Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

MABANDA YA VIDEO KICHOCHEO UBAKAJI

$
0
0
IMEBAINIKA kuwa uwepo wa mabanda ya kuoneshea video mitaani ambayo hayapo kisheria, kumechangia vitendo vya ubakaji na ulawiti wa watoto wadogo ambao ni wanafunzi wa shule za msingi wilayani Kibaha mkoani Pwani.

Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hii mjini Kibaha, umebaini kuwa watoto hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo nyakati za usiku, wanapokuwa wamekwenda kuangalia video ambapo waoneshaji wa video hizo huonesha picha chafu za ngono.

Mabanda hayo ambayo mengi yamejengwa kwa mbao au mifuko ya sandarusi na kuezekwa na makuti au nyasi na yasiyo na mvuto yamekuwa yakionesha picha hizo maarufu kama pilau, kachumbari na ubwabwa na majina mengine ambayo kwa mtu wa kawaida si rahisi kujua maana yake.


Baadhi ya wakazi ambao wamelaani mabanda hayo, ambayo huanza kuonesha video majira ya asubuhi hadi usiku na kusababisha baadhi ya wanafunzi kushinda humo, huku wakiwa wameaga wanakwenda shule na kuishia mabandani na endapo wazazi hawatafuatilia kuna hatari ya wanafunzi kutohudhuria darasani kabisa.

Walilielezea njia wanazotumia wabakaji hao ni kuwalipia kiingilio cha kuangalia picha ambacho ni sh. 500 kwa filamu zitakazooneshwa kwa siku hiyo, ambazo huoneshwa kwa awamu na huchukua kila awamu zaidi ya saa tatu, kisha kubadili picha zingine.

Picha zinapokuwa zinaendelea mara hubadili na kuweka picha chafu za ngono, hivyo kuhamasisha vitendo hivyo na kwa kuwa vijana hao wanaobaka watoto wanakuwa wamewalipia kiingilio, huwachukua na kuwapakata watoto hao na wanapokuwa wamepandwa na msisimko huanza kuwaingilia watoto hao hadi wanapomaliza haja zao.

“Mara wamalizapo haja zao huwapa fedha kwa ajili ya kuwataka wasiseme kwa wazazi wao ambapo watoto hao, baadaye huzoea na kujikuta kila wakati wakienda kwenye mabanda hayo na kufanyiwa vitendo hivyo na kuzoea hali ambayo inawaathiri kisaikolojia na kufanya maendeleo yao shuleni kushuka,” alisema mmoja wa wakazi hao ambaye hakupenda kutajwa jina .

Akizungumzia hali hiyo, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Lulanzi wilayani Kibaha mkoani Pwani, Anna Bilali alisema wanafunzi wengi wameathiriwa na hali hiyo, ambapo mbali ya kwenda kwenye mabanda hayo mara wasipokwenda shule huandika kazi walizofanya wenzao, kisha kujisahishia ili kuwadanganya wazazi wao.

“Wanafunzi wa namna hii wamekuwa wakijisahishia madaftari yao, lakini sisi tunagundua kwani usahishaji wao ni tofauti na wa walimu na tunapowaambia, baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatetea watoto wao hali inayosababisha ugumu wa kuwadhibiti, kwani baadhi ya wanafunzi hukaa kwenye mabanda hayo hadi saa tatu usiku bila hata kuulizwa walikokuwa,” alisema mwalimu huyo.

Alisema pia baadhi yao humiliki simu, ambazo wanakwenda nazo shuleni na kuangalia picha hizo na kujikuta muda mwingi wakiutumia kwa kuangalia picha hizo kupitia simu, ambazo huwa wanazificha na inakuwa vigumu kuwagundua hadi wenzao watoe taarifa.

Aliongeza kuwa kuna watu wamekuwa wakiwaonesha picha hizo kupitia simu, kisha huwatoza kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kupata huduma hiyo, hali amabayo inaendelea kuongeza kusambaa kwa vitendo viovu.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mwantumu Mahiza alisema udhibiti wa mitandao kama hiyo ya uoneshaji wa picha za ngono ni viongozi wa mtaa na vijiji kwa kuwachukulia hatua, kwani hayako kisheria hivyo hayana sababu ya kuwepo ili kuondoa tatizo hilo.

