Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

PSPF YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA JESHI LA MAGEREZA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0





Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimkabidhi seemu ya vifaa vya michezo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, Agosti 25, 2016. Vifaa hovyo ni vya michezo ya ngumi, mpira wa miguu na mpira wa pete.

Afisa Masoko wa PSPF, Magira Werema, (kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.


NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umekabidhi vifaa vya michezo kwa wanamichezo wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam na kasha kufuatiwa na PSPF bonanza la michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Ngumi na Judo.

Akikabidhi vifaa hivyo vya michezo Agosti 25, 2016, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, alisema, PSPF imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua michezo nchini.


“Nyinyi mkiwa kama sehemu kubwa ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, tunayo furaha kutoa vifaa hivi vya michezo kwani baada ya kutekeleza majukumu mazito ya kitaifa mnahitaji kushiriki michezo ili kujenga afya lakini pia kuinua vipaji vyenu,” alisema na kuongeza,

“Nichukue fursa hii kuwahamasisha mjiunge na PSPF kwani kuna faida nyingi mtapata kutokana na kutoa mafao mbalimbali yatakayoboresha maisha yenu kama ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema, PSPF ni chaguo lako sahihi na kamwe hutajutia uamuzi wako wa kujiunga na Mfuko huu.” Alisisitiza Njaidi.

Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya wanamichezo hao, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza-Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, aliishukuru PSPF kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwani vitawawezesha wanamichezo hao kushiriki michezo katika mazingira bora ya kiuanamichezo.

Baada ya makabidhiano hayo, wanamichezo hao walionyesha uwezo wao katika michezo ya mpira wa miguu, ngumi, mpira wa pete, na judo.
Afisa Matekelezo (Compliance), wa PSPF, George Mnasizu, (kushoto), akigawa vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na Mfuko huo kwa baadhi ya wanamichezo wa Jeshi la Magereza
Njaidi akiwa na Mkuu wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kikosi Maalum cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Rajabu Nyange Bakari, na wacheza judo wa kikosi hicho wakiwa katika picha ya pamoja na vipeperushi vya PSPF.
Njaidi akimkabidhi sehemu ya vifaa hicho, Nahodha wa timu ya mpira wa pete (Netball), wa timu ya Magereza Ukonga, Pili Enzi
Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo kocha wa soka wa timu ya Magereza, Sajenti Hassan Mulego
 Njaidi akikagua timu ya soka ya Magereza Ukonga, ambayo ilimenyana na Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, wakati wa bonanza hilo la michezo
  Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
  Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
  Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza
 Hizi ndio Gloves na flana zilizotolewa kwa wana masumbwi (ngumi)
 Pambano la masumbwi likiendelea
  Pambano la masumbwi likiendelea
 Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akiwa na Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, wakati akitoa nasaha kwa wanamichezo kabla ya kuanza kwa bonanza hilo
Nasaha za mgeni rasmi kwa wanamichezo
 Wanamichezo wakishangilia hotuba
 Onyesho la Judo
 Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo, Kocha na Afisa Michezo wa Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, Inspekta Francis Tabu
 Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza


Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.

MAKABIDHIANO YA UWANJA WA UHURU-DAR ES SALAAM

KANISA LA EAGT LUMALA MPYA, MWANZA KUFANYA HARAMBEE YA UJENZI WA KANISA JIPYA

$
0
0

Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, chini ya Mchungaji kiongozi, Dkt.Daniel Moses Kulola, linapenda kuwakaribisha watu wote kwenye Harambee ya Ujenzi wa Kanisa jipya na la kisasa linalotarajiwa kujengwa katika viwanja vya kanisa hilo.

Harambee hiyo inatarajiwa kufanyika kesho jumapili Agosti 28,2016 kanisani hapo ambapo watu wote wakiwemo waumini na viongozi wa Madhehebu mbalimbali, Viongozi wa Serikali na Taasisi binafsi, wanakaribishwa ili kuungana na viongozi na waumini wa Kanisa hilo katika kushiriki kwenye harambee hiyo.

Kumbuka "Bwana Hufurahi Anapojengewa Hekalu Lenye Kufana" hivyo utabarikiwa ikiwa utashiriki katika harambee hiyo. Kwa mawasiliano zaidi, tumia nambari za simu; 076774 90 40 AU 0787 74 90 40.

WAFANYAKAZI WA NMB TAWI LA NELSON MANDELA WASHIRIKI ZOEZI LA USAFI MJINI MOSHI LEO

$
0
0

Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa wamebeba vifaa kwa ajili ya kufanya usafi katika eneo la njia mbili maarufu kama Double Road mjini Moshi leo.

Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakivuka barabara tayari kuanza zoezi la kufanya usafi katika eneo la Double Road mjini Moshi leo.





Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakifanya usafi katika maeneo ya maduka yaliyopo eneo la Double Road mjini Moshi.







Meneja wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi Emanuel Kishosha akiowaongoza wafanyakazi wenzake katika zoezi la kufanya usafi .





Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi wakiokota taka zilizokusanywa wakati wa zoezi la usafi lilofanyika katika eneo la Double Road mjini Moshi.







Wafanyakazi wa NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiwa na taka zilizokusanywa wakienda kuzitupa katika eneo la kusanyia takataka.



Wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Nelson Mandela mjini Moshi wakiendelea na usafi katikati ya barabara .



Meneja wa NMB tawi la Neslon Mandela Emanuel Kishosha akiwa amebeba taka mara baada ya kumaliza kuzikusanya wakati wa zoezi hilo la usafi.



Hivi ndivyo yalivyooonekana maeneo ambayo wafanyakazi wa Benki ya NMB tawi la Moshi walishiriki kuyafanyia usafi mjini Moshi hii leo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

RAIS MAGUFULI AHUDHURIA MISA YA MIAKA 50 YA NDOA YA RAIS MSTAAFU MKAPA NA MKEWE

$
0
0

Rais Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe wakati akiwasili kuhudhuria Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


"Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiingia kanisani tayari kwa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


"Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiingia kanisani tayari kwa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiwa tayari kwa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa na wageni waalikwa akiwemo Rais Dkt John Pombe Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


MC Mavunde akipiga kinanda wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Sehemu ya waumini na wageni waalikwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Sehemu ya waumini na wageni waalikwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Sehemu ya waumini na wageni waalikwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Sehemu ya waumini na wageni waalikwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Sehemu ya waumini na wageni waalikwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Sehemu ya waumini na wageni waalikwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Sehemu ya waumini na wageni waalikwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Sehemu ya waumini na wageni waalikwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Wanakwaya katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Kiongozi wa kwaya katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Sehemu ya wanafamilia wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Bw. Nicholaus Mkapa, mtoto wa Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa akisoma somo la kwanza katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongea na wana familia, waumini na wageni waalikwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa hiyo katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Rais Dkt Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli, Mama Maria Nyerere, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na waumini na wageni waalikwa wakiwa katika Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akimvisha pete Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akivishwa pete na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakifurahia jambo baada ya zoezi hilo


Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe akitoa neno kwa "maharusi" hao wenye furaha


Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe akitoa neno kwa "maharusi" . Kulia ni Balozi Anthony Nyaki aliyesimamia harusi yao siku kama ya leo miaka 50 iliyopita. Matron alikuwa Marehemu Lucy Lameck.


"Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wanaketi baada ya ukumbusho wa viapo vya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016


Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akiongea na kadamnasi


Rais Dkt Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli, Mama Maria Nyerere, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na waumini na wageni wakiendelea na misa


Mawaziri wakuu wastaafu walikuwepo. Kutoka kushoto ni Jaji Joseph Sinde Warioba na mkewe Evelyn Warioba. Mzee Cleopa Msuya, Mama Amne Salim na mumewe Dkt. Salim Ahmed Salim na Mhe Edward Lowasssa na mkewe mama Regina Lowassa


Sir Andy Chande akiungana na waalikwa katika misa hiyo


Mohamed Dewji na mkewe wakiwa katika misa hiyo


Mstari wa mbele


Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndg Philip Mangula na mkewe pamoja na wageni wengine


Mawaziri wakuu wastaafu walikuwepo. Kutoka kushoto ni Jaji Joseph Sinde Warioba na mkewe Evelyn Warioba. Mzee Cleopa Msuya, Mama Amne Salim na mumewe Dkt. Salim Ahmed Salim na Mhe Edward Lowasssa na mkewe mama Regina Lowassa


Katibu Mkuu Kiongozi Eng. John Kijazi, Maspika wastafu Mzee Pius Msekwa na Mama Anne makinda na Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue


Sehemu ya waalikwa


Jaji Mkuu mstaafu Mhe. Barnabas Samatta na mkewe pamoja na waalikwa wengine


Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Mhe. Marten Lumbanga na mkewe pamoja na Waziri mstaafu Profesa Philemon Sarungi na mkewe Mama Sarungi


Waalikwa


Wageni waalikwa


Waalikwa


Sehemu ya waalikwa


Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiongoza wana familia kupeleka matolea altereni


Kwaya


Sehemu ya waalikwa


Waalikwa


Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongoza misa


Misa ikiendelea


Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu akiongoza misa


Misa ikendelea


Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mama Anna Mkapa


Mama Janeth Magufuli na Mama Maria Nyerere wakiwatakia amani Mzee Mkapa na Mama Anna Mkapa


Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mhe. Edward Lowassa


Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea hati malumu ya ndoa kutoka Vatican kwa Baba Mtakatifu Papa Francis kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo

DC MTATURU AWATAKA WANANCHI WALIOVAMIA ENEO LA HIFADHI KUHAMA NDANI YA MWEZI MMOJA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akisikiliza Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere Beatus Kapatya akitoa taarifa juu ya kusimama kwa ujenzi wa Zahanati hiyo.
Baadhi ya wananchi wakimsikiliza kwa Makini Mkuu wa Wilaya ya ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri wakati akitoa maelezo wakati wa kikao cha serikali ya kijiji

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mhe Miraji Jumanne Mtaturu akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali wakati wa ziara yake Wilayani humo
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kaugere Beatus Kapatya akitoa ufafanuzi mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu
Umakini wa wananchi ukiwa umetawala wakati wa Mkutano wa Kijiji, Wilayani ikungi

Na Mathias Canal, Singida

Serikali ilitangaza eneo la Hifadhi ya msitu wa wananchi waliomo ndani mwaka 2003 ambao kutangazwa huko kuliashiria wananchi kuhama katika maeneo hayo ili kutoa fursa kwa serikali kusimamia kwa karibu eneo hilo lakini wananchi hao mpaka sasa hawajahama kwa kukaidi agizo hilo.

Jambo hili limemsukuma Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu kufanya ziara na kuzungumza na wananchi wa maeneo hayo kwa lengo la kuwaelemisha juu ya uvunjaji sheria za nchi kwa kuendelea kusalia katika maeneo ambao wametakiwa kuhama jambo ambalo kama watashindwa kulitekeleza serikali itawatoa kwa nguvu kwani kwa kiasi kikubwa wanaharibu mazingira.

Akizungumza na Wananchi hao katika Kijiji cha Kaugeri Kata ya Mwaru Wilayani hapa Dc Mtaturu ametoa mwezi mmoja kwa wananchi hao kuhama haraka iwezekanavyo ili kupisha eneo hilo la Hifadhi ya msitu kufanya Kazi iliyokusudiwa kwa zaidi ya miaka kumi sasa.

Mtaturu amesema kuwa Kwa mujibu wa sheria Kijiji kinapaswa kutoa Ardhi hekari zisizozidi hamsini kwa mwekezaji lakini uongozi wa Kijiji hicho umegawa kwa mwekezaji hekta 150 hadi 200 kinyume kabisa na taratibu za kiutendaji ukiwa ni pamoja na kuingia mikataba ya kinyonyaji.

Pamoja na hayo pia viongozi hao wametoa Ardhi hiyo bila kushirikisha wananchi jambo ambalo limeibua hisia Kali kwa wananchi ambao wanatambua uporwaji huo wa maeneo yao.

Kufuatia kadhia hiyo ya viongozi hao kugawaji Ardhi kinyume na taratibu Dc Mtaturu amewaweka lumande Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaugeri Mange Nkuba, Aliyekuwa Kaimu Afisa Mtendaji Laurent Bomba, na mjumbe wa serikali ya Kijiji Paul Kilo huku Amani Clement ambaye alitoweka kabla Ya mkutano kumalizika anaendelea kutafutwa mpaka apatikane.

Katika hatua nyingine Dc Mtaturu ameagiza mkandarasi Samwel John kukamatwa na kuhojiwa kwa kushindwa kukamilisha ujenzi wa zahanati ya kijiji tangu Mwaka 2013 ambapo tayari alishapewa kitita cha shilingi milioni 19 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.

Hata hivyo pamoja na mkandarasi kukabidhiwa fedha hizo alianza ujenzi lakini jengo hilo halijafika hata kwenye Renta huku likiwa limejengwa chini kiwango.

Sambamba na hayo pia Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi amemuagiza mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya hiyo kupitia idara ya ujenzi kutoa taarifa kwanini hawakushiriki kutoa huduma za kiutaalamu katika kusimamia jengo hilo la umma kabla na wakati ujenzi unaanza.

RC SINGIDA AKABIDHI MADAWATI 630 KWA WAKURUGENZI WA WILAYA NA MANISPAA

$
0
0
Na Mathias Canal, Singida

Wakurugenzi wa Manispaa na Halmashauri za Mkoa wa Singida wamekabidhiwa jumla ya madawati 90 kwa kila Halmashauri ili kuondoa adha waliyokuwa wanakumbana nayo wanafunzi wa shule za msingi na sekondari Mkoani humo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono kampeni ya kuchangia madawati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli alipowaagiza wakuu wa mikoa yote nchini wakati akiwaapisha Ikulu, jijini Dar es Salaam Machi 15, 2016.

Wakurugenzi hao wametakiwa kuyachukua haraka madawati hayo na kuyapeleka Katika shule zenye kadhia hiyo ikiwa ni ishara ya kuamsha taswira ya elimu kwa wanafunzi mchini kuondokana na mateso ya kukaa chini wakiwa darasani.

 Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe wakati wa makabidhiano hayo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkoa huo huku akisifu wadau na Taasisi mbalimbali kujitolea kuunga mkono uchangiaji wa madawati ambao awali ulianza kwa ngazi ya Halmashauri kabla ya kuhusisha taasisi mbalimba sambamba na wadau wa maendeleo Mkoani humo.
Mtigumwe amesema kuwaHali ya Madawati katika Mkoa ilikuwa chini ya asilimia 40% lakini chini ya uongozi wake kwa kushirikiana na wadau 67 wa Maendeleo wameweza kuchangia jumla ya shilingi milioni 42,626,500 hivyo kufanikisha lengo la utengenezaji wa madawati kufikia asilimia 98% ambapo hata hivyo upungufu Mkubwa ulikuwa zaidi katika Halmashauri za Singida na Manyoni.


Alisema kuwa mwanzoni mwa mwezi June mwaka huu aliteua kamati ndogo ya uratibu wa madawati kwa kushirikisha wadau mbalimbali katika Mkoa baada ya kuona juhudi za serikali kupitia mamlaka za Halmashauri yaManispaa na Wilaya.

Ameeleza kuwa kamati hiyo iliweza kukusanya Jumla ya shilingi milioni 42,626,500/= kutoka kwa wadau 67 (Pesa taslimu ikiwa ni 29,046,500) wadau watano walitoa madawato 60 yenye thamani ya shilingi 3,580,000/= na madawati 100 kutoka bonite Bottles Ltd yenye thamaniya shilingi 10,000,000/= ambapo jumla ya madawati yaliyotengenezwa ilikuwa ni 470.
 Akisoma Taarifa ya utengenezaji wa madawati Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye ni Afisa Mifugo wa mkoa wa Singida Elias Donaty Seng’ongo amesema kuwa kupitia kamati ya kuratibu madawati walishirikisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na Taasisi za serikali (TBA,Gispa, Tanroads, Sido, Veta, Temesa, Sekretarieti ya Mkoa (RS), Takukuru na TRA, Mashirika ya huduma (NHC, Tanesco, Suwasa, Posta, Taasisi za fedha (NMB, na CRDB), Mifuko ya hifadhi ya jamii (NHIF, NSSF, na PSPF), Mashirika yasiyo ya serikali (NGO’s, SEMA, HAPA, TUNAJALI, na HELVETAS).
Amewataja wadau wengine waliochangia kuwa ni Vyuo vya idara za serikali (NAO, Madini, Hazina Ndogo, Chuo cha Uhasibu, TIA, Utumishi wa Umma, Chuo cha walimu Singida, Abet English Medium School, Maasai English medium  School, Lake School, Viwanda vya usagishaji mafuta (Mount Meru na Umoja wa wakamuaji mafuta Mkoa wa Singida, Wafanyabiasharambalimbali, wauzaji wa vinywaji baridi) Bonite Bottles Ltd, Wauzaji wa vipuri vya magari, Makandarasi, Wakala wa huduma za misitu TFSAmaduka ya vifaa vya ujenzi, Hoteli na Baba na Mama Lishe Mkoani humo.
Seng’ongo alisema kuwakupitia taarifa kutoka Ofisi ya Elimu Mkoa uliweza kufikia lengo la utengenezaji wa madawati kwa asilimia 98% ambapo juhudi bado zinaendelea kuhakikisha kuwa zoezi hilo linakuwa endelevu kwa siku zijazo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Rustika Turuka akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wakurugenzi wote wa Halmashauri za mkoa wa Singida amewashukuru wadau wote waliochangia fedha Taslimu ama Madawati yakiwa tayari yametengenezwa huku akiwasihi wadau wote kuendelee kujitolea katika kuchangia shughuli za maendeleo katika Mkoa huo.

Pia amesema kuwa madwati hayo ana imani yatatunzwa vizuri ili wanafunzi waweze kusoma vizuri wakiwa wamekaa kwenye madawati kwani mwanafunzi akiketi kwenye dawati hata mwandiko na ufahamu wake unakuwa mzuri tofauti na mwanafunzi ambaye atasoma akiwa amekaa sakafuni hivyo kupitia upatikanaji wa madawati hayo ana imani kubwa kuwa mkoa wa singida utaimarika kielimu na kuimarisha ufaulu wa wanafunzi.
Naye Mfanyabiashara, Mkulima na Mfugaji ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Hassan Tati akizungumza kwa niaba ya wadau wote waliochangia amesema kuwa Mkuu wa mkoa wa Singida Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amebuni njia nzuri ya kuwapa motisha kwa kutoa Hati kwa wadau wote waliochangia jambo ambalo litaamsha ari zaidi katika kuchangia shughuli za Maendeleo ya Mkoa na taifakwa ujumla.
  Tati alisema kuwa anasikitika sana pale anaposikia kuwa mkoa wa Singida unashika nafasi ya Tano kwa umasikini katika Mikoa yote nchini ilihali ni mkoa wenye rutuba ya kutosha na eneo pana katika uwekezaji hivyo amewasihi wananchi na wadau kwa pamoja kushirikiana kwa pamoja katika kukomesha umasikini huo.


SHUKRANI ZA FAMILIA YA MAREHEMU MOHAMED MTATURU MKONONGO

$
0
0

Marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongoenzi za uhai wake
 
Familia ya marehemu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo na mkewe Bi. Naiz Edriss Mavura pamoja na familia ya Mama Amina Mtaturu, Mheshimiwa DC Miraji Jumanne Mtaturu na Mzee Salum Chima; tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wote kwa upendo na faraja mliyowapatia na kwa kushiriki kwenu kikamilifu katika kufanikisha maziko ya mpendwa wetu, Ndugu Mohamed Jumanne Mtaturu Mkonongo (pichani), ambaye aliitwa na Mungu alhamisi, 21 Julai 2016 saa 1:40 asubuhi, kwa ajali ya gari.


Familia inapenda kuwashukuru kipekee Wakwe wa marehemu - familia ya Mzee Edriss Mavura; Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Huria, Prof Elifas T. Bisanda pamoja na uongozi wa chuo na wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT);

Uongozi na wafanyakazi wote wa Shirika la Afya duniani (WHO) Uganda na Tanzania; Dr Harvinder Palaha wa Aga Khan Hospital, na madaktari wenzie, wauguzi na wafanyakazi wote wa Aga Khan Hospitali kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU);

Mzee wetu Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi na familia yake; Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi; Ubalozi wa Uturuki nchini Tanzania na Bw. Ziya Kaharan, Balozi wa Heshima wa Tanzania nchini Uturuki; Prof. Fatmahan Atalar, Mkurugenzi wa MUHAS Genetic Laboratory ya Chuo Kikuu cha Muhimbili; Wanajumuiya wa Ikungi Development Association (IDEA); Umoja wa Wanafunzi waliosoma Uturuki, Masheikh wa Dar es Salaam na Ikungi; na Majirani wote wa Dar es Salaam na Singida.

Kwa kuwa si rahisi kumshukuru mtu mmoja mmoja, tunaomba wote mlioguswa na msiba huu mpokee shukrani zetu za dhati.

