Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

PASTOR DANIEL MOSES KULOLA OF EAGT LUMALA MPYA MWANZA TO VISIT USA

$
0
0
"Greetings my friend, Again God has given to me a chance to come to America, this time i wont stay in USA for long time it is just for 2 weeks then i come back home Tanzania.

My schedule will be in Boston from 9th to 14th August then 15th August to Dallas, Houston to 22nd, on 23rd to Arizona. my ticket back to Tanzania reads on 25th from Arizona to Boston and Boston to Tanzania.

I thought it is good to let you know so that you can pray for me and also call me for greetings". Pastor Kulola States.

MWILI WA MAREHEMU JOSEPH SENGA WAWASILI DAR, KUAGWA JUMAPILI VIWANJA VYA SINZA-UZURI

$
0
0

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, (watatu kushoto), mbunge wa Nsumve Richard Ndasa, (wanne kushoto) nabaadhi ya waaandishi na wapiga picha, wakilitama jeneza lenye mwikli wa hayati Joseph Senga, aliyekuwa Mpiga Picha Mkuu wa gazetila Tanzania Daima, wakati wafanyakazi wa Swissport wakilitoa jeenza hilo kwenye uwanjawa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Julai 30, 2016 ulipowasili kutoka nchini India. MarehemuSenga alifariki katikati ya wiki hii nchini India, alikokwenda kwa matibabu. Taarifaza ndugu wa marehemu kuhusu taratibu za mazishi zinasema, Mwili wa marehemu umehifadhiwa kwenye hospitali ya Taifa Muhimbili, ambapo Jumapili asubuhi utapelekwa nyumbani kwake Sinza, kwa ajili ya ibada fupi na kisha utapelekwa viwanja vya Sinza-Uzuri kwa wananchi ndugu jamaa na marafiki kuuuaga. Taarifa hiyo pia inasema, Mwili wa Marehemu utasafirishwa baada ya zoezi la kuuaga Jumapili Julai 31, 2016. (PICHA NA K0-VIS MEDIA/Khalfan Said)


Ndugu wa karibu akitokwa na machozi baada ya kuona jeneza lililobeba mwili wa marehemu Senga likiwasili


Waombolezaji wakisubiri mwaili kuwasili kutoka nchini India, kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere


Waombolezaji wakibeba jeneza lenye mwili wa marehemu tayari kwa safari ya kutoka uwanjani hapo kuelekea Muhimbili kuhifadhiwa






Othmani Michuzi,(kulia). wa Blog ya Mtaa kwa Mtaa, akimfariji mpiga picha wa Tanzania Daima, Loveness Bernard ambaye alifanya kazi ofisi moja na marehemu Senga


Baadhi ya wapiga picha na waombolezaji wengine wakiondoka baada ya mwili kuwasili


Mbunge wa Nsumve, Richard Ndasa, (kushoto) akimsikiliza aliyekuwa Mhariri Mtendaji wa magazeti ya Serikali, Daily News na Habari Leo, Gabriel Nderumaki wakati wakisubiri mwaili wa marehemu Senga kuwasili


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (kulia), akiteta jambona Mhariri Mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima, Neville Meena, wakati wakisubiri kuwasili kwa mwili wa marehemu Joseph Senga, aliyekuwa mpiga picha mkuu wa gazeti hilo


Gari lililobeba jeneza lenye mwili wa marehemu Senga, likiwa tayari kuondoka uwanjani hapo


Msafara wa magari ukiwa tayari kuondoka

TANAPA YAKABIDHI JENGO LA BWALO LA CHAKULA KATIKA SHULE YA SEKONDARI YA MWIKA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiq pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakitia saini hati ya makabidhiano ya jengo la Bwalo la chakula katika shule ya sekondari ya Mwika jana wilayani Moshi,Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Tanapa kwa kushirkiana na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na nguvu za wananchi ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil 186,494,890 zimetumika..
Baadhi ya Wanafunzi katika shule ya sekondari ya Mwika wakiwa katika hafla fupi ya makabidhiano ya jengo la Bwalo kwa ajili ya Chakula.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akimkabidhi hati ,Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiq baada ya saini hati ya makabidhiano ya jengo la Bwalo la chakula katika shule ya sekondari ya Mwika jana wilayani Moshi,Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Tanapa kwa kushirkiana na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na nguvu za wananchi ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil 186,494,890 zimetumika.

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiq akizindua jengo la Bwalo la chakula katika shule ya sekondari ya Mwika jana wilayani Moshi,Jengo hilo limejengwa kwa ufadhili wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa kushirkiana na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na nguvu za wananchi ,ambapo jumla ya kiasi cha Sh Mil 186,494,890 zimetumika.kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi
Baadhi ya Wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Mwika.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,Said Meck Sadiq akizungumza mara baada ya kuzindua jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya sekondari ya Mwika lililojengwa kutokana na msaada wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) .
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya jengo la Bwalo la kulia chakula kwa wanafunzi wa shule ya sekondari ya Mwika.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) Betrita Loibooki akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Jengo la Bwalo la Chakula katika shule ya sekondari ya Mwika lililojengwa kwa msaada wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) kwa ushirikiano na Halmashauri ya wilaya ya Moshi pamoja na wananchi .




Na Dixon Busagaga wa Michzu Blog ,Kanda ya Kaskazini.

 

WAUMINI WA KKKT MTAA WA KULASI WILAYANI KOROGWE WAJENGEWA KANISA JIPYA

$
0
0
Muonekano wa Jengo la Kanisa lililokuwa likitumiwa na Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe .

Muonekano wa Jengo jipya la Kanisa linalotumiwa na Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe .
Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe wakiandamana wakati wa sherehe ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa lililojengwa na wazawa wa kijiji hicho waishio maeneo mbalimbali nchini.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga (wa kwanza kushoto) akiongoza wachungaji wa kanisa hilo kupokea waumini wakati wa ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akiongoza ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.
Baadhi ya Waumini wa kanisa hilo wakiimba nyimbo wakati wa ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akikata utepe kufungua rasmi jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akifungua mlango wa kanisa ili waumini wapate kuingia ndani.
Muonekano wa ndani wa jengo jipya la Kanisa la KKKT mtaa wa kulasi.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akisoma neno mara baada ya waumini kuingia ndani ya kanisa hilo.
Waumini wa kanisa la Mtaa wa Kulasi wakiwa wameshika kuta za kanisa hilo wakati wa sala ya kubariki jengo la kanisa.
Baadhi ya waumini wa kanisa la mtaa wa Kulasi wakiwa katika ibada hiyo .