Hivi karibuni wanafunzi wanne wa Shule ya Msingi Lulanzi, walikamatwa na polisi wilayani Kibaha kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi mwenzao wa darasa la pili, mwenye umri wa miaka tisa na kumsababishia maumivu makali na kulazwa hospitali ya Tumbi ambapo aliruhusiwa kutoka wiki iliyopita baada ya kupata matibabu.


KESI DAWA ZA KULEVYA YACHANGANYA MAWAKILI

$
0
0
Kesi ya dawa za kulevya inayomkabili raia wa Kenya, Mwanaidi Ramadhani Mfundo, maarufu kwa jina la Mama Leila au Naima Mohammed Nyakiniwa na wenzake wanane, imeendelea kugubikwa na utata wa kisheria na kuzua mvutano uliosababisha iahirishwe kwa mara nyingine ili kusubiri uamuzi wa Mahakama.

Jana, Mahakama Kuu ilitengua hoja iliyozua mvutano mkubwa juzi kwa kuruhusu upande wa mashtaka kuwasilisha notisi ya kuongeza shahidi muhimu kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Eva Mamuya jambo lililopingwa na upande wa utetezi. Mbali ya Mama Leila, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Anthony Arthur Karanja na Ben Ngare Macharia (wote Wakenya). Wengine ni Watanzania watano, Sarah Munuo, Almas Said, Yahya Ibrahim, Aisha Kungwi, Rajabu Juma Mzome na John William.

Wakati upande wa utetezi ukipinga uamuzi huo wa jana, upande wa mashtaka ulitoa hoja nyingine ya kuongeza shahidi wa pili, ASP Neema na kuibua mvutano mkali wa kisheria uliomlazimu Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi hiyo, kuiahirisha hadi Ijumaa wiki hii atakapotoa uamuzi kama upande wa mashtaka ulikuwa sahihi au la kuwasilisha notisi hiyo mahakamani kabla ya uamuzi wa jana.
Mvutano wa kisheria Ubishi ulianza mapema mahakamani wakati Jaji Mwakipesile alipokuwa akijiandaa kusoma uamuzi wake juu ya maombi ya upande wa mashtaka kuwasilisha notisi ya kuongeza shahidi.
Wakili wa utetezi, Yassin Member alisimama na kumwomba jaji kutokusoma uamuzi wake kwani tayari walikuwa na notisi ya upande wa mashtaka ya kuongeza ushahidi wakati ni kinyume cha sheria.
Member alilalamika kuwa upande wa mashtaka uliomba kuongeza shahidi mmoja lakini notisi ilionyesha walikuwa wanataka kuongeza mashahidi wawili.“Mheshimiwa tunaomba usisome kwani tunashangaa tayari tumepewa notisi ya upande wa mashtaka wakati ukiwa bado hata hujatoa uamuzi wa maombi yao ya kuwasilisha notisi ya kuongeza shahidi. Kibaya zaidi wanataka kuongeza mashahidi wawili na siyo mmoja,” alisema Member.
Jaji Mwakipesile alijibu kwa kutaka upande wa utetezi kuipa nafasi mahakama kutoa uamuzi wake wa maombi ya upande wa mashtaka yaliyosababisha kesi hiyo kuahirishwa juzi.“Ipe nafasi Mahakama kutoa uamuzi wake wa ombi la upande wa mashtaka la kuahirisha kesi ili waweze ku-file notice (kuwasilisha taarifa) ya additional witness (shahidi wa nyongeza), jambo ambalo ninyi mlipinga,’’ alisema Jaji Mwakipesile na kisha kutoa uamuzi wake na kukubali upande wa mashtaka kuongeza shahidi. Uamuzi huo ulisababisha mvutano mkali mawakili wa utetezi wakisema haikuwa sahihi kwa upande wa mashtaka kuongeza mashahidi wakati ulishindwa kwenye Mahakama za chini wakati wa usikilizwaji wa mwanzo.

KIATU KIREFU CHAMUUMBUA JAYDEE

$
0
0
MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura 'Lady Jaydee' a.k.a Annaconda, amejikuta katika wakati mgumu baada ya kiatu kirefu alichokivaa, kutaka kumwangusha jukwaani alipokuwa anatumbuiza kwenye tamasha la hitimisho la Kili Music Tour.

Tukio hilo la kutaka kuanguka lilitokea mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Leaders Club, Kinondoni lilipofanyika tamasha hilo huku kiatu hicho kuonekana ndiyo chanzo cha msanii huyo kutaka kuanguka.