Tunapenda kuwataarifu kuwa Dua ya arobaini (40) ya marehemu itasomwa Jumamosi, tarehe 03 Septemba 2016, Makiungu-Ikungi, Singida, saa 5 asubuhi Wote mnakaribishwa.






INNA LILLAHI WA INNA ILLAHI RAJIUUN


DC NDEJEMBI AJIONEA KITUO CHA AFYA KILICHOJENGWA CHINI YA KIWANGO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wananchi waliofika kupatiwa huduma ya afya


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Kituo cha afya Mlali


DcNdejembi alipotembelea wodi wa wagojwa
Dc Ndejembi akisisitiza jambo kabla ya kuondoka katika kituo cha afya Mlali

Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma Mhe Deogratius Ndejembi amezuru katika kituo cha Afya cha Mlali kilichopo Katika Kata ya Mlali Wilayani humo kusikiliza kero wanazokumbana nazo wakati wanapofika hospitalini kupatiwa tiba.

Huu ni muendelezo wa ziara za kusikiliza kero za wananchi nakuzitatua kwa dhamira ya kupunguza na kuziondoa kabisa kero ndogo ndogo ambazo zimesababishwa na wananchi wenyewe ama watendaji wa serikali katika maeneo yote ya Wilaya hususani sekta ya Afya.

Mara baada ya kuwasili katika kituo hicho cha Afya alitembelea maeneo mbalimbali yakiwemo majengo mbalimbali, wodi, na Jengo la Upasuaji ambalo wameshindwa kulitumia kwa kutokana na kujengwa chini ya kiwango huku likiwa na eneo Dogo kiasi cha kupelekea kushindwa kuweka vitanda vya kutosha kwa ajili ya wagonjwa.

Licha ya jengo hilo kujengwa chini ya kiwango chini ya usimamizi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa kabla ya Mkuu huyo wa Wilaya kuteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kuhudumu katika Wilaya hiyo.

Hata hivyo kufuatia kadhia hiyo Mhe Ndejembi ameagiza Mkandarasi kutafutwa haraka iwezekanavyo ili aweze kuhakikisha jengo hilo linarekebiswa upwa kwa kutumia gharama zake mwenyewe.

Dc Ndejembi amemtaka mganga mkuu wa Kituo cha afya Mlali  kuhakikisha anasimamia vyema Mali na majengo ya umma ili kuendelea kutoa huduma nzuri na zenye ufanisi kwa kila Mtanzania anayefika katika Zahanati hiyo.

Kwa upande wa wananchi waliofika kupatiwa huduma kutoka katika Kijiji cha Mlale na maeneo Jirani wamesema kuwa huduma zinazotolewa katika Kituo hicho cha Afya zina ahueni kubwa huku changamoto kubwa ikiwa ni uduni katika huduma za chanjo kwa watoto kwani hawapati huduma hiyo kwa wakati.

Sambamba na hayo Dc Ndejembi ameagiza kusimamiwa haraka na kutatuliwa kwa kadhia hiyo ili wananchi wafurahie huduma bora zitolewazo katika vituo vya Afya sawia na kuimarisha Afya zao ili kufanya Kazi kwa salama na kuitikia dhana ya HapaKaziTu kwa vitendo.

TANZANIA YAFANIKIWA KUPUNGUZA IDADI YA WAGONJWA WA TRAKOMA

$
0
0
Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara hiyo Dkt. Magreth Muhando akizungumza kwa niaba ya Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwenye ufunguzi wa Mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya Trakoma unaofanyika jijini Arusha.
Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Upendo John Mwingira akizungumza wakati wa mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya Trakoma unaofanyika jijini Arusha.


Na. Aron Msigwa - ARUSHA.

Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Trakoma (Vikope) kufuatia kupungua kwa idadi ya wagonjwa na maeneo yaliyokuwa yakipata dawa za kutibu ugonjwa huo chini ya Kampeni ya utoaji wa dawa kwa watu wengi (Mass Drug Administration) iliyoanzishwa mwaka 1999.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwenye ufunguzi wa Mkutano wa pili wa mwaka wa nchi 7 za Afrika Mashariki zilizo katika mapambano dhidi ya Trakoma unaofanyika jijini Arusha, Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara hiyo Dkt. Magreth Muhando amesema Tanzania imepata mafanikio hayo kutokana na juhudi kubwa zilizofanywa na Serikali na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Sasa hivi wilaya 22 tumeziacha kati ya 56 zilizokuwa zikipata dawa chini ya mpango wa kutoa dawa kwa watu wengi ulioanza mwaka 1999, hii kutokana na kupata mafanikio mazuri na tunategemea kupata mafanikio zaidi kwa kuendelea kuzipunguza zilizobaki Amesema.

Ameeleza kuwa kupungua kwa idadi ya wagonjwa Trakoma nchini Tanzania mwaka hadi mwaka kunatokana na juhudi za Serikali na wadau kupitia afua mbalimbali chini mpango ujulikanao kama SAFE unaohusisha huduma za Upasuaji, utoaji wa dawa za Antibayotiki mapema, kampeni ya kuhamasisha wananchi kuosha uso pamoja na uzingatiaji wa usafi wa mazingira.

Dkt. Muhando amebainisha kuwa Trakoma umekuwa chanzo cha upofu na umasikini pale mgonjwa anapochelewa kutibiwa mapema na kusisitiza kuwa lengo la nchi hizo kukutana nchini Tanzania ni kuweka mkakati wa pamoja wa ushirikiano juu ya namna bora ya kudhibiti maabukizi ya ugonjwa huo kutoka sehemu moja hadi nyingine kutokana sababu za kijiografia na mwingiliano wa watu kutoka nchi moja moja hadi nyingine hali inayoweza kuchangia kusambaza ugonjwa huo.

Amesisitiza kuwa bado watanzania wanalojukumu la kuhakikisha ugonjwa huo unatoweka katika maeneo yao kwa kuzingatia na kufuata kanuni za afya, kufanya usafi wa mwili hususan uso kila siku kwa maji safi na sabuni pamoja na kufanya usafi wa mazingira ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.

Tumeona ni muhimu nchi hizi saba za Tanzania, Kenya, Eritera, Sudani, Sudani ya Kusini, Uganda na Ethiopia kushirikiana kikamilifu katika mpango wa kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa vikope kwa sababu watu wa nchi hizi hutembeleana kutoka sehemu moja hadi nyingine, tusipokuwa na njia mahususi za pamoja za udhibiti ugonjwa huu unaweza kuendelea kusambaa” Amesisitiza.

Ameongeza kuwa kazi inayofanywa sasa na nchi hizo ni kuendelea kutoa elimu hasa kwenye maeneo ambayo yana madhara ya ugonjwa huo kuielimisha jamii kutambua kuwa tatizo hilo lipo na jamii zinazoishi kwenye halmashauri zenye matatizo hayo kuendelea kupewa elimu dhidi ya kinga pia kuwahimiza wananchi kuzingatia usafi kama njia pekee ya kujikinga na ugonjwa huo, kuhakikisha tiba ya ugonjwa huo inapatikana pamoja na kuwaelimisha wale waliopata madhara ya ugonjwa huo ambao wanatakiwa kufanyiwa upasuaji kuwa tayari kwa tiba hiyo.