Kwaya Walawi ya jijini Arusha ikiimba nyimbo za kusifu kwa watu waliojitoa kwa ajili ya ujenzi wa kanisa hilo.
Kwaya ya watoto wa kanisa la mtaa wa Kulasi wakiiiomba nyimbo wakati wa ibada hiyo.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akitoa mahubiri katika ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akimpa mkono Sayuni Shelutete kwa kushiriki katika utoaji wa msaada wa ujenzi wa kanisa hilo.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akimpa mkono Pascal Shelutete kwa kushiriki katika utoaji wa msaada wa ujenzi wa kanisa hilo.
Waumini wa kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe wakitoa zawadi kwa familia ya Pascal Shelutete kwa msaada waliotoa kwa ajili ya kufanikisha kazi ya ujenzi wa kanisa la mtaa wa Kulasi.
Kiongozi wa familia ya Mzee Shelutete,Bwana Nicolaus Kingazi akizungumza kwa niaba ya familia hiyo wakati wa ibada ya ufunguzi wa jengo jipya la kanisa la mtaa wa Kulasi.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akihitimisha ibada ya ufunguzi wa kanisa la mtaa wa Kulasi wilayani Korogwe.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akipeana mikono na wachungaji mara baada ya kumaliza ibada ya ufunguzi wa jengo la kanisa.
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga akisaidiana na Pascal Shelutete kuotesha mti wa kumbukumbu katika viunga vya kanisa hilo.
Bwana,Pascal Shelutete (Kushoto) na Bibi Sayuni Shelutete (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Mashariki Dkt Stephen Munga mara baada ya kukamilika kwa ibada ya ufunguzi wa kanisa jipya la mtaa wa Kulasi.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.

MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WAZANIBARI BOSTON, SEHEMU YA PILI

$
0
0
Na Mwandishi wetu Boston
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, amemaliza awamu ya pili ya ziara zake za Kimataafa hapa nchini Marekani iliyoanza wiki mbili zilizopita.
Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na Wazanzibar 
Maalim Seif, ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) alikamilisha ziara yake hiyo tarehe 30 Julai kwa kuzungumza na Wazanzibari kwenye Mkutano wa hadhara uliofanyika katika jimbo la Massachusetts.
Mgeni huyo rasmi alikaribishwa kwa risala ya Jumuiya ya Wazanzibari waishio katika jiji la Boston kulikofanyika mkutano huo, Bwana Mohammed Lali, iliyoelezea imani yao juu ya uongozi wa Maalim Seif katika mapambano ya kupigania haki sawa na demokrasia Visiwani Zanzibar.
Akijibu risala hiyo, Mwanasiasa huyo alielezea shukrani zake za dhati kwa imani ya Wazanzibari juu uongozi wake na kuwahakikishia kuwa haki yao itapatikana.
Madhumuni ya Ziara zake.
Maalim Seif, aliyekuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, alielezea lengo la mizunguko yake hiyo kuwa ni kukutana na viongozi wa ngazi za juu wa nchi na taasisi alizozitembelea ili kuwapa picha halisi ya hali ya mambo ilivyo huko Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika nyanja za demokrasia na haki za binadamu kufuatia uchaguzi huo.
"Tumekuwa tukiwasiliana ili kuwapa 'brief' (maelezo) ya hali halisi ilivyo" aligogoteza Maalim.
Alisema kuwa nchi nyingi kwa kupitia Balozi zao zilikuwa zikitetea demokrasia, na wala siyo chama au kiongozi fulani.
"Nchi nyingi kwa kupitia Balozi zao zilikuwa zinatetea demokrasia, na wala siyo CUF wala Maalim Seif", alisema gwiji huyo wa siasa, na kuongeza kuwa, "Msimamo huo ndio uliotusukuma kutembelea nchi hizi ili kuwapa 'utandu na ukoko', kwani kwa kufanya hivi tunapata nafasi ya kukutana na watunga sera wenyewe"
Hii ni kutokana na kuwa Mabalozi wanafanya kazi kutokana na maagizo ya viongozi wa nchi zao, "na kama hamkujikaza swala hili linaweza kusahaulika", alisistiza.
Migogoro ya Zanzibar.
Katika mkutano huo, mwanasiasa huyo mkongwe alielezea kwa mukhtasari juu ya historia ya migogoro visiwani Zanzibar kwa kusema kuwa migogoro visiwani humo ni tofauti na migogoro katika nchi nyengine ambako huwa inajikita katika misingi ya ukabila au udini. lakini swala la ukabila au udini haliko Zanzibar licha ya kuwa 97% ya watu wake ni Waislamu.
"Mgogoro zaidi ni wa kisiasa tangu zama hizo zinazoitwa za siasa", alifafanua mweledi huyo, na kuongeza: "Baada ya kuanzishwa kwa vyama vya ASP, ZNP na ZPP, siasa iliwagawa Wazanzibari na baadaye yakaja Mapinduzi ya mwaka 1964"
Mapinduzi hayo yalikomesha mfumo wa vyama vingi vya kisiasa, na kuendelea na Chama kimoja mpaka vyama vingi viliporukhusiwa tena mwaka 1992. Hata hivyo Chama tawala kiliukubali mfumo huo kwa vile ulikuja kutoakana na wimbi la mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi ulimwenguni.
"Baada ya kurejeshwa kwa shingo upande, waliukubali kwa shingo upande", alisema Maalim Seif aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Serikali ya Zanzibar, na kuongeza "Tulitukanwa na kufanyiwa mambo mengi hata kabla ya kuzaliwa kwa CUF"
Itakumbukwa kuwa Chama Cha Wananchi (CUF) kilitimiza masharti ya usajili wa muda mapema mara tu baada ya vyama vingi kurukhusiwa lakini kikapata wakati mgumu kupata uajili.
"Chama chetu kilitimiza masharti mapema, lakini kupata usajili ikawa nongwa", alisema Maalim na kusisitiza kuwa "Baadaye ikwa hawana budi kutupa usajili, na CUF ikapata usajili namabari mbili baada ya Chama Cha Mapinduzi - CCM"
Mara baada ya hapo zilifuata chuki na uhasama miongoni mwa wananchi badala ya kuwa kitu kimoja kama Wazanaibari. Chuki hizo na uhasama vikaendela na kufuatiwa na machafuka ya kisiasa kiasi kwamba kufikia mwaka 2001, kwa mara ya kwanza kabisa katika historia, Tanzania ikazalisha wakimbizi.
Itakumbukwa kwamba, wafuasi wa CUF walifanya maandamano mnamo mwezi wa Januari 2001, maandamano ambayo yalikabiliwa vikali na vyombo vya dola na kuplekea watu kadhaa kupoteza maisha na wengine kulazimika kuihama nchi na kukimbilia nchini Kenya na Somalia.
Maalim Seif, anayesifika kwa busara na hekima, aliendelea kueleza kuwa hali ya uhasama ikaendelea kuvigubika visiwa hivyo vya marashi ya karafuu mpaka mwaka 2009, ambapo alikutana na Rais wa Zanzibar wa wakati huo Dakta Amani Karume na kufikia maridhiano ya kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Alisema: "Hali iliendelea kuwa ya uhasama mpaka 2009 tulipokutana na Rais Karume na kufikia maridhiano yaliyoungwa mkono na Baraza la Wawakilishi na wanachi"
Itafaa kukumbusha kuwa tangu kufanyika uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi mwaka 1995, Zanzibar ilikuwa ikikabiliwa na migogoro ya kisiasa iliyofuatiwa na mazungumzo ya upatanishi yakizishirikiahs pande mbalimbali za Kimataifa na kufikiwa miafaka tete ambayo ilivunjika mara tu baada ya chaguzi. Hata hivyo, Maalim Seif na Rais Amani Karume walikutana na kufikia maridhiano ya kizalendo ambayo hayakushirikisha upande wowote wa nje.
Maridhiano hayo yaliyotaka kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa yalipitishwa na wananchi katika kura ya maoni na kuidhinishwa rasmi na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.

