Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

TONI BRAXTON AUMBUKA JUKWAANI

$
0
0
 MUIMBAJI Toni Braxton amejikuta katika wakati mgumu alipokuwa akitumbiza jukwaani baada ya nguo yake aliyekuwa amevaa kupata 'hitilafu' kuchanika na kumuacha wazi sehemu ya makalio kwa muda mrefu bila ya kugundua.

Hayo yalimtokea wakati akifanya onesho lake hivi karibuni huko New Jersy Marekani ambapo staa huyo
mkongwe anayetamba na nyimbo inayojulikana kwa jina la 'Unbreak my heart' aliendelea kuimba na kucheza mbele ya maelfu ya mashabiki waliohudhuria onyesho hilo bila ya kujua kama nguo yake aliyoivaa imechanika.


Muimbaji huyo alijikuta katika wakati mgumu baada ya kigauni chake kutereza upande wa nyuma na
kusababisha makalio yake kuonekana na nguo ya ndani aliyoivaa 'bikini' kuonekana.

Toni bila ya kujua kinachoendelea aliendelea kutoa burudani hiyo ingawa baadhi ya waimbaji wenzake
waliweza kungudua kuwa nguo ya muimbaji huyo imeachia lakini walishindwa jinsi ya kumsaidia.

Baada ya muda kidogo Toni aliweza kujua kuwa nguo yake imeachia ndipo alipoanza kutafuta njia ya kujiziba huku akiendelea kuimba lakini ilishindikana, ndipommoja wa shabiki wa kiume aliyepanda jukwaani hapo aliweza kumvalisha koti.

Muda mfupi baada ya kuvishwa koti msaidizi wake aliweza kumsaidia kuirekebisha nguo hiyo, huku mwanamuziki huyo akiendelea kuimba lakini wakati huo ilishindikana nguo hiyo kurekebishika ndipo alipokuja msaidizi wake wa kume kuivua nguo hiyo.Toni alilazimika kuendelea kuimba akiwa na koti alilopewa na shabiki wake baada ya nguo yakekushindwa kurekebishika.


KIONGOZI MKUU WA BROTHERHOOD AKAMATWA

$
0
0

KIONGOZI  mkuu wa vuguvugu la Muslim Brotherhood nchini Misri, Mohammed Badie amekamatwa na maafisa wa usalama kutoka makaazi yake eneo la Nasr 'City', Mjini Cairo. Badie aliwekewa kibali cha kumkamata kwa tuhuma za kuchochea ghasia na mauaji. Hali ya hatari imetangazwa Misri huku serikali ikiendelea kuwawinda wafuasi wa Brotherhood ambao wamepinga kuondolewa madarakani kwa Rais Mohammed Mosri.

Mohammed Badie amekua akiwaomba wafuasi wa Muslim Brotherhood kuandamana na kuweka kambi zao mjini Cairo. Hata hivyo alikwenda mafichoni tangu Julai 10. Jeshi lilivunja kambi hizo na watu wengi waliuawa na kujeruhiwa.Karibu watu 900 wameuawa wakiwemo mahabusu wa Brotherhood 37 ambao walifariki dunia wakipelekwa katika jela moja nje ya mji wa Cairo.Mamia ya wafuasi wa vuguvugu hilo akiwemo Naibu wake Badie, Khairat al-Shatir wamekamatwa tangu kuondolewa kwa Mohammed Mosri hapo Julai Tatu.

Kiongozi huyo anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea ghasia na mauaji ya raia wanane mahasimu wa Muslim Brotherhood.Kukamatwa kwa Badie kunajiri siku kadhaa baada ya mwanawe wa kiume Ammar kupigwa risasi na kuuawa katika maandamano yaliyofanyika medani ya Ramses.

Vuguvugu hilo limesema hatua ya kumkamata kiongozi wao hazitakandamiza wafuasi wake na kwamba mamilioni wataendelea kupinga mapinduzi dhidi ya utawala uliochaguliwa kidemokrasia.Mrengo wa Brotherhood wa kisiasa, mbacho ni chama cha Freedom And Justice umemtangaza Mahmoud Ezzat kuchukua nafasi ya kiongozi mkuu.

Ezzat ni Naibu mwenyekiti wa chama hicho. Wakati huo huo Misri imetangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufuatia mauaji ya maafisa 25 wa polisi katika Rasi la Sinai, hapo Jumatatu.

Wanamgambo wa kiisilamu wamelaumiwa kutekeleza mauaji hayo.Shambulio hilo lilifanyika katika mji wa Rafah ulioko mpaka na Ukanda wa Gaza.

MAAFISA 24 WA POLISI WAUWAWA MISRI

$
0
0

Takriban maafisa 24 wa polisi kutoka Misri wameuawa kwenye shambulizi la kuvizia katika eneo la Rasi la Sinai. Duru zinaarifu polisi hao walikuwa kwenye msafara wa mabasi mawili yaliyoshambuliwa na kundi la watu waliokua na silaha karibu na mji wa Rafa mpaka na Ukanda na Gaza.

Polisi watatu walijeruhiwa kwenye shambulio hilo. Katika siku za karibuni jeshi la Misri limeimarisha operesheni dhidi ya wanamgambo eneo la Sinai hususan baada ya mashambulizi kuongezeka tangu kuanguka kwa uliokua utawala wa Hosni Mubarak mwaka 2011.

