoja wa mataifa ya kuchunguza matumizi ya silaha za kemikali nchini humo itakapokamilisha kazi yake.

Msemaji huyo alielezea hali ya Marekani ya kutoridhika na hali ya upole inayoendelea katika Umoja wa Mataifa, na akasisitiza kwamba kwa wakati huu Marekani haioni matumaini yoyote ya kuungwa mkono na Baraza la Usalama la umoja wa Mataifa na kwa sasa itatilia mkazo mashauriano na mataifa mengine washirika kabla ya kuchukua hatua yoyote inayofaa hivi karibuni.

Alisema kuwa hadi kufikia sasa Rais Obama hajafanya uamuzi wowote juu ya hatua inayopaswa kuchukuliwa, lakini akaongeza kuwa ni dhahiri kuwa silaha za kemikali zilitumiwa nchini Syria na kwamba wa kulaumiwa ni utawala wa Rais Assad.

ZAIDI YA WATU 40 WAFARIKI KWENYE AJALI KENYA


Takriban watu 41 wanadaiwa kuuawa baada ya basi moja la abiria lililokuwa likitoka Nairobi kuelekea Homabay Magharibi mwa Kenya kuanguka na kubingirikia mara kadhaa katika eneo la Narok.Polisi wamethibitisha kuwa miongoni mwa waliouawa ni watoto wanne.

Mkuu wa polisi wilayani Narok Patterson Maelo amesema kuwa dereva wa basi hilo alishindwa kulithibiti katika eneo la kona na hivyo basi hilo kupoteza mwelekeo na kuanguka.

Maafisa wa shirika la msalaba mwekundi ambao tayari wamefika katika eneo la tukio hilo wamesema kuwa watu wengine 33 waliojeruhiwa wamesafirishwa hadi hospitali ya wilaya ya Narok kwa matibabu.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ni miongoni wa viongozi waliotuma risala zao za rambi rambi kwa jamaa na marafiki wa abiria waliouawa.

Katika ripoti iliyochapishwa katika mtandao wake wa twitter, rais Kenyatta ametoa amri kwa idara ya polisi kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wa magari ya umma wanaokiuka sheria za barabarani.

RED CARPET ILIVYOKUWA UZINDUZI FILAMU FOOLISH AGE

BAADHI YA WASANII WALIOHUDHURIA UZINDUZI


 Shilole naye alikuwepo

 Monalisa akiwa na mama yake katika uzinduzi huo
 Baadhi ya wasanii wakongwe nao walihudhuria uzinduzi huo
 Msanii JB pamoja na Ray wakifwatiria kwa makini matukio yaliyokuwa yakiendelea katika uzinduzi huo

Batuli ni miongoni wa wasanii wa bongo movi aliyehudhuria uzinduzi huo

WEMA AMLIZA MAMA KANUMBA

 MSANII wa filamu nchini Wema Sepetu amtoa machozi mama Kanumba Bi. Flora Mtegoa a.k.a mkwe wake pindi walipokutana katika uzinduzi wa filamu ya  Elizabeth Michael iliyopewa jina la Foolish Age.

Filamu hiyo ilizinduliwa mwisho mwa wiki katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambapo
mama Kanumba alijikuta akitokwa na machozi mfululizo mara baada ya kukutana na msanii huyo.

Mama huyo ambaye alijikuta akivutiwa na uchezaji wa Wema ukumbini hapo wakati bendi ya Machozi ikitumbuiza aliamua kumfuata na kutaka kumtunza kutokana na uchezaji wake.



MAXMALIPO WAWAFIKIA WATEJA DAR ES SALAAM

 Ofisa Uhusiano na Masoko wa Maxmalipo Bw. Isaac Nyimbo akimpa maelekezo mteja baada ya kutembelea banda lao katika viwanja vya Posta Dar es Salaam jana.  Wakati wa tamasha la 'Elimu exprience'

 Ofisa Uhusiano na Masoko wa Maxmalipo Bw. Isaac Nyimbo akiwa na baadhi ya wafanyakazi wenzie akitoa maelekezo kwa mteja baada ya kutembelea banda lao katika viwanja vya Posta Dar es Salaam jana.  Wakati wa tamasha la 'Elimu exprience'

Viewing all 3497 articles
Browse latest View live