Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

BUZWAGI YAIKABIDHI SH. MILIONI 700 WILAYA YA KAHAMA KAMA MALIPO YA HUDUMA

$
0
0
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya ushuru wa huduma kwa halmashauri ya mji wa Kahama, hafla hiyo ilifanyika baada ya kukamilika kwa hafla ya kukabidhi madarasa ya shule ya msingi Budushi na nyumba za walimu Mwime.
Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakishuhudia wakati wa hafla ya makabidhiano ya hundi

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
Mgodi wa Buzwagi umekabidhi wa halmashauri ya mji wa Kahama hundi yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba na kumi na saba (717,276,055/=) ikiwa ni sehemu ya malipo ya kodi ya huduma(service levy) ambayo hulipwa kwa halmashauri hiyo.

Akizungumzia malipo hayo ya hundi Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Mhandisi Asa Mwaipopo amesema kiasi hicho ni malipo ya kuanzia mwezi januari hadi juni mwaka huu.
Mwaipopo ameongeza kuwa licha ya Kampuni yake kulipa kodi mbalimbali na kujishughulisha katika kufadhili miradi ya Maendeleo, amesema ipo haja ya Jamii kuilinda na kuitunza miradi hiyo ili iwe na manufaa kwa Jamii nzima.

“Acacia kupitia Mgodi wetu wa Buzwagi tunajivunia kuwa wadau muhimu wa maendeleo wa halmashauli ya mji wa Kahama na serikali kwa ujumla, na tunafarijika sana kwa ushirikiano ambao tumekuwa tukiupata, ombi letu kwa Jamii zinazonufaika na miradi yetu kuilinda na kuitunza kwa manufaa ya Jamii nzima.”

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea hundi ya kodi ya huduma kutoka kwa uongozi wa Mgodi wa Buzwagi na baadae kuikabidhi kwa mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutekeleza miradi ya Maendeleo”

Akizungumza kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.
Mbunge wa Kahama Mjini Mhe. Jumanne Kishimba akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 700
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu wakati wa makabidhiano ya hundi ya malipo ya huduma.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu akihutubia wananchi wa Kahama wakati wa kupokea hundi ya ushuru wa huduma
Baadhi ya wananchi katika wilaya ya Kahama wakishuhudia makabidhiano hayo.





RAIS MAGUFULI AZUNGUMZA NA WANANCHI MAENEO MBALIMBALI AKIWA NJIANI KUELEKEA MWANZA MJINI

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanahabari baada ya kuhutubia maeneo mbalimbali akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanahabari baada ya kuhutubia maeneo mbalimbali akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongela akitoa taarifa fupi kwaRais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kabla kumualika kuongea na wakazi wa Sengerema akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
Dkt. Charles John Tizeba ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Buchosa na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi akisalimia wananchi mjini Sengerema kabla Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli hajaongea
Mbunge wa Sengerema Mhe. William Ngeleja akiwashukuru wananchi wa jimbo lake kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli jimboni mwake akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
Wakazi wa Sengerema wakimshangilia Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipozungumza nao akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi wa Sengerema akiwa njiani kuelekea jijini Mwanza
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wakazi na wasafiri mbalimbali wa eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Bw. Gerson Msigwa akimsaidia mwanahabari wa ITV kuripoti ziara ya Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza na wakazi na wasafiri mbalimbali wa eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini.
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Misungwe Mhe. Charles Kitwanga baada ya kuzungumza na wakazi na wasafiri eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini.
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mwalimu Mstaafu Mama Zena Seif (61) ambaye alimfundisha darasa la tatu wakati akisoma shule ya msingi ya Chato. Hii ni baada ya kuzungumza na wakazi na wasafiri mbalimbali wa eneo la Busisi kabla ya kuvuka na kuelekea Mwanza mjini.

Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na wabunge na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Mwanza akiwa katika pantoni MV Misungwi wakati akivuka kuelekea Mwanza mjini.
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na wabunge na baadhi ya viongozi wa mkoa wa Mwanza akitoka kwenye pantoni MV Misungwi wakati akivuka kuelekea Mwanza mjini.
Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wananchi eneo la Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi.
  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia wananchi eneo la Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi.

  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia mtoto na mama yake baada ya kuongea na wananchi eneo la  Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia wananchi mbalimbali wa Kigongo mara baada ya kuvuka upande wa pili kutokea Busisi. 
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mbunge wa Misungwe Mhe. Charles Kitwanga akimtajia badhi ya changamoto jimboni kwake mbele ya  wakazi  wa Usagara katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Mkuu wa Wilaya Mstaafu wa Biharamulo akiongea na kumkaribisha  mbele ya  wakazi  wa Usagara katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na  Mkuu wa Wilaya Mstaafu wa Biharamulo  eneo la Usagara katika jimbo la Misungwi mkoani Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na wakazi mbalimbali wa Usagara
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wakazi mbalimbali wa Usagara
 Wakazi wa Usagara wakimuaga Rais
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono kuwaaga wakazi mbalimbali wa Usagara
 Sehemu nyingi alikuta wananchi wametanda barabarani wakimtaka awasalimu na kuongea nao
 Mbunge wa Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula akiongea na wananchi waliokuwa wametanda barabarani kutaka kumsikia Rais
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Buhongwa nje kidogo ya jiji la Mwanza
  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mamia ya wananchi wa Mwanza waliofurika barabarani kumsubiri
 Palikuwa hapatoshi
 Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anawaambia wananchi kwamba yeye ni Rais wa kila mtu nchini na atawatumikia wote bila kuwabagua
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli huku wakimtaka aendelee kuongea nao
  
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Kila mtu alikuwa na shauku yakumuona na kumsikia Rais
 Wengi walitumia simu zao za mkononi kunasa kila alichokisema
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Wananchi wameziba njia ili kumtaka Rais asiwapite bila kuongea nao
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuongea na wananchi wa Mwanza 
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahakikishia wananchi wa Mwanza kwamba atawatumikia wote bila kujali dini zao, makabila yao wala  itikadi zao za kisiasa
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
  Wananchi wa Mwanza wakimshangilia  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli 
 Msafara unapokaribia katikati ya jiji la Mwanza unakutana na umati mkubwa wa wananchi
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anajikuta hana jinsi bali kuzungumza nao 
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katikati ya jiji la Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiendelea kuzungumza na wananchi katikati ya jiji la Mwanza.
  Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi katikati ya jiji la Mwanza.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiaga baada ya kuzungumza na wananchi baada ya kuwasili katikati ya jiji la Mwanza. PICHA ZOTE NA IKULU

WADHAMINI WARUDISHA HADHI YA SHINDANO LA MISS TANGA 2016

$
0
0
Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha akiwapungia mikono wananchi waliojitokeza kushuhudia shindano hilo mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi

Miss Tanga 2016, Eligiva Mwasha akiwapungia mikono watazamaji waliojitokeza akiwa na mshindi wa pili na tatu katika Shindano hilo ambalo liliandaliwa na Radio Tanga Kunani (TK) na Hotel ya Tanga Beach Resort.

Warembo walioingia tano bora wakiwa jukwaani


Kamati ya Miss Tanzania nao walikuwepo wakifuatilia shindano hilo ambalo lilifanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort mjini Tanga.


Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF) Mussa Mbaruku akizungu mza wakati wa shindano hilo


Msanii Nevy Kenzo akitumbuiza wakati wa shindano la kumtafuta mlimbwende wa mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)lililofanyika hivi karibuni kwenye hotel ya Tanga Beach Resort



WAKATI shindano la kumsaka malkia wa Mkoa wa Tanga (Miss Tanga 2016)likifanyika mwishoni mwa wiki na hatimaye mrembo Eligiva Mwasha kuibuka na ushindi kwenye kinyang’anyiro hicho dhidi ya washiriki wengine 10. 

Shindano hilo ambalo lilisimama kwa muda baada ya serikali kulisimamisha lile la Taifa msimu huu lilionekana kuwa na msisimuko wa hali ya juu kuanzia wapenzi,wadau na washiriki iliyochangiwa na waratibu wa shindano hilo Radio ya Tanga Kunani FM (TK) wakishirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort. 

Ushindani wa washiriki hao ulianza kuonekana tokea wakati warembo hao wakiwa kwenye kambi yao ambayo ilifanyika kwenye hotel hiyo ambapo kila mmoja alionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuondoka na taji hilo. 

Hali iliendelea kuwa ya mvutano zaidi baada ya baadhi ya washiriki kuaga mashindano hayo na kutoa fursa yaw engine kuingia nafasi ya tano bora katika kinyanganyiro hicho ambacho kilihudhuriwa na wapenzi wengi kuliko kawaida. 