Baadhi ya duru zinasema washambuliaji hao walitumia maroketi kulenga mabasi hayo. Utawala wa mpito umetangaza hali ya hatari kufuatia maandamano ya umma yaliofuatia kuondolewa mamlakani kwa Muhammed Morsi kama Rais wa nchi hiyo. Amri ya kutotoka nje usiku imewekwa mji mkuu Cairo.Misri imekua ikishika doria eneo la Sinai chini ya mkataba wa mwaka 1979 kati ya Israel na Misri.Mashirika ya habari yanaripoti kwamba wanaume wanne waliojihami kwa silaha walisimamisha mabasi hayo na kuwaamrisha abiria wote kuondoka kisha wakaanza kuwapiga risasi.

Zaidi ya watu 800 wakiwemo polisi 70 wameuawa tangu Jumatano ya wiki jana wakati jeshi lilipovunja kambi za wafuasi wa vuguvugu la Muslim Brotherhood anakotokea Morsi. Na hapo Jumapili mahabusu 36 walikufa wakati wakisafirishwa katika jela moja nje ya mji wa Cairo.Serikali na jeshi wamesema mahabusu hao walikosa hewa kwenye gari walimokua. Hata hivyo Muslim Brotherhood wametaja kitendo hicho kama mauaji ya kinyama.

Huku haya yakiarifiwa Muungano wa Ulaya umeitisha kikao cha dharura kujadili uhusiano wake na Misri. Muungano huo umetoa taarifa ya pamoja na kusisitiza haja ya kumaliza ghasia mara moja.Wafuasi wa Morsi wametaja kuondolewa kwake kama mapinduzi, lakini jeshi na serikali zinasema vuguvugu la Muslim Brotherhood liliendesha kampeini ya ugaidi tangu kuondolewa kwa kiongozi wake kama Rais.

MWANAMKE MWENYE NYWELE NDEFU DUNIANI

$
0
0

MWANAMKE anayetambulika kwa jina la Asha Mandela anaongoza kwa kuwa na rasta ndefu zaidi duniani zenye urefu wa futi 55.

Mwanamke huyo ambaye anadaiwa kuonywa na madakati juu ya urefu wa nywele zake unaweza kumsababishia tatizo la kupooza Asha amedai hawezi kuzikata nywele hizo.


Mama huyo aishiye Atlanta mwenye umri wa miaka 47 anayeweka rekodi ya kuwa na rasta ndefu duniani ameweka wazi humchukua siku mbili kuosha pamoja na kuzikausha nywele zake.

Katika moja ya mahojiano aliyowahi kufanya mwanamke huyo ameeleza kuwa nywele zake zimekuwa ni sehemu ya maisha yake na hatoweza kuzikata kwani akifanya hivyo ni sawa na kujiuua.

TAKWIMU ZA WALIOHUKUMIWA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0

SERIKALI imetoa takwimu za mahabusi waliohukumiwa kwa kesi ya dawa za kulevya ambapo takwimu hiyo inaonyesha jumla ya watu 10 wamehukumiwa kwa kipindi cha mwaka 2010,2012.

Hayo yamesemwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Assah Mwambene leo jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara hiyo.

Alisema kuwa jumla ya washitakiwa wanne walihukumiwa kifungo cha maisha jela Mahakama Kuu mkoani Mtwara baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na kilo nne za dawa za kulevya aina ya heroin Mwaka 2010.

Mwaka 2012 Mahakama Kuu Mkoani Tanga iliwahukumu washitakiwa 5 kifungo cha miaka 25 jela na kulipa faini ya TSh. 1,438,364,000/= kila mmoja baada ya kupatikana na hatia ya kusafirisha kilo 92.2 za dawa za kulevya aina ya heroin. Pamoja na hukumu hiyo, mahakama iliamuru utaifishaji wa magari mawili yaliyotumiwa kusafirisha dawa hizo.

Mwaka 2012 Mahakama Kuu ilitoa hukumu ya miaka 20 jela kwa mshtakiwa mmoja aliyekamatwa na kilo 3 za dawa za kulevya aina ya heroin mkoani Kilimanjaro.  Aliongezea kuwa “Kwa yeyote aliyekuwa anafikiria kufanya biashara ya dawa za kulevya ajue muda wake umekwisha” alisema Mwambene.

Mwambene alisema kuwa tatizo hili litakuwa historia kwani ulinzi umeimarishwa, hivyo ametoa rai kwamtu yeyote mwenye nia ya kufanya biashara hiyo aache mara moja. Mkurugenzi huyo alisisitiza kuwa Serikali imeweka jitihada kubwa ya kutoa elimu kwa watumiaji na waathirika wa dawa za kuelevya ili waweze kubadili tabia zao za kutumia dawa hizo na kuwa watu wema katika jamii.















UTENGENEZAJI VIDEO CRAZY MAN

$
0
0
 Kundi la TNG lipo katika hatua ya mwisho ya utengenezaji wa video ya wimbo wao unaojulikana kwa jina la 'crazy man'. Hizi ni baadhi ya picha zinazoonyesha wakiwa wanarekodi video hiyo.


KENYA YASAINI DOLA NA CHINA

$
0
0

Kenya imesaini mkataba na China ambao unatoa dola bilioni tano kuimarisha huduma za Reli,Kawi na Uhifadhi wa Wanyama Pori kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.Makubaliano hayo yaliafikiwa katika ziara ya Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta nchini China.