BANCABC YAZINDUA HUDUMA YA "MKOPORAHISI", MKOPO NDANI YA SAA 48

$
0
0

Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Rahisi, (Easy Banking), wa BancABC,Thompson Mwasikili, (kushoto), akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara cha benki hiyo, Joyce Malai, wakati akizindua huduma mpya ya “Mkoporahisi”, makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, Agosti 2, 2016. BancABC, ambayo ni sehemu ya Atlas Mara, imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake ambapo mteja wa benki hiyo ambaye ni mtumishi wa serikali anaweza kupatiwa mkopo ndani ya masaa 48
                                                       

NA MWANDISHI WETU
BANCABC ambayo ni sehemu ya Atlas Mara imerahisisha upatikanaji wa mikopo kwa wateja wake kwani imeanza kutoa mikopo ndani ya saa 48 kupitia huduma mpya ya ‘mkoporahisi’.

Akizungumza na waandishi wa habari Agosti 1, 2016, makao makuu ya benki hiyo, kwenye jingo la Uhuru Hights jijini Dares Salaam, Mkuu wa kitengo cha Easy Banking wa BancABC, Thomson Mwasikili, (pichani juu), alisema wameamua kuanzisha huduma hiyo ili kuwavutia wateja wengi zaidi kutoka sekta mbalimbali ikiwemo serekalini ili kuhakikisha wanapata huduma hii kwa haraka.


“Kwa kupitia huduma hii ya mkoporahisi tutahakikisha kuwa wateja wetu ambao ni waajiriwa wa Serikali, wanapata mikopo yao ndani ya saa 48 kuanzia muda ambao maombi yaliwasilishwa..tutalisimamia hili na kuhakikisha linatekelezeka,” alisema Mwasikili.

Bw. Mwasikili alisema benki yake inatoa mikopo ya hadi Tsh milioni 40 kwa riba ya kiwango cha chini hadi asilimia 1.6 kwa mwezi ambayo ni miongoni mwa riba za chini kabisa katika soko la sasa.

“Waombaji wataweza kulipa mikopo yao kwa muda mrefu wa hadi miaka 6 na hakuna pingamizi kuhusu lini unaweza kuongeza mkopo wako,” alisema na kuongeza kuwa muombaji ana uhuru wa kupata mkopo wa muda mfupi hata wa mwezi mmoja.

Kwa mujibu wa Mwasikili, tofauti na mikopo mingine, waombaji wana uhuru wa kuchagua matumizi ya fedha kwa mfano kulipia ada, kununua gari, kukarabati nyumba, kulipia kodi na kumaliza ujenzi na benki haitamlazimisha mkopaji matumizi ya mkopo wake.


Waombaji pia watapata fursa ya kuchanganya mikopo yao yote na kuwa na mkopo mmoja kwani BancABC inaweza kununua mikopo yote hiyo na kumpunguzia mteja usumbufu.

“Endapo muombaji wa mkopo atafariki, mkopo utafidiwa kupitia bima ya mikopo na fedha kiasi cha Tsh 500,000 taslimu zitatolewa kugharamia mazishi,” alisema

“Tunatoa rai kwa wateja wetu wote na pia wale ambao hawana akaunti na benki yetu kuchangamkia huduma hii ya mkoporahisi kwani hii ndio benki pekee ambayo inakusogeza karibu na ndoto zako , pata mikopo ndani ya saa 48,” alisema.

Atlas Mara iliorodheshwa katika soko la hisa la London Disemba 2013. Atlas Mara ina lengo la kujitanua na kuwa kinara katika masuala ya kifedha katika ukanda wa sub sahara kwa kutumia uzoefu wake na uwezo wa kukuza mitaji. Malengo yake ni kuunganisha na kukuza uwezo wa taasisi za kifedha na pia kuendeleza uchumi katika nchi ambazo inafanya shughuli zake.


MKUU WA WILAYA: KUMKUWA NA MATUMIZI MABAYA YA DEMOKRASIA WILAYANI

$
0
0



Na Mathias Canal, Singida

Ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo kwa kutumia nguvu na akili katika kukamilisha na kumiliki miradi ya kijamii imetajwa kuwa njia mojawapo itakayowafanya wananchi kuwa na uchungu na mali pamoja na maendeleo ya katika jamii husika.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Miraji Jumanne Mtaturu amesema kuwa kumekuwa na matumizi mabaya ya demokrasia katika Wilaya hiyo hususani katika shughuli za kijamii kama vile kuchangia ujenzi wa maabara jambo lililopelekea Wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika ujenzi wa maabara kwa ajili ya shule za sekondari zilizopo katika Wilaya ya Ikungi.

Mtaturu amesema kuwa hakuna demokrasia yoyote duniani inayohubiri wananchi kutoshiriki shughuli za maendeleo hivyo mwananchi anapaswa kushirikishwa katika kuchagua viongozi wake, kukaa na viongozi wake kupanga miradi ya maendeleo kama vile kuchangia ujenzi wa shule, zahanati na maabara.

“Wataalamu wa Sayansi na viongozi mashuhuri wamewahi kusema Demokrasia bila maendeleo sio demokrasia, Hayati Mwalimu julius Kambarage Nyerere na Profesa Issa Shivji waliwahi kuandika kuwa demokrasia ya kweli ni ile inayowasaidia wananchi kutoka katika hali moja kwenda kwenye hali nyingine ambayo ni bora zaidi kuliko ile waliyo nayo, hivyo tukiongelea kuwashirikisha wananchi katika mipango na mikakati ya kuondokana na umasiki na si vinginevyo” Alisema Mtaturu

Dc Mtaturu amesema kuwakuwa mwenyekiti wa Kijiji kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM), CHADEMA, ACT WAZALENDO, CUF au chama chochote hapaswi kuongoza wananchi kwa matakwa yake binafsi bali ni lazima kufuata taratibu, kanuni, sheria na taratibu zinazowaongoza katika kutekeleza majukumu yao.

Ameyasema hayo wakati wa kikao cha kazi kati ya Mkuu waWilaya Wakuu wa idara na vitengo, Maafisa Tarafa, Weneyeviti wa Vijiji na Watendaji wa Kata na Vijiji katika mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo.  

