Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

WAZIRI NAPE AFUNGA MASHINDANO YA GOFU YA WAZI YA TANZANIA JIJINI ARUSHA,WAKENYA WATAMBA

$
0
0

Richard Owiti kutoka nchini Kenya akionesha kombe lake la ushindi mara baada kushika nafasi ya kwanza kwa wachezaji wa ridhaa,kwenye mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye (wa pili kulia).Kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango wakishuhudia kwa pamoja.


Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimkabidhi vifaa vya mchezo huo wa Gofu mshindi wa kwanza wa wachezaji wa ridhaa katika Mashindano ya Gofu ya wazi ya Tanzania,Richard Owit kutoka nchini Kenya,yaliofungwa jana jioni katika viwanja vya Kili Golf-USA River jijini Arusha,pichani kushoto ni Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango. Mashindano hayo yaliyokuwa na msisimko mkubwa yalishirikisha washiriki wapatao zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania,Kenya na Unganda.


Mshindi wa kwanza kwa wachezaji wa kulipwa wa mchezo huo wa Gofu kutoka nchini Kenya,Jacob Okelo akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni sita,kwenye hafla fupi ya kuhitimisha mashindano hayo ya Gofu ya Wazi ya Tanzania ,yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya USA River na kuhitimishwa jana jioni,ambapo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye.
Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni moja Afisa Maendeleo ya jamii na Uhusiano,Justine Kesi ikiwa ni sehemu ya kiasi cha fedha kilichotolewa na Wadhamini waliodhamnini mashindano hayo ya Gofu kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya huduma za jamii mbalimbali kwa vijiji vinavyozunguka viwanja vya Kili Golf,jijini Arusha.

Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali jana jioni wakati wa kufunga mashindano ya Gofu ya Wazi ya Tanzania yaliyoanza kufanyika juzi ijumaa katika viwanja vya Kili Golf- USA River  jijini Arusha na kuhitimishwa jana jioni,ambapo wageni waalikwa wakiwemo wachezaji wa kulipwa na ridhaa wa mchezo huo walishiriki.PICHA NA MICHUZI JR-ARUSHA
Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhidia hitmisho la mashindano hayo ya gofu,wakifuatilia hotuba fupi iliyokuwa ikisomwa na Waziri Nape

Baadhi ya wageni waalikwa waliofika kushuhidia hitmisho la mashindano hayo ya gofu,wakifuatilia hotuba fupi iliyokuwa ikisomwa na Waziri Nape

Wazir Nape (wanne kulia) akiwa na wadau mbalimbali wa mchezo huo wa Gofu hapo jana kabla ya kuhitimisha mashindano hayo
Baadhi ya Wadau nao walikuwepo kufuatilia kuhitimishwa kwa mashindano hayo ya Gofu jana jioni jijini Arusha

Waziri Nape pia alikutana na wadau ambao walidhamini mashindano hayo ya Gofu

Waziri wa Habari ,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye akimsikiliza Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA),Mh Godbless Lema,kwenye viwanja vya Kiligolf,USA-River jijini Arusha,ambapo Mh Nape alikuwa mgeni rasmi katika kuhitimisha mashindano hayo ya Gofu ya Wazi ya Tanzania.Pichani kulia ni Diwani wa kata ya Maroroni,Mh.Bryason Issangya (CHADEMA)
Waziri Nape (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Gofu kwenye viwanja vya Kiligolf jijini Arusha,kutoka kulia ni Makamu Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania,Chris Martin,Mkurugenzi wa viwanja vya Gofu (KiliGolf),Jerome Bruins,Mmoja wa wasimamizi waku wa kampuni ya Group Six International LTD,Janson Huang,na kushoto kwa Waziri ni Mke wa Mbunge wa Arumeru Mashariki,Mh Joshua Nassari,Mh Joshua Nassari,Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU),Joseph Tango pamoja na Diwani wa kata ya Maroroni,Mh.Bryason Issangya (CHADEMA)
Waziri Nape akishiriki kucheza mchezo wa Gofu

Waziri Nape akipata maelezo mafupi kuhusiana na uwanja huo wenye viwango vyote kimataifa cha Kiligolf.
Waziri Nape akifurahia jambo na Mhe Nassri,kulia ni Mke wa Mh Nassari


Waziri Nape pia alipata wasaa wa kutembelea mashimo ya mchezo huo wa Gofu yapatayo 18 ndani ya uwanja wa Kili Gofu,uliopo USA River jijini Arusha.

DC MTATURU AMALIZA MGOGORO KATI YA MWEKEZAJI NA WANANCHI

$
0
0

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mang’onyi wakati wa kutatua mgogoro kati ya wananchi na muwekezaji Shanta Gold Mine
Wanachi Kijijini Mang’onyi wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mkuu wao wa Wilaya
Baadhi ya viongozi wakisikiliza maelezo ya awali katika ufunguzi wa mkutano huo uliodumukwa zaidi ya masaa matatu
Na Mathias Canal, Singida

Mgogoro uliodumu katika kipindi cha zaidi ya miaka kumi kati ya wananchi wa Kijiji cha Mang'oni na Muwekezaji Shanta Gold Mine umechukua sura mpya ya maelewano baada ya wananchi kupatiwa elimu kuhusu umuhimu wa uwekezekezaji na fursa watakazozipata ikiwa ni pamoja na ajira kwa wananchi wenyewe na maendeleo ya Vijiji, Kata, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa.

Akiwa katika kijiji cha Mang'onyi, Kata ya Mang'onyi Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu amezungumza na wananchi hao kujua kadhia iliyopelekea kutoelewana kwa kipindi chote hicho jambo ambalo limerudisha nyuma maendeleo tarajiwa kwa pande zote mbili.


Mgogoro huo umemalizika kwa Mkuu huyo kuamua kuwa wananchi walipwe fidia haraka iwezekenavyo ili kupisha uanzishwaji wa Mgodi huo ambapo tayari takribani wananchi 67 watalipwa katika awamu ya kwanza huku wengi zaidi 130 kulipwa katika awamu ya pili.

Dc Mtaturu amefanya mkutano wake wa hadhara wa mwanzo tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Wilaya ya Ikungi ambapo amewaagiza wawekezaji hao kukutana na kuwa na kikao cha pamoja kati yao na wananchi waliofanyiwa tathmini kwa ajili ya makubaliano ya namna bora ya malipo yao ikiwa ni pamoja na kuwashauri kila mmoja kufungua Account Bank ili iwe rahisi na salama katika uhifadhi wa fedha zao.

Baadhi ya Wananchi katika kijiji hicho cha Mang'oni hivi karibuni walizuia njia kwa kuweka magogo na mawe barabarani kama ishara ya kuwazuia wawekezaji hao kupita katika eneo lao kwa madai ya kutolipwa fidia kwa wakati na mwekezaji kuweka alama za mipaka ya eneo lake pasina wananchi kushirikishwa.

Hata hivyo Dc Mtaturu alisema kuwa huenda wananchi walikuwa na hoja ya msingi lakini kutolipwa fidia hakumfanyi mtu kupata uhalali wa kuharibu mali za muwekezaji kwani kufanya hivyo ni sehemu mojawapo inayochelewesha ulipaji wa fidia.

Mtaturu ameonyesha kukerwa na viongozi wanaowapotosha wananchi hao ilihali wakiwa wamejificha ama wanaishi mbali na kijijini hapo na kusema kuwa hiyo ni nidhamu ya woga kwani muwakilishi mzuri wa wananchi ni yule anayetanguliza maslahi ya wananchi mbele kuliko masalahi ya kisiasa, Chama ama maslahi yake binafsi.

Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa kiongozi mzuri daima ni yule anayetatua changamoto za wananchi sio kuzipinga kwani siasa safi na nzuri ni ile inayoleta maendeleo sio kupinga maendeleo.
Amewataka wawekezaji hao kuwa na mahusiano mazuri na wananchi kwani unapokuwa na mradi wako katika Kijiji chochote nchini usipokuwa na mawasiliano mema na wananchi wa eneo husika ni dhahiri kuwa mradi wako utakuwa hauna tofauti na mradi mfu.