Kitendo hicho kinaonekana kinawezesha kurudisha hamasa na heshima ya shindano hilo ambalo hufanyika kila mwaka mkoani hapa lakini pia kuhamasisha hasa vijana kujitokeza kwa wingi kushiriki msimu ujao. 

Katika shindano hilo nafasi ya pili ilichukuliwa na Aisha Ally huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Rukaiya Hassani katika shindano hilo ambalo lilikuwa na ushindani mkubwa kutokana na kusheheni warembo wakali. 

Halikadhalika nafasi ya mrembo kwenye kipaji katika shindano hilo ilinyakuliwa na Edna Chisabo ambapo kinyang’anyiro hicho kilifanyika siku moja kabla ya onyesho la kumsaka mrembo wa mkoa huu kwenye ukumbi wa Tanga City Lounge uliopo mjini hapa. 

Licha ya kufanyika shindano hilo lakini yapo mambo ambayo kimsingi yameweza kuleta msisimuko na kulifanya kuonekana kuwa na ubora wa hali ya juu.  Mambo hayo ndio yamechangia kwa asilimia kubwa kupelekea shindano hilo kuwa na mvuto mkubwa kuliko mashindano mengine ambaye yalikwisha kufanyika mkoani hapa lakini pia uwepo wa watazamaji wengi. 

La kwanza ni eneo ambapo onyesho hilo limefanyika,moja kati ya mambo ambayo yalichangia kuonekana kuwa na mvuta mkubwa ilitokana na shindano hilo msimu huu kufanyika kwenye Hotel ya Tanga Beach Resort. 

Tunasema hivyo kwa sababu kila mtu anapokwenda kuangalia burudani ya aina yoyote lazima aangalia ulinzi na uimara wa eneo husika hasa ukizingatia wapo baadhi yao huenda na vyombo vyao vya usafiri. 

Kama ujuavyo ulinzi wa mahali husika ndio huwafanya watu kwenda kupata burudani lakini pia ni eneo tulivu ambalowatu wanaweza kufanya mambo yao kila kupata usumbufu wa aina yoyote.  Jambo hilo limesababisha baadhi wa watu kuacha kwenda kwenye maeneo yaliyopo karibu nao na kwenda maeneo mengine ya mbali kwa ajili yakusaka utulivu lakini pia ulinzi. 

Jambo jingine ambalo lilisababisha onyesho hilo kuwa bora ni uwepo wa warembo makini na wenye muonekana bomba na hivyo kupelekea wapenzi na wadau wao kujitokeza kwa wingi kushuhudia mtanange huo ambao ulikuwa wa aina yake.
Kilicholifanya shindano hilo kuendelea kuvutia wapenzi na mashabiki ambao walijitokeza ni wasanii ambao walikuwa wakitumbuiza kabla ya kuanza.
Wasanii wanaounda kundi la Nevy Kenzo wazee wa Kamati Chini ilikuwa ni kichocheo kikubwa cha umati mkubwa wa wadau wa tasnia ya urembo na burudani kujitokeza kwa wingi kushuhudia shindano .
Nevy Kenzo ambao walipanda jukwaani kutumbuiza walisababisha ukumbi mzima kulipuka kwa shangwe na nderemo huku baadhi yao wakiimba nyimbo zao ikionyesha namna wanavyokubalika.
Nevy Kenzo wakati akiimba ilifikia wakati mpaka wapenzi na mashabiki wa tasnia ya urembo waliviona viti vyao vya moto na kulazimika kupanda jukwaani kucheza sambamba na wasanii hao.
Haikuishia hapo lakini wasanii ambao walipanda jukwaani kabla ya Nevy Kenzo kutumbuiza wa Kundi la Wazenji Classic lenye makazi yake mjini Tanga walikuwa na moto na kusababisha shangwe kila mahali.
Shangwe hizo zinaonyesha namna kundi hilo lilivyoweza kujizolea
umaarufu mkubwa ndani na nje ya Tanga hasa kwa kipindi kifupi kutokana na aina ya mziki ambao wanaufanya staili ya mduara na bongo fleva.
Sababu kubwa ya kuona kundi hilo kuonekana litakuwa hatari ni namna wanayoweza kulitawala jukwaa wanapokuwa stejini na kuonekana kuinua mara kwa mara wapenzi na mashabiki wao
Suala jingine ambalo lilikuwa kivutio kikubwa ni namna warembo
walivyokuwa wakipanda jukwaani na kuanza kujitambulisha na kujielezea kwa watazamaji.
Hali hiyo ilisababisha wakati mwengine baadhi ya warembo kupanda jukwaani kwa madoido makubwa kwa lengo la kuonyesha umahiri wao ili kuwashawisha majaji kuwapa alama nzuri.
Mbunge wa Jimbo la Tanga atinga Miss Tanga.


Kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Tanga (CUF)Mussa Mbaruku kuhudhuria shindano la kumsaka mlimbwende wa mkoa wa Tanga mwaka huu kilionyesha namna alivyokuwa kiongozi mpenda michezo na kuithamini.



Mbunge huyo ambaye alikuwa kwenye shughuli zake za kikazi lakini alilazimika kuungana na wakazi wa jimbo lake kumshuhudia mrembo ambaye anapatikana.



Akizungumza mara kabla ya kutangaza mshindi wa Taji la Miss Tanga 2016,Mbunge Mussa alisema tasnia ya urembo imekuwa ikiwapa vijana maisha mazuri lakini pia imekuwa ni daraja la wao kupata mafanikio



Alisema lazima watanzania ikiwemo wazazi kubadilika na kuondokana na dhana ya kuwa ya kuwa urembo ni suala la uhuni kwani imekuwa ikisaidia vijana wengi kupata maendeleo.



"Ndugu zangu lazima tubadilike na kuishi kutokana na utandawazi

uliopo ile dhana ya kuwa urembo ni uhuni mimi nadhani imepitwa na wakati na uhuni mtu anaweza kuwa nao hata asiposhiriki mashindano hayo hivyo wazazi na walezi ruhusuni watoto wenu washiri kwenye mashindano haya "Alisema.



Mussa alisema kuwa anaamini washindi wa shindano hilo wataweza

kuuwakilisha vema mkoa wa Tanga kwenye mashindano ya Kitaifa na kuweza kushinda kama walivyofanya kwenye onyesho hilo.



“Ninaimani kubwa na washindi ambao wamepatikana kwenye shindano hilo wanaweza kuwa chachu ya mabadiliko kwenye tasnia ya urembo mkoa huu kwani wanaweza hata kuleta taji la Miss Tanzania msimu huu “Alisema.



"Neno la Mshindi wa taji la Miss Tanga 2016 Eligiva Mwasha" Alisema kuwa kwanza anawashukuru wakazi wa Mkoa wa Tanga kwa ujumla kwa sapoti yao walionyesha katika fainali za miss tanga 2016 na yeye kupata fursa ya kunyakua taji hilo



Licha ya kuibuka na ushindi lakini niwaombe niombea kwani kwa sasa safari aliokua nayo bado kubwa sana kwani anamtihani wakwenda kuiwakilisha Tanga katika fainali za Miss Kanda na badae kulekea Katika fainali za miss Tanzania baadae mwaka huu.

DALADALA LAPINDUKA KITUONI MBAGALA-SABASABA JIJINI DAR ES SALAAM, WATU KADHAA WAJERUHIWA

$
0
0


HABARI/PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID


DALADALA namba T274 DEX,(pichani), lililokuwa likisafiri kutoka Mbagala RangiTatu kuelekea Temeke jijini Dar es Salaam, limeanguka mita chache kutoka kituo cha Daladala Sabasaba-Mbagala leo asubuhi Agosti 11, 2016 na kujeruhi watu kadhaa.

Mashuhuda wanasema, Daladala hilo lililokuwa katika mwendo kasi, liliserereka na kuacha njia wakati likikaribia kusimama kituoni. Dereva wa Daladala hilo aliruka na kukimbia, nakuwaachaabiria wakitaharuki kila mmoja akijaribu kukoa maisha yake.

“Unajua mvua hizi zilizonyesha asubuhi zinafanya barabara iteleze na hawa jamaa mwendo wao unajua tena, sasa alijaribu kufunga breki gari likaanza kuserereka na alipojaribu kurudi barabarani likakataa na kutumbukia mtaroni,” anasimulia mmoja wa mashuhuda aliyekuwa eneo la ajali.