Hii ndio ziara ya kwanza ya Rais Kenyatta tangu kuchaguliwa hapo mwezi Machi mwaka huu.Serikali ya Kenya imepongeza mkataba huo na kusema utasaidia nchi kukua kiuchumi na kuboresha maisha ya raia wake.

Mwenyeji wa Kenyatta, Rais wa ChinaXi Jinping , ameelezea kuridhishwa kwake na juhudi za serikali ya Bw Kenyatta katika kuimarisha taifa la Kenya.

Uhusiano kati ya Uhuru Kenyatta na dola za magharibi umedorora kufuatia mashtaka dhidi yake katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita-ICC. Kenyatta anatarajiwa kwanza kesi dhidi yake baadaye mwaka huu.

Ametuhumiwa kwa kufadhili ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007, japo amekanusha madai hayo. Wakati wa kampeini za uchaguzi mkuu nchini Kenya Muungano wa Ulaya ukitishia kupuuza Kenyatta endapo angechaguliwa Rais.

Nayo Marekani ilionya Wakenya dhidi ya kuwachagua washukiwa wa dhuluma za kivita.Bw. Kenyatta amelaani dola za Magharibi kwa kile alichokitaja kama mwingilio wa masuala ya ndani ya nchi.

Mmoja wa miradi inayotarajiwa kuimarishwa ni huduma ya reli itakayounganisha bandari ya Mombasa na Mji wa Malaba ulioko mpaka na Uganda.China pia inatarajia kufadhili miradi ya kilimo, mbolea na teknolojia nchini Kenya.

BROTHERHOOD YALAANI KUKAMATWA KWA KIONGOZI WAKE

$
0
0

Vugu vugu la Muslim Brotherhood limelaani kukamatwa kwa kiongozi wake Mkuu Mohammed Badie, kwa tuhuma za kuchochea ghasia na mauaji.Msemaji wa kundi hilo amesema kukamatwa kwa kiongozi huyo ni njama ya kulipiza kisasi mapinduzi ya umma yaliyomuondoa madarakani Rais wa zamani Hosni Mubarak mwaka wa 2011. Badie alikamatwa na maafisa wa polisi kutoka makaazi yake karibu na kitovu cha maandamano ya wafuasi wa Brotherhood Mjini Cairo.

Bw ElBaradei aliondoka nchini Misri baada ya kujiuzulu kufuatia hatua ya jeshi kuvunja kambi za wapinzani na kusababisha maafa ya mamia ya watu.Utawala wa mpito umetangaza hali ya hatari nchini Misri na kumekua na operesheni kali dhidi ya wafuasi wa Rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Morsi.Jeshi la Misri lilivunja kambi hizo wiki jana ambapo kulitokea maafa ya raia wengi. Wakati huo huo Aliyekua Makamu wa Rais Mohamed ElBaradei anakabiliwa na mashtaka ya kusaliti imani ya taifa.

Hapo Jumanne Vugu vugu la Muslim Brotherhood limewaomba wafuasi wao kuendelea na maandamano kushinikiza jeshi imrejeshe madarakani Bw. Morsi. Kwenye mkutano na waandishi wa habari mmoja wa viongozi wa chama cha Justice And Freedom Party, mrengo wa kisiasa wa Brotherhood alisema kukamatwa kwa kiongozi wake hakutadidimiza harakati zao.

Naibu kiongozi wa vugu vugu hilo Mahmoud Ezzat ametangazwa kama kaimu kiongozi. Mohammed Badie amekua akiongoza maandamano ya wafuasi wa Bw Morsi. Hata hivyo aliingia mafichoni baada ya serikali kutangaza onyo la kuvunja kambi za waandamanaji.

Kiongozi huyo anakabiliwa na mashtaka ya kuchochea ghasia na mauaji ya raia wanane waliopinga Muslim Brotherhood. Mzozo wa kisiasa nchini Misri umepelekea mauaji ya watu 900 na maelfu kujeruhiwa.

Mauaji hayo yamepelekea laana za kimataifa, baadhi ya wafadhili wakitarajiwa kukutana Jumatano kuamua ikiwa watasitisha msaada kwa utawala wa Misri.

Wakati huo huo Misri imetangaza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufuatia mauaji ya maafisa 24 wa polisi katika Rasi ya Sinai. Wanamgambo wa kiisilamu wamelaumiwa kwa kutekeleza mauaji hayo.

TIKETI ZIMEANZA KUISHA KOMBE LA DUNIA BRAZIL

$
0
0

Shirikisho la soka duninai FIFA imesema kuwa zaidi ya tiketi milioni moja za kombe la dunia zimeombwa kupitia mtandao wake ndani ya saa saba pekee tangu zianze kuuzwa. Wengi walioagiza tiketi hizo ni mashabiki kutoka Brazil, Argentina, Marekani na Uingereza.

Mechi za ufunguzi tarehe 12 Juni na ile fainali ya uwanja wa Maracana ndizo zilizovutia mashabiki wengi zaidi. Halmashauri ya Utalii nchini Brazil imetoa wito kwa FIFA pamoja na wamiliki wa mahoteli nchini humo kupunguza bei za juu walizoweka wakisema kuwa inaharibia jina nchi hiyo.

Bei hizo zimepanda maradufu tangu matayarisho ya kombe la Dunia yashike kasi. Mashabiki wa soka wanaweza kuomba tiketi hizo kupitia mtandao wa FIFA hadi tarehe kumi Oktoba.

MAKAHABA WAOMBA ULINZI WAWEPO KAZINI

$
0
0
BAADA ya kugundua kuwa biashara ya ukahaba inalipa kwa upande wao, wanawake wanaojishughurisha na biashara hiyo nchini Kenya waomba watambuliwe na wapewe ulinzi wanapokuwa kazini ili na wao walipe kodi kwa serikali, hatua hiyo itachangia biashara hiyo kutambulika  rasmi.

Wanawake hao wametoa maombi hayo kupitia chama chao kinachojulikana kwa jina la Africa Sex Workers Alliance (ASWA) kinachopatikana nchini humo na kubainisha  kuwa biashara yao ni sekta ambayo inatoa fursa nzuri kwa nchi kujiendeleza kiuchumi.


Akizungumza kwa niaba ya viongozi wa Mkurugenzi wa chama hicho Doughtie Ogutu alisema chama hicho kilianzishwa kwa madhumuni ya kutetea maslahi ya wanachama ambao wamepitia mengi yakiwemo kupigwa kuuwawa na hata kulazimishwa kushiriki ngoni na wanyama.

"Tunataka watu watuangalie kama tunaweza kusaidia kukuza uchumi na wala si kuangalia kwamba tunaendeleza mmomonyoko wa maaadili" alisema.

Ingawa wanaamua kuendelea na biashara hiyo makahaba wanakiri kwamba biashara hiyo ni hatari hasa iwapo wanapata wateja wabaya .

Bi Ogutu alielezea kwamba anakumbuka miaka minane iliyopita mmoja wao alipopata mteja mzungu lakini akarejea akiwa maiti, tena mwanzoni mwaka huu wasichana wakakamatwa katika eneo la pwani wakiwa na mwanamume mwengine wa kigeni na kushtakiwa kwa kujihusisha na ngoni isiyostahili.

Kwa sasa chama hicho kinapanuka kutokana na kuwepo kwa mataifa kumi na kinaelekea magharibi na Afrika ya kati, lakini ushawishi nchini Kenya unakumbwa na changamoto nyingi.

MICHAEL SCOLFIELD AJITANGAZA KUWA SHOGA

$
0
0

MUIGIZAJI aliyejipatia umaarufu katika tamthilia ya 'Prison Break' Wentworth Miller maarufu kwa jina la 'Michael Scolfield' ameamua kujitangaza rasmi kuwa yeye ni shoga.

Muigizaji huyo ameamua kuweka wazi kitendo hicho baada ya kupokea barua ya mwaliko wa kuhudhuria tamasha la filamu la kimataifa lililotarajiwa kufanyika St. Petersburg nchini Urusi

Kwa mujibu wa taarifa iliyoandikwa kupitia mtandao wa 'People.com' imeweka wazi kuwa Scolfield amekataa mwaliko huyo wa kuitembelea nchi hiyo kutokana na sheria zao zinazowabana wanaume wanaojihusisha na ushoga.


Taarifa hiyo ilieleza kuwa baada ya muigizaji huyo kuipokea barua hiyo ya mwaliko ndipo alipoamua kuijibu kwa kuweka wazi kuwa kitendo cha nchi hiyo kuweka sheria ya kuwabana mashoga ndio sababu kubwa inayompelekea kushindwa kuhudhuria tamasha hilo.

"Nashukuru kwa mwaliko wenu, mimi nina asili kiasi ya Urusi ingenipa faraja sana kuitembelea nchi hiyo, lakini kutokana na sheria zenu mimi nikiwa kama shoga lazima niukatae mualiko huo" aliandika Scolfield na kuongezea kuwa."Ninaumiwa kwa kiasi kikubwa na jinsi mashoga wanavyotendewa na serikali hiyo".

Scolfield alieleza kuwa kutokana na sheria hiyo na jinsi serikali ya nchi hiyo inavyowachukulia mashoga hao hawezi kushiriki kwa amani kwenye tukio hilo lililoandaliwa na nchi inayowanyanyasa watu kama wao ikiwa pamoja na kuwanyima haki yao ya msingi ya kusihi.

Mwezi June nchi hiyo ilianzisha sheria dhidi ya ushoga iliyosainiwa na rais wa nchi hiyo Vladimir Putin ambayo imezua mijadala ya wazi jinsi sheria hiyo inavyokataza wapenzi wa jinsia moja.

Wentworth ni muigizaji aliyejipatia umaarufu kwenye tamthilia ya Prison Break mnamo mwaka 2005 hadi 2009, ingawa ameweza kushiriki pamoja na kuandaa filamu nyingine tofauti tofauti ikiwemo 'Stoker'.

UN YATAKA UCHUNGUZI SYRIA

$
0
0
Baraza la usalama la umoja wa mataifa limefanya kikao cha dharura kujadili madai kwamba wanajeshi wa serikali ya Syria wametumia silaha za kemikali pale walipofanya shambulio dhidi ya eneo lililopo nje kidogo ya mji mkuu wa Damascus hapo jana jumatano.

Wanaharakati wa upinzani wamesema kuwa mamia ya watu wakiwemo watoto wameuwawa huku muungano wa upinzani ukiyataja mauaji hayo ya halaiki. Serikali ya Syria imekanusha kwamba imetumia silaha hizo.

Mwenyekiti wa baraza la usalama, Maria Parceval, ambaye ni balozi wa Argentinean katika umoja wa mataifa amesema kuwa wanachama wa baraza hilo wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na madai hayo.

"Naweza kusema kuwa kuna wasiwasi mkubwa miongoni mwa wanachama wa baraza kuhusu madai hayo. Kuna hisia kwamba kuna haja ya kuwa wazi kuhusu kilichotokea na hali kufuatiliwa kwa makini,'' anasema Bi. Maria Parceval.

''Wanachama wote wanakubaliana kwamba matumizi yoyote ya silaha za kemikali, kwa yeyote katika mzozo huu, na katika mazingira yoyote ni ukiukaji wa sheria za kimataifa. Kulikuwa pia na makubaliano ya kutoa wito wa kusitishwa uhasama na vita.''

Kadhalika Bi. Perceval amesema kuwa kulikuwa na makubaliano kuhusu haja ya kuanzisha uchunguzi wa kina kuhusiana na swala hilo.

''Wanachama wa baraza la usalama wametaka katibu mkuu aingilie kati ili kuhakikisha kuwa uchunguzi wa haraka na wa kina usioegemea upande wowote unafanywa. Wanachama wa baraza wameelezea haja ya kutolewa mara moja msaada wa kibinadamu kwa waathiriwa. Hatimaye baraza la usalama limetoa rambi rambi kwa waathiriwa pamoja na familia zao,'' ameongeza kusema Bi. Maria Perceval, mwenyekiti wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa.

BAADA YA BOMOA BOMOA KURASINI KINACHOENDELEA

KUNDI LA PAGAD LAUA WATANZANIA 3, WAHUSISHWA NA DAWA ZA KULEVYA

$
0
0
Watanzania watatu wameuawa hivi karibuni jijini Cape Town, Afrika ya Kusini kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya. Watanzania hao walipigwa risasi na kundi la watu waliokuwa wameficha nyuso zao nje ya duka lijulikano kama Maisha Tuck Shop jumanne iliyopita katika barabara ya Veld, Athlone, Cape Town.

Watanzania wawili walifariki papo hapo na mmoja kufia hosipitali. Mtu mwingine, raia wa Afrika Kusini, alijeruhiwa vibaya katika shambulio hilo. Mmiliki wa duka la Maisha Tuck, Ashim Nassoro, alisema kuwa aliona kundi la watu wakiwa na bunduki za aina ya AK-47 na pistols wakipiga risasi nje ya duka lake.

Bw. Nassoro alidai waliouawa walikuwa marafiki zake, alisema yeye alikuwa nyumbani na mke wake na mtoto wake, ambapo ni karibu na duka hilo aliposikia milio ya risasi.


“Nilikuwa ndani na nilimwambia mke na mtoto wangu walale chini mpaka milio ya risasi iishe” alisema Nassoro na kuongeza “waliwapiga risasi watu waliokuwa ndani ya nyumba halafu wakaenda kwenye duka. Walipiga risasi watu wawili dukani, mmoja aliyekuwa kwenye geti na mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye nyumba.”

Nasroro aliongeza kuwa alikuwa anawajuwa Watanzania hao kwa sababu wote wanatoka Tanzania na wamekuwa wakiishi pamoja tokea walipowasili Cape Town miaka mitano iliyopita. Mtu mwingine aliyeshughudia tukio hilo alisema kuwa waliowauwa Watanzania hao walikuwa hawana wasiwasi na walirudi kwenye gari yao taratibu na kuondoka eneo la tukio.



Kufuatia tukio hilo, polisi ilimkamata Abdus Salaam Ebrahim ambaye ni kiongozi wa kikundi kinachopiga vita dhidi ya uhalifu na madawa ya kulevya nchini humo kinachojulikana kama People Against Gangsterism and Drugs (Pagad). Abdus Salaam Ebrahim amefikishwa mahakami leo kwa mashtaka ya mauaji.

Hata hivyo, mahakama imeyaondoa mashtaka hayo kwa muda kufuatia ombi la mwendesha mashtaka ili kuruhusu uchunguzi zaidi kufanyika. Wakati hakimu akiyandoa mashtaka hayo, wafuasi wa kikundi hicho cha Pagad waliokuwa wamejazana mahakamani hapo walishangilia huku wakisema “Allahu Akbar”. Majina ya Watanzania waliouawa hayakuwekwa kwenye charge sheet.

Pagad ni kikundi kilichoanziswa mwaka 1995 kupambana na uhalifu na madawa ya kulevya kwenye jiji la Cape Town baada baada ya juhudi za serikali kulegalega. Kampeni ya kikundi hiki ilianza mwaka 1996 baada kumkamata, kumpiga na kumchoma moto hadi kufa Rashaad Staggie ambaye alikuwa kiongozi wa kikundi cha uhalifu jijini Cape Town. Serikali ya Afrika Kusini ilishawahi kudai huko nyuma kuwa Pagad ni kikundi cha kigaidi baada ya kudaiwa kulipua kwa bomu hoteli ya Planet Hollywood mwaka 1998. Hata hivyo, Pagad ilipinga kuhusika kwenye shambulio hilo.

Kikundi hiki kilipotea lakini kikaja kuibuka tena kuanzia mwaka 2011 na kampeni yake ya kuchukua mitaa inayotawaliwa na uhalifu na biashara ya madawa ya kulevya. Wadadisi wa mambo wanadai kuwa kurudi tena kwa Pagad kwa gia ya kupambana na uhalifu, hasa madawa ya kulevya, itafanya hali kuwa mbaya hasa kwenye jimbo la Western Cape.

Hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la milipuko ya mabomu kwenye sehemu zinazouza magari na pia kwenye nyumba za makazi ya watu zilizopo Athlone na maeneo mengine jijini Cape Town. Matukio haya yamekuwa yakitokea zaidi kwenye nyuma za makazi zinazotuhumiwa kutumika kufanyia biashara ya madawa ya kulevya. Kikundi cha Pagad kimekanusha kujihusisha na matukio hayo.

AIRTEL YAGAWA VITABU

$
0
0

Airtel Tanzania imeendelea na mradi wake wa kusambaza vitabu katika shule ya Sekondari nchini chini ya mradi wa ‘Shule yetu’ ambapo shule mbalimbali za sekondari nchini zimenufaika na mradi.
Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi akimkabithi Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe bi Siberia Ruboha vitabu vya ada na kiada wakati Airtel ilipotembelea wilaya ya karagwe mkoani bukoba
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema kampuni ya Airtel inaendelea kukabiliana na changamoto katika sekta ya elimu nchini hasa tatizo la vitabu vya kiada kwa shule za sekondari.

Kupitia mradi wa ‘Shule yetu’ watoto wengi wa kike watanufaika kwani mradi huu unalenga hasa katika  kumkwamua mtoto wa kike kutoka katika ujinga, umaskini na maradhi,”
Afisa mauzo wa kanda ya ziwa Mohamed Kabeke akikabithi vitabu Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe  bi Siberia Ruboha wakati Airtel ilipotembelea wilaya ya karagwe mkoani bukoba, akishuhudia ni  Meneja Mahusiano ya Kijamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi
Hawa aliongeza kwa kusema Leo tunatoa msaada wa vitabu kwa shule ya sekondari ya Bwelanyake hapa Karagwe Bukoba ikiwa ni mwendelezo wa shughuli zetu za kijamii katika kupambana na tatizo la vitabu mashuleni. Vitabu hivi vitawawezesha wanafunzi wa shule ya Bwelanyake kupata nafasi ya kujifunza na kujisomea na kuwawezesha walimu kupata nyenzo muhimu za kufundishia.

Kwa upande wake Afisa elimu msaidizi sekondari wilaya ya karagwe  bi Siberia Ruboha alisema “elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo tunawashukuru sana Airtel kwa kushirikiana na Serikali kupunguza tatizo la vitabu vya kiada vya shule za sekondari hapa nchini. 

Tunaamini msaada huu wa vitabu tulioupata leo utasaidia katika kuinua kiwango cha ufaulu na kuongeza taaluma zaidi kwa wanafunzi wetu na kuongeza idadi ya wanafunzi wa masomo ya sayansi hapa shuleni. 

Nachukua fursa hii kuwaomba wanafunzi wavitumie fursa hii kujisomea na wavitunze vitabu hivi ili viweze kutumika na wanafunzi wengi zaidi na kutoa matunda bora na mengi zaidi.

Mpaka sasa Airtel kupitia mradi huo imewafikia shule takribani  900 za sekondari nchi nzima kwa kuzipatia vitabu vya kiada hasa kwenye masomo ya Fizikia, Hisabati, kemia na Biolojia. mradi huu wa Shule yetu unasambaza vitabu kwa shule za sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne pamoja na vitabu vya  walimu kwa ajili ya kufundishia.

WAKENYA WAMUUA AFISA MSAAFU WA JESHI KWA MAPANGA

$
0
0

"Alisaidia kuendesha mbuga za Kenya wakati mtoto wa mfalme Prince William alipomchumbia mpenzi wake Kate Middleton"
           
Imeripotiwa kuwa aliyekuwa afisa wa jeshi la Uingereza ameuwawa kwa shambulizi baada ya kundi la watu wasiojulikana kumvamia nyumbani kwake Kenya.

Luteni Kanali David Parkinson, 58(pichani kushoto akiwa na mkewe), aliuawa kwa kukatwa katwa kwa mapanga baada ya kuvamiwa na majambazi ambao pia walikuwa na bunduki walipovunja nyumba mapema jana(jumapili) asubuhi.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Telegraph, mkewe alifanikiwa kutoroka na kujifungia stoo mpaka kundi hilo lilipoondoka. Mama huyo alipotoka stoo ndipo alimkuta mumewe amefariki.

Wawili hao walikutwa jumbani lao eneo la miinuko ya Loldaiga eneo la Nanyuki, Laikipia nchini Kenya.
Kabla ya kuhamia katika eneo hilo, Parkinson aliyekuwa mwanajeshi katika kikosi cha parashuti kwa miaka 30, alisaidia kuendesha mbuga ambayo Duke wa Cambridge na Kate Middleton walipochumbiana, gazeti hilo limeripoti.
Inadaiwa kuwa Parkinson aliteuliwa kuwa kaimu mkurugenzi wa hifadhi ya mbuga ya Lewa baada ya kustaafu kama mwanajeshi.

SOMA ZAIDI . . .
Prince William alitembelea mbuga hizo mwaka 2005 kabla ya kurudi na Kate mwaka mara nyingine tena mwaka 2010 alipomchumbia mpenzi wake wakiwa eneo hilo.

Msemaji wa mtoto wa mfalme wa Uingereza alisema wamwesikitishwa sana kwa kifo cha Parkinson, ambaye walikutana katika mbuga hizo.
Polisi wa Kenya wamedai majambazi hayo yaliondoka na kompyuta (laptop), simu pamoja na vito vya thamani.

Msemaji wa polisi eneo hilo, Bw. Marius Tum aliwaambia waandishi wa habari, “Mkewe ambaye alikuwa amefungwa alifanikiwa kuwatoroka na kujificha kwenye stoo, na baadae kurudi na kukuta mumewe akiwa na majeraha ya kutisha”
Alisema uchunguzi wa mwili wa marehemu utafanywa ilikutambua chanzo cha kifo hicho. Mshukiwa mmoja amekamatwa katika kijiji kilichopo karibu na eneo hilo kufuatia msako mkali uliofanywa na polisi wakishirikiana na mbwa wanaotambua harufu.

Ofisi ya Mambo ya Nje imedhibitisha kifo cha Parkinson.

“Tunafahamu kuhusiana na kifo chake na tuko tayari kutoa ushirikiano na kusaidia familia yake katika kipindi hiki kigumu” alisema msemaji wa Ofisi hiyo.


MAJANGA: DRIVE-IN YA NGONO IMEANZA RASMI

$
0
0


“Jiji limehalalisha na kufungua vyumba 9 ambavyo vitatumiwa na machangudoa na wateja wao kihalali na kwa usalama zaidi”

Drive-in ya ngono imefunguliwa rasmi, Zurich katika mkakati wa kuwalinda makahaba ili kuhamisha biashara ya umalaya nje ya mji wa Swiss.
Vibanda(pichani kulia) tisa vya ngono vilivyojificha ndani ya uzio mkubwa vimeandalikwa kwaajili ya wauza miili ‘malaya’ na wateja wao kuanzia leo na kuendelea.
Kuna saini ndogo inayoonesha muda wa kazi, mwamvuli mwekundu kutambulisha eneo hilo kama eneo la shughuli hiyo ambalo zamani lilikuwa ni eneo la viwanda magharibi mwa jiji hilo.
Pamoja na hayo kuna sharia maalumu zimewekwa(kushoto pichani). Mteja lazima awe na umri usiopungua miaka 18, mtu mmoja tu kwenye gari, na kondom lazma itupwe kwenye vyombo maalumu baada ya kutumika.
Kuna eneo ambalo mteja anaweza kuchagua mwanamke anayemfaa, pamoja na makubaliano ya bei kabla ya kuelekea kwenye kibanda, ambacho ni cha mbao kinacho fanana na eneo la kuegesha gari.
Kila kiboksi kina alamu ili kuwalinda Malaya hao.
Michael Herzig, mkurugenzi katika huduma ya jamii ya wafanyakazi wa ngono jijini alisema “Umalaya ni biashara “
“Hatuwezi kuzuia, hivyo tunataka kudhibiti ili kuwasaidia wafanyakazi wa ngono na jamii, sababu bila kufanya hivyo uhalifu unaongezeka na wahuni wanazidi kuwa wengi”

Ursula Kocher, Mkurugenzi wa Flora Dora, mtandao unaounga mkono Malaya, alisema kuwa machangu doa mara nyingi huchukuliwa na kupelekwa kwenye porini au nje ya mji na kujikuta katika mazingira hatari.
Alisema “ hapa wanabakia humuhumu ndani na kuhudumia wateja wao haraka”
Eneo hilo la drive-in ya ngono limehalalishwa na wakazi wa Zurich katika sharia ya mwezi machi, 2012baada ya kupigiwa kura kwa asilimia 52.6 kukubaliana nalo.
Eneo hilo pia lina makubaliano mazuri tu yanayohusisha vyama vyote vya siasa nchini humo, likiwa na wanachama wengi wa chama cha Swiss People's Party (SVP) wanaopinga mpango huo.
"haitofanikiwa, labda kwasababu wateja hawatokuja au eneo hilo halitotumiwa na machangudoa” alisema Sven Oliver Dogwiler, mwanasiasa wa eneo hilo ambae ni mwanachama wa SVP.

KESI YA BO XILAI IMEKWISHA

$
0
0
Upande wa mashtaka katika kesi ya mwanasiasa mashuhuri nchini Uchina Bo Xilai, umetoa taarifa yake ya mwisho dhidi ya kiongozi huyo ambaye awali alitarajiwa na wengi kuchukua uongozi wa taifa hilo.

Katika taarifa hiyo, waendesha mashtaka wamesema kuwa kiongozi huyo wa zamani hafai kupewa hukumu hafifu kutokana na uzito wa mashtaka yanayomkabili ya ufisadi na utumizi mbaya wa mamlaka.

Bo Xilai sasa ana fursa ya kuzungumzia kuhusu shinikizo za kisiasa mbali na kuwakosoa wapinzani wake.

Mwandishi wa BBC anasema kwamba licha ya kuwa kulikuwa na uwazi wakati wa kusikilizwa kwa keshi hiyo, kesi hiyo bado inadhibitiwa na chama cha Kikomunisti.

MAPIGANO TENA GOMA

$
0
0
Mapigano mapya yamezuka mwishoni mwa juma katika eneo la Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo ripoti zinasema watu watatu walifariki baada ya makombora kurushwa katika maeneo ya makaazi ya watu.

Haijulikani ni nani aliyerusha makombora hayo lakini wanainchi wameandamana wakililaumu jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa MONUSCO kwa kile wanachodai limewashambulia waasi katika juhudi za kuwatimua kwenye eneo hilo.

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamewalaumu waasi kwa kurusha makombora hayo lakini hakuna kundi lolote la waasi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo.

Afrika Kusini, ambayo imechangia kikosi hicho cha kulinda amani, imekiri kuwa mwanajeshi wake mmoja amejeruhiwa katika mlipuko huo wa bomu.

Akizungumza kwa simu na BBC, Msemaji wa jeshi la Afrika Kusini, Brigedia Generali Kolani Mabanga, amesema mwanajeshi wake mmoja alijeruhiwa vibaya na kwa sasa anaendelea kupata matibabu huku mipango ya kumrejesha nyumbani kwa matibabu zaidi ikiendelea.

Hali ya ulinzi imeimarisha katika eneo hilo lakini wakaazi wa mji huo na viunga vyake wanasema hali bado ni ya wasi wasi.

WOTE KUKAGULIWA KASORO RAIS, MAKAMU, PM, JAJI MKUU NA SPIKA

$
0
0
Kuanzia sasa viongozi wote serikalini watakaopita kwenye viwanja vya ndege nchini, watakuwa wakikaguliwa kama abiria wengine, isipokuwa Rais, Makamu wake, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge.

Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe(Kulia pichani) amesema ipo tabia ya viongozi wenye madaraka, kukiuka utaratibu na kupita katika viwanja vya ndege bila kukaguliwa.

Alisema kutokana na hali hiyo, amewaambia watumishi wanaofanya kazi katika viwanja hivyo, hususan Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) viongozi wasiokaguliwa ni Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na Spika wa Bunge.

Alitoa msimamo huo wiki iliyopita kupitia kipindi cha Jenerali on Monday, kinachorushwa na Televisheni ya Channel Ten. Alisema viongozi wengine wote, wakiwamo mabalozi na mawaziri lazima wakaguliwe.

Dk Mwakyembe alisema aliwaambia viongozi wasiopenda kukaguliwa, wasipande ndege. Alisema pamoja na 
baadhi kuona ni usumbufu, inawezekana wakajikuta wamesahau vitu hatari, kama vile risasi na wakaenda kugundulika nje ya nchi ikawa tatizo.

Alitoa mfano kwamba aliwahi kupigiwa simu na mmoja wa mabalozi, akilalamika kwamba vijana wake wamemkagua uwanja wa ndege.

Alisema alimjibu kwamba wanatimiza wajibu wao. Katika mahojiano yaliyojikita juu ya tatizo la dawa za kulevya nchini, Dk Mwakyembe alisisitiza kwamba hatua alizoanza kuchukua kudhibiti upitishaji dawa hizo kwenye viwanja vya ndege, siyo moto wa kifuu wala nguvu ya soda.

“Ninachokifanya hapa ni kile ambacho kinapaswa kufanywa… na hili la dawa za kulevya katika viwanja vya ndege, nitalikomesha,” alisema. Alisisitiza kwamba udhibiti huo ni kwa viwanja vyote vya ndege nchini. Dk Mwakyembe alisema, “kwa sasa mizigo yote inayoingia katika eneo hilo, lazima ikaguliwe, kwani huo sio mzaha, sio moto wa kifuu wala nguvu ya soda.”

Kwa mujibu wa Waziri, mizigo inayoingia imekuwa haikaguliwi. Alisema katika kutekeleza ukaguzi huo wa mizigo inayoingia, imenunuliwa mitambo kwa ajili hiyo.
Kuhusu wanaomeza dawa za kulevya, alisema wamekuwa wakigundulika kutokana na ufuatiliaji kuanzia kwenye ndege. Alitoa mfano kwamba kwa sasa endapo abiria atapanda ndege katika uwanja wa ndege wa Dar es Salaam, mathalani kwenda Dubai, akipewa chai au pombe, akakataa kunywa, kwa vyovyote huyo lazima akaguliwe zaidi.

Katika hilo, aliwaasa vijana wa Tanzania kujiepusha na hali hiyo, kwani pindi akishuka kwenye uwanja wowote, namba yake ya kiti itashikiliwa na atakaguliwa ipasavyo, kubaini kama amemeza dawa.

Hatua ya Mwakyembe kuamua kuvalia njuga dawa za kulevya, inatokana na kile ambacho kinaelezwa kuwa ni kuchafuka kwa Tanzania, kutokana na baadhi ya watanzania kukamatwa nje ya nchi, wakisafirisha dawa hizo, wakiwa wamezipitisha uwanja wa ndege.

Dk Mwakyembe alieleza kuwa hatua yake ya kuvalia njuga suala hilo, inaungwa mkono na serikali kwa ujumla. Hivi karibuni waziri huyo alifanya ziara ya ghafla katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere na kubaini kuwa tatizo si vifaa vya ukaguzi, bali ni baadhi ya wafanyakazi wasio waadilifu.

Msemaji Mkuu wa Serikali ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema hivi karibuni serikali imeanzisha mkakati wa kutokomeza wimbi la dawa za kulevya kwa kudhibiti viwanja vya ndege na sehemu mbalimbali za mipakani, zinazotumiwa kupitisha.

Viewing all 3497 articles
Browse latest View live