Dkt. Muhando amewashukuru wadau mbalimbali wa maendeleo kwa kuendelea kutambua mchango wa Tanzania katika mapambano dhidi ya magonjwa yasiyopewa kipaumbele pamoja na kutimiza malengo ya kidunia ambayo yanatoa wito kwa Tanzania kuwa imeondoa ugonjwa huo ifikapo mwaka 2020.

Aidha, amezitaja baadhi ya changamoto zinazoikabili kampeni ya kuwafikia wale walioathirika katika maeneo yenye maambukizi ya ugonjwa huo kuwa ni pamoja na maeneo ya jamii za wafugaji kuwa katoka mwingiliano mkubwa kutokana na sababu za mazingira hali inayohitaji nguvu kubwa za udhibiti baina ya nchi husika.

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya kupambana na Trakoma (International Trachoma Initiative) Dkt. Paul Emerson akizungumza katika Mkutano huo ameipongeza Tanzania kwa kazi nzuri inayofanya ya kuhakikisha ugonjwa wa Trakoma unatokomezwa.
Amesema kuwa yeye kama Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya Kupambana na Trakoma (ITI) amefurahishwa na na kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto ya Tanzania pamoja na juhudi za kuendelea kuwaelimisha wananchi na kutoa tiba katika maeneo yanakabiliwa na ugonjwa huo.

Aidha, amesema katika bara la Afrika maeneo ambayo yana vita na mapigano bado yanakabiliwa na kiwango kikubwa cha maabukizi ya ugonjwa huo huku akizitaja nchi za Ethiopia, Sudani ya Kusini, Sudan, Uganda na Kenya kuwa miongozni mwa nchi za bara hilo zenye idadi kubwa ya wagonjwa wa Trakoma.

Kwa upande wake Mratibu wa Taifa wa Magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Upendo John Mwingira akizungumza wakati wa mkutano huo amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za Bara la Afrika ambazo zimepata mafanikio katika utokomezaji wa ugonjwa wa Trakoma tangu kuanza kwa mpango maalumu wa kupambana na ugonjwa huo mwaka 1999. 

Amesema ugonjwa wa Trakoma/Vikope nchini Tanzania kwa mujibu wa Takwimu uko katika wilaya 56 na kueleza kuwa juhudi ambazo zimekuwa zikichukuliwa na Serikali kukabiliana nao hali iliyochangia maabukizi mapya kudhibitiwa katika wilaya 22 ambako wananchi hawahitaji tena dawa.

Amewatoa hofu wananchi kuhusu matibabu ya Trakoma kwa kuwaomba wale ambao kope zao zimeathirika kujitokeza ili waweze kufanyiwa huduma ya upasuaji ambayo inamuwezesha mgonjwa kurudi katika hali yake ya kawaida.

Natoa wito kwa wagonjwa wajitokeze wasiogope, ni jambo linalofanyika kwa utaalamu wa hali ya juu na mtu akifanyiwa urekebishaji wa kope anarudi na kuweza kuona kama kawaida
Aidha amesema kuwa licha ya halmashauri nyingi za Tanzania kipata mafanikio katika kudhibiti hali ya maambukizi ya ugonjwa huo bado maeneo ya jamii za wafugaji hasa wilaya za Longido, Monduli na Ngorongoro bado zina maambukizi hali inayohitaji ushirikiano wa udhibiti wa tatizo hilo kati ya Tanzania na Kenya.

Kwenye mafanikio huwezi kukosa changamoto, Tanzania maambukizi yamepungua halmashauri nyingi kiwango cha maambukizi kimepungua isipokuwa kwenye jamii zile za wafugaji wa jamii ya maasai kwenye wilaya tatu za Longido, Monduli na Ngorongoro ambapo tunahitaji juhudi za pamoja kati yetu na Kenya kwa kuwa kuna mwingiliano mkubwa baina ya watu wa maeneo haya na ndiyo maana tumekutana Amesisitiza. 

Kuhusu hali ya maambukizi ameyataja maeneo yenye ukame na yale yenye shida ya maji yaliyo mkoa wa Manyara na Dodoma kuwa bado yanakabiliwa na tatizo hilo na kuongeza baadhiya maeneo ya Arusha , Manyara, Dodoma katika wilaya ya Kongwa, Chemba na Chamwino yanahitaji huduma ya dawa.


Kuhusu takwimu za hali ya maambukizi nchini amesema kuwa takribani watu 160,000 wameambukizwa huo na kubainisha kwamba kupitia mikakati mbalimbali ya Wizara na wadau mbalimbali wameweza kuendesha huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wenye tatizo hilo 80,000.
Washiriki wa mkutano huo kutoka nchi 7 za Bara la Afrika wakiwa katika picha ya pamoja.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Kimataifa ya kupambana na Trakoma (International Trachoma Initiative) Dkt. Paul Emerson akizungumza katika Mkutano huo  ambapo ameipongeza Tanzania kwa kazi nzuri inayofanya ya kuhakikisha ugonjwa wa Trakoma unatokomezwa.


MWANDISHI SIMON KIVAMWO ANAHITAJI DAMU KUOKOA MAISHA YAKE, SHIMYE WANAHABARI NA WADAU

$
0
0

Bw. Simon Kivamwo

Waandishi wa habariwakitoa damu ili kuwezeshamatibabu ya Mwandishi wa habari mkongwe hapa nchini Bw. Simon Kivamwo ambaye anapatiwa matibabu kwenye hospitali ya Ocean Raod iluyoko jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016. Kwa mujibu wa Mwandishi wa Habari anayeratibu zoezi hilo Bw.Thompson, Kivamwo ambaye anaugua kwa muda mrefu sasa, amezidiwa na maradhi leo hii na kukimbizwa kwenye hospitali hiyo ambapo madaktari walihitaji kumuongezea damu. Benjamin Thomspon ametoa wito kwa wanahabari na jamii kwa ujumla kujitokeza kumchangia damu mwanidhi mwenzetu ili kuokoa maisha yake. Sehemu ya kutolea damu ni Hospitali ya Mnazi Mmoja, Kariakoo jijini Dar es Salaam




TAMKO LA TEF KUHUSU KUFUNGWA VITUO VYA REDIO 5 NA MAGIC FM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA OMR MBABANE- SWAZILAND

$
0
0

 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika -SADC- ambaye pia ni Rais wa Botswana Luteni Jenerali Dokta SERETSE KHAMA IAN KHAMA amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta John Pombe Magufuli kwa kuchaguliwa kwake kwa kishindo katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana.

Rais huyo wa Botswana ametoa kauli hiyo ya pongezi katika hotuba yake kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 36 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC unaofanyika Mbabane- Swaziland ambapo Katika Mkutano huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dakta JOHN POMBE MAGUFULI anawakilishwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MHE. SAMIA SULUHU HASSAN.

Rais huyo wa Botswana amesema ukuaji wa demokrasia katika nchi wanachama wa jumuiya ya SADC unaendelea kuimarika hivyo ni muhimu jitihada hizo zikaendelezwa zaidi.

Amesema ana Imani  kubwa na Viongozi waliochaguliwa kwa njia ya amani,uhuru  na haki katika ukanda wa SADC akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Visiwa shelisheli kwamba watafanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo kwa wananchi wao.


Wakuu wa nchi na Serikali wa SADC katika mkutano huo wameshuhudia utoaji wa zawadi mbalimbali kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika utunzi wa insha na kwa wanahabari ambao wameandika habari mbalimbali kuhusu SADC ikiwemo masuala ya huduma ya maji.

Aidha Katika Mkutano huo wa 36 wa SADC viongozi wanaohudhuria watafanya uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama ( SADC Troika)

Katika mkutano huo Wakuu wa nchi na serikali pia watapokea rasimu za maboresho ya mikataba mbalimbali kutoka kwenye Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kutia saini. Miongoni mwa rasimu hizo ni mkataba wa kuboresha itifaki ya SADC dhidi ya rushwa, maboresho ya itifaki ya ushirikiano wa siasa, ulinzi na usalama ya SADC na maboresho ya itifaki ya biashara.

*    Imetolewa na
*    Ofisi ya Makamu wa Rais
*    Mbabane- Swaziland
*    30-Aug-16

TANESCO KUBORESHA KITUO KIKUU CHA KUPOZA NA KUSAMBAZA UMEME CHA ILALA

$
0
0





NA K-VIS MEDIA

SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), linapenda kuuarifu umma kuwa kutakuwepo na katizo la umeme KUANZIA Septemba 3, 2016 kwenye maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam kutokana na kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza cha Msongo wa Kilovolti 132 cha Ubungo-Ilala.


Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano ya Shirika hilo, Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016, katizo hilo la umeme litaanza rasmi Septemba 3 na umeme utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na kurejea saa 11 jioni kwa utaratibu na tarehe kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11, Septemba 17-18, na Septemba 24-25, 2016.

Taarifa hiyo imetaja maeneo yatakayoathirika na zoezi hilo kuwa ni pamoja na eneo lote la katikati ya jiji (City centre), Maeneoyote ya Upanga, maeneo yote ya Kariakoo, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya Mbagala, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya Ilala, Maeneo yote ya Chang’ombe, Maeneo ya Temeke, Uwanja wa Taifa, Unilever, Makao Makuu ya Puma, Temesa, Jamana printers, Quality Plaza, Notco, Bima ya Afya, Bandari Gate pamoja na maeneo ya jirani.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa ili jiji la Dar es Salaam lipate umeme ulio bora na wa uhakika, Shirika laUmeem Tanzania (TANESCO), limemruhusu mkandarasi, (TAKAOKA), kubadilisha vikombe na nyaya na kuweka nyaya zenye uwezo mkubwa za njia mbili (Two-lines) za Msongo wa Kilovolti 132.


Kuboresha vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Ilala na Ubungo kwa kuweka nyaya zenye uwezo mkubwa zaidi. Kubadilisha vifaa vya kupima umeme kwenye njia mbili (Two-lines) za Ubungo-Ilala.

MAONESHO YA BASHARA YA AFRIKA MASHARIKI YAFUNGULIWA RASMI JIJINI MWANZA

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Massale, hii leo akifungua Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.

Maonesho hayo yameandaliwa na Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo nchini TCCIA, yalianza Agosti 26,2016 na yanatarajiwa kufikia tamati Septemba 04,2016 katika viwanja wa Rock City Mall.

Na BMG
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Dkt.Leonard Massale, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.

Wafanyabiashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wamehimizwa kuchangamkia fursa za kibiashara na uwekezaji zilizopo katika soko la pamoja la nchi hizo kutokana na soko hilo kuwa na idadi kubwa ya wateja.

Akifungua maonesho ya 11 ya biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika kwenye viwanja vya Rock City Mall jijini Mwanza,Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela amesema soko lililopo kwenye nchi hizo lina zaidi ya wateja milioni 140 na hivyo likitumika vizuri litatoa fursa ya kuuziana bidhaa wenyewe kwa wenyewe.

Kwenye hotuba ya ufunguzi iliyosomwa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Dkt.Leonard Massale,mkuu huyo wa mkoa amesema badala ya wafanyabiashara hao kutegemea masoko ya nje yanayofikika kwa gharama kubwa,wanapaswa kuuziana bidhaa ndani ya nchi za Afrika Mashariki na hivyo kuinua uchumi wa nchi hizo.

Aidha amewahimiza waandaaji wa maonesho hayo chemba ya wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo nchini, TCCIA, kuyatangaza zaidi ili yavutie makampuni mengi kutoka nchi zingine.

Katika hotuba yake Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Elibariki Mmari, amesema licha ya kuandaa maonesho hayo kwa miaka 11 mfululizo bado wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na eneo linalofaa kwa ajili ya maonesho hayo na hivyo kulazimika kuhama mara kwa mara na kuiomba serikali kuharakisha upimaji wa eneo la maonesho Nyamuhongolo ili kujenga majengo ya kudumu.

Maonesho ya mwaka huu yanashirikisha zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Kenya, Uganda, China na wenyeji Tanzania ambapo kuna mabanda ya bidhaa mbalimbali pamoja na wanyama hai.
 
Mwenyekiti wa TCCIA mkoa wa Mwanza, Elibariki Mmari, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa TCCIA mkoani Mara, akizungumza kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika Jijini Mwanza.
Picha ya pamoja.

Bonyeza HAPA Kujua Zaidi

IKUNGI HALF MARATHON 2016 KUANZA KURINDIMA WILAYANI IKUNGI JUMAMOSI WIKI HII

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akielezea dhamira ya kuanzishwa kwa Ikungi Half Marathon ofisini kwake

Na Mathias Canal, Singida

Ni kama vile kuwa na kiu kizito kinachohitaji maji ya kunywa na kisha maji yakakutikana kusikojulikana, ndivyo itakavyokuwa Wilayani Ikungi Mkoani Singida mara baada ya kutangazwa mashindano ya riadha yanayojulikana kama Ikungi Half Marathon 2016.

Mashindano hayo yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi siku ya Jumamosi Septemba 3, 2016 katika Vijiji 101 vilivyopo Wilayani Ikungi.
Akizungumzia dhamira ya kuanzishwa kwa mashindano hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa itakuwa ni kuibua vipaji kwa vijana na kuviendeleza, Kujenga umoja na mshikamano miongoni mwa vijana na kuwaandaa vijana katika Wilaya hiyo kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa.

Alisema kuwa Mashindano ya mbio ndefu yenye umbali wa kilomita 21 yatahusisha vijana wenye umri wa kuanzia miaka 17 hadi 30 waishio Wilayani Ikungi na yatafanyika kila mwaka ili kuinua hamasa ya Mchezo wa riadha huku yakiambatana na mbio fupi za mita 100, mita 200, mita 400 na mita 800.

Mashindano hayo yataanzia katika ngazi ya Vijiji Septemba 3, 2016, ngazi ya Kata itakuwa ni Octoba Mosi, Ngazi ya Tarafa ni Octoba 15, 2016 na kwa ngazi ya Wilaya itakuwa ni Octoba 29, 2016.

Dc Mtaturu alisema kuwa kuanzishwa kwa kuzinduliwa kwa mashindano hayo ni katika kuhakikisha Wilaya ya Ikungi inaibua changamoto katika sekta ya michezo nchini hivyo hiyo ni fursa muhimu kwa washiriki kujitokeza ili kuonyesha uwezo wao katika kusakata riadha.

Mtaturu alisema kuwa mwaka 2017 panapo majaaliwa wamejipanga kufanya mashindano ya Ikungi Marathon yatakayohusisha mbio ndefu za kilomita 42 ambapo jambo hili itakuwa ni kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Ameeleza kuwa mashindano hayo pia yamedhamiria kuitambulisha Wilaya hiyo Kitaifa na Kimataifa kupitia shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo michezo mbalimbali hususani mashindano ya Riadha.

Aidha amewaomba vijana wote wenye umri uliofikia miaka 17 kujitokeza kwa wingi katika mashindano hayo ili kuimarisha afya zao na kuachana na mawazo ovu yakiwemo yale ya kujihusisha na wizi na ujambazi, Ngono zembe pamoja na ubakaji.

Kwa upande wake Afisa michezo Wilayani Ikungi Abubakary Kisuda alisema kuwa mashindano ya ngazi ya Vijiji yatafanyika kwa lengo la kupata vijana watakaoshindana ili kushiriki mashindano ya ngazi ya Kata, ambapo mashindano ya Kata yatafanyika kwa lengo la kupata vijana watakaoshindana ili kushiriki mashindano ya ngazi ya Tarafa.

Kisuda alisema kuwa hili ni tukio la awali kabisa kuanzishwa Wilayani humo tangu kuanzishwa kwa Halmashauri ya Wilaya hiyo miaka mitatu iliyopita hivyo litaibua hisia chanya na kuigwa na Taifa zima.

YALIOJIRI MKUTANO WA NCHI ZA JUMUIYA YA MADOLA KANDA YA AFRIKA NCHINI MAURITIUS

$
0
0
Viongozi Wakuu pamoja na Sekretieti ya Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya ufunguzi wake, katikati mwenye suti Waziri Mkuu wa Mauritius Sir Anerood Jugnauth.
Ujumbe wa Tanzania walioshiki Mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid katikati kulia Mwenyekiti wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Mussa Zungu na kushoto Dk Raphael Chegeni.Kutoka kushoto Maryam Rajab, Mbarikiwa Masinga, Mhe,Maria (MB) Mhe. Raphael Chegeni (MB)Mhe Juma Hamad Omar (MB) Mhe Simai Mohammed Said (BLW) Aziza Makwai.  
 Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akibadilishana mawazo na Wajumbe kutoka Tanzania kabla ya kuaza kwa Mkutano huo.

Mjumbe wa Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Simai Mohammed Said, akiwasilisha Mada wakati wa Mkutano huo inayozungumzia Suala la Nishati kwa Bara la Afrika, uliofanyika nchini Mauritius Balaclava.
Spika wa Baraza la Wawkilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid akiwa na Wajumbe kutoka Tanzania wakishirika katika Mkutano huo wakifuatilia Mada zinazowasilishwa na Wajumbe wakati wa Mkutano huo nchini Mauritius.
Mtoto wa Mfalme wa Lesotho HRH Prince Seeiso B Seeiso, Raisi wa Senate na Mwenyekiti wa Kamati ya Biashara kutoka Bunge la Falme ya nchi ya Lesotho akichangia mada iliyowasilishwa na Tanzania inayohusiana na nishati ya umeme.
Mjumbe wa Sekterieti kutoka Tanzania Aziza Mwakwai kushoto akimsaidia Spika wa Rwanda wakati wa Kikao hicho za kuwasilisha Mada kwa Nchi husika.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said wakipitia makabrasha yao kabla ya kuaza Kikao cha Kanda ya Afrika Mashariki. katika ukumbi wa Hoteli ya Meridian Mauritius
Mjumbe wa Mkutano wa Nchi za Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Mhe. Simai Mohammed Said akizungumza na Spika wa Bunge la Mauritius na Rais wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola Kanda ya Afrika Hon Mrs.Santi Bai Hanoomanjee. kulia kwake Katibu wa Bunge la Mauritius.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid kutoka kulia akiwa katika picha ya pamoja na Spika wa Kenya Mhe.Justin Muturi, Spika wa Uganda Mhe Rebecca Kadaga na Mwenyekiti wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Zungu akimwakilisha Spika wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Job Ndungai.
Spika la Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zuberi Ali Maulid (katikati) akifurahia jambo wakati wakibadilishana mawazo na Wajumbe wa Mkutano huo, kushoto Spika wa Bunge la Uganda Mhe. Rebecca Kadaga na Mhe Simai Mohammed Said Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu Zanzibar, wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano baada ya kuahirishwa kwa mapumziko ya mchana.
Katibu wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano la Tanzania ambaye pia Katibu wa Nchi za Jumuiya ya Madola Dk Thomas Kashillilah wa tatu kutoka kulia mwenye suti, akizungumza na Wajumbe wa Sekterieti ya Jumuiya ya Kanda ya Afrika wakiwa nje ya Ukumbi wa Mkutano huo uliofanyika Nchini Mauritius.
Mwakilishi kutoka Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano huo, pamoja na Spika wa Bunge la Kenya Mhe Justin Muturi mwenye kaunda suti pamoja wa Wawakilishi kutoka Kisiwa cha Rodrigues Mauritius.
Waziri wa Afya kutoka Nchini Botswana Hon Dorcas Makgato akiwa na Mjumbe kutoka Tanzania Zanzibar Mhe Simai Mohammed Said wakiwa katika picha ya pamoja ya kumbukumbu.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe Zuberi Ali Maulid akiwa na Mhe Simai Mohammed Said wakiwa katika eneo maarufu la Kitalii nchini lijulikanali kwa jina la Trou Aux Cerfs (Valcano in Vacoas - Phoenix, Mauritius).
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe.Zuberi Ali Maulid akiwa na Wajumbe wa Mkutano huo wakitembelea Kiwanda cha Kufulia Umeme na Sukari Nchini Mauritius wakipata maelezo kutoka kwa Kiongozi wa Kiwanda hicho cha Omnicane Limited.
Msanii wa Sanaa za kutengeneza Boti kwa ajili ya Watalii wanaotembelea Nchi hiyo akiwa katika harakati za kutengeza za boti zinazopatika katika eneo la Curepipe Mauritius hutengenezwa kwa mbao kama majahazi ya Zanzibar.

Sanamu la pili refu duniani baada la Nchini India lijukanali kwa jina Lord Shiva Nchini Mauritius likiwa katika maeneo ya Ganga Talao.
Mandhari ya kutoka juu ya bustani ya Trou Aux Cerfs.

Imetayarishwa na Zanzinews.com

TANAPA KUTUMIA KUPATWA KWA JUA KUFUNGUA LANGO LA PILI LA KUINGIA RUAHA NATIONAL PARK.