Hata hivyo pamoja na faida kwa wananchi kulipwa fidia na serikali kupata pato lake lakini wananchi 60 kutoka Kijijini hapo wataajiriwa katika Mradi huo kati ya ajira 120 zilizopo ambapo wengine 60 watatoka nje ya eneo hilo ili kutoa fursa kwa watanzania wote kujipatia ajira.

Dc Mtaturu akikemea tabia ya wanasiasa kutoa matamko ya kisiasa kwa maslahi yao binafsi huku wakiwa mbali na eneo la wawakilishi wao
Wananchi wakimlaki Mkuu wao wa Wilayaya Ikungi
Dc Mtaturu akikemea tabia ya wananchi kuwachagua viongozi ambao wakipewa ridhaa tu wanahamia Dar es salaam ilihali wananchi wao wanabaki kuteseka pasina kuona umuhimu wa viongozi wao
Dc Mtaturu akitoa agizo kwa muwekezaji Shanta Gold Mine kuwalipa fidia haraka wananchi ili mradi huo uanze haraka iwezekanavyo
Nyumbani ni salamu na unyumbani ni kuongea Kinyumbani, moja ya tabasamu kati ya mwananchi na Dc wake wakizungumza kwa lugha moja baada ya mkutano
Wananchi wakielemishwa na Mkuu wa wilaya juu ya siasa zinazokwamisha maendeleo yao huku wanasiasa wenyewe wakishindwa kufanya uwakilishi katika maeneo yao badala yake wamekuwa wawakilishi wa kitaifa
Msingi wa kikao ni kusikilizana Mkuu wa Wilaya ya ikungi Miraji jumanne Mtaturu, Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya, Uongozi wa Shanta Gold Mine na wananchi Kijijini Mang’onyi wakiwa kwenye mkutano wa kutatua mgogoro wao


WIZARA YA NISHATI NA MADINI YANGALIA ENEO LITAKAPOJENGWA GATI KWA AJILI YA KUSHUSHIA MAFUTA GHAFI

$
0
0


 Greda likisafisha eneo ambalo linatarajiwa kujengwa gati kwa ajili ya kushushia mafuta ghafi
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kulia akiwa na viongozi kutoka Wizara ya Nishati na Madini walipotembelea sehemu  ambayo litajengwa gati mpya eneo la Chongoleani jijini Tanga kushushia mafuta ghafi kulia ni Kaimu Kamishna Msaidizi wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini ,Mwanamani Kidaya kushoto ni Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika

Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa pili kutoka kushoto akisisitiza jambo wakati walipotembelea eneo la Chongoleani ambapo kutajengwa gati ya kushushia mafuta ghafi



Kaimu Kamishna Msaidizi wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Mwanamani Kidaya akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kulitembelea eneo hilo leo
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella akizungumzia namna mkoa huo ulivyojipanga na fursa hiyo mara baada ya kulitembelea eneo hilo
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga,Henry Arika kulia akisisitiza jambo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella wa tatu kutoka kushoto namna walivyojipanga kutokana na fursa hiyo
Kaimu Kamishna Msaidizi wa Petroli kutoka Wizara ya Nishati na Madini,Mwanamani Kidaya kushoto akimuonyesha kiti Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shigella mara baada ya kutembelea eneo hilo






Muonekano wa eneo ambalo kutajengwa gati mpya kwa ajili ya kushushia mafuta ghafi
Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.

DC AKEMEA SIASA TAKA ZINAZOCHANGIA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akizungumza na watumishi wa Hospitali ya
Malkia wa Ulimwengu iliyopo Kijiji na Kata ya Puma
Dc Mtaturu akizungumza na viongozi wa ngazi ya juu katika Hospitali Teule ya Wilaya ya ikungi Makiungu mara baada ya kuwasili katika Hospitali hiyo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akikagua jengo jipya linalojengwa kwa ajili ya wodi na baadhi ya Ofisi za Hospitali ya Malkia wa ulimwengu
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa  Hospitali ya Malkia wa ulimwengu, Na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya

Na Mathias Canal, Singida

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu ametoa onyo kwa wanasiasa wanaotumia vibaya madaraka yao kwa kushindwa kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa uchangiaji huduma za afya na badala yake kuwafanya kudumaa kifikra na hatimaye kushindwa kufika hospitalini kupatiwa matibabu hivyo kupelekea vifo vya baadhi ya wananchi ambao wameamini maneno ya kisiasa kuliko kauli za watendaji za kufika Hospitalini kwa ajili ya matibabu.

Ametoa onyo hilo hii leo wakati alipotembelea na kuzungumza na watumishi wa Hospitali teuli ya Makiungu Wilaya ya Ikungi, Mkoani Singida pamoja na Hospitali ya Misheni Cathoric Malkia wa Ulimwengu inayomilikiwa na Shirika la Mothers of the Holy Cross an Missionaries of the Holy Cross.


Mtaturu amesema kuwa serikali inatambua umuhimu na huduma bora zinazotolewa na taasisi za dini katika Wilaya ya Ikungi kwani sekta ya afya ni sehemu muhimu kusukuma maendeleo ya nchi endapo wananchi watakuwa na afya bora itakuwa nguzo yao ya kufanya kazi na kuendana na falsafa ya Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli ya Hapa Kazi Tu.

Kauli ya watumishi wa umma ambao wanatumia vyeo vyao vibaya ikiwemo kuzuia wananchi kuchangia shughuli za maendeleo kama vile ujenzi wa Vituo vya afya na Dispensari jambo ambalo linajikita zaidi katika kudhoofisha afya za watanzania waishio katika maeneo ambayo hayana huduma za afya karibu.

Mtaturu amesema kuwa serikali kwa kushirikiana na hospitali hizo ili kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali zinatatuliwa ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa vifaa tiba, uwepo wa madaktari bingwa lakini ni muhimu wananchi kuchangia huduma za kijamii hususani sekta ya afya ili kuimarisha afya zao na kupunguza vifo visivyokuwa vya lazima.

Hospitali ya Makiungu ilianzishwa na Masista Wamisionari wa huduma ya tiba mnamo mwaka 1954 kwa mwaliko wa Baba Askofu Winters aliyekuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida wakati ule na ndio ilikuwa Taasisi ya kwanza kutoa huduma za afya katika Mkoa wa Singida.

Pamoja na huduma za tiba katika Hospitali ya Makiungu pia inatoa huduma za kinga kwa vijiji vilivyo karibu na hospitali katika vituo vitano kwa njia ya kiliniki tembezi walengwa wakuu wakiwa ni wajawazito na watoto wenye umri chini ya Miaka mitano.

Dc Mtaturu amesema kuwa katika Wilaya ya Ikungi kuna jumla ya Zahanati 34 katika Vijiji 34 pekee kati ya Vijiji 101 vilivyopo Wilayani humo kinyume kabisa na sera ya Taifa inavyoelekeza ya kuwa na Zahanati kwa kila Kijiji ili kupunguza kadhia wanazokumbana nazo madaktari bingwa kwa kuwahudumia wagonjwa wenye mafua badala ya magonjwa sugu na makubwa.

Amesema kuwa uchache na kusuasua kwa ujenzi na upatikanaji wa huduma za afya umechagizwa na kauli za kisiasa za kuzuia wananchi kuchangia shughuli za maendeleo jambo ambalo linazidi kurudisha nyuma maendeleo ya Vijiji, Tarafa, Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla.

Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu inahudumia wagonjwa wa ndani ya Wilaya ya Ikungi na Wilaya nyingine za Mkoa wa Singida na hata nje ya Mkoa wa Singida kama Shinyanga, Manyara, Tanga, Dodoma, Mwanza, Arusha na hata nchi jirani kama vile Kenya na Malawi.