Msanii huyo alipanda jukwaani hapo akiwa amevaa 'High heels' kama kawaida ya shoo zake, lakini siku hiyo kiatu hicho kilionekana kutaka kumuumbua.


Jaydee alifafanua sababu ya kutokea kwa tukio hilo kwa kupitia ukurasa wake wa Twitter pamoja na Facebook, ambapo aliweka wazi kuwa kuanguka ni ajali kama ajali nyingine.

"Kuanguka jukwaani ni ajali kama ajali nyingine, isitoshe sikuanguka bali nilikaribia kuanguka, poleni kwa mlioumizwa na kitendo hicho, nitapunguza urefu wa viatu siku nyingine," aliandika katika ukurasa wake wa Facebook.

Msanii huyo ni miongoni mwa wasanii wenye mafanikio makubwa, huku akiwa ni mmoja kati ya wasanii wa kike wachache wenye mafanikio ya kimuziki, ambapo anatamba na kibao chake cha Yahaya kilichomo ndani ya albamu yake ya 13.

SITTA AJIONEA UZALISHAJI KIWANDA CHA BIA SERENGETI

$
0
0

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akisikiliza maelezo kutoka kwa Packaging Manager wa kiwanda cha bia cha Serengeti (SBL) kilichopo jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea kiwanda hicho kujionea uzalishaji unaofanya pamoja na changamoto zinazozikumba kiwanda hicho.

IDD AZZAN ATOA ONYO KWA WAHITIMU DARASA LA SABA

$
0
0

MBUNGE wa Jimbo la Kinondoni Idd Azzan amewataka wanafunzi waliomaliza elimu ya darasa la saba wasijidumbukize katika makundi ya madawa ya kulevya na badala yake waendelee na masomo ili wapate mafanikio hapo baadaye.

Hayo alisema juzi katika mahafali ya pili ya darasa la saba katika shule ya msingi ya hekima iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam.

Alisema kuna ushawishi mkubwa wa wanafunzi wanaomaliza darasa la saba kuingia katika vishawishi vya uvutaji wa madawa ya kulevya kwa sababu wanamuda mrefu wanakuwa nyumbani hivyo hujifunza vitu mbalimbali ambavyo vingine ni kujiingiza katika makundi yasiyofaa.

Hivyo aliwataka wazazi na walezi wawapeleke watoto wao shule hata kama hajabahatika kuchaguliwa kujiunga  kidato cha kwanza.

Vile vile, aliwataka wazazi hao wawapeleke  watoto wao pre form one huku wakiwa wanasubili majibu yao kutoka na si kumuacha nyumbani na kumsababishia kujiunga katika makundi maovu.

Pia katika mahafali hayo mwalimu mkuu wa  shule hiyo Munga Mtengeti alimwambia Mbunge huyo kuwa shule yao inaupungufu wa madawati 363 na vyumba vya madarasa 3 na hawana uzio katika shule hiyo hali inayosababisha kupata kero nyingi kutoka katika nyumba zilizokuwa karibu na shule hiyo.

Hata hivyo Mbunge huyo ameahidi kutoa madawati 100,ma kujenga chumba kimoja cha darasa na amewataka wazazi na walezi wa shule hiyo kujichangisha wenyewe kwa wenyewe kwa ajili  ya kujenga vyumba viwili vya madarasa.

Katika suala la uzio wa shule Azzan amewata uongozi mzima wa shule wakishrikiana na wazazi waanze kujenga uzio huo na watakapofikia yeye atamalizia ili kuondoa kero wanazopata wanafunzi hivi sasa.

HAKIMU ACHOMWA KISU

$
0
0
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo iliyopo eneo la Nguzo Nane, Kata ya Kambarage Mjini Shinyanga, Satto Nyangoha amejeruhiwa kwa kuchomwa kisu katika shavu lake la kushoto baada ya kutoa hukumu ya kesi ya wizi wa baiskeli.

Kitendo hicho kinadaiwa kufanywa na mlalamikaji katika kesi hiyo, Emmanuel Izengo (28), mkazi wa Tambukareli, Shinyanga baada ya kutokuridhishwa na hukumu iliyotolewa bila ya mshtakiwa, Daniel Makelezia, mkazi wa Lubaga Shinyanga na mdhamini wake, Marko Nkelezia kuwepo mahakamani.