Polisi wa usalama barabarani alifika muda mfupi baada ya ajali hiyona taratibu ya kuliondoa gari hilo zilianza. Abiria wote walitoka salama, wachache walijeruhiwa na baadhi yao walionekana wakilia kutokana na mshtuko wa ajali hiyo ya asubuhi.
Mmoja wa abiria aliyenusurika akilia kwa huzuni kutokana na ajali hiyo
  Mmoja wa abiria aliyenusurika akilia kwa huzuni kutokana na ajali hiyo
Wapita njia wakimuuliza abiria huyu (aliyekaa), ambaye alikuwa ndani ya daladala hilo
Polisi wa usalama barabarani, akikagua mazingira ya ajali hiyo huku akizungumza na simu yake ya mkononi
Mtu huyu ambaye haikujulikana maramoja kama ni muhudumu wa daladala hilo au abiria akitoka ndani ya daladala hilo baada ya "kupiga mwereka'
Mashuhuda kama kawaida yao

MAXMALIPO KUTUMIKA KUJAZA SALIO KWENYE KADI ZA MABASI YA MWENDO KASI

$
0
0
Mkuu wa kitengo cha biashara Kampuni ya Maxmalipo Bw.Deogratius Lazari Akifafanua Jambo kwa Waandishi wa habari na Kushoto ni Mkuu wa uendeshaji Kampuni ya Maxmalipo Bw. Ahmed Lussasi


Mkurugenzi Uendeshaji wa kampuni ya Maxmalipo (kulia) Bw. Ahmed Lussasi Akielezea Jinsi kampuni ilivyo piga hatua katika teknolojia, Kushoto ni Msemaji wa kampuni ya Uendeshaji wa Mabasi ya mwendo haraka Bw. Deus Bugaywa .

Kuanzia sasa wasafiri wenye kadi maalumu za Usafiri (Dart card) wameongezewa njia mbadala za kuweka salio katika kadi zao za Usafiri kwa kuwatumia mawakala wa Maxmalipo. Mteja mwenye kadi hii ya usafiri anaweza kufika kwa Wakala yeyote wa Maxmalipo na kuweka salio kiasi chochote kwenye kadi yake

Akiongea kwenye uzinduzi huu afisa Mwendesgaji mkuu wa Maxmalipo Bw. Ahmed Lussasi Amesema “ Lengo kubwa la kampuni ya Maxcom Africa imekua ni kujenga na kutengeneza mifumo imara na madhubuti ambayo inalenga kurahisisha ukusanyaji wa mapato kwa njia ya kielektroniki pia kusimamia na kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kwa kutumia mifumo ya Kielektroniki. Bw. Ahmed ameendelea kuelezea kwamba Tangu Mradi huu wa Mwendo kasi umeanza kumekua na maboresho mbalimbali na mbinu za kitaalamu zinazopelekea kukua kwa makusanyo, kuepusha na kudhibiti upotevu wa Mapato na kuhakikisha kuna uwazi wa hali ya juu katika utoaji wa taarifa za makusanyo (Real time Revenue reporting)”

Naye Msemaji wa kampuni ya undeshaji wa Mabasi haya ya Mwendokasi Bw. Deus Bugaywa Ameelezea kwa Ufupi mafanikio kampuni iliyo yapata kwa kutumia mifumo hii ya kielektroniki moja ikiwa ni uhakika wa mapato, ukuaji wa mapato pamoja na usalama wa fedha zao”. Deus ameongeza kwa kusema “ Naweza kuwadhihirishia kwa ushirikiano huu tulio nao na Maxmalipo katika mradi huu umeleta Mageuzi makubwa katika sekta ya usafirishaji nchini kwetu barani Africa na Duniani kwa ujumla; Huu ndio mfumo pekee unaowezesha watu kuweka salio katika kadi zao kupitia MItandao ya simu na ndio mfumo Pekee uliokua kiteknolojia ndani ya muda mfupi Zaidi, na leo salio na ticket vinaweza kupatikana kwa mawakala waliopo hata mitaani (hawa wa Maxmalipo). Ni pongezi kwa Maxmalipo kama kampuni ya kitanzania kwa kufanya haya, lakini Zaidi Tutoe shukrani zetu kwa serikali kwa kuunga mkono Jitihada hizi katika sekta nzima ya usafiri.

Naye Mkuu wa Kitengo cha biashara katika kampuni ya Maxmalipo – Bw. Deogratius Lazari , amwewaambia wana habari kwamba Maxcom Africa ina Zaidi ya mawakala 15000 nchi nzima ambao wamewezeshwa kutoa huduma hii kwa watumiaji wa kadi hizi za mwendo haraka. Bw Deogratius ameainisha pia kwamba Mawakala hawa wa Maxmalipo wapo jirani na makazi ya watu hvyo wasafiri wanaweza kujipatia huduma hii kabla ya kufika kwnye vituo vya mabasi ya mwendo haraka.

Kufuatia Uzinduzi huu kampuni ya Maxcom Africa inatarajia kupungua kwa foleni za abiria kwnye vituo vya mabasi ya mwendo hasa wale wanaokua wakihitaji kuweka salio kwnye kadi zao pia wanataraji kuongezeka kwa Ajira katika sekta isiyo rasmi kwa watanzania wengi kuchamgamkia Fursa ya kuwa mawakala wa Maxmalipo ambayo itawaongezea kipato.

Maxcom Africa imekua ni Moja ya Kampuni za Kitanzania iliyofanikiwa sana katika uwekaji wa mifumo madhubuti ya ukusanyaji na usimamizi wa mapato hapa Tanzania hasa katika miradi mikubwa ikiwamo huu wa mabasi ya Mwendo Kasi, TRA, Vivuko, Mahospitali (Moi) na kwenye Kodi za halmashauri.

SERIKALI YAFAFANUA UPUNGUFU WA CHANJO YA KICHAA CHA MBWA NA HOMA YA MANJANO

$
0
0
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mohamed Mohamed akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya hatua iliyochukuliwa na Serikali kuagiza na kusambaza dozi mbalimbali za chanjo kupitia mpango Serikali wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chanjo uliojitokeza nchini.

Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Dafrosa Lyimo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari kuhusu mpango wa utoaji wa chanjo zilizokuwa na upungufu zikiwemo za kifua Kikuu, Polio, Surua na Lubela ambazo MSD wamekwisaha anza kuzisambaza.


Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Bohari Kuu ya Dawa (MSD) inatarajia kupokea dozi 14,000 za chanjo ya homa ya manjano mwanzoni mwa mwezi Septemba, 2016 ili kutosheleza mahitaji ya wasafiri watakaohitaji huduma hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima.

Aidha, Wizara hiyo imekwisha nunua dozi za chanjo ya Kifua Kikuu na Polio 739,700 na kusambaza dozi zipatazo milioni 7 kwenye mikoa ya Morogoro, Singida, Dodoma, Tabora na Kigoma.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mohamed Mohamed amesema kuwa uagizaji na usambazaji wa dozi hizo ni mpango Serikali wa kukabiliana na changamoto ya upungufu wa chanjo uliojitokeza nchini.

Akifafanua kuhusu kukosekana kwa baadhi ya chanjo ikiwemo ya Homa ya Manjano amesema hali hiyo imetokana na kutokea kwa mlipuko wa homa hiyo katika nchi za jirani ikiwemo Angola jambo lililosababisha akiba ya chanjo hiyo dunia nzima kupelekwa kwenye nchi zenye mlipuko wa ugonjwa huo kwa lengo la kuwachanja wananchi wote ili kuzuia ugonjwa huo kusambaa.

Amesema kutokana na hali hiyo akiba iliyokuwa imewekwa kwa ajili ya kuzigawia nchi nyingine hasa matumizi kwa ajili ya wasafiri ilibidi ipelekwe katika maeneo yaliyokuwa na upungufu wa dozi hizo kutokana na uharaka na uhitaji wa chanjo hizo.

Amesema wizara kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) inatekeleza mradi wa majaribio wa kutokomeza kichaa cha mbwa kwenye mikoa ya Lindi, Mtwara, Morogoro, Pwani na Dar es salaam ambayo sasa ina chanjo za kichaa cha mbwa.

Amebainisha kuwa jijini Dar es salaam chanjo hizo zinapatikana katika hospitali ya wilaya ya Temeke, Kituo cha Afya Magomeni.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara hiyo Dk. Neema Rusimabayila akitoa ufafanuzi kuhusu baadhi ya watoto waliokosa chanjo katika awamu tofauti amesema kuwa wote waliokosa chanjo kuhakikisha kuwa wanamaliza chanjo zao kwa mujibu wa idadi ya chanjo walizopangiwa pindi zitakapopatikana.