"Changamoto zote mlizo nazo tumezichukua na serikali itazifanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kuinua huduma za afya na kuokoa vifo vya wananchi kisa matamko ya kisiasa, Lakini pia nataka niwakumbushe kuwa siasa zilishamalizika Tarehe 25 mwezi Octoba mwaka jana baada ya wananchi kufanya maamuzi yao kwenye uchaguzi Mkuu hivyo huu ni muda wa kufanya kazi kama ambavyo tumekuwa tukimsikia Rais akisema, Kwahiyo kuanzia leo sitaki siasa taka zenye kurudisha nyuma shughuli za maendeleo" Alisema Mtaturu

Aidha Dc Mtaturu amewapongeza watumishi wote katika Hospitali hizo mbili kwa jinsi ambavyo wanawahudumia wananchi kwa moyo mkunjufu pamoja na uchache wa vifaa tiba pamoja na uchache wa madaktari na Wauguzi lakini ameziomba Hospitali hizo kupunguza gharama za Dawa kwani kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya gharama kubwa zinazotakiwa baada ya matibabu sawia na kuwataka watumishi wote kutumia lugha nzuri kwa wagonjwa ili wagonjwa hao kupata tiba kwa amani na upendo.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi kwa ajili ya Hospitali Teule ya Wilaya ya Makiungu Afisa utumishi katika hospitali hiyo, Mary Shirima ameiomba serikali kusaidia upatikanaji wa gari la wagonjwa katika Hospitali hiyo ambalo litafanya kazi masaa 24 ili kusaidia kupunguza vifo vya akina mama wajawazito ambao wengi wao wanaathirika kutokana na umbali wanaotoka kwa ajili ya kufika hospitalini kupatiwa tiba.
Shirima alisema kuwa mbali na gari la kubeba wagonjwa pia Hospitali hiyo inaidai serikali jumla ya shilingi milioni 466,072,500/= ikiwa ni fedha za serikali na baadhi ya watumishi ambao serikali imeshindwa kuwalipa watumishi katika kipindi cha mwaka mzima baada ya kusaini mkataba na Askofu wa Jimbo katoliki la Singida wa Hospitali ya Makiungu kuwa teule mwaka 2008.

Kwa upande wake Diwani wa Viti maalumu Tarafa ya Ihanja Rabeka Ntandu Chaimbo Amempongeza Mkuu huyo wa Wilaya kwa kuzuru katika Taasisi hizo zinazotoa huduma za afya kwa wananchi kwani zimekuwa msaada mkubwa kwa Wilaya ya Ikungi sambamba na Wilaya na Mikoa mingine nchini.

Naye Mkurugenzi wa Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu Padri Manoel Tsino amesema kuwa wananchi wanapaswa kujiunga na Mfuko wa Bima ya Afya (CHF) ili kuwa na uhakika wa huduma bora ili pindi wanapoenda kupatiwa matibabu iwe rahisi kwao.

Sawia na ushauri huo kwa wanachi Padri Tsino pia amewashauri watumishi wote wa Hospitali hiyo kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya kufikia mwishoni mwa mwezi huu ili kuwa mfano bora kwa wananchi ambao hawajajiunga na mfuko huo.



Ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu hii leo ni ziara ya kwanza kuzitembelea Taasisi hizo tangu alipoteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akikagua Mtambo wa oxygen jinsi unavyofanya kazi mara baada ya kuzuru katika Hospitali Teuli ya Wilaya
Baadhi ya wagonjwa wakiwa katika hali ya ahueni mara baada ya kulazwa katika Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu iliyopo katika Kijiji cha Puma
Dc Mtaturu Mtaturu akiwasisitiza watumishi wa Hospitali ya Malkia wa Ulimwengu kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ili wawe mabalozi katika kuwashawishi wananchi nao kujiunga katika mfuko huo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwa katika picha ya pamoja na watumishi ngazi ya juu katika Hospitali ya teule ya Makiungu pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya
 Dc Mtaturu akisisitiza jambo kuhusu utoaji bora wa huduma za afya
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwasalimu baadhi ya wagonjwa ambao wamefikakupatiwa tiba hospitalini
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofisi za Mganga Mkuu wa Hospitali Teuli ya Makiungu
 Baadhi ya watumishi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu akiwasisitiza wanawake wajawazito kuhudhuria Kliniki wiki 12 za mwanzo mara baada ya kuhisi kuwa ni wajawazito sawia na kuwashauri kufika Hospitalini wakiwa wameambatana na waume zao




CHUO CHA CBE, TFDA NA AFRICAN RELIEF ORGANISATION WAMKABIDHI PAUL MAKONDA SH 31.7M ZA MADAWATI

$
0
0
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dk. Emmanuel Munishi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kushoto) Mfano wa hundi ya shilingi milioni 8,000,000/= zilizotolewa na Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kama mchango wa chuo hicho kwa jamii kwa ajili ya kununulia madawati yatakayotumiwa na wanafunzi wa shule za msingi katika mkoa huo.Katikati ni Afisa Uhusiano wa Jamii wa Chuo hicho Leonidas Tibanga.
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dk. Emmanuel Munishi (katikati) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kukabidhi mchango wa wa madawati wa shilingi milioni 8 kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kulia) leo jijini Dar es salaam. Mchango huo umetolewa na chuo hicho kununulia madawati yatakayotumiwa na wanafunzi wa shule za msingi za mkoa huo, Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Jamii wa Chuo hicho Leonidas Tibanga.

Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ametoa wito kwa Taasisi na Mashirika mbalimbali jijini Dar es salaam kujitokeza kwa wingi kuunga mkono zoezi la uchangiaji wa hiari wa madawati kwa shule za msingi linaoendelea jijini humo ili kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia yatakayozalisha wanafunzi bora wa shule za msingi.

Akizungumza mara baada ya kupokea mchango wa fedha za kununulia madawati kiasi cha shilingi milioni 31.7 kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE),Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Taasisi ya kidini ya masuala ya jaamii ya African Relief Organisation leo jijini Dar es salaam Mhe. Makonda amesema kuwa bado jamii inao wajibu na jukumu la kuhakikisha kuwa mazingira ya kusomea ya wanafunzi wa shule za msingi yanakuwa bora ili kuzalisha wahitimu walio na msingi imara.

“Napenda kutumia fursa hii kuzishukuru taasisi hizi ambazo zimeitikia wito wa kutoa michango yao ili kuwezesha upatikananji wa madawati, nawashukuru sana viongozi wa taasisi hizi kwa kuitikia wito wa mkoa wetu na kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuhakikisha shule zetu zina madawati na hakuna mwanafunzi anayekaa chini” Amesisitiza Makonda.

Ametoa wito kwa wananchi ambao wanaguswa kwa namna moja au nyingine kuendelea kutoa michango yao ili kuwasaidia wanafunzi wa shule za Msingi katika jiji la Dar es salaam ambao walikuwa wanapata shida ya kusomea katika mazingira magumu.

Ameongeza kuwa ili taifa liweze kuwa na wataalam wazuri katika Nyanja zote lazima msingi wa elimu katika shule za msingi uwe mzuri na kufafanua kuwa ndoto ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkoa wa Dar es salaam ni kukamilisha upatikanaji wa madawati na majengo ya madarasa.

Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Dkt. Emmanuel Munishi akizungumza mara baada ya kukabidhi mfsno wa hundi ya shilingi milioni 8 kama mchano wa chuo hicho kwa jamii amesema kuwa wao kama Chuo cha Elimu ya Biashara chenye kampasi mikoa minne ya Tanzania ukiwemo Mwanza, Dar es salaam, Dodoma na Mbeya kimeguswa kuchangia kiasi hicho cha fedha kwa kuwa kinawategemea wanafunzi waliofundishwa vizuri kutoka shule za Msingi.

Amesema wameamua kuunga mkono Juhudi za Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ili kuhakikisha kuwa shule Zote za Dar es salaam zinaondokana na shida ya madawati.