Katika hukumu yake, Hakimu Nyangoha alisema mshtakiwa atakapopatikana atatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatikana na hatia ya wizi wa baiskeli hiyo aina ya Neria yenye thamani ya Sh150,000.

Awali, ilielezwa kwamba baada ya tukio hilo la wizi lililotokea Agosti Mosi, mwaka huu katika eneo la Nguzo Nane, mshtakiwa alikamatwa na kuwekwa mahabusu na kufunguliwa kesi namba 460 ya 2013 kabla ya kuachiwa kwa dhamana Agosti 23, mwaka huu huku kesi yake ikiendelea na pande zote mbili zilitoa maelezo.


Hata hivyo, baada ya kutoa maelezo, si mshtakiwa wala mdhamini wake aliyehudhuria mahakamani hapo licha ya kesi hiyo kusikilizwa mara mbili bila ya taarifa yoyote kabla ya hakimu huyo kutoa hukumu hiyo jana.

Kushambuliwa

Baada ya hukumu hiyo mlalamikaji alitoa shukrani na kuwashika mikono wote waliokuwamo mahakamani humo na kutoka nje.

Ilidaiwa kuwa baada ya dakika 15, Izengo alirudi mahakamani hapo na kudai kuwa ameleta risiti ya kumwonyesha hakimu thamani ya baiskeli yake alipoingia ndani ndipo kelele za Mshauri wa Baraza, Mary Wamba zikaanza kusikika akisema: ‘Njooni jamani hakimu kavamiwa anapigwa’.

Baada ya watu waliokuwa karibu kuingia katika ofisi ya Mahakama hiyo walikuta hakimu ameshacwhomwa kisu katika shavu la upande wa kushoto huku akivuja damu nyingi huku mtuhumiwa huyo akiendelea kumshambulia. Baada ya tukio hilo, wasamaria wema walimpeleka hakimu huyo katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga ambako alilazwa kwa matibabu.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Evarist Mangala alisema mtuhumiwa alikamatwa mara baada ya tukio hilo kusubiri hatua za kisheria dhidi yake.



MSHINDI WA KIGOLI KUIBUKA NA GARI LA THAMANI YA MILIONI 8 NA LAKI 5

$
0
0
 Mashindano ya kumtafuta Kigoli wa Tanzania yapamba moto huku mshindi kuwa na uwakika wa kuondoka na gari lenye thamani ya sh milioni 8 na laki 5, huku washindi wengine wawili kupata ajira kwenye kampuni ya Chicago General Traders

Picha ikimuonesha Mratibu wa shindano la Kigoli Maimatha wa Jesse akipokea ufungua wa gari kutoka kwa Mkurugenzi wa kampuni ya Chicago Bw. Salim Chicago (kama linavyoonekana pichani), ambapo kampuni hiyo imedhamini pia mashindano hayo huku nusu fainali zikitarajiwa kufanyika 29 mwezi huyu huku washiriki 8 watakao patikana ndio wataingia kambini


HALI TETE KUOKOA MATEKA JENGO LA WESTGATE KENYA

$
0
0
HUKU  hali ya mshikemshike ikiendelea kushuhudiwa katika jengo la Westgate lenye maduka, ufyatulianaji risasi umesikika ndani ya jengo hilo lenye maduka na migahawa zaidi ya themanini.

Wapiganaji wa Al shabaab wamewateka nyara raia ambao idadi yao haijulikani bado, waliokuwemo ndani ya jengo wakiendelea na shughuli zao kuanzia Jumamosi mchana wakati wapiganaji wa Al shabaab walipowavamia na kuanza kufyatua risasi kiholela.

Inaarifiwa kuwa  kuna miili ya watu kumi waliopoteza maisha katika ghorofa ya kwanza ya jengo hilo, aidha wapiganaji hao wanaoaminika kuwa wanachama wa Al Shabaab ni kati ya kumi na kumi na watano na bado wapo ndani ya jengo hilo.

Ripoti zinasema kuwa ufyatulianaji mkubwa wa risasi pamoja na milipuko imesikika katika jengo hilo kwa takriban dakika 15.

Harakati za kuendelea kumaliza operesheni hiyo zinaendelea lakini hali ya mateka walio ndani ya jengo hilo inaendelea kudorora. Wapo baadhi ya wakenya  waliofanikiwa kuondoka katika jengo la Westgate kwa usaidizi wa polisi.