Amewaelekeza wenyeviti wa Vijiji kuwa majukumu  yao ni kuongoza vikao vya Halmashauri ya Kijiji na kuongoza mkutano mkuu wa Kijiji sio kuuza ardhi ya kijiji kiholela, Kumnyang’anya mtu ardhi au kupiga faini yoyote wanayojisikia na ndio maana kunakuwa na watendaji wa Vijiji ambao ni wataalamu hivyo wana majukumu muhimu katika kuwashauri wenyeviti wa Vijiji.

Dc Mtaturu pia amewataka viongozi hao kutambua kuwa uchaguzi ulimalizika Octoba mwaka jana na chama kilichoshika dola ni Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo kutokana na uchaguzi huo Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipewa ridhaa ya kuongoza Tanzania kwa kipindi cha miaka mitano 2015-2020 hivyo ilani inayotekelezwa na serikali ya awamu ya Tano ni ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivyo kwa vile kila kiongozi wa Kijiji yupo ndani ya serikali anapaswa kutelekeza ilani ya CCM kwani huo ni utaratibu wa vyama vinavyoshinda popote dunia.

Baadhi ya watendaji wa Kata, Wenyeviti wa Vijiji, na baadhi ya watendaji wa Vijiji Wilayani Ikungi hawajawahi kupatiwa mafunzo ya muongozo wa kiutendaji hali iliyopelekea baadhi yao kutotimiza wajibu wao na wengine kufanya kazi nje ya mipaka yao.

“ Kupitia kikao/mafunzo haya Uonevu wowote, kosa lolote, matumizi mabaya ya madaraka yatakayofanywa aidha na Mtendaji wa Kata, Mwenyekiti wa Kijiji, Mtendaji wa Kijiji sitalifumbia macho nitakuchukulia hatua kwa mujibu wa sheria, kanuni, tulizowekeana kama serikali” Alisema Mtaturu

Sambama na hayo Dc Mtaturu amewasihi viongozi hao kuwaunga mkono askari polisi katika kuimarisha ulinzi na usalama kwani bila usalama na amani katika jamii inayotuzunguka hakuwezi kuwa na maendeleo.

MCHUNGAJI KULOLA WA EAGT LUMALA MPYA MWANZA KUITETEMESHA INJILI NCHINI MAREKANI

$
0
0
Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Jijini Mwanza, akihubiri katika moja ya mikutano yake iliyofanyika mkoani Morogoro.
Kwa mara nyingine Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo Sabasaba Ilemela Jijini Mwanza, Dkt.Daniel Moses Kulola, amepata kibali cha kupeleka neno la Mungu katika bara la Amerika.

Itakumbukwa kwamba ni miezi michache tu baada ya kupata kibali kama hicho ambapo alihubiri katika majimbo ya Dallas, Houston, Fortworth, Boston, Connectcut, Ohio Cincinnati na New York nchini Marekani.

Pia Dkt.Kulola, alipata kibali cha kuhudumu nchini Canada katika Kanisa kubwa la The Global Kingdom pamoja na miji mbalimbali kama vile Ottawa, Quebec na Toronto.

"Watu wengi walibarikiwa na kuinuliwa kimwili na kiroho kwani injili yangu ni kuyashughulikia maisha ya watu kiroho na kimwili". Anasema Dkt.Kulola ambaye awamu hii amepata kibali cha kuhudumu katika miji ya Boston, Dallas na Arizona nchini Marekani.

"Nataraji Bwana atatenda mambo makubwa huko, ninaomba maombi yenu kwa nguvu zote". Anadokeza Dkt.Kulola na kuwasihili watakaohitaji kuwasiliana nae watumie nambari za simu +255 767 749 040 kwa Tanzania na +1 832 777 5032 kwa Marekani.
Huduma za Mchungaji Dkt.Kulola zinatarajia kuanza agost 09,2016 nchini Marekani na kufikia tamati Agost 25,2016 ambapo safari ya kurejea Tanzania itakua imewadia.


Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya la Jijini Mwanza, akihubiri katika moja ya mikutano yake iliyofanyika barani Amerika.



Bonyeza Hapa Kusoma Safari ya USA

SERIKALI MKOANI SIMIYU YAAMUA 2% YA USHURU WA PAMBA IJENGE MADARASA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony J. Mtaka (Katikati) akizungumza na Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, (kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini na (kulia) Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, mhe. Festo S. Kiswaga

Wakuu wa Wilaya wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo, mstari wa kwanza kutoka kushoto, Mhe. Benson Kilangi (Itilima), Joseph Chilongani (Meatu), Seif Shekalaghe, Tano Mwera (Busega) na mstari wa pili, kutoka kushoto, Mhe. Stanslaus Nyongo(Mbunge Maswa Mashariki), Mhe. Mashimba Ndaki (Mbunge Maswa Magharibi).

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne A. Sagini akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony J. Mtaka (kulia) ili azungumze na Viongozi wa Mkoa huo na Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi kutoka katika Halmashauri za Mkoa huo, katika kikao kilichofanyika Mjini Bariadi, kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa.


Viongozi na baadhi Wajumbe wa Kamati za Fedha, Mipango na Uongozi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo kilichofanyika Mjini Bariadi.

Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Maswa, Mhe. Dila Mayeka akitoa mchango wake wa mawazo katika kikao cha kujadili mikakati ya ujenzi wa vyumba vya madarasa mkoani humo, kilichofanyika Mjini Bariadi

MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WAZANZIBARI BOSTON

$
0
0
Na Mwandishi wetu Boston 
Karibuni wapenzi Wasomaji wetu katika sehemu ya nne ya mfululizo wetu wa makala ya "Maalim Seif azungumza na Wazanzibari Boston" katika mkutano wake na Wazanzibari uliofanyika katika jimbo la Massachusetts, Marekani 30 Julai 2016.
Katika sehemu iliyopita, Maalim Seif alielezea kile kilichotokea katika uchaguzi wa Oktoba, 2015 mpaka uchaguzi wa marudio uliofanyika Machi 20, 2016. Sasa endelea na sehemu ya nne:
Baada ya Uchaguzi wa Marudio
Kile kinachoitwa uchaguzi wa marudio visiwani Zanzibar, hakikupata uungwaji mkono tangu ndani hadi nje ya visiwa hivyo. Jamii ya Kimataifa ilikataa kushiriki katika uangalizi wa uchaguzi huo kwa vile haukuwa na mashiko yoyote ya Uhalali.
Na kwa upande wa ndani, Chama Kikuu cha upinzani Cha Wananchi (CUF) ambacho kiliususia uchaguzi huo hakikuitambua serikali mpya iliyoundwa na Mheshimiwa Ali Mohammed Shein, na kikaamua kuisusia kama kilivyoususia uchaguzi wenyewe.
Maalim Seif alisema kuwa wananchi wa Zanzibar wameigomea serekali hiyo na sasa iko taabani, na kusisitiza: "Na wala hatushirikiani nayo kwa jambo lolote lile" Aliendelea kuelezea kuwa CUF walikaa kimya kwa muda, jambo ambalo liliwafanya viongozi wa chama Tawala cha CCM waamini kuwa wamemaliza Simba wa Nyika. "Tulikaa kimya kwa muda na wao wakadai CUF tumeimaliza......, mpaka tulipoanza ziara za Wilaya mbalimbali Unguja na Pemba zikifuatiwa na kuwatembelea wagonjwa..."
Ni vizuri kukumbusha kuwa Maalim Seif alianza ziara zake hizo kwa kuzitembelea wilaya za Pemba ambako alipokelewa na halaiki ya wananchi waliokuwa wakisema "raisi..raisi...raisi". Kufuatia ziara hizo aliitwa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar na kuhojiwa kwa muda wa masaa kadhaa.
Mgomo wa wananchi umeimarika, na umekuwa ukiitikisa serikali na kupelekea ukamataji ovyo wa wananchi kinyume na sheria: "Wameghumiwa, mgomo wa wananchi umeshika kasi...., wakaanza kukamata watu kinyume cha sheria" alisisitiza Maalim Seif.
Badala ya kushughulikia maendeleo ya nchi, serikali imejikita kwenye mikakati ya kuimaliza CUF na wafuasi wake. Hata hivyo, mikakati hiyo imekuwa ikiwaathiri wananchama wa CCM pia. Alitoa mfano wa sakata la kukamatwa ng'ombe na wenyewe kutakiwa kwenda kuwagomboa.
"Kila wanachofanya ni kuwamaliza CUF, lakini ukweli ni kwamba wenye ng'ombe wengi ni wanachama wa CCM", alisema . Maalim Seif aliendelea kufafanua juu ya dhulma wanazofanyiwa raia na mali zao na kutoa mfano wa "jumba la treni", kwa kusema "Watu walihamishwa, kwa ajili ya ukarabati wa jengo lile, na mpaka leo hata ramani haipo" Itakumbukwa kuwa michoro ya kile kinachodaiwa kuwa ni ramani mpya ya mwonekano wa jengo hilo litakavyokuwa ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii, lakini kwa mujibu wa maelezo ya Maalim Sif, ilikuwa ni kiini macho tu.
Aidha Maalim Seif alifafanua kuwa Mji Mkongwe ni sehemu ya Turathi za Kimataifa. Kwa hivyo uvunjaji wa jengo lolote la kihistoria unapaswa kupata ridhaa ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni. Hata hivyo, mpaka wakati tunaingia mitamboni hakuna karatasi yoyote inayoonesha kuwa tayari Serikali ya Zanzibar imewasiliana na kushauriana na shirika hilo. Kwa hivyo ni wazi kuwa uhamishwaji wa wanachi kutoka jengo la treni ulikuwa na malengo ya kisiasa na kuwadhalilisha wananchi.
Upande wa Tanzania.
Kwa vile Tanzania ni Jamhuri ya Muungano nchi mbili huru Tanganyika na Zanzibar, yanayotokea upande mmoja yanaathiri upande mwengine wa Muungano huo kwa njia moja au nyengine. Kwa hivyo, Makamo wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, hakusahau kuigusia hali ilivyo nchini Tanzania chini ya Utawala wa Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli. Maalim Seif aliilezea hali ilivyo nchini Tanzania kisiasa kuwa si yakuridhisha, na serikali iliyopo madarakani inaipelekea nchi pabaya.
Maalim Seif alikosoa hatua ya kuzuiliwa vikao vya Bunge kuonehswa moja kwa moja kwenye televisheni, na kusema lengo lake kuu ni kuua upinzani. Hii ni kutokana na kuwa Bunge lenye mijadala huru ndilo linalojenga upinzani.
Akakosoa hatua ya Wabunge 11 wa upinzani kuzuiliwa kushiriki katika vikao vya Bunge bila ya sababu yoyote ya kimsingi: "Nini kosa lao?, alihoji Maalim Seif, na kujibu mwenyewe kuwa: "Kosa lao kubwa ni kuikosoa Serikali".
Alielezea masikitiko yake kuwa majimbo ambayo Wabunge wao wamezuiliwa yatakosa uwakilishi Bungeni kwa muda mrefu kwani wengine wamefungiwa mpaka mwezi wa Januari mwakani.
Akijibu swali iwapo kuna Mbunge yeyote wa CUF kati ya 11 waliofungiwa, Maalim Seif mwenye upeo wa kuona mbali alisema kuwa hakuna Mbunge yeyote kutoka chama hicho kati ya hao walioathirika na hatua hiyo na kusisitiza: "Nia ni kuugawa upinzani, ili waseme kuwa CUF ni wasaliti"
Alifafanua kauli hiyo kwa kusema kuwa kuna Wabunge wengi wa CUF ambao ni wasemaji wazuri na wakosoaji wakubwa wa Serikali, lakini hawakufungiwa ili watu wenye nyoyo dhaifu waone kuwa CUF ni wasaliti, au vibaraka.
Aidha, mwanasiasa huyo shupavu, aliifananisha hali ilivyo Bungeni na uwanja wa vita kutokana na kuwepo kwa askari wengi ambao mara kadhaa wamekuwa wakiingia ndani ya Bunge."Ukienda Bungeni utadhani uwanja wa vita", alisema.
Alitoa mfano wa nchi kama Uturuki amabko kumetokea mitafatuku Bungeni, lakini hakuna Polisi aliyeingia ndani ya Bunge. Halkadhalika Maalim Seif alielezea wasiwasi wake mkubwa juu ya matumizi mabaya ya Sheria ya Mtandao (Cyber Act) nchini Tanzania.
Aliendelea kwa kuelezea kutoridhishwa kwake na jinsi rais Magufuli anavyoingilia kazi za Mawaziri wake, akitoa mfano wa matamshi ya vitisho aliyoyatoa Mheshimiwa Magufuli dhidi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukhusu tangazo lao la kutisha mikutano ya nchio nzima mnamo tarehe mosi Septemba. "Swali kama hilo umwachie Waziri wako wa Mambo ya Ndani kuingiulia", alisema Maalim.
Kukhusu amri ya kuhamia Dodoma, Maalim Seif alisema kuwa hakuna umuhimu wowote wa kuhamia Dodoma kwa lazima, na kukosoa kauli za vitisho za rais Magufuli dhidi ya watendaji amabao hawataki kuhamia Dodoma waache kazi, na kuelezea khofu yake kuwa hakuna maandalizi ya kutosha."Maandalizi gani yamefanywa?" Alihoji Maalim Seif.
Alielezea wasiwasi wake juu ya upatikanaji wa huduma muhimu katika mji wa Dodoma: "Sote Dodoma tunaijua..., kuna watu wana watoto wanakwenda shule, halafu uwaambie wahame kwa ghafla, rais anapohama ni lazima Mabalozi wamfuate, watakaa wapi Mabalozi?" alihji Maalim Seif.
"Kwa hiyo, hivyo ndivyo Tanzania inavyoendeshwa, ninaposema uvunjaji wa haki za binadamu, siyo Zanzibar tu, bali ni Tanzania kwa ujumla" alisema na kuonya kuwa Visiwani kukichafuka, Bara pia kutaathirika" Akijibu swali kukhusu Masheikh wa UAMSHO walioko gerezani Tanzania Bara, Maalim Seif alijibu kwa kusema: "Hatukuona sababu yoyote ya kupelekwa Bara", na kendelea kuwa Mahakama ya Zanzibar ina mamlaka ya kisheria kuwahukumu watu wote wanaotuhumiwa kwa makosa mbalimbali, bila kuwajibika kuwapeleka Bara.
Aliongeza kuwa: "Kama wana makosa, wangeshtakiwa Zanzibar", akisistiza: "Huu ni udhaifu wa serikali iliyopo, kila lisemwalo na Bara, wao hewallah" Ni vizuri kukumbusha kuwa, Masheikh kadhaa wa Jumuiya ya UAMSHO kutoka Zanzibar walikamatwa na kupelekwa Bara bila kufunguliwa mashtaka katika Mahakama za Zanzibar, jambo ambalo lilizusha mjadala wa kisheria.
Masheikh hao wanatuhumiwa kwa makosa ya kile kinachoitwa ugaidi, na kwa muda wa miaka kadhaa sasa wako rumande na wamenyimwa dhamana kwa madai eti upepelezi bado unaendelea. Hata hivyo Wazanzibari wanaamini kuwa Waumini hao hawana hatia yoyote sipokuwa msimamo wao imara wa kutetea hadhi ya Zanzibar ndani ya Muungano wa Tanzania, khususan ikizingatiwa kuwa walikuwa msitari wa mbele katika kutetea mamlaka kamilii ya Zanzibar wakati wa mchakato wa Katiba mpya iliyofeli ya Tanzania.