“Sisi tumeguswa na uchangiaji wa madawati kwa kuwa ni taasisi ya ya elimu ya juu, kama taasisi ya elimu ya juu hatuwezi kupata wanafunzi wetu kama hakuna shule za msingi, tumeamua tusiwe watu wa kuvuna tu tukaamua kwenda moja kwa moja kwenye msingi ili kujenga msingi imara wa shule zetu” Amesisitiza.

Ameziomba taasisi zote za Elimu ya juu nchini kuiga mfano wa CBE katika kuchangia sekta ya elimu hapa nchini.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Kidini ya Masuala ya Kijamii ya African Relief Organization ya jijini Dar es salaam Shekh Abdallah Ndauga iliyochangia shilingi milioni 6 amemshukuru Mkuu wa Mkoa huo kwa moyo wake wa kuendelea kuwahamasisha wananchi ambao wamekuwa wakijitokeza kwa wingi kuchangia madawati.

Amsesema Taasisi ya African Relief Organisation itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali na mkoa wa Dar es salaam katika kuleta maendeleo ya wananchi wake kupitia miradi mbalimbali wanayotekeleza ikiwemo uchimbaji wa visima katika maeneo mbalimbali nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada uliotolewa na Mamlaka hiyo wa shilingi milioni 17.7 amesema TFDA inaunga mkono jitihada za Rais, Dkt. John Pombe Magufuli za kuhakikisha kuwa kila mtoto anakaa katika dawati ambapo katika bajeti yake ya mwaka 2015/16 inatoa mchango wa madawati 236.

Sillo ameongeza kuwa TFDA pamoja na majukumu iliyonayo inatambua kuwa elimu ndiyo nguzo muhimu katika kupambana na maadui wakubwa wa maendeleo, hivyo itaendelea kutoa mchango wake katika kusaidia sekta ya elimu hapa nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo (kulia) akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 17,700,000/= Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kushoto) kama mchango wa madawati kwa wanafunzi wa shule za Msingi jijini Dar es salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda (kushoto) akiangalia mfano wa hundi ya shilingi milioni 6 zilizotolewa na Taasisi ya Kijamii inayojihusisha na masuala ya Kijamii ya African Relief Organisation ya jijini Dar es salaam kwa ajili ya kununulia madawati. Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Shekh Abdallah Ndauga na Mratibu wa Miradi wa Taasisi hiyo Moadh Shannawi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kupokea msaada wa Fedha kutoka Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Taasisi ya Kidini ya Masuala ya Kijamii ya African Relief Organisation kwa ajili ya kununulia madawati kwa shule za Msingi za Dar es salaam. Picha/Aron




SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU-CCM

$
0
0
SHIRIKISHO LA VYUO VYA ELIMU YA JUU CCM TANZANIA     

TAARIFA KWA UMMA

Katibu wa Shirikisho la Vyuo vya Elimu
 ya Juu-CCM, Siraji Madebe
Shirikisho la vyuo vya Elimu ya Juu CCM  katika kikao chake cha kazi cha Agosti 11, 2016, pamoja na mambo mengine. 
Kimeazimia yafuatayo:-

Kuunga mkono utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo kwa kuelimisha wananchi kumuunga mkono Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM taifa Dk. John Pombe Magufuli, kuhusu umuhimu wa kila mwananchi kudai risiti na muuzaji kutoa risti katika kila manunuzi, kwa lengo la kuwezesha serikali kupata fedha kupitia kodi, kutoa elimu kwa jamii na uelewa wa Tanzania yenye viwanda ikiendana na uwanzishaji wa mashamba darasa ya shirikisho na viwanda vya kati vya kusindika mazao.


Vilevile Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, tunafungua milango kwa vijana mbali mbali wenye lengo la kuunda vikundi vyenye dhamira ya kujikwamua kiuchumi na kutaka kujiajili, kufika kwenye ofisi zetu za Shirikisho zilizopo mikoani na Makao Makuu, mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam, ili kupata ushauri wakitaalamu na kusaidiwa kuandika maandiko yatakayo waongoza kwenye uanzishwaji wa miradi itakayo saidia kutoa fursa za ajira kwa vijana.

Pia Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, linamuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli, kuwashughulikia kikamilifu wale wote waliohujumu mali za CCM, kwani vitendo hivyo vinadhoohofisha nguvu ya chama na wakati mwingine kuwafanya wanachama kuwa wanyonge kwenye Chama chao.

Shirikisho la vyuo vya Elimu ya juu - CCM, kwa kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM, kwa kuhamia Dodoma, tumeazimia kuwa Ofisi ya Makao Makuu ya Shirikisho nayo itahamia Dodoma rasmi hivi karbuni, baada ya taratibu za upatikanaji wa Ofisi kukamiliaka.

Mwisho, Shirikisho la Vyuo vya Elimu ya Juu-CCM, linapenda kuwaomba Watanzania kuendelea kumuunga mkono na kumuamini kwa dhati kabisa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Dk. John Pombe Magufuli kwani dhamira yake ni kuitumikia jamii ya Watanzania na si kufanya siasa kwenye maisha ya watu wenye shida.

KUDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Imetolewa na:-
Idara ya Habari na Mawasiliano
Shirikisho Makao Makuu

SERIKALI YAMPONGEZA MWANDISHI WA KAMUSI YA UKRISTO

$
0
0

MGODI WA BULYANHULU WATENGENEZA AJIRA VIJIJINI KUPITIA MRADI WA MADAWATI.

$
0
0
Afisa Mahusiano wa Mgodi wa Bulayanhulu Sara Teri (kulia) na Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulayanhulu Elias Kasitila wakikabidhi madawati kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama pamoja na viongozi wengine wa Wilaya ya Nyangw’ale.
Meneja wa Ufanisi wa Mgodi wa Bulyanhulu uliopo mkoani Geita ,Elias Kasitila akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya madawati yaliyotolewa na mgodi huo kwa ajili ya shule zilizoko katika wilaya ya Nyang'wale.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.

Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umetengeneza mamia ya ajira kwa vijana na wanawake wanaoishi maeneo mbalimbali mkoani shinyanga na Geita kupitia mpango wa kutengeneza madawati elfu sita katika maeneo mbalimbali ya mikoa hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 200.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti vijana wamesema neema ya kujiingizia vipato kwa kushiriki kwenye shughuli mbalimbali katika zoezi la kutengeneza madawati imebadili maisha yao hasa katika msimu huu wa kiangazi ambao wengi wao ajira zao zimesimama kwani walio wengi wanategemea mvua kwenye ajira yao ya msingi ya kilimo.

“Tunashukuru sana msimu huu wa kiangazi, tumepata nafasi ya kupata kazi za ambazo zinatupatia kipato kupitia utengenezaji wa madawati, mimi hapa ni fundi chuma, nachomelea vyuma na kazi yangu hii huku vijijini wateja ni wachache sana, muda mwingi huwa tuko doro kwenye kijiwe chetu lakini sasa hivi tuna kazi nyingi sana za kutengeneza madawati hapa imebidi niajiri vijana wengine watano kuweza kunisaidia kukamilisha kazi ya kuunganisha vyuma kwa ajili ya madawati mia tano ambayo tumepata tenda na Kampuni iliyoshinda tenda ya kutengeneza madawati kwa gharama ya mgodi wa dhahabu ya Bulyanhulu.” Anasema Abbas Mbua mkazi wa kata ya Msalala wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita.

“Sisi wapiga msasa tunajipatia shilingi elfu kumi na tano kwa kila dawati 5 hii si haba, kiasi hiki kimenisaidia sana maana sikupata vizuri mazao mwaka huu kwa hiyo pesa niliyoingiza kwenye kazi ya kupiga msasa imebadili kabisa hali halisi nyumbani, nimenunua gunia za mahindi, maharage na mchele, hali imetulia kwa kweli siwezi kusema uongo” anasema Maige Deus mkazi wa Kahama.