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya ,Reuben Fune akiangalia jua kwa kutumia kifaa maalum ambacho kinachuja mwanga ili usiweze kuathiri macho kifaa hicho kitatumika katika tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .Kushoto ni mnajimu Dkt Noorali Jiwaji akimuelekeza namna ya kukitumia.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete akizungumza na wanahabari wilayani Mbarali (hawapo pichani) namna ambavyo Tanapa ilivyo jipanga na tukio la kupatwa kwa jua litakalotokea Septemba mosi. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali , Reuben Fune

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Mbarali,Mbeya .

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kuonekana Septemba mosi mwaka huu kufungua lango la Ikoga katika wilaya ya Mbarari mkoani Mbeya ili kuongeza watalii katika HIFADHI ya Taifa ya Ruaha

Kufuguliwa kwa lango hilo kunafanya idadi ya milango ya kuingilia katika hifadhi hiyo kufikia miwili ukiacha lango kuu la Way Junction ambalo limekuwa likitumika kwa muda mrefu sasa

Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete anasema kuongezeka kwa geti la Ikoga ni fursa kubwa ya kuhamasisha utalii wa ndani kwa kuwa eneo la Ihefu linakivutio kikubwa cha wanyama wa aina mbalimbali .


Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, anasema Wilaya hiyo ina vivutio vingi, hivyo amewataka wananchi watakaofika kuangalia kupatwa kwa jua hiyo Septemba Mosi , kutumia fursa hiyo kutembelea vivutio vilivyopo Wilayani humo.

Tukio la kupatwa kwa jua linategemea kutokea Septeba mosi majira ya nne asubuhi hadi saa nane mchana katika kata ya Rujewa eneo la Mpunga Relini Kiometa 3.5 kutoka barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kueleka Mbeya .
Mtaalam wa masuala ya anga (Mnajimu) Dkt Noorali Jiwaji akizungumza na waandishi wa habari wilayani Mbarali mkoani Mbeya kuhusu maandalizi na uwepo wa vifaa vya kuangalizia jua wakati wa tukio la kupatwa litakalotokea Septemba Mosi.
Mahema yakiwa yameanza kuwekwa katika eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .
Eneo la Mpunga Relini ,Rujewa wilayani Mbarali,eneo lililotengwa maalum kwa ajili ya kutizamia tukio la kupatwa kwa jua linalotarajia kutokea Septemba mosi .







ALICHOKISEMA ALIYEKUWA KATIBU WA CHADEMA MKOANI MWANZA BAADA YA KUTIMKIA CCM

$
0
0
Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (kulia), akirejesha kadi ya chama hicho kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo katika ofisi za CCM hii leo.

Na BMG

Nzwalile ambaye pia alikuwa Mjumbe wa Mkutano Mkuu Chadema Taifa, Mjumbe Baraza Kuu Chadema Taifa, Mwenyekiti wa Baraza la Mashauriano Chadema Mkoa wa Mwanza, amefikia uamuzi huo baada ya jana kujivua vyeo hivyo.

Amesema amefikia hatua hiyo kutokana na kwamba Chadema imepoteza mwelekeo kwani kimekuwa kikiibuka na oparesheni za kuichonganisha serikali na wananchi huku pia demokrasia ikikosekana ndani ya chama hicho.

"Kama ni udikiteta basi mimi niseme Chadema ndiko kuna udikiteta kwani zaidi ya mara tatu nimemsikia Lowasa (Edward Lowasa, aliyekuwa mgombea urais 2015) akisema yeye ndiye mgombea urais mwaka 2020, kwa kikao gani". Amesema Nzwalile na kuongeza kwamba yale mambo yote mabaya yaliyokuwa yakifanyika ndani ya CCM yamenyooshwa hivyo hakuna haja ya yeye kuendelea kukaa Chadema.

Amesema atazunguka Wilaya zote ili kuhakikisha anawarejesha wengine ndani ya CCM huku akiwa na jukumu moja la kuubomoa Ukuta unaoelezwa kujengwa na Chadema kwani ni ukuta wa tope hivyo atatumia tu maji kuubomoa.

Nzwalile amekaribishwa ndani ya CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo, ambaye pia amewakaribisha makada wengine wa upinzani kuhamia CCM akisema kwamba chama hicho kinaendesha mambo yake kidemokrasia.
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo (kushoto) akipokea kadi ya Chadema ya aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (katikati).
Mwenyekiti wa CCM mkoani Mwanza, Dkt.Antony Diallo (kushoto) akimkabidhi kadi ya CCM aliyekuwa Katibu wa Chadema mkoani Mwanza, John Nzwalile (kulia).
Soma HAPA Taarifa ya awali.

WATETEZI WA HAKI ZA BINADAMU WATAKA SERIKALI KUTOWAONA WACHOCHEZI KATIKA JAMII

$
0
0

Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.


Na George Binagi-GB Pazzo @BMG

Serikali imeshauriwa kutoa ushirikiano kwa watetezi wa haki za binadamu ili kurahisisha utendaji kazi wao badala ya kuwaona watetezi hao kama wachochezi katika jamii na wakati mwingine kuwafungulia mashitaka.

Ushauri huo umetolewa hii leo Jijini Mwanza na Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, kwenye mafunzo ya siku tatu kwa watetezi wa haki za binadamu kutoka mikoa mbalimbali nchini.

Amesema katika baadhi ya maeneo kama Loliondo mkoani Arusha kwenye mgogoro wa ardhi kati ya wananchi na mwekezaji, watetezi wa haki za binadamu wamechukuliwa kama wachochezi na kufunguliwa mashitaka jambo linalosababisha baadhi yao kushindwa kutekeleza majukumu yao na wengine kuacha kabisa shughuli za utetezi.

Akifungua Mafunzo hayo, Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, amesema serikali itaendelea kuwaelimisha wachimbaji wadogo ili waifahamu vyema sheria ya madini namba 4 ya mwaka 2010 ili kupunguza migogoro iliyopo na kwamba imetenga zaidi ya hekta elfu 12 kwa ajili ya wachimbaji wadogo wadogo wa madini.

Pia amesema serikali imetenga shilingi bilioni 6.6 kwa ajili ya ruzuku kwa wachimbaji wadogo na kuwahimiza kujiunga kwenye vikundi ili wapatiwe ruzuku hiyo.

Baadhi ya washiriki wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kuimarisha utendaji wao wa kazi jambo litakalowasaidia kutimiza vyema wajibu wao katika jamii bila kuonekana wachochezi huku pia wakiwa katika upande salama dhidi ya maisha yao.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Madini Kanda ya Ziwa Victoria magharibi, Mayigi Makobela, akizungumza na wanahabari nje ya Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza katika ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mratibu wa Taifa wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini, Onesmo Olengurumwa, akizungumza na Wanahabari nje ya ufunguzi wa Mafunzo ya Watetezi wa Haki za Binadamu yanayofanyika Jijini Mwanza.
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Miongoni mwa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akihojiwa na wanahabari
Washiriki wa Semina
Mwonekano kwenye semina
Picha ya pamoja
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live