Ametoa wito kwa wataalam wa afya wanaohusika na utoaji wa chanjo kuwapatia taarifa wazazi wenye watoto ambao walihudhuria vituo vya afya kisha kukosa chanjo hizo, kuhakikisha kuwa wanarudi katika vituo vya afya ili waweze kumalizia idadi ya chanjo walizotakiwa kupata pindi zitakapofikishwa kwenye vituo vyao.

Kuhusu Mradi wa majaribio wa kipindi cha miaka 5 wa chanjo ya kichaa cha mbwa wenye lengo la kuondoa kichaa cha mbwa amesema kuwa unalenga kupunguza idadi ya wagonjwa na vifo vya watu vinavyotokana na kichaa cha mbwa.

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Chanjo wa Wizara hiyo Dk. Dafrosa Lyimo akifafanua kuhusu mpango wa utoaji wa chanjo zilizokuwa na upungufu hizo amesema kuwa mpaka sasa utaratibu wa kupokea chanjo zaidi zikiwemo za kifua` Kikuu, Polio, Surua na Lubela ambapo MSD wamekwisaha anza kuzisambaza.
Ametoa wito kwa wazazi wenye watoto waliokosa chanjo kuwasiliana na vituo husika ili waweze kupangiwa ratiba ya kupatiwa chanjo hizo kwenye vituo vya kutolea huduma vya serikali ndani ya umri wa miaka 5. 

WANAOSAFIRI NJE YA NCHI WATAHADHARISHWA KUHUSU KADI YA HOMA YA MANJANO

$
0
0
Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara hiyo Dk. Neema Rusimabayila akitoa ufafanuzi kuhusu mkakati wa Serikali kudhibiti vitendo vya baadhi ya watumishi wa afya wasiowaaminifu ambao hulipwa fedha ili waweze kuwatengenezea wasafiri kadi za Chanjo ya Homa ya Manjano na kisha kuzitumia nje ya nchi jambo ambalo kinyume cha sheria na hatari kwa usalama wa Afya zao.


Aron Msigwa - Dar es Salaam.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewatahadharisha wananchi wanaopanga kusafiri kwenda nje ya nchi kuhakikisha kuwa wanafika katika vituo vya afya na kuchanjwa chanjo ya kuzuia maambukizi ya Homa ya Manjano badala ya kuwalipa fedha baadhi ya watumishi wa afya wasio waaminifu ili wawatengenezee kadi za chanjo kinyume cha sheria.

Mkurugenzi wa Huduma za Kinga wa Wizara hiyo Dk. Neema Rusimabayila akitoa ufafanuzi kuhusu suala hilo leo jijini Dar es salaam amesema baadhi ya wasafiri wamekuwa wakishirikiana na watumishi wa afya wasiowaaminifu kwa kuwalipa fedha ili waweze kuwatengenezea kadi hizo na kisha kuzitumia nje ya nchi jambo ambalo ni hatari kwa usalama wa Afya zao.

“Kumekuwa na baadhi ya watumishi wasio waaminifu ambao hupokea fedha na kisha kutengenezesha kadi za wasafiri zinazoonesha kuwa wamepatiwa chanjo, Jambo hili ni hatari kwa afya ya msafiri, sasa tunaona mlipuko wa ugonjwa huu ukitokea katika nchi za karibu ni muhimu mtu kuchanja ili kuepuka kuwa chanzo cha kuleta ugonjwa huu” Amesisitiza Dk.Neema.

Amesema ni jambo lisilokubalika kwa msafiri kubeba kadi ya chanjo ya Kinga ya Homa ya Manjano ili hali akijua kabisa hajachanjwa chanjo hiyo na kuongeza kuwa jambo hilo linamuweka muhusika katika hatari ya kupata maambukizi akisafiri kwenye nchi zenye mlipuko wa ugonjwa huo.

“Napenda kusisitiza kuwa ni muhimu sana msafiri akachanjwa chanjo hii kwa ajili ya kinga ya afya yake mwenyewe, kupata kadi bila kuchanjwa na kwenda mahali ambapo kuna ugonjwa huu ni kujidanganya, epuka kuwa chanzo cha kusambaza ugonjwa huu” Amesisitiza Dk. Neema.

Kuhusu gharama za chanjo hiyo amesema kuwa msafiri anayetaka kupata chanjo hiyo anatakiwa kulipia gharama ya Elfu Ishirini (20,000/=) ikiwa ni malipo halali ya Serikali na mlipaji hupatiwa stakabadhi halali.

Aidha, amesema mbali na hatua zinazochukuliwa kudhibiti hali hiyo, Wizara inakamilisha utaratibu wa kuwa na kadi maalum ambazo zitakuwa tofauti, zenye nembo maalum ambazo mtu hataweza kughushi wala kufanya udanganyifu wa aina yoyote.



MHE.ZAMBI APOKEA KADI YA MFUMO WA "WOTE SCHEME" KUTOKA PPF

$
0
0
PPF Kadi ya Wote Scheme
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akipokea kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme" kupitia Mfuko wa Pensheni wa PPF kutoka kwa Meneja wa PPF kanda ya Kusini Ndg. Kwame Temu.
PPF Kadi ya Wote Scheme

Meneja wa PPF kanda ya Kusini Ndg. Kwame Temu akimueleza jambo Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi wakati wa kumkabidhi Kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme".
PPF Kadi ya Wote Scheme
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi akitoa neno la shukrani kwa Meneja wa PPF (Hayupo pichani) wakati wa kupokea kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme" kupitia Mfuko wa Pensheni wa PPF.

Na. Fungwa Kilozo, Lindi

Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Godfrey Zambi ameweza kupokea Kadi ya Mfumo wa "Wote Scheme" kupitia Mfuko wa Pensheni wa PPF.

Mhe. Zambi amepatiwa kadi hiyo ikiwa ni Siku nne tu zimepita baada ya Kujiunga na Mfumo huo katika Banda la PPF lililokuwa katika maonyesho ya Kilimo na Biashara Nane nane yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Lindi katika Viwanja vya Ngongo.

Katika Hafla hiyo ya makabidhiano ya Kadi hiyo Mh. Zambi ameutaka Mfuko wa PPF kutanua wigo na kuwafikia wananchi wengi zaidi hasa wale wa vijijini kwani amesema kuwa mfuko huo unafaida nyingi ambazo wananchi hao ambao hawajabahatika kufika katika banda la maonyesho ya Nane nane watazikosa hasa mfumo wa "Wote Scheme" ambao hata yeye amefurahishwa nao na akaamua kujiunga.

WIMBO MPYA WA WAPANCRAS WAKIMSHIRIKISHA ABUU MKALI-NITUNZIE SIRI WATOKA RASMI

$
0
0
Kundi la muziki la Wapancras linalojumuisha wasanii ndugu, Mecrass na Payus, la Jijini Mwanza, limeachia wimbo mpya uitwao "Nitunzie Siri", wakimshirikisha Abuu Mkali.

Wimbo umetengenezwa pande za Vibe Nation & Quick Sound ikiwa ni mikono ya Producers, Aniwylee na Day Dream.
Bonyeza HAPA Kusikiliza au bonyeza play hapo chini.
 Na BMG

MWENYEKITI WA CCM RAIS DKT MAGUFULI APOKELEWA DSM KWA NDEREMO NA VIFIJO

$
0
0

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipungia wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere, Jijini Dar es salaam kabla ya kwenda kuwahutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es salaam.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akifurahia burudani za aina mbalimbali wakati alipowasili Jijini Dar es salaam leo, akitokea Jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipiga ngoma kutoka kwa moja ya vikundi vilivyokuwepo uwanjani hapo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiwapungia wananchi waliofika Uwanjani hapo kumlaki leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndehe wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanaCCM pindi alipowasili Ofisi Ndogo ya Chama hicho, Mchana wa leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongozana na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana, Naibu Katibu Mkuu Bara, Ndg. Rajab Luhwavi mara baada ya kuwasili Ofisi ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es salaam leo.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisaini Kitabu cha wageni kwenye Ofisi Ndogo ya CCM, iliopo Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akikifanya Mazungumzo na Viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, katika Ofisi Ndogo ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es salaam leo agosti 12, 2016.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ndg. Ramadhan Madabiba.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisikiliza jambo kutoka kwa Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana .
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwa na Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson.
Mke wa Rais, Mama Jannet Magufuli akiwasalimia wananchi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wana-CCM wa Dar es salaam baada ya kupokelewa kwa nderemo na vifijo Ofisi Ndogo za CCM mtaa wa Lumbumba jijini Dar es es salaam leo agosti 12, 2016.
Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda akiteja jambo na Wakuu wa Wilaya za Ilala (Sophia Mjema) na Kindondoni (Ally Hapi).



TANZANIA KUTUMIA DOLA MIL500 KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba akifungua warsha ya wadau wa kuhusu ripoti ya taarufa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Veta mjini Tanga kulia ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi na kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi akizungumza katika warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika kwenye ukumbi wa Veta Mkoani Tanga.


Baadhi ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya Taarifa ya Mchango wa Tanzania katika Juhudi za Kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini Tanga wakimsikiliwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba alikuwa akifungua mkutano huo




Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo kulia ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi kushoto ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani Richard Muyungi



TANZANIA inatarajiwa kutumia takribani dola mil500 hadi ifikapo mwaka 2030 ili kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchi.

Kiasi hicho cha bajeti kinatarajiwa kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo itasaidia kupunguza juhudi za kupunguza joto zinazosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Aliitaja baadhi ya miradi ambayo itatekelezwa ili kupunguza gesi joto hapa nchini kuwa ni dampo la mtoni katika Jiji la Dar Es Salaam,miradi ya nishati jadidifu katika maeneo ya Mbinga,Makete,Njombe Usa River na Ifakara.

“Miradi hiyo yote inajumla ya megawati tano(5MW) za uzalishaji wa hewa ukaa ambapo iwapo hatua za haraka hazitaweza kuchukuliwa athari za kimazingira zinaweza kuendelea kujitokeza”alisema Waziri Makamba.

Ambapo alisema katika kushiriki juhudi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi joto tayari serikali ya Tanzania imeshaanza kutoa fursa kwa wadau ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi .

Makamba alisema kuwa mikakati hiyo kwa sasa imeshaanza kutekelezwa katika ngazi za mikoa wilaya pamoja na Halimashauri mbalimbali hapa nchini.

“Juhudi za serikali ni kuhimiza matumizi ya gesi asilia katika uzalishaji wa nishati ya umeme yanaongezeka ili kuweza kupunguza matumizi ya vifaa vinavyozalisha hewa ukaa ili kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya tabia nchi”alisisitiza Waziri Makamba.

Kwa upande wake Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani Richard Muyungi alisema kuwa sasa wapo kwenye mkakati wa kutoa elimu kwa wadau wa mazingira kwenye kanda mbalimbali nchini.

Alisema ilikuweza kuwa na mipango madhubuti katika utekelezaji mkakati wa taifa wa mawasilinao wa mabadiliko ya tabia nchi kupitia wizara za kisekta.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

LAPF YAWAFUNDA WAHARIRI WA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MAANDALIZI KABLA YA KUSTAAFU

$
0
0
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akizungumza wakati wa semina na wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali kuhusu maandalizi ya mafao ya kustaafu inayofanyika kwenye jengo la LAPF Tower Makumbusho jijini Dar es salaam, ambapo mada mbalimbali zimetolewa kuhusu mafao yanayotolewa na mfuko huo Kutoka kulia ni Kafifi Kafifi Afisa Matekelezo Mwandamizi Kanda ya Mashariki LAPF, Amina Kassim Meneja wa Kanda LAPF.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe akizungumzawakati wa semina ya wahariri wa Vyombo vya habari mbalimbali kuhusu maandalizi ya mafao ya kustaafu inayofanyika kwenye jengo la LAPF Tower Makumbusho jijini Dar es salaam, Kutoka kulia ni Kafifi Kafifi Afisa Matekelezo Mwandamizi Kanda ya Mashariki LAPF, Amina Kassim Meneja wa Kanda LAPF, Theophil Makunga Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri na kushoto ni Victor Kikoti Meneja Matekelezo LAPF.
Baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari wakiwa katika semina hiyo inayofanyika kwenye jengo la LAPF Tower jijini Dar es salaam.

Afisa Habari wa LAPF Rehema Mkamba akigawa vifaa kwa ajili ya semina ya wahariri wa vyombo vya habari katika semina ya mafao ya kustaafu yaliyofanyika kwenye jengo la LAPF Tower jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri TEF Bw. Thephil Makunga akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, kulia ni Amina Kassim Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki na kushoto ni Meneja Masoko na Mawasiliano wa Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa LAPF Bw. James Mlowe
Amina Kassim Meneja wa LAPF Kanda ya Mashariki akitoa mada katika semina hiyo

VIONGOZI WA CUF WAKIONGOZWA NA MAALIM SEIF WAMTEMBELEA SPIKA WA BUNGE

$
0
0
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akiwaeleza jambo viongozi wa CUF walioongozwa na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo Agosti 13, 2016. Mhe. Spika, Job Ndugai amerejea nchini hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akifurahia jambo na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Katikati) na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Julius Mtatiro waliomtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam leo leo Agosti 13, 2016 .
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (Kulia) akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (kushoto) aliyeambatana na viongozi wenzake wa CUF nyumbani kwa Mhe. Spika Job Ndugai leo leo Agosti 13, 2016 jijini Dar es salaam.
Naibu katibu mkuu wa CUF, Bara na Mbunge wa Kaliua, Tabora Mhe. Magdalena Sakaya akimweleza jambo Mhe. Spika, Job Ndugai (hayupo pichani) mara baada ya kumtembelea Mhe. Spika leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
Viongozi wa Chama cha Wananchi CUF wakimwombea dua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (kulia) ili aendelee kuwa na afya njema ya kumuwezesha kutekeleza majukumu yake kikamilifu walipomtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad (Kushoto) akimuaga Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake leo jijini Dar es salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro akimuaga Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai mara baada ya kumtembelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam. Viongozi wa CUF wamefika nyumbani kwa Mhe. Spika, Job Ndugai kumjulia hali baada ya kurejea hivi karibuni akitokea nchini India alikokwenda kwa ajili ya uchunguzi na matibabu. Picha/Aron Msigwa

RC MAKONDA AKUTANA NA WAJUMBE WA KAMATI YA USHAURI YA MKOA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Makonda (kushoto) akifungua kikao chake cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) jijini Dar es salaam.Wengine kutoka kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabida.
Picha na 1. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Makonda (kushoto) akifungua kikao chake cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) jijini Dar es salaam.Wengine kutoka kulia ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabida.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es salaam Mhe. Isaya Mwita akizungumza na wajumbe wa Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Ramadhani Madabida.
Wakuu wa wilaya za mkoa wa Dar es salaam wakifuatilia kikao cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC) jijini Dar es salaam. Kutoka kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe. Sophia Mjema, akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Kigamboni Mhe. Hashim Mgandilwa, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mhe. Hamphrey Polepole na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Ally Hapi.

Na.Aron Msigwa - Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda amewataka watendaji wa mkoa huo kuhakikisha kuwa wanasimamia ubora wa madawati yanayotengenezwa na vyumba vya madarasa vinavyojengwa maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Aidha, amezitaka manispaa za mkoa huo kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya kujenga madarasa mapya na kuwahamasisha wananchi na wadau mbalimbali wa maendeleo kujitolea kufanikisha mpango huo na kutoa wito kwa madiwani kujiwekea mkakati wa kujenga walau madarasa mawili kwenye Kata zao.

Akifungua kikao chake cha kwanza cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Dar es salaam (RCC), Mhe Makonda amesema kuwa licha jiji hilo kukabiliwa na changamoto za kimaendeleo za muda mrefu kwenye sekta ya elimu, miundombinu ya Afya, maji na barabara mafanikio yameanza kuonekana kutokana na juhudi za pamoja za viongozi wa mkoa huo.


UPATIKANAJI WA MADAWATI

Kuhusu upatikanaji wa madawati amesema kuwa toka Mhe. Rais wa Jamhuri ya Tanzania atangaze kampeni ya upatikanaji wa madawati kwa ajili ya shule za Msingi kumekuwa na mwitikio mzuri kwa kutoka kwa viongozi wa mkoa huo wa kuhakikisha madawati yanapatikana.

Amesema mkoa wake ulikua na upungufu wa madawati zadi ya 66,031 yaliyokuwa yakihitajika katika shule za msingi huku Sekondari zikihitaji madawati zaidi ya 30,000.

Amesema wabunge wa majimbo ya Dar es salaam tayari wametoa madawati 5000 kila mmoja katika yao na juhudi zinaendelea kufanywa na madiwani na Mameya kutenga fedha kwenye bajeti za Halmashauri zao kwa ajili ya ununuzi wa madawati.

Amewashukuru Wakuu wa wilaya kwa kuwa mstari wa mbele kuwahamasisha wananchi na wadau mbalimbali kuchangia madawati kwa kujitolea na kufanikisha mkoa huo kuwa umepata madawati yote yaliyobaki ifikapo Agosti 31 mwaka huu.