Rais Kenyatta amesema kuwa jeshi linajitahidi kuhakikisha kuwa linakabiliana vilivyo na wanamgambo hao.

Helikopta za polisi zinazunguka juu ya jengo hilo pamoja na ndege za kijeshi kushika doria. Vikosi vya usalama vinaendelea na operesheni kujaribu kuwanusuru waathiriwa wakati hali ikiwa ikiendelea kuwa tete katika eneo la shambulizi.


Awali jeshi la Kenya lilisema limeweza kudhibiti jengo hilo lote ingawa bado limetaja hali kuwa tete mno hasa katika kujaribu kuwaokoa mateka waliosalia ndani ya jengo hilo.

Ripoti zinasema kuwa watu 69 wamefariki katika shambulizi hilo la Al Shabaab kufikia sasa huku 175 wakijeruhiwa.

Baadhi wametibiwa na kuondoka hospitalini. Baadhi ya majeraha waliyopata ni majereha ya risasi na kutokana na guruneti ambalo Al shabaab waliwarushia wale waliokuwa ndani ya migahawa siku ya Jumamosi.

Kundi hilo limekiri kutekeleza shambulio hilo kutokana na hatua ya Kenya kupeleka majeshi yake nchini Somalia ili kukabiliana na wapiganaji hao.

J COLE KURUDISHA KUNDI LA TLC KWENYE 'GEMU'

$
0
0
RAPPER maarufu nchini Marekani J Cole yupo katika mikakati ya kuwarudisha tena kwenye ulimwengu wa muziki wadada wanaounda kundi la TLC.

Hali hiyo imetokana na baada ya kundi hilo kupotea kwenye gemu la muziki pamoja na kushindwa  kuachia albamu yao mpya  kwa muda mrefu, hali inayochagia mashabiki wao kuwasahau.

J Cole ameweka mikakati ya kurudisha kundi hilo ambapo teyari amesharekodi nyimbo aliyoshirikiana na kundi hilo inayojulikana kwa jina la 'Crooked Smile', ambapo amekiri kuwa wadada hao wamefanya vizuri kwenye nyimbo hiyo.


Rapper huyo ameeleza kutoa mchango kwenye kutengeneza albamu mpya ya TLC, ili kuhakikisha wadada hao wanarudi tena kwenye gemu hilo.

Mbali na hayo rapper huyo ambaye yupo chini ya Lebel ya Jay Z, anategemea kuuza albamu yake inayojulikana kwa jina la 'Born Sinner' nakala milioni moja duniani.

KEYSHIA COLE NDOA YAKE YAYUMBA

$
0
0
Ndoa ya muimbaji Keyshia Cole inaonekana kuyumba baada ya wawili hao kuthibitisha kupitia ujumbe uliotumwa katika mitandao ya kijamii.Keyshia Cole na mumewe Daniel Gibson wanapitia kipindi kigumu cha ndoa yao na wamekuwa wakiandika ujumbe unaonesha kutengana.

Keyshia aliandika kwenye mtandao wa Instagram kuwa "Mji wa  Cleveland ulikuwa mtamu kwa mumewangu na mimi pia tumeacha kumbukumbu kubwa hapa "

KUNGUNI WAVAMIA BUNDA

$
0
0
WAKAZI  wa Kijiji cha Kunzugu  kata ya Kunzugu wilayani Bunda  wameiomba Idara ya afya kuwanusuru na uvamizi wa wadudu aina ya  Kunguni  katika nyumba zao zenye kaya 399.

Wakazi hao wametoa  ombi hilo jana kwa mbunge wa jimbo la Bunda Stephen Wasira katika mkutano wa adhara kijijini hapo  ambapo walieleza  kuwa kuna kunguni wa kutisha hasa baada ya idara ya afya  kunyunyuzi  katika nyumba hizo  dawa ya kuua mbu.

Walidai kunguni hao wamevamia nyumba zao na kuishi kwenye vitanda, mashuka, meza, viti, nguo na kila kona ya nyumba ambapo wametumia  kila njia ya kuwaangamiza  bila ufanisi.


Akitoa kero hiyo kwa niaba ya wenzake, Paulo Mwangwa mkazi wa Kijiji hicho aliishambulia wizara ya afya kwa madai kuwa kunguni wamesabishwa na  unyunyizaji wa dawa za mbu katika nyumba zao.