“Ninaiomba sana serikali yetu iendelee kuvumbua miradi mingine ili sisi vijana tuendelee kuchapa kazi, maana vinginevyo tunakaa vijiweni kazi hamna, lakini mradi huu wa madawati ulivyokuja hatuna hata muda wa kuvuta sigara, tuko bize kutwa nzima tunatengeneza madawati, hapa mimi ndiyo fundi mkuu kwenye hiki kiwanda naunganisha mbao na kuhakikisha madawati yako vizuri kwa ajili ya wanafunzi.” Anasema Abdul Karim Ramadhani akiwa katika kiwanda cha Zacharia and Deus Timber Supply cha Nyang’wale mkoani Geita.

Halikadharika mama nilitie nao wanasema si haba mradi wa kuchonga madawati umeongeza idadi ya wateja katika migahawa yao, Devotha Sonda wa Sonda Mama Nitiliea katika kijiji cha Msalala anasema “ Kabla ya mradi wa madawati vyakula hapa tulikwa tunapika kidogo na wateja walikuwa ni wa kubangaiza tu lakini sasa hivi kutokana uchongaji wa madawati vijana ni wengi sana na binafsi nimepewa tenda kabisa ya kupikia vijana wanaotengeneza madwati na ninalipwa vizuri na kwa muda, naomba miradi kama hii iendelee tu hadi madawati yatoshe na sisi mitaji itakuwa imekua. Mwaka huu maswala ya ada kwa watoto, mavazi sasa ni jambo rahisi.”

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya kizawa ya Zacharia and Deus Timber Supply Deus Mlela iliyopo Nyang’wale kilomita hamsini kutoka mgodi wa Bulyanhulu amesema, “Tenda ya kutengeneza madawati mia tano kutoka Bulyanhulu kwetu tumepata faida mara mbili kwanza imetuongezea mtaji na pili imetupa uwezo na kujulikana kwa wadau wengine, sasa hivi tumepatiwa tena tenda na Halamashauri ya wilaya kutengeneza madawati mengine elfu moja na kampuni nyingine imetupa tenda na madawati mia mbili, bila kazi ya Bulyanhulu kutufungulia mlango ingekuwa vigumu kuweza kupokea tenda hizo kwa sababu mtaji ulikuwa mdogo. Tunaomba wadau waendelee kutuamini ili na sie tuweze kuendelea kusambaza ajira kwa vijana ambao hawana ajira.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Hamim Gwiyama amesema, “Kimsingi kuwa karibu na Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu imewafanya watu wa Nyang’wale ule uzito wa kazi ya madawati kuwa tofauti na sehemu nyingine, japo hatujamaliza kabisa tuna mapungufu kidogo, faida ya mradi wa madati faida yake ya kwanza ni kwa watoto wa shule ambayo ni walengwa, wanapata madawati wake vizuri na waweze kuelewa masomo yao vizuri, kwa njia nyingine mpango huu umetengeneza ajira, wale watengeneza mawadaati wamepata kazi ya kufanya na kipato, wanajipatia mahitaji wengine wananunua mifugo, kwa mfano katika mradi huu bulyanhulu imedhamini madawati yenye thamani ya shilingi million thethini na tano na hii pesa imezunguka kwa watu wote, mafundi seremala, waendesha mikokoteni, mama nitilie, na wengine wengi wamejipatia kipato na hata mitaji.”

Mwaka 2013 Mgodi wa Bulyanhulu ulitoa madawati 1329 kwa ajili ya shule 10 za msingi zinazozunguka mgodi wa Bulyahulu.

Mwaka huu 2016 Madawati 1380 kwa halmashauri ya Msalala madawati 500 kwa wilaya ya Nyang’wale 500, madawati 2000 yatatolewa hivi karibuni kwa mkoa wa Shinyanga na pia Bulyanhulu itaipatia dola za kimarekani elfu 6000 shule ya msingi ya binafsi ya St. Josephine Bhakita iliyoko km 12 kutoka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu katika kijiji cha Ilogi kata ya Bulyanhulu.
Utengenezaji wa Madawati ulitoa fursa ya ajira kwa fundi Deus Mlela aliyepewa tenda na Mgodi wa Bulyahulu ya kutengeneza madawati mia tano.
Fursa ya ajira iliendelea kusambaa kwa dereva wa trekta Bw ,Machibya aliyepata tenda ya kusafirisha Madawati kwenda katika shule zilizokusudiwa kupata Madawati hayo.
Lakini pia wakati wa shughuli za utengezaji wa Madawati hayo mafundi walihitaji kupata chakula na hii pia ikawa Fursa kwa Mama Nitilie Devotha Sonda wa Sonda ambaye alikuwa akitoa huduma ya chakula kwa mafundi hao.






BENKI YA DTB YAKABIDHI VITI KITUO CHA AGA KHAN KWAAJILI YA PROGRAMU YA MAKUZI NA MAENDELEO YA MTOTO MADRASA

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Benki ya DTB Tawi la Zanzibar Ndg Shahr Mohammed kushoko akimkabidhi msaada wa Vitu kwa ajili ya Madrasa hiyo inayotowa Elimu ya Mafunzo kwa Walimu wa Skuli za Maandalizi Zanzibar, akipokea msaada huo wa Vitu 40 kwa ajili ya Taasisi hiyo ya Programu ya Makuzi na Maendeleo ya Watoto Madrasa Ndg Khamis Said Abdallah hafla hiyo imefanyika katika Kityuo hicho kiponda Zanzibar wakishuhudia Wafanyakazi wa DTB na Kituo hicho.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Benki ya DTB Ndg Shahr Mohammed akikabidhi msaada wa Vitu vilivyotolewa na Benki hiyo kwa ajili ya matumizi ya Kituo hicho akipokea msaada huo Mkurugenzi wa Programu ya Makuzi na Maendeleo ya Watoto na Madrasa Ndg Khamis Said Abdalla.
Mkuu wa Kitengo cha Fedha Benki ya DTB Tawi la Zanzibar Ndg Shahr Mohammed, akizungumza na wakati wa hafla hiyo ya kukabidhi viti hivyo 40 kwa ajili ya Kituo hicho ni moja ya misaada yao kwa jamii kutumia faida wanayoipata kusaidi miradi ya Jamii.Hafla hiyo imefanyika katika Kituo chaMadrasa Kiponda Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kituo hicho cha Programu ya Makuzi na Maendeleo ya Watoto na Madrasa Ndg. Khamis Said Abdallah akitowa shukrani kwa Benki ya DTB kwa msaada wao huo wameotowa wakati muafaka wakati kituo hicho kina upungufu wa thamanin kwa walimu wanaopata mafunzo katika kituo hicho.

MAONESHO YA BIASHARA YA AFRIKA MASHARIKI 2016 KUFANYIKA ROCK CITY MALL JIJINI MWANZA

$
0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema (wa pili kushoto), akitoa ufafanuzi hii leo Jijini Mwanza kuhusiana na Maonesho ya Wafanyabiashara Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Agost 26,2016 hadi Septemba 04,2016 katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza. 

Wengine ni, Hassan Karambi ambaye ni Katibu Mtendaji wa TCCIA Mwanza (wa kwanza kushoto), Tungu Misululu, Makamu Mwenyekiti TCCIA kitengo cha Biashara mkoani Mwanza (wa pili kulia) na Majid Igangula (wa kwanza kulia), kutoka bodi ya Washauri TCCIA.

Makampuni pamoja na wajasiriamali mbalimbali katika nchi za Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania, yametakiwa kutumia Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki katika kutangaza na kuuza bidhaa zao.

Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema, ametoa rai hiyo leo Jijini Mwanza, wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusiana na Maonesho hayo.

"Maonesho haya yanatoa fursa kwa makampuni mbalimbali Afrika Mashariki kujitangaza, kukutana na wateja wao, kutafuta wabia wapya wa kibiashara pamoja na kufanya utafiti wa kimasoko". Ametanabaisha Lema.

Maonesho hayo yanatarajiwa kuanza agost 26,2016 hadi Septemba 04,2016 katika viunga vya Rock City Mall Jijini Mwanza na yanatarajiwa kushirikisha wafanyabiashara kutoka mataifa ya Afrika Mashariki na nje ya Afrika Mashariki.
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema (katikati), akiwa katika mkutano na wanahabari (hawapo pichani) kuhusiana na Maonesho ya Wafanyabiashara Afrika Mashariki yanayotarajiwa kuanza Agost 26,2016 hadi Septemba 04,2016 katika viwanja vya Rock City Jijini Mwanza.

Wengine ni, Hassan Karambi ambaye ni Katibu Mtendaji wa TCCIA Mwanza (kushoto), Tungu Misululu, Makamu Mwenyekiti TCCIA kitengo cha Biashara mkoani Mwanza (kulia).
Wanahabari Jijini Mwanza, wakiwa katika Mkutano wa TCCIA kuhusu Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki Jijini Mwanza, uliofanyika leo.
Wanahabari wakiwa katika mkutano huo
Makamu Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA mkoani Mwanza, Leopard Lema, akitoa ufafanuzi kwa wanahabari.
Taswira ya Mkutano wa Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo TCCIA, na Wanahabari ulioketi hii leo Jijini Mwanza, kuhusu Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashari yanayotarajiwa kuanza Agost 26 mwaka huu viwanja vya Rock City Mall Jijini Mwanza.

Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG

BENKI YA DUNIA KUENDELEA KUISAIDIA SEKTA YA MAJI NCHINI

$
0
0
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Gerson Lwenge akifungua kikao cha pamoja na ujumbe wa Benki ya dunia, Wizara ya Maji ,Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasco ) na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (Dawasa) namna ya kutatua changamoto za usambaza Maji kwenye Jiji la Dar es Salaam yakiwamo Mivujo na Miundombinu chavu , kilichofanyika Jijini Dar es salaam.



Dar es Salaam.

KATIKA kuhakikisha sekta ya Maji inakua kwa kasi na inatosheleza mahitaji ya sasa ya huduma ya maji, Benki ya Dunia imejitolea kulisaidia Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es salaam (DAWASCO), ili kusaidia katika upatikanaji wa huduma ya Majisafi na Majitaka katika maeneo mbalimbali ya wakazi wa jiji la Dar es salaam pamoja na Miji ya Kibaha na Bagamoyo mkoani Pwani.

Hayo yamezungumzwa na Mwakilishi wa Benki ya Dunia nchini, Bi. Bella Bird, ambaye alikuwa ameambatana na wajumbe wake katika kikao cha pamoja na Waziri wa Maji, Mhandisi Gerson Lwenge, pamoja na Shirika la Majisafi na Majitaka jijini Dar es Salaam (DAWASCO).


Kikao ambacho kililenga uboreshaji na upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo kadhaa ya jijini Dar es Salaam hasa maeneo ambayo hayajafikiwa na huduma hiyo.
Aidha, Mwakilishi huyo wa Benki ya Dunia, ameridhishwa na juhudi za makusudi zinazofanywa na Dawasco katika kuwapatia wananchi huduma ya Majisafi, pamoja na kupambana na kiwango cha Maji kinachopotea bila sababu ya msingi.

Ameeleza kuwa Benki ya dunia imetenga fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya Majisafi na Majitaka ili kuimarisha uendeshaji wa utoaji wa huduma ya Maji kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutekeleza kikamilifu kampeni ya “Mama Tua Ndoo Kichwani” ili kuwapunguzia akina mama wengi tatizo la Maji, kwani ndio wanaoonekana kuwa wahanga wakuu wa tatizo hilo.

“Nimeridhishwa na utendaji wenu wa kazi, jinsi ambavyo mmejipanga katika kufanya kazi, hasa juhudi zenu mnazoziweka katika kupambana na upotevu wa Maji na kuwapatia wananchi huduma ya Maji” alisema Bi. Bird

Naye, Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameishukuru Benki ya Dunia kwa ushirikiano mzuri waliouonesha, na kwamba kiasi cha fedha kilichotengwa na Benki ya Dunia kitatumika katika kuboresha na kutatua changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika katika utoaji wa huduma ya Maji.

“Changamoto ni nyingi katika utoaji wa huduma ya Maji, naamini kuwa kiasi cha fedha kilichotengwa kitasaidia kuondoa changamoto hizo” alisema Mhandisi Luhemeja.

Benki ya dunia imekuwa ikifadhili miradi mingi ya maendeleo hapa nchini ikiwamo miradi mbalimbali katika sekta ya Maji, Nishati na Madini, Kilimo na Mifugo, pamoja na Uchumi na Biashara.




SBL YATANGAZA KUDHAMINI ELIMU KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU

$
0
0


Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha ( kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) Wakati wa kutangaza mpango kampuni hiyo wa kugharamia elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zisizo na uwezo ili kuwapa walengwa fursa ya kutimiza malengo na ndoto zao za kimaisha.Pembeni yake ni Meneja wa Miradi ya Jamii wa SBL Hawa Ladha katika mkutano uliofanyika mapema leo katika ofisi za SBL,Temeke jijini Dar es salaam.


Meneja wa Miradi ya Jamii Hawa Ladha akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (Hawapo pichani) wakati wa kutangaza mpango wa kampuni hiyo kugharamia elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zisizo na uwezo ili kuwapa walengwa fursa ya kutimiza malengo na ndoto zao za kimaisha,kulia kwake ni Mkurungezi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mapema leo katika ofisi za SBL zilizopo Temeke Jijini Dar es salaam. 

Dar es Salaam, Agosti 18, 2016 

Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) kwa mara nyingine imetangaza mpango wa kugharamia elimu ya vyuo vikuu kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zisizo na uwezo ili kuwapa walengwa fursa ya kutimiza malengo na ndoto zao za kimaisha.

Huu ni mwaka wa sita mfululizo ambapo SBL inatoa msaada kwa wanafunzi wa ndani wanaochukua kozi za shahada katika vyuo vikuu vya Tanzania chini ya programu ya kampuni ijulikanayo kama “Skills for Life”. Jumla ya wanafunzi 31wa Tanzania tayari wameshanufaika na mpango huu ambao ni sehemu ya Mfuko wa Kampuni ya Bia ya Afrika Mashariki (EABL Foundation).

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mahusiano wa SBL John Wanyancha fomu za maombi kwa ajili ya udhamini zinapatikana katika ofisi za kampuni hiyo zilizopo Dar es Salaam, Moshi na Mwanza au kupitia tovuti ya www.eablfoundation.com.

Wanyancha amesema mpango huo uko wazi kwa wanafunzi kutoka nchi nzima ya Tanzania ambao ambao tayari wamepata usajili wa kujiunga na vyuo vikuu nchini katika fani za Biashara, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Uhandisi na Sayansi ya Chakula katika ngazi ya shahada kutoka vyuo vikuu hapa nchini.

Mfuko wa EABL ulianza kutoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi kuanzia wanaojiunga na vyuo vikuu mwaka 2005 ambapo hadi sasa zaidi ya wanafunzi 238 wamenufaika kwa mpango huo wakiwemo 31 kutoka Tanzania. Wengi walionufaika tayari walishamaliza masomo yao na wanafanyakazi katika makampuni mbalimbali katika ukanda huo. Mpango huu upo katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda ambapo mfuko wa EABL umetumia jumla ya zaidi ya Tshs billion 5 kuugharamia tangu mwaka wa 2005. 
Udhamini huu hugharamia ada ya masomo, vitabu, malazi, fedha za kujikimu na programu za ushauri kwa waombaji watakaofanikiwa. “Lengo letu kuu kupitia mpango huu ni kuwawezesha waombaji kutimiza ndoto zao maisha,” alisema Wanyancha na kuongeza kuwa tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni Septemba 20, 2016.

Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini kuchangamkia fursa hiyo ili kwa kutuma maombi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja ujao.

MAHITAJI MUHIMU: Fomu za maombi zilizojazwa vizuri zikiwa zimeambatanishwa na barua ya usajili kutoka kwa taasisi ya elimu ya juu, udhibitisho wa hitaji la kifedha na nakala za vyeti vya elimu ya sekondari kidato cha nne na cha sita.

Wanafunzi ambao bado hawajapokea barua za kusajiliwa kujiunga na vyuo vikuu na ambao wanakidhi masharti pia wanaweza kutuma maombi.


Waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini mkutano huo mapema leo asubuhi katika ofisi za SBL zilizopo Temeke jijini Dar es salaam.



MLIMBWENDE WA TAJI LA MISS MWANZA 2016 APATIKANA

$
0
0
Usiku wa jana Ijumaa Agost 19,2016 kuamkia leo Jumamosi Agost 20,2016, kulikuwa na mtifuano mkali wa kumtafuta mlimbwende wa taji la MISS MWANZA 2016 ambapo warembo 16 kutoka wilaya mbalimbali mkoani Mwanza walijitosa kusaka taji hilo.

Ilikuwa ni furaha kubwa kwa mrembo, Mary Peter (katikati), pale alipotangazwa kuwa MISS MWANZA 2016. Pia mwendelezo wa furaha uliwaendea warembo, Victoria Boniphace (kushoto) aliyetangazwa Miss Mwanza nambari mbili na Winnie Shayo (kulia), aliyetangazwa Miss Mwanza nambari tatu.

Kinyang'anyiro cha Miss Mwanza 2016, kiliandaliwa na Kampuni ya "Big D Entertainment" na baada ya kinyang'anyiro hicho, unafuata mtifuano wa MISS LAKE ZONE 2016 utakaofanyika Septemba 10,2016 ambapo washiriki wa Miss Mwanza 2016 waliongia nafasi tano bora, wanashiriki moja kwa moja kwenye shindano hilo.
Na BMG
Miss Mwanza 2015, Donny Roberty (kushoto), akimkabidhi taji Miss Mwanza 2016, Mary Peter (kulia) baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.

Washiriki wa Miss Mwanza, walioingia nafasi tano bora
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016.
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
Majaji walikuwa na Kazi pevu kuchagua mshindi
Baadhi ya waliohudhuria kwenye tukio
Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza akidondosha burudani kwenye Miss Mwanza 2016
Burudani za kiafrika pia zilikuwepo
Mkali wa Moyo Mashine, Ben Pol, alidondosha burudani poa sana
Ben Pol kazini
Kupitia BMG, Ben Pol, aliwashukuru wakazi wa Jiji la Mwanza kwa namna wanavyopenda kazi zake na kuahidi kufanya kazi nzuri zaidi.
Miss Mwanza 2016 aliiambia BMG kwamba, maandalizi yake mazuri ndiyo yaliyompa fursa ya kunyakua taji hilo na kwamba amejiandaa vyema kwa ajili ya taji la Miss Lake Zone 2016 na pia Miss Tanzania 2016.
Miss Mwanza 2016 nambari mbili akibonga na BMG. Anasema shauku yake ni kuongeza juhudi zaidi ili kunyakua taji la Miss Lake Zone 2016.

TANAPA KUTUMIA TUKIO LA KUPATWA KWA JUA KUTANGAZA HIFADHI ZAKE

$
0
0

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog.

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limesema litatumia fursa ya tukio la kupatwa kwa jua kama njia mojawapo ya kutangaza hifadhi za taifa hususani zinazopatikana katika mikoa ya nyanda za juu kusini na Magharibi mwa Tanzania.

Tukio la kupatwa kwa jua linataraji kuonekana vizuri ukilinganisha na maeneo mengine Duniani katika eneo la Rujewa wilayani Mbarali mkoani hapa,eneo ambalo liko jirani na Hifadhi za taifa za Ruaha,Kitulo na Katavi.

Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) Pascal Shelutete alisema maandalizi kwa ajili ya kupokea wageni wanao tarajia kufika nchini kwa ajili ya tukio hilo ambalo limekuwa likitokea kwa nadra.

“ Wataaam na wanasayansi wa kitaifa na kimataifa wathibitisha kuwa eneo pekee ambalo tukio hilo litaonekana vizuri kuliko maeneo yote duniani ni Tanzania katika mikoa ya nyanda za juu kusini,eneo ambalo lina vivutio utalii vinavyopatikana katika hifadhi zetu za Katavi.Kitulo na Ruaha”alisema Shelutete .

“Shirika limejipanga kuhakikisha kuwa wageni wanoukuja kwa ajili ya tukio hilo pia wanapata fursa ya kuingia katika moja ya hifadhi zetu,niwaomba wadau wa sekta ya utalii nchini kutumia nafasi hii adhimu kukutana na wageni wanaokuja ili kuuza bidhaa zao za utalii”aliongeza Shelutete.

Naye mkuu wa hifadhi ya taifa ya Ruaha Christopher Timbuka alisema kituo kikubwa ambacho kimethibitishwa kutumika kwa ajili ya watu kujionea vizuri tukio hilo ni katika eneo la rujewa wilaya ya mbarali ambako maandalizi yote muhimu yamefanyika.

Kwa upande wake mhifadhi wa idara ya utalii Tutindaga Mdoe alisema baada ya tarifa za tukio hilo kuthibitishwa idadi ya wageni imeanza kuongezeka na kwamba wameandaa mahema na eneo la vyakula na vinywaji kwa wageni watakaofika kushuhudia tukio hilo katika eneo la Bonde la Ihefu lililopo katika hifadhi ya taifa ya Ruaha.

Utafiti mdogo uliofanywa na gazeti hili katika eneo hilo maarufu kwa kilimo cha mpunga umebaini asilimia kubwa ya nyumba za kulala wageni tayari zimejaa kwa tarehe ya tukio hilo.

MCHUNGAJI KULOLA WA KANISA LA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA AKIHUDUMU NCHINI MAREKANI

$
0
0
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola (pichani) yuko nchini Marekani kwa huduma ya kiroho tangu jumanne iliyopita Agost 16,2016 ambapo alianza kuhudumu ijumaa Agost 19,2016 katika Kanisa la "Assemblies Of God Agape Church" lililopo Boston Marekani.

Huduma ya Mchungaji Dkt.Kulola inaendelea katika majimbo mbalimbali nchini Marekani ikiwemo Dallas, Texas, Houston na Arizona.

Aidha Mchungaji Kulola ametoa shukurani zake za dhati kwa familia yake, Kanisa la EAGT Lumala Mpya, ndugu, jamaa pamoja na marafiki kwa kuendelea kumuombea kwa huduma anayoifanya nchini Marekani ambapo watu wengi wanaokoka na kuponywa.
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola, akihudumu nchini Marekani.
Picha ya pamoja baada ya huduma katika jimbo la Boston
Mchungaji Kulola (katikati) na familia yake
Mchungaji Dkt.Daniel Kulola (kushoto), akiwa na Mama Mchungaji, Mercy Kulola(kulia).


HITILAFU YA MKONGO WA MAWASILIANO YATATIZA HUDUMA ZA TANESCO WILAYANI BAGAMOYO

$
0
0

Sehemu ya Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani 



NA MWANDISHI MAALUM

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) linaendelea kuwatangazia wateja wake wote wa Wilaya ya Bagamoyo kuwa, kutokana na kukatika kwa waya wa mawasiliano, (Optic Fiber) kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo, Ofisi ya Shirika hilo wilayani Bagamoyo bado inashindwa kutoa huduma za kupokea malipo na kuuza LUKU kwa muda mpaka hapo waya huo utakapoungwa. 

Kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Uhusiano MakaoMakuu yaTANESCO, Kwa sasa Shirika linawaomba wateja wake wanaotaka kununua umeme au kulipia huduma zingine za umeme kutumia njia mbadala ya mitandao ya Simu na makampuni mengine yenye mikataba na TANESCO.
Jitihada zinaendelea ili kuhakikisha mkongo huo wa mawasiliano unaungwa mapema iwezekanavyo.
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza. 

WAZIRI NAPE APOKEA UWANJA WA TAIFA WA UHURU, "SHAMBA LA BIBI" JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SERIKALI imekabidhiwa rasmi uwanja wa Taifa wa Uhuru, (pichani juu), jijini Dar es Salaam, leo Agosti 22, 2016, baada ya ukarabati mkubwa wa uwanja huo kukamilika.

Akipokea uwanja huo kwa niaba ya Serikali, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amewapongeza wakandarasi ambao ni kampuni ya China ya Beijing Construction Engineering Group Company Limited, (BCEG), na mshauri mwelekezi wa uwanja huo kampuni ya kizalendo chini ya uongozi wa ke, Injinia Aloyce Peter Mushi kwa kazi nzuri iliyofanyika licha ya mikwamo ya hapa na pale.

“Ndugu zetu Wachina, wameonyesha sio tu uhusiano mzuri bali wameonyesha kuwa wao ni ndugu zetu, kwani walishiriki wakati nchi yetu ikipata uhuru laini toka wakati huo hadi hivi sasa, bado wanashiriki katika kusaidia kuimarisha uchumi wetu,” alisema.

Waziri Nanuye aliwataka watumiaji wa uwanja huo kulipa ada za matumizi kama inavyostahili, ili hatimaye fedha hizo ziweze kugharimia matunzo ya uwanja.

Akitoa taarifa ya ujezni huo, mshauri huyo mwelekezi wa ujenzi, Injinia Aloyce Peter Mushi alisema, uwanja huo una uwezo wa kuchukua watu milioni 22 na ulikamilika na kuanza kutumika kwa mara ya kwanza Mei 22, 2015.

Naye Meneja Mkuu wa Kampuni ya BCAG, Cheng Long Hai, alisema, uwanja huo umewekewa mifumo yote muhimu kama vile tangi la kuhifadhia maji na mifumo ya maji taka, na kuishukuru serikaliya Tanzania kwa kuiaminikampuni yake kutekeleza mradi huo mkubwa.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel, alisema, amekuwa akipokea maombi mbalimbali ya wanamichezo na watu wengine kuomba kuutumia uwanja huo na kuwahakikishia kuwa utaratibu unapangwa ili watanzania waanze kufaidi matunda ya uwanja huo ambao kutokana na ukongwe wake ulipachikwa jina la shamba la bibi.

“Nitoe rai tu kwa watanzania, leohii Agosti 22, 2016 ambapo tumekabidhiwa uwanja huu rasmi ukiwa umekamilika, naomba hilo jina la shambala bibi nalo lifikie kikomo kwani uwanja huu sa sa unauonekano mpya na wa kisasa.” Alisema Profesa Gabriel.

Ukarabati huo mkubwa ulihusisha ujenzi wa jukwaa na paa, ikiwa ni pamoja na miundombinu mingine ya uwanja kama vile, mifumo ya kusambaza maji, na kutoa maji taka, uwekani wa tanki la kuhifadhia maji, pamoja na ujenzi wa vyoo vya kutosha uwanjani.
Waziri Nape akizungumza kabla ya kukabidhiwa uwanja huo Agosti 22, 2016. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Profesa Elisante Ole Gabriel, na kushoto ni mshauri wa ujenzi, Injinia Aloyce Peter Mushi (PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID)
Waziri Nape, (wapili kushoto), Katibu Mkuu Profesa Ole Gabriel, (wakwanza kushoto),


Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo, Alex Makoye Nkenyenge, (watatu kushoto) na Injinia Mushi, wakikagua uwanja huo
Waziri Nape, akikagua nyasi bandia uwanjani

Alama ya uwanja wa Uhuru ni jukwaa hili kuu, kama linavyoonekana leo Agosti 22, 2016
Vyoo vya kisasa, (kushoto) wanawakena kulia wanaume

Waziri akimpongeza Meneja wa Kampuni ya Kichina ya Beijing Construction Engineering Group Company Limited, (BCEG),
Cheng Long Hai
Katibu Mkuu Profesa Ole Gabriel, (kulia) na Meneja Mkuu wa (BCEG), Cheng Long Hai, wakisaini hati za makabidhiano ya uwanja mbele ya Waziri Nape
Waziri Nape akishuhudia makabidhiano ya hati kuthibitisha sasa uwanja uko mikononimwa serikali
Profesa Gabriel
Injinia Mushi
Cheng Long Hai
Waziri akizungumza jambo wakati wa ukaguzi wa nje wa uwanja huo

KOREA KUSINI YATOA BILIONI 8 KUJENGA KITUO CHA TAARIFA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

$
0
0
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo kwa Afrika katika Bnge la Korea Kusini wakiwasili katika uwanja mdogo wa ndege uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Meneja Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa,TANAPA,Victor Ketance akipokea ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi blog Kanda ya Kaskazini.
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kushirikiana na serikali ya Korea ya Kusini imeanza mchakato wa ujenzi wa kituo cha kimataifa cha kutunza tarifa za mienendo ya Wanyamapori kitakachojulikana kama Serengeti Internatinal Media Centre.
Kituo hicho kinachotarajiwa kugharimu zaidi shilingi bilioni nne kitajengwa katika Hifahi ya Taifa ya Serengeti .

Tayari serikali ya Korea Kusini imeshatuma wajumbe wake kuja nchini tanzania kujionea eneo kitakapojengwa kituo hicho na kukamilisha taratibu nyingine muhimu ambapo kiongozi wa wajumbe hao Park Joosung amesema mradi huo ni mwendelezo wa ushirikiano wa Korea Kusini na Tanzania katika kuimarisha uhifadhi.

Akizungumza na ujumbe huo mkuu wa hifadhi ya taifa ya serengeti Wiliam Mwakilema amesema kituo hicho kikikamilika kitaongeza chachu utalii na kitatoa fursa kwa wageni kuona aina nyingi zaidi za wanyama.

Naye mratibu wa ujenzi bw Victor Ketance amesema ujenzi utaanza mwezi october mwaka huu na unatarajiwa kumalizika baada ya miezi 14.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akipokea ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akisalimiana na wadau wa utalii,Zainabu Ansel ,Mkurugenzi wa kampuni ya Utalii ya Zara(katikati) na Mkurugenzi wa Kibo Safari's Willy Chamburo.(kushoto) waliokuwepo uwanjani hapo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kibo Safari's ,Willy Chamburo (katikati) akizungumza jambo na kiongozi wa ugeni wa Korea Kusini Won Yul Chui (kushoto) baada ya kukutana katika uwanja mdogo wa ndege uliopo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti William Mwakilema.
Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Afrika katika Bunge la Korea Kusini wakitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa kamati ya Maendeleoo ya Afrika ya Bunge la Korea Kusini waliofika katika Hifadhi hiyo kwa ajili ya ufuatiliaji wa maenedeleo ya kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha Taarifa katika Hifadhi hiyo.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema akiongoza Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini walioko katika kamati ya Maendeleo ya Afrika kutembelea maeneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa.
Moja ya eneo lilipo sasa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo inatumika kutoa taarifa kwa njia ya picha za video za Hifadhi hiyo.
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakitizama picha ya Hayati Baba wa Taifa ,Mwl Julius K. Nyerere akiwa na rafiki yake Prof,Dkt Bernhard Grzimek huku wakipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema.
Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakipata maelezo katika michoro ya kituo cha kisasa cha taarifa katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema akitoa zawadi kwa wajumbe wa Bunge la Korea Kusini mara baada ya kutembelea eneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa katika hifadhi hiyo.
Wajumbe wa Bunge la Korea Kusini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Shirika la Hifadhhi za Taifa (TANAPA ) na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.




BRAND NEW MUSIC: BEN SWAX ft KALA JEREMIAH KESHA (Official video)

RC SIMIYU AFAFANUA TAARIFA KUHUSU WALIMU WAKUU KUVULIWA MADARAKA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.

Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema(kulia) akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) wa kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akizungumza na Maafisa Elimu na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka.

Viewing all 3497 articles
Browse latest View live