VYUMBA VYA MADARASA

Amesema bado mkoa unakabiliwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na kuongeza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Pombe Magufuli katika ahadi zake aliupatia mkoa huo kiasi cha shilingi bilioni 2.7 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya madawati zihamishiwe kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa na kazi ya kumalizia upatikanaji wa madawati yaliyobaki ibaki kwa viongozi wa mkoa huo.

Amesema fedha hizo zimekwishakutengwa na kuanza kusambazwa kwenye wilaya husika na kusisitiza kuwa ujenzi wa madarasa hayo unaendelea lengo likiwa kujenga madarasa 123 kwa fedha zilizotolewa na Mhe.Rais Dkt. John Magufuli.

“Kama mkoa tunamshukuru Rais alitupatia shilingi bilioni 2 na akawabana mawaziri wake wakachanga milioni 107, tukafikisha jumla ya shilingi bilioni 2.1 fedha hizi ilikua ziende kwenye madawati, nikamwomba Mhe. Rais aturuhusu tuzitumie kwa ajili ya ujenzi wa madarasa ili madawati tuendelee kupambana nayo sisi wenyewe”Amesisitiza Mhe. Makonda.

Aidha, wadau mbalimbali kutoka ndani ya nchi wamekuwa mstari wa mbele kuunga mkono kampeni juhudi za Serikali kwa kutoa michango mbalimbali na kufanikisha ujenzi wa madarasa kupitia uchangiaji wa mabati mabati 10,000 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa pia wadau kuchangia tani zipatazo 35 za nondo.


USAFI WA MAZINGIRA.

Amesema mkoa wa Dar es salaam una changamoto ya uzalishaji wa taka nyingi ikilinganishwa na maeneo mengine nchini kwa kuwa una idadi kubwa ya watu takribani wakazi zaidi ya milioni 5 ambao

Amesema juhudi za kuendelea kuliweka jiji hilo katika hali ya usafi zinaendelea kwa kuwahamasisha wananchi kujenga utamaduni wa kusafisha mazingira yao ili kujikinga na magonjwa ya milipuko ikiwemo kipindupindu yanayosababishwa na uchafu.

Amewataka viongozi wa mkoa huo kusimamia wajibu wa kuliweka jiji katika hali ya usafi kwa kusimamia sheria ili jiji hilo liwe katika hali ya usafi ikiwa ni pamoja na kuwaagiza wamiliki wa maduka yote katika jiji hilo kuwa na vifaa vya kutupia taka nje ya maduka yao.

Amepongeza juhudi za watendaji wa mkoa huo kutenga fedha kwenye bajeti ya 2016/2017 kwa ajili ya kununulia magari ya kubebea taka.

Ili kuhakikisha kuwa kampeni hiyo inakuwa endelevu na inafanywa kwa kasi na nguvu kubwa ameanzisha mpango wa utoaji wa gari (pick-up) na fedha kama motisha kwa Mwenyekiti wa mtaa atakayefanya vizuri kwenye usafi kuanzia mwezi huu, huku wajumbe 5 wa Serikali ya mtaa na mtendaji wa mtaa utakaofanya vizuri wakipatiwa kiasi cha shilingi milioni 5 kila mmoja.

"Napenda kuwajulisha kuwa mwezi huu niliahidi kukabidhi gari aina ya pick- up kwa mwenyekiti wa Serikali ya mtaa atakayefanya vizuri kwenye usafi,kwenye mtaaa wake na tayari nimeshainunua nalenga kutoa motisha kwa viongozi hao” Amesema.
Amesema zawadi hizo zitatolewa kwa kwa kuzingatia vigezo vya Afya vilivyowekwa na tayari timu iliyoundwa kufuatilia suala hilo imeanza kazi ya kupita katika maeneo mbalibali kufuatilia utekelezaji wa kampeni hiyo kubaini mitaa na viongozi waliofanya vizuri na kusisitiza kwamba viongozi wa mitaa watakaozembea kusimamia usafi katika maeneo yao watatangazwa hadharani kupitia vyombo vya habari ili jamii iwajue kuwa wanakwamisha kampeni ya usafi.


SOKO LA KARIAKOO

Mhe. Makonda amepongeza juhudi zinazofanywa na viongozi na watendaji wa halmashauri ya Ilala na jiji kuifanya Kariakoo kuwa katika hali ya usafi na na kuwawezesha wananchi kupita kwa urahisi tofauti na ilivyokuwa awali.

Amesema yeye kama mkuu wa mkoa aliyekabidhiwa jukumu la kusimamia mkoa huo atahakikisha kuwa maeneo yote ya jiji la Dar es salaam ikiwemo Kariakoo na Ubungo yanabaki kuwa maeneo yanayowezesha wananchi kupita kwa huru bila hofu yoyote.

“ Mimi nawapongeza Mameya wa jiji, wakuu wa wilaya, wakurugenzi na Maafisa Biashara kwa kazi nzuri mnayoendelea kuifanya kuifanya Kariakoo na Ubungo iweze kupitika, nawahakikishia maadam mimi ndiyo Mkuu wa Mkoa itabaki hivyo, maeneo hayo yatabaki salama kwa watu kupita na wale wanaofanya biashara na kulipa kodi wafanye kazi yao kwa uhuru ” Amesisitiza.


WAMACHINGA KATIKATI YA JIJI.

Amewataka wafuate sheria zinazosimamia jiji kwa kuacha kufanya biashara maeneo yasiyoruhusiwa na kuwa tayari kwenda kwenye maeneo waliyopangiwa na kuongeza kuwa ataendelea kusimamia sheria, kanuni na taratibu zinazouongoza mkoa huo kuhakikisha kuwa maeneo yaliyopangwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao na halmashauri husika yanatumika kama ilivyokusudiwa ili Dar es salaam iwe mahali pazuri na salama pa kuishi.

Mhe. Makonda amekiri kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wafanyabiashara wenye maduka eneo la kariakoo ambao wamekua wakikwamishwa na wafanyabiashara wadogo ambao wamekuwa wakipanga barabarani, nje ya maduka yao bidhaa zilezile wanazouza wao katika maduka yao huku wakiwa hawalipii kodi jambo ambalo linawasababishia hasara.

Amewaagiza wakuu wa wilaya watangaze barabara zitakazotengwa katika kata kwa ajili ya kufungwa mwisho wa Juma (week end) ili zitumiwe na wafanyabiashara wadogo kama alivyoagiza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa akiwahutubia wakazi wa jiji la Mwanza Agosti 11, 2016 na kuongeza kuwa barabara zitakazofungwa zitahusisha zile za Kata ambazo zitakuwa zinahudumiwa na Ofisi za kata ili kuwawezesha wananchi kufanya biashara kwa uhuru na kusimamia usafi wa mazingira katika maeneo yao.

OMBAOMBA.

Kuhusu ombaomba amesema kuwa mkoa wake utalishughulikia kwa nama ya kipekee kwa kuwa kumekuwa na ongezeko la ombaomba ambao wamegawanyika katika makundi ya watu wazima na watoto ambao sasa wamekuwa kero kwa wakihusishwa na vitendo vya ukwapuaji wa mali za watu, kuharibu magari pindi wanapokosa fedha walizoomba kutoka kwa watumia barabara.

Amewaagiza wenyeviti wa Kamati za ulinzi na Usalama wa mkoa huo katika kila wilaya kulifanyanyia kazi suala hilo wakishirikiana na maafisa Maendeleo ya Jamii kuhakikisha hakuna watoto wanaozunguka kuombaomba kwa kuwa walitakiwa kuwa shule na elimu sasa inatolewa bure.


KERO YA USAFIRI.

Amepongeza juhudi zilizofanywa na Serikali kupitia Mradi wa Mabasi ya mwendokasi ambayo yamekuwa msaada kwa wakazi wa jiji hilo pia uwepo wa Treni za abiria za reli ya Kati katika jiji la Dar es salaam kutokea Dar es salaam stesheni hadi Ubungo na Pugu.

Aidha, mkoa umeiomba Wizara ya Ujenzi, Mawasliano na Uchukuzi kuangalia uwezekano wa kuanzisha boti tatu za kisasa zitakazoanzia safari yake Feri kwenda Mtoni Kijichi na Mbagala na wataalam wa wizara husika wanafanya upembuzi yakinifu kuwezesha jambo hilo wakati ukisubiriwa utekelezaji wa Awamu ya pili na tatu wa ujenzi wa mradi wa mabasi ya mwendokasi katika jiji hilo.

Kuhusu msongamano wa malori ya mafuta yanayokuja katika Bandari ya Dar es salaam kuchukua mafuta, mkoa huo kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi pamoja na Wizara ya Nishati na Madini umeweka mkakati wa kuangalia uwezekano wa kujenga bomba la mafuta litakalotoka Kurasini hadi chalinze kupitia njia ya mradi wa Tazama ambalo litapunguza msongamano wa malori yapatayo 1000 hadi 1500 yanayoingia na kutoka katika jiji hilo.


ULINZI NA USALAMA.

Amesema kuwa Serikali ya mkoa wa Dar es salaam itaendelea kuhakikisha kuwa jiji la Dar es salaam linakuwa salama na kuvitaka vyombo vya Ulinzi na Usalama hasa Jeshi la Polisi kuendelea kutekeleza sheria na majukumu yao ipasavyo ili kudhibiti vitendo vya kiharifu na uvunjaji wa sheria, ujambazi, umiliki silaha haramu, madawa ya kulevya, vitendo vya udharirishaji wa binadamu .

“Kipindi cha nyuma silaha zilikua zinalia hovyo sasa nalishukuru Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kwa kazi nzuri, tutaendelea kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo kwa kufanya oparesheni za wamiliki silaha kinyume cha sheria kuondoa kila aina ya uharifu unaofanyika ndani ya majumba ya watu katika jiji hili” Amesisitiza Mhe. Makonda.

SIMIYU KUWACHUKULIA HATUA WATENDAJI WANAOTOA TAKWIMU ZA UONGO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akizungumza na Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo (hawapo pichani), katika Mafunzo elekezi yaliyotolewa kwa viongozi hao Mjini Bariadi kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini(kushoto) akitoa maelezo ya utangulizi kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo (hawapo pichani) kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa huo Anthony Mtaka (kulia) kufungua Mafunzo elekezi kwa viongozi hao
Baadhi ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, yaliyotolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji.Mstari wa Kwanza kutoka kushoto Wakuu wa Wilaya,Tano Mwera (Busega), Seif Shekalaghe (Maswa), Joseph Chilongani (Meatu), Benson Kilangi (Itilima) na Festo Kiswaga (Bariadi).

Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, yaliyotolewa kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji. Kutoka (kushoto) Kamanda wa Polisi Mkoa, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Afisa Uhamiaji, Kamanda wa Zimamoto na Mkuu wa TAKUKURU
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (wa pili kulia kwa waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Vyombo Vya Ulinzi na Usalama Mkoa, Makatibu Tawala Wasaidizi, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, baada ya kufungua Mafunzo elekezi yaliyotolewa kwa viongozi hao wa Wilaya Mjini Bariadi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa Kiutendaji. (wa pili kushoto)Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini (kushoto)Mkuu wa Wilaya Busega, Tano Mwera na( kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga.




Na Stella Kalinga, SIMIYU

Serikali Mkoani Simiyu imesema haiko tayari kuwavumilia na kuwaacha katika vyeo na majukumu waliyonayo watendaji wanaotoa takwimu zisizo za kweli.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa huo, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ufunguzi wa mafunzo elekezi yaliyotolewa kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa huo, yaliyofanyika jana Mjini Bariadi, kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kiutendaji, kwa kuwa baadhi ya viongozi hao wametoka katika sekta binafsi ambazo zina mifumo tofauti ya kitendaji na mfumo wa Serikali.

“Tunawezaje kukaa na Mtendaji ambaye ukimwomba taarifa za upungufu wa madawati anadanganya, idadi ya wanafunzi anadanganya, walimu anadaganya tutamchukulia hatua tu. Lazima tupeleke ujumbe kwamba taarifa za uongo hazina nafasi tena katika Mkoa wa Simiyu. Namwagiza Katibu Tawala Mkoa, aanze kuchukua hatua stahiki dhidi ya watendaji wote waliotoa taarifa zisizo za kweli hususani katika takwimu za wanafunzi, walimu, madawati na vyumba vya madarasa”, alisema Mtaka.

Mtaka amesema azma ya Serikali Mkoani humo ni kuhakikisha Nafasi za watendaji wasio waadlifu zinajazwa na watumishi waadilifu, wenye sifa na elimu ya kutosha waliopo katika Halmashauri za Mkoa huo.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka viongozi hao wa Wilaya kubaini watumishi wenye sifa na uwezo wa kutekeleza majukumu ya Serikali katika maeneo yao na wawape fursa watumie talanta zao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Pamoja na kubaini watumishi wenye sifa, viongozi hao wameelekezwa kuwachukulia hatua watumishi wanaopenda kufanya kazi kwa mazoea, ikiwa ni pamoja na kuwapangia majukumu yanayoendana na uwezo wao wa kufanya kazi.

Katika kuboresha ukusanyaji wa mapato, Mtaka ametoa wito kwa viongozi hao kuibua vyanzo vipya vya mapato na kusimamia ukusanyaji wa Mapato hayo kwa kuzingatia maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ya kutowabugudhi wananchi wanyonge na akawataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha wanatenga asilimia 10 ya mapato yao ya ndani kwa ajili ya kuimarisha vikundi vya uzalishaji vya vijana na wanawake

Sanjari na hilo Mtaka amewataka Viongozi hao wa Wilaya kutambua fursa za maendeleo katika maeneo yao na kuzitekelezafursa hizo kwa manufaa ya Wananchi walio katika maeneo yao.

Akizungumza baada ya mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe, Tano Mwera alisema mafunzo hayo yamemsaidia kumpa mwanga na dira ya utendaji katika nafasi yake hasa katika utaratibu wa mawasiliano na mahusiano kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa kwa Mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Nchi, Nafasi yake kama Kiongozi wa Serikali Wilayani pamoja na Sheria na Miongozo ya Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Mafunzo hayo ya siku moja kwa Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri ambayo yaliongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini. yaliendeshwa na Makatibu Tawala Wasaidizi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa huo.

KIPINDI CHA KWANZA KURUKA HEWANI NDANI YA 102.5 LAKE FM MWANZA

$
0
0
102.5 Lake Fm Mwanza #RahaYaRockCity #RedioYaWananzengo, leo imeanza rasmi kurusha vipindi vyake ambapo kipindi cha kwanza kilichoruka hewani ni #MshikeMshike kinachofanywa na #AishaMussa.

Bonyeza HAPA Kusikiliza. Au Bonyeza Play hapo chini

ZADIA YAWAPA POLE WAZANZIBARI WOTE KUFUATIA KIFO CHA MZEE ABOUD JUMBE

$
0
0
215 459 4449
zadia.org
انا لله وانا اليه راجعون

TAARIFA



Jumuiya ya Wazanzibari Nchini Marekani (ZADIA), imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.

Mzee Jumbe aliyewahi kuwa rais wa Zanzibar na Makamo wa Kwanza wa Rais wa Tanzania, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika harakati za kuleta maendeleo na mabadiliko ya kisiasa visiwani Zanzibar.

Chini ya Uongozi wake, kwa mara ya kwanza Zanzibar ilipata katiba yake na hivyo kuanzishwa kwa Baraza la Wawakilishi kama chombo cha uwakilishi wa Umma na kutunga sheria.

Atakumbukwa pia kwa msimamo wake shupavu wa kupigania haki sawa ndani ya Mungano wa Tanganyika na Zanzibar khususan madai yake ya kutaka kuwa na serikali tatu.

Marehemu Jumbe alikuwa rais wa Zanzibar kuanzia mwaka 1972 kufuatia kifo cha rais wa kwanza wa Zanzinbar Marehemu Abeid Aman Karume. Alilzaimishwa kujiuzulu nyadhifa zake zote za kisiasa mwaka 1984 baada ya kutuhumiwa kuchafua hali ya hewa ya kisisasa Zanzibar. Uchafuzi ambao si chochote ila ushupavu wake wa kutetea maslahi ya Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mnasaba huu, ZADIA inatoa mkono wa pole kwa Wazanzibari wote kwa ujumla kwa kuondokewa na kiongozi wao mzalendo.

Aidha kono wa pole makhasusi uwafikie wanafamilia ya Marehemu, tukimwomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awape subira katika kipindi hiki kigumu cha msiba, na kumwomba Mola Mlezi amlaze marehemu mahali pema Peponi. Amin.

Omar H Ali, Mwenyekiti, ZADIA
Agosti 14, 2016

TANAPA,NGORONGORO NA IDARA YA WANYAMAPORI SASA KWENDA KIJESHI

$
0
0
Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi za Taifa likiingia katika viwanja vya mazoezi katika kambi ya mafunzo ya Mlele wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipokea salamu ya utii kutoka kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (hawapo pichani) wakati wa ufungaji mafunzo kwa askari na maafisa hao yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi

Askari na Maafisa wa Hifadhi wakipita kwa heshima mbele ya mgeni rasmi kwa mwendo wa pole na haraka wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu kutoka mfumo wa kiraia.
  
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakipokea salamu za heshima kwa kupiga saluti wakati gwaride likipita mbele kwa heshima wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa askari wa shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya taifa Ngorongoro.
Bendi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa wa Hifadhi ,Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
Askari na Maafisa wa Hifadhi za Taifa wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Witness Shoo (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko wakifuatilia maonesho ya matumizi ya silaha kutoka kwa wahitimu hao.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akisherehesha wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na Maafisa wa Hifadhi waliyopata katika kambi ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.

DC MTATURU: SERIKALI IPO TAYARI KUCHUKIWA NA WAVIVU

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mirajji Jumanne Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa kufunga mafunzo ya waendesha pikipiki.
Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha na kupunguza umasikini na kutunza mazingira nchini Tanzania (APEC), Respicius Timanywa akiwashukuru washiriki wote wa mafunzo hayo

Na Mathias Canal, Singida

Serikali imeeleza kuwa ipo tayari kuchukiwa na wananchi wavivu wasiotaka kujishughulisha na Ujasiriamali, Kilimo, Uvuvi, Ufugaji na Biashara ili kukuza pato la kaya zao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakati wa kufunga mafunzo ya usalama Barabarani kwa Waendesha pikipiki maarufu kama Bodaboda wa Wilaya ya Ikungi yaliyohusisha Kata ya Issuna na na Kata ya Mkiwa na kufanyika JMC Hotel Kijijini Issuna B.

Katika mafunzo hayo yaliyochukua siku sita yamewakutanisha pamoja waendesha Bodaboda 84 ambao wamefundishwa Alama na sheria zote za usalama Barabarani, Upatikanaji wa leseni, Faida za kulipa kodi na somo la ujasiriamali, Polisi jamii, Ulinzi shirikishi na elimu juu ya maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na Ukosefu wa Kinga Mwilini (UKIMWI).

Akiwahutubia wananchi hao Mtaturu amemshukuru Rais wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuanzisha ajira ya pikipiki kwani kwa kiasi kikubwa imesaidia kupunguza uhalifu na kuandaa ajira kwa vijana wengi nchini hivyo kuachana na kujihusisha na mambo yasiyo na tija kwa jamii ikiwemo kushinda vijiweni.

Amesema kuwa mafunzo hayo yanayotolewa na shirika lisilo la kiserikali la APEC yatasaidia kupunguza ajali za pikipiki zinazosababishwa na uzembe wa baadhi ya waendesha pikipiki katika Wilaya zote za Mkoa wa Singida.


Dc Mtaturu amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi kwa kushirikiana na Mkuu wa Polisi Wilaya kuhakikisha madereva Bodaboda waliokwepa mafunzo ya awamu hii wanasajiliwa ili wahudhurie mafunzo yatakayorudiwa kwa awamu ya pili kwa Wilaya nzima, hivyo kwa wale ambao hawatapata mafunzo hawataruhusiwa kuendesha pikipiki zao ili kuepusha ajali mpaka pale watakapopata mafunzo.

“Dereva bila elimu ni sawa na bunduki bila risasi, hivyo nakuagiza mkuu wa Polisi kutowakamata kwa kosa la kutokuwa na leseni angalau kwa kipindi cha miezi miwili wakati wanafuatilia leseni zao”  Alisema Mtaturu

Akizungumzia kuhusu alama za barabarani Mtaturu alisema kuwa tayari ameshamwagiza Mhandisi wa Ujenzi wa Halmashauri kufanya mawasiliano na wakala wa barabara katika maeneo yote ambapo alama za barabarani hazipo.

Ili kuvunja makusudi makusudi ya kuvunja sheria Mkuu huyo amemuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) amuelekeze mkuu wa Trafiki Wilaya (DTO) ambapo alisema kuanzia leo kila dereva wa pikipiki anapaswa kutembea na kivuli cha cheti na leseni. 

Akisoma risala iliyoandaliwa na wahitimu wa mafunzo ya udereva wa pikipiki Kata ya Mkiwa na Issuna Yohana Chawenda amezitaja changamoto zinazowakabili waendesha bodaboda hao kuwa ni pamoja na kukabwa na kuibiwa pikipiki zao, Upatikanaji wa leseni, baadhi ya abiria kukataa kuvaa kofia ngumu, Baadhi ya waendesha pikipiki kukataa kushiriki mafunzo ya usalama barabarani, Baadhi ya wananchi kuharibu alama za barabarani na Baadhi ya maafisa wa usalama Barabarani kusimamisha pikipiki sehemu isiyo rasmi jambo ambalo linachangia kuongezeka kwa ajali za barabarani.

Mkurugenzi wa Taasisi inayojihusisha na kupunguza umasikini na kutunza mazingira nchini Tanzania (APEC), Respicius Timanywa, amesema kuwa lengo la Taasisi hiyo kutoa mafunzo hayo ni kupunguza ajali na kuwaandaa vijana kujihusisha na ujasiliamali wa uendeshaji wa Bodaboda huku wakiwa katika hali ya usalama.

Timanywa amesema kuwa mafuzno hayo yataendelea katika maeneo mengine ili kutoa fursa kwa watanzania wote wanaopenda kushiriki kwa ajili ya kujifunza kwa manufaa ya leo na kesho.

Zaidi sana amesema kuwa mafunzo hayo pia yamelenga kuwafanya vijana waweze kumiliki fursa kubwa na kutengeneza faida kubwa iliwaweze kulipa ushuru na kodi za serikali.


Dc Mtaturu (Kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa APEC Respicius Timanywa zawadi ya kuku iliyotolewa na wahitimu wa mafunzo hayo
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mirajji Jumanne Mtaturu akisisitiza juu ya umuhimu wa mafunzo ya usalama barabarani.
Dc Mtaturu akionyesha kuku aliyokabidhiwa kama zawadi baada ya kukubali kuwa mgeni rasmi  wakati wa kufunga mafunzo hayo
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya elimu ya usalama barabarani wakionyesha alama za barabarani walizozichora wao wenyewe kwa ajili ya kuashiria kuelewa mafunzo waliyopatiwa
Baadhiya Bodaboda za washiriki zikiwa zimepaki bila kufanya kazi ya kubeba abiria ambapo wamiliki walikuwa kwenye mafunzo




MFUKO KICHOCHEO WA SAGCOT WASAINI MAKUBALIANO NA SHIRIKA LA BOTHAR KUTOKA NCHINI IRELAND

$
0
0

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCO Bwa. John J. Kyaruzi akisaini makubaliano hayo na Mwasisi wa Shirika la Bothar Bwa. Peter Ireton huku wakishuhudiwa na Dkt. Bernard Muyeya (kulia) Mkurugenzi wa Huduma za Nje ya Nchi wa Bothar na Bwa. Abdallah S. Msambachi ( kushoto) Mratibu wa Biashara wa Mfuko wa SAGCOT.

Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa kuongeza tija na uzalishaji kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa mkoani Njombe, Iringa na Mbeya, Mfuko Kichocheo wa SAGCOT yaani SAGCOT CATALYTIC TRUST FUND tarehe 12 Agosti 2016 umesaini makubaliano na Shirika la Bothar kutoka nchini Ireland ambalo linajihusisha na kutoa misaada mbalimbali inayolenga kutoa fursa kwa familia zenye kipato cha chini kuweza kuboresha maisha yao kupitia uwekezaji wa shughuli zinazowaletea kipato hususani kaya zinazojishughulisha na ufugaji.

Katika makubaliano hayo jumla ya Ng’ombe wa kisasa 630 wanatarajiwa kuingizwa nchini katika kipindi cha miaka mitatu. Ng’ombe hao watagawiwa kwa wafugaji walioandaliwa chini ya miradi inayotekelezwa na Mfuko huo, Aidha wafugaji watahakikishiwa masoko pamoja na huduma mbalimbali za mifugo kupitia wataaalamu wa Halmashauri husika.

Katibu Mtendaji wa Mfuko Kichocheo wa SAGCOT Bwa. John. J. Kyaruzi ( kushoto) akisaini makubaliano na Muasisi wa Bothar Bwa. Peter Ireton .
Bwa. John. J. Kyaruzi na Bwa. Peter Ireton wakibadilishana hati za makubaliano.
Mkurugenzi wa huduma za nje ya Nchi wa Bothar,Dkt Bernard Muyeya akitoa maelezo kwa wajumbe namna shirika hilo linavyotoa huduma zake.
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live