“Mheshimiwa mbunge wetu, kabla ya dawa hii ya mbukunyunyizwa majumbani  kwetu hatukuwa na
kunguni , sisi tulidhani dawa hii inaua wadudu wote kwa nini sisi imetuletea kunguni?alihoji Mwangwa akishangiliwa na wananchi wenzake.

Wasira aliagiza idara ya afya kufanya uchunguzi wa kuwepo kwa Kunguni hao huku Mmoja  wa mganga
kutoka idara ya afya wilayani humo aliyejitambulisha kwa jina la Kateire akidai  dawa ya kuangamiza mbu aina ya anopheles  uua wadudu aina zote hivyo watafanyia uchunguzi suala hilo.

CHRISTINA AVALISHWA PETE YA UCHUMBA

$
0
0
Muimbaji Christina Milian ameonesha pete ya uchumba aliyovalishwa na mpenziwe mpya Jas Prince, na akaliambia jarida la People kuwa "Hakika nimezama kwenye penzi la mtu niko katika mahusiano yenye furaha sana, mahusiano madhubuti jambo ambalo ni kubwa, na ananisapoti sana hakika tunaangalia mbele"

VIKOSI VYA KENYA VADHIBITI JENGO WESTGATE

$
0
0
Hatimaye vikosi vya usalama nchini Kenya vinasema vimelidhibiti jengo zima la Westgate mjini Nairobi, ikiwa ni zaidi ya siku tatu baada ya jengo hilo kuvamiwa na wanamgambo.Milipuko ikifuatiwa na milio ya risasi imesikika kutoka ndani ya jengo hilo asubuhi ya leo huku duru zikisema kuwa vikosi vya usalama vinaelekea kukamilisha operesheni hiyo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, magaidi sita waliokuwa wamesalia wameuawa huku wengine watatu wakiuawa hapo jana.Serikali imesema zaidi ya watu 60 wameuawa na wengine zaidi ya 170 kujeruhiwa katika shambulio hilo ambalo Al shabaab imekiri kulitekeleza.

Wizara ya mambo ya ndani imesema wanajeshi wanaendelea kulisaka jengo zima la Westgate kutoka gorofa moja hadi nyingine kuhakikisha kwamba hakuna mateka aliyesaliaWakati huohuo, waziri wa mambo ya nje amesema kuwa wawili kati ya wanamgambo watatu waliofanya shambulii hilo ni raia wa Marekani pamoja na mwanamke muingereza.


Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha televisheni nchini Marekani, Amina Mohamed alisema kuwa wamarekani walikuwa kati ya umri wa miaka 18 na 19 ingawa wenye asili ya kisomali au kiarabu na waliishi mjini Minnesota. Mshukiwa mwingine alikuwa mwanamnke Muingereza ambaye inasemekana alikuwa amefanya vitendo vingi vya aina hii kwa niaba ya Al Shabaab.

Shirika la Red Cross limeambia BBC kuwa watu 63 wangali hawajulikani waliko. Wanajeshi wa Kenya katika juhudi za kuokoa mateka na kukomboa jengo la Westgate Haijulikani idadi ya wanamgambo waliokuwa ndani ya jengo hilo , lakini maafisa wa usalama wamesema kuwa wanamgambo watatu wameuawa.

Kundi la kigaidi la al-Shabab limekiri kutekeleza mauaji hayo, kulipiza kisasi hatua ya Kenya kujihusisha kijeshi nchini Somalia.

MAGAIDI WAWILI WAUAWA, IDADI YA VIFO YAFIKIA 62

$
0
0
Wakati magaidi wawili wakiwa wameuawa, Serikali ya Kenya imesema idadi ya watu waliokufa katika tukio la kigaidi kwenye maduka makubwa ya Westgate, Nairobi imefikia 62.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mchana, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Joseph Ole Lenku alisema watu waliojeruhiwa ni 175 baada ya magaidi hao kuvamia eneo hilo la maduka tangu Jumamosi iliyopita.

Ole Lenku alisema pia kuwa askari 10 wamejeruhiwa katika operesheni hiyo inayowahusisha maofisa wa Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad), wale wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI)Alisema askari waliojeruhiwa na raia wanatibiwa katika hospitali mbalimbali za Nairobi.

Magaidi wawili wauawaAlisema magaidi wawili waliuawa na vikosi vya usalama huku mapambano yakiendelea. Alisema waasi hao wamebanwa baada ya vikosi vya ulinzi na usalama kudhibiti sehemu kubwa ya jengo hilo. Magaidi hao wanaoaminika kuwa wafuasi wa kundi la Al-Shabaab la Somalia walivamia jengo hilo la ghorofa nne ambalo lina maduka ya kifahari na kuua, kujeruhi na kuwashikilia wengine mateka.


“Tumeua magaidi wawili na wengine kadhaa wamejeruhiwa, tutatoa taarifa nyingine baadaye. Hakuna gaidi hata mmoja ambaye ataondoka,” alisema Ole Lenku na kuongeza: “Ni labda wajisalimishe au wauawe.”

Alisema magaidi hao wamejaribu kuwasha moto katika duka la Nakumatt lililopo katika jengo hilo la Westgate ili kuvichanganya vikosi vya usalama lakini hawakufanikiwa kutokana na vikosi hivyo kuwa imara.

Ole Lenku alisema kazi ya kupambana na magaidi hao imechukua muda mrefu kutokana na vikosi vya usalama kufanya jitihada za kuokoa mateka ambao bado wanashikiliwa.

“Hadi sasa bado hatujui kuna mateka wangapi ndani ya jumba hilo,” alisema Ole Lenku.

Milio ya risasi iliendelea kurindima siku nzima ya jana ndani ya jengo hilo huku askari wengi wakiwa wamelizunguka.

AMERICAN MUSIC AWARDS FULL NOMINATIONS LIST 2013


MUANGALIE RIHANNA NA TATOO MPYA

DEREVA WA F1 AFARIKI DUNIA

$
0
0
Dereva mashuhuri mwanamke wa mashindano ya langalanga Formula 1 Maria De Villota amepatikana amefariki ndani ya chumba cha hoteli moja mjini Seville,Hispania.

Msemaji wa polisi alisema."Tunachukulia kilikua kifo cha kawaida,lakini hatuwezi kuthibitisha chochote na uchunguzi utafanywa kuhusu kifo chake"

De Villota (kulia), mwenye umri wa miaka 33,alikua dereva wa akiba wa langalanga. Alipofuka jicho lake la kulia katika ajali ya mwezi wa Julai mwaka jana alipokua akifanya mazoezi na timu ya Marussia.

Alipata majeraha mabaya kichwani na usoni baada ya kugongana na lorry katika jimbo la Cambridgeshire, Uingereza lakini aliruhusiwa kuanza tena kuendesha gari.

Iliarifiwa De Villota, binti wa dereva wa zamani wa mashindano ya Formula 1, Emilio De Villota,alikwenda Seville kuzindua kitabu kuhusu maisha yake.

Timu na madereva wa langalanga wameelezea kushtushwa kwao na msiba huo.

Jenson Button wa Uingereza amesema. "inasikitisha sana. Msichana huyu amekumbwa na masaibu mengi sana, kupita yale yanayowakumba watu wengi duniani. Ni habari zilizotushtuwa timu nzima na jamii nzima ya mbio za langalanga."

"tulimuona mwaka huu mjini Barcelona.Tukifanya kazi kwa wakfu wa kuwasaidia watoto na alikua wa kwanza kujitolea na kuwashawishi madereva wengi kujiunga nasi.Alikua akichangia mengi kwa jamii ."

BRAZIL KUKIPIGA NA ZAMBIA MUDA SI MREFU

$
0
0
Timu ya taifa ya Zambia, Chipolopolo ndani ya saa moja kutokea sasa wataingia uwanjani kucheza mechi ya kirafiki na timu ya taifa ya Brazil. Mechi hiyo ambayo ni muhimu kwa Zambia ikiwa ni mechi yao ya kwanza kucheza na Brazil ambao ni mabingwa mara tano wa kombe la dunia.

“Tunawaheshimu lakini hatuwaogopi” alisema mmoja wa wachezaji wa timu ya Chipolopolo ambao wako jijini Beijing kwaajili ya mechi hiyo, itakayochezwa saa saba kamili saa za Zambia ambayo ni sawa na saa moja usiku Beijing China, katika uwanja maarufu uliojengwa kama kiota cha ndege.