MKUU WA MKOA WA MWANZA AFUNGUA RASMI MAONESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (wa pili kulia, akikagua banda la Benki Kuu, kwenye Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kwenye uwanja wa Nyamuhongolo Jijini Mwanza, kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa.

Na BMG
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Biashara Tan-trade kukamilisha ramani ya viwanja vya Nyamuhongolo vinavyotumika kwa maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane ili kuanza ujenzi wa majengo ya kudumu kwenye viwanja hivyo.

Akifungua rasmi jana maonesho ya Nanenane yanayohusisha mikoa ya Kanda ya ziwa, Mongela, alisema kukamilika kwa ramani hiyo kutaharakisha kuanza kwa ujenzi wa mabanda ya kudumu kwenye viwanja hivyo ili kuwezesha kuendelea kwa shughuli mbalimbali hata maonesho yatakapomalizika.


Alisema mkoa wa Mwanza kwa kushirikiana na mikoa mingine ya kanda ya ziwa, umejipanga kuandaa maonesho ya Nanenane kitaifa ndani ya miaka miwili ijayo, hivyo ujenzi wa mabanda hayo utachangia kuongeza hamasha ya mikoa hiyo kuwa mwenyeji.

Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza ameungana na mwenzake wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, kuwahamasisha wakulima wa mikoa hiyo kufufua kilimo cha pamba ambacho amesema kitachangia kufufua viwanda mbalimbali na kuongeza fursa za ajira hasa kwa vijana na hivyo kukuza pato la familia na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wao baadhi ya washiriki wa maonesho hayo zikiwemo taasisi za serikali na wajasirimali, wamesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kutembelea maonyesho hayo tofauti na maonesho ya miaka iliyopita.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo, Damian Chang’a, amesema maonesho ya mwaka huu yanashirikisha jumla ya Halmashauri 18 kutoka mikoa ya Mwanza, Geita, Shinyangana na Mara huku mikoa ya Simiyu na Kagera ikishindwa kushiriki.

Itakumbukwa kwamba, alieyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, nae aliwahi kutoa ahadi kama aliyoitoa Mongela, katika Maonesho ya Nanenane miaka iliyopita.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Benki kuu, kwenye maoneshp ya Nanenane Jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongela (kushoto), akifuatilia jambo kwenye maonesho ya Nanenane Jijini Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack (kushoto) akiteta jambo na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella (kulia).
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye Maonesho ya Nanenane Kanda ya Ziwa.
Burudani ya asili kutoka kikundi cha ngoma za asili Bujora
Mchezo wa nyoka kutoka Bujora
Wapiga picha wakifuatilia wacheza ngoma kutoka Bujora
Taasisi ya Kuzuia na Kutokomeza Ukatili wa Watoto Majumbani, Foundation Karibu Tanzania pia inatoa elimu kwenye Maonesho ya Nanenane Jijini Mwanza.
Bonyeza 