Huku Chipolopolo ikiwa imetolewa katima michuano ya maandalizi ya kombe la dunia mwaka 2014, Brazil itaingia uwanjani, ikiwa ni mechi muhimu pia kwa katika maandalizi ya michuano ya dunia.

Hata hivyo timu ya Zambia itaingia uwanjani huku wachezaji wake  6 wakishindwa kuhudhuria mechi hiyo kutokana na kuugua na majeraha mbalimbali.

Kwa mujibu wa mtandao wa Times of Zambia, wachezaji hao wanao umwa ni Rainford Kalaba, Stoppila Sunzu, Nathan Sinkala, Collins Mbesuma, Davies Nkausu na Mukuka Mulenga

Hata hivyo daktari wa timu ya Chipolopolo alikanisha kuwaruhusu wachezaji hao kusafiri huku wakiwa wagonjwa.

RIHANNA AONESHA JEURI YA PESA

$
0
0
MSANII wa muziki kutoka nchini Marekani Rihanna amethibitisha kuwa ni miongoni mwa wasanii wadogo waliopata mafanikio baada ya kumnunulia mama yake nyumba ya kifahari kwa dola za marekani milioni 22 ambayo ni sawa na bilioni 35 za kitanzania.

Rihanna amemnunulia mama yake jumba hilo la kifahari mjini Barbados ambapo msanii huyo ndipo alipozaliwa na kukulia ingawa hurudi nyumbani hapo kila mwisho wa mwaka kwa ajili ya kusherehekea sikukuu za Christimas na familia yake.


Mbali na hilo Rihanna ameandika historia nyingine baada ya kujazaa mashabiki wengi katika shoo yake aliyoifanya katika uwanja wa mpira wa miguu nchini Afrika Kusini.

Msanii huyo ambaye yupo nchini humo kwa ajili ya ziara ya shoo yake 'Diamonds World Tour' ambapo ameweza kuvunja rekodi kwa kuweza kuujaza uwanja huo wa mpira ambao hujaa katika mechi kubwa za mpira hasa za kimataifa.

Kwa mujibu wa mtandao wa Entertainment Wise ulidai kuwa tiketi zote za show hiyo zilimalizika na zaidi ya watu elfu 67 walihudhuria show hiyo uwanjani hapo, hali iliyopelekea msanii huyo mwenye umri wa miaka 25 kuwa wa kwanza kuujaza uwanja huo na tiketi zote kuisha.



GOSBY APATA SHAVU

$
0
0

MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini mkali wa 'King of Swaghili' Gosbert Kibanza 'Gosby' amekuwa msanii wa kwanza Afrika Mashariki kuingiza nyimbo yake katika mixtape ya Coast to Coast nchini Marekani.

Nyimbo ya msanii huyo  iliyoingia katika mixtape inajulikana kwa jina la BMS 'Baby Making Swag', ambapo msanii huyo aliweza kupokea email mwanzoni mwa wiki hii  iliyothibitisha kuingia kwa nyimbo hiyo.


Akizungumza na jarida hili kwa njia ya simu Gosby aliweka wazi kuwa amekuwa miongoni wa wasanii wanaotafuta nafasi za kuutangaza muziki nje ya nchi.

Aliweka wazi kuwa kilichomsaidia yeye ni kutafuta nafasi na kutumia mitandao mbalimbali ya kijamii ili aweze kuutangaza muziki wake ingawa pia ubora wa muziki, uliojaa ubunifu na kuchanganya lugha ya kiswahili na kingereza ndio kilichomsaidia nyimbo hiyo kuchaguliwa.

"Jamaa wa Coast to Coast waliiona nyimbo yangu kwenye mtandao mmoja wa nchini Marekani unaoitwa 'Rapgenius' ambayo huweka mashairi ya wasanii wa muziki wakubwa wa Marekani na duniani kwa sababu mimi ni msanii wa pekee Afrika Mashariki hivyo wao ilikuwa rahisi kunipa" alisema Gosby na kuongezea kuwa.

" Baada ya kunipata waliomba niweke nyimbo yangu hii ya BMS ili watu waipigie kura hali iliyopelekea nyimbo yangu kufanikiwa kuingia kwenye mixtape" alisema.

Pamoja na hayo msanii huyo hivi karibuni ameachia nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Monifere' aliowashirikisha baadhi ya wasanii wa hapa nchini akiwemo Vanessa Mdee.



Viewing all 3497 articles
Browse latest View live