MAALIM SEIF AZUNGUMZA NA WAZANZIBARI BOSTON, SEHEMU YA MWISHO

$
0
0
Na Mwandishi wetu Boston 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, jana aliwasili Zanzibar akitokea Ughaibuni baada ya kukamilisha awamu ya pili ya ziara yake ya Mataifa mbalimbali Ulimwenguni.
Wazanzibari wakimsikiliza Maalim Seif  (Picha na swahilivilla.Blog)
Katika awamu hiyo ya pili, Maalim Seif alitembelea Marekani na kupata nafasi ya kuzungumza na Wazanzibari katika jimbo la Massachusetts. Ifuatayo ni sehemu ya mwisho ya mfululizo wa makala zetu za "Maalim Seif azungumza na Wazanzibari Boston"
Akiwa mwishoni mwishoni mwa hotuba yake, Mwanasiasa huyo Mkongwe alikariri msimamo wa CUF wa kutoitambua serikali ya Zanzibar iliyoko madarakani kwa vile haikupata ridhaa ya wananchi, akisisitiza kuwa serikali hiyo pia haitambuliki Kimataifa.
"Hatuitambui serikali ya Dakta Shein, na hakuna taifa hata moja linaloitambua", alisisitiza.
Maalim Seif alielezea kwamba, wakati wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, wafanyazi wa serikali walikuwa wakipokea mishahara yao kwa wakati. Lakini matokeo ya serikali hiyo kugomewa na wanchi na kutengwa kimataifa, kumezidisha hali ya kiuchumi kuwa mbaya kiasi kwamba serikali inashindwa kuwalipa mishahara wafanyakazi wake kwa wakati.
"Tulifikia hatua nzuri, kiasi kwamba tarehe 22-23 watu walikuwa wameshapata mishahara yao. Sasa hali imezidi kuwa mbaya kiuchumi kiasi kwamba inafika mpaka tarehe 3 watu hawajalipwa", alisisitiza.
Kama Wahenga walivyosema: "Baada ya dhiki faraja", Maalim Seif naye aliwataka Wazanzibari kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha mpito, akiwahakikishia kuwa serikali iliyopo madarakani haitodumu.
".... Wananchi wavumiliye, na mwisho serikali hii itaondoka madarakani", alisihi, na kutamba: "Tutaendelea kufanya wajibu wetu na hatuchoki. Wala wasidhani kuwa tutarudi nyuma kwa kutukamata".
Aidha alikariri wito wake kwa jamii ya Kimataifa wa kuendelea kuibana serikali akisema: "Tunaiomba Jamii ya Kimataifa waendelee kuibana serikali........, na Inshallah itaondoka" alisema huku akijibiwa kwa akauli za "Amin"
Kuvunjika kwa koleo sio mwisho wa uhunzi. Kwa hivyo, kukhusu vitisho vilivyotolewa dhidi yake vya uwezekano wa kukamatwa, Maalim Seif aliyewahi kuwekwa gerezani kwa miaka kadhaa alisema kuwa kukamatwa kwake siyo mwisho wa harakati za Wazanzibari kudai haki yao, akisisitiza: "Kuna Maalim Seif zaidi ya mmoja" Aliongeza kwa kuwaonya viongozi wa Zanzibar dhidi ya kuchukuwa khatua kama hiyo kwa kusema: "....Washukuru sasa hivi kuna mtu ambaye angalau anaweza kusema na watu wakamsikiliza...."
Kukhusu suluhisho la mzozo wa sasa wa kisiasa Visiwani Zanzibar, Maalim Seif alitoa rai ya kuundwa kwa serikali ya mpito itakayosimamiwa na watu wanaoheshimika na ambao hawaelemei upande wowote wa kisiasa. Jukumu kubwa la serikali hiyo ya mpito litakuwa kufanya marekebisho ya sheria za uchaguzi visiwani humo: "Khaswa khaswa Tume ya Uchaguzi", aligogoteza.
Mahakama Ya Kimataifa:
Ni vizuri kukumbusha kuwa katika awamu yake hii ya pili ya ziara zake za Kimataifa, Maalim Seif na ujumbe aliofuatana nao walifika jijini The Hague, Uholanzi, na kufikisha malalamiko ya Wazanzibari.
Alipoulizwa iwapo khatua hiyo ina umuhimu wowote, khususan kwa vile viongozi wengi wa Kiafrika wamekuwa wakitoa wito wa kujitoa kwenye mkataba wa Kimataifa unaokhusiana na mahakama hiyo, Maalim Seif alisema: "Azimio lenyewe halikupita kwenye Mkutano wa Kilele wa Umoja Wa Afrika uliopita"
"Tumejidhatiti kikweli kweli kwa hili, kama wanadhani tunatania, wasubiri", alisistiza na kuongeza: "Tumepata Wakili mahiri, na anasubiri tumpatie vielelezo zaidi tu..., kwa hivyo tuko 'serious' kwa hili" Akijibu swali kukhusu kile kilichoandikwa na baadhi ya magazeti ya Tanzania kuwa Mahaka hiyo ya Uhalifu (ICC) imeitaka CUF kukanusha madai yake, msaidizi wa Maalim Seif aliyefuatana naye kwenye mkutano huo Bwana Issa Kheri Hussein, alitupilia mbali uzushi huo na kusema kuwa hiyo ni propaganda tu.
Aidha alisema kuwa hizo ni mbinu za kuitafuta CUF itoe maelezo kukhusu kile kinachoendelea The Hague kwa vile bado watu hawajui khaswa kinachoendelea na madai yaliyomo katika shauri hilo.

ASASI YA FEDHA YAAMSHA FIKRA KWA VIJANA WA CHUO CHA KILIMANJARO ILI KUFIKIA UHURU WA KIPATO

$
0
0

Muanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa Asasi ya FEDHA Jafari Selemani akizungumzia changamoto za vijana na watanzania kwaujumla juu ya kutokufikia Uhuru wa kifedha (financial freedom) ikiwemo ukosefu wa elimu ya usimamizi fedha binafsi ambapo inapelekea umasikini wa watanzania wengi, pia alitumia nafasi hiyo kuzindua progranu ya FEDHA KLABU ambayo itakayowapa fursa vijana kupata elimu ya udhibiti fedha binafsi buree kila jumamosi chuoni hapo.

Ni mshauri wa vijana pia ni Meneja Masoko wa Taasisi ya FEDHA Abdalah Kipinga akiongea na wanafunzi wa chuo ch Kilimanjaro ambapo alizungumzia juu ya maisha ya wanavyuo na changamoto zake na jinsi ya kuzikabili.

Mhamasishaji wa vijana Elly David akizungumza na wanafunzi wa chuo cha Kilimanjaro (hawapo pichani) ambapo alizungumza kuhusu siri ya mafanikio kwa vijana na kuwaasa kusimamia ndoto zao lkatika kongamano lililofanyika mwishoni wa wiki iliyopita chuoni hapo

Wanafunzi wa chuo cha kilimanjaro wakifurahia jambo wakati wa kongamano hilo lililowezeshwa na Taasisi ya Fedha mwsihoni wa wiki iliyopita

Baadhi ya washiriki wa kongamano wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji katika kongamano hilo lilifnayika mwisho wa wiki iliyopita chuoni hapo Sinza Mapambano ,Jijini Dar es salaam.


DAWASCO YAFUTA TATIZO LA MIAKA 10 LA MAJI SALASALA, DAR ES SALAAM

$
0
0
Meneja wa mkoa wa Dawasco -Tegeta Alpha Ambokile akizungumza na wakazi wa mtaa wa Upendo Salasala jijini Dar es Salaam ambao wameanza kupata huduma ya maji safi katika maeneo yao.
  Bomba likitoa maji katika moja ya mitaa ya Salasala jijini Dar es Salaam.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi blog.
WANANCHI zaidi ya 265 wa mtaa wa Upendo, Mbezi Salasala wilayani Kinondoni wamelishukuru Shirika la Majisafi na Majitaka Dar es salaam (DAWASCO), kwa kuwafikishia huduma ya Majisafi waliyoipatia shida kwa zaidi ya miaka 10 iliyopita.

Akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja wa serikali za mitaa na DAWASCO, Mjumbe wa mtaa wa Upendo Bw. Robert Massawe amepongeza juhudi zilizofanywa na Dawasco za kuwapatia huduma ya Maji wananchi wa eneo lake na kwamba juhudi hizo zinaendana na kauli ya serikali ya awamu ya tano inayosema hapa kazi tu.

Akieleza historia fupi ya eneo hilo Bw. Massawe alisema tangu watu waanze kuhamia eneo hilo huduma ya Maji ilikuwa ni ya kununua kutoka mtaa mwingine wa mbali ambao ulikuwa umefikiwa na huduma hiyo ya Maji.
“Ilifikia kipindi gharama ya kununua Maji ni kubwa kuliko gharama ya chakula, na wananchi wengi walikuwa wakitumia muda wao mwingi kuhangaika kutafuta Maji jambo ambalo lilikuwa likikwamisha kutekeleza majukumu mengine ya kujenga nchi” alisema Massawe.
Nae mmoja wa wakazi wa eneo hilo, Bi. Sofia alisema; “Kweli DAWASCO imemtua mama ndoo ya Maji kichwani, sisi akina mama ndio tuliokuwa tukiteseka zaidi na suala la Maji, lakini akina mama wa mtaa huu tulijitoa ili kupambana na janga la Maji ambalo lilikuwa likitukabili, na hatimaye tumefanikiwa kupata huduma ya Maji”

Kwa upande wa Dawasco, Meneja wa Mkoa wa Tegeta, Bw. Alpha Ambokile amewataka wakazi wa mtaa huo kujitokeza kwa wingi kufanya maombi ya kuungiwa huduma ya Maji kwa kuwa tayari huduma hiyo imefika katika makazi yao, baada ya kuhangaika kwa muda mrefu wakisaka huduma hiyo, na ameahidi kuwaunganishia huduma Maji mapema na kwa uharaka zaidi, mara tu baada ya kupokea maombi yao ya kuungiwa huduma.

“Ninawaomba mjitokeze kwa wingi ili kwa pamoja tuweze kuwaunganishia huduma ya Maji, nitawatengea siku yenu maalum ambayo timu yangu ya ufundi itakuja kuwafanyia maunganisho ya Maji, ambao bado hamjafanya maombi, fanyeni haraka ili tuweze kuwaunganishia wote kwa pamoja huduma ya Maji” alisema Ambokile
 Baadhi ya wakazi wa Salasala wakimsikiliza Meneja wa Dawasco-Tegeta Alpha Ambokile (hayupo pichani)
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kabla ya kuanza kupatikana kwa huduma ya maji katika eneo la Salasala ambapo kwa sasa wakazi wa eneo hilo wanapata huduma ya maji.

RC SIMIYU:WANUFAIKA WA TASAF AMBAO NI ULEVI WAONDOLEWE KWENYE MPANGO

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani) kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo.
Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua jambo kwa wakazi wa Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani) kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo.

Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkoa wa Simiyu)

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewataka viongozi wa kata na vijiji kuwabaini wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya TASAF III(PSSN) wanaojihusisha na ulevi na kuwaondoa katika orodha ya wanufaika wa mpango huo.

Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega katika zoezi la uhawilishaji fedha za TASAF III PSSN, ambapo jumla ya shilingi 2,976,000 zimegawiwa kwa wanufaika 82 kijijini hapo.

Mtaka amesema lengo la mpango wa TASAF III ni kuwatoa watanzania katika hali ya umaskini kwa kuwapa ruzuku itakayowasadia kupata huduma muhimu ikiwa ni pamoja huduma za afya, kuwasaidia watoto wao waweze kwenda shule lakini baadhi ya wanufaika wamekuwa wakitumia fedha hizo kulewa badala ya kuanzisha miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku, mbuzi na kondoo pamoja na kilimo ili miradi hiyo iwasaidie kuwaongezea kipato.

“Hatuwezi kuleta fedha tukifikiri zitawasaidia kujikwamua katika Umaskini lakini mnashinda baa na vilabuni kulewa , wengine mnaongeza wake, tukiwabaini mtaondolewa kwenye huu mpango” , alisema Mtaka.

Mtaka amewataka wanufaika hao kujishugulisha na kilimo na ufugaji na kuondokana na dhana ya kuwa watakuwa wanufaika wa mpango huo siku zote, ambapo alieleza azma ya Serikali ya awamu ya tano ya kuwatoa wananchi katika umaskini na kuwaondolea changamoto mbalimbali kama kutoa elimu ya bila malipo na kuanzisha Mfuko wa Huduma ya Afya Watanzania wasio na uwezo waweze kupata matibabu kwa gharama nafuu na akatoa wito kwa wanufaika hao kujiunga na Mfuko wa Huduma ya Afya ya Jamii (CHF)ambao utawasaidia wao wenyewe pamoja na wategemezi wao kupata huduma za Afya katika Vituo vya kutolea huduma za Afya.

Aidha, ametoa wito kwa wazazi kuwakumbusha watoto wao wajibu wa kuwatunza kwa sababu kumekuwa na baadhi ya wazee ambao wametambuliwa kuwa ni maskini, wakati wana watoto wenye nguvu na uwezo wa kuwasaidia lakini hawatimizi wajibu wao kuwatunza kwa kuwapa mahitaji muhimu.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo Bibi. Christina Robert ambaye ni mnufaika wa mpango wa TASAF amesema mpango huo umemsaidia kuondokana na kuishi katika nyumba ya nyasi na matope na kumuwezesha kujenga nyumba ya matofali na bati.

“Naishukuru TASAF maana imenisaidia sana, ruzuku niliyopewa mara ya kwanza ilinisaidia kutibiwa nilipofanyiwa upasuaji, mara ya pili nilitumia tena kwenye matibabu, mara ya tatu nilinunua kuku na bata, mara ya nne nikanunua bati nikajenga nyumba ya vyumba viwili”, alisema Christina.

Pamoja na kusisitiza juu ya matumizi sahihi ya fedha za ruzuku za TASAF Mtaka amewataka wananchi wa Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuongeza juhudi katika kilimo cha mazao ya mikunde kwa kuwa tayari Serikali ya India imekubali kununua zaidi ya tani milioni sita ya choroko, dengu na mbaazi kutoka Tanzania, hivyo wakati utekelezaji wa makubaliano hayo utakapoanza wananchi walime kwa wingi mazao hayo kwa kuwa kutakuwa na soko la uhakika.

Jumla ya kaya 4260 zilibainishwa katika vijiji 41 vya wilaya ya Busega ambapo kaya 53 ziliondolewa katika mpango wa TASAF III PSSN baada ya uhakiki na kubaini kuwa hazikukidhi vigezo.
Baadhi ya wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III katika kijiji cha Mwamgoba Wilayani Busega, wakiwasikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na katibu tawala Jumanne Sagini (hawapo pichani), walipozungumza nao kabla ya zoezi la uhawilishaji wa fedha za ruzuku kwa ajili ya mpango huo.
Bw. Methesela Mrobi akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na viongozi wengine wa Mkoa na Wilaya(hawapo pichani) Bwawa dogo alilochimba kwa kutumia fedha za ruzuku za Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III, ambalo analitumia kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji
Mkuu wa Wilaya ya Busega , Mhe. Tano Mwera (katikati) na Katibu Tawala Wilaya ya Busega, Bw. Sebastian Masanja (kulia) wakizungumza jambo kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijiji cha Mwamgoba, Wilayani Busega (kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akimkabidhi fedha Bw. Methesela Mrobi wakati wa zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III ,katika kijiji cha Mwamgoba, Wilaya ya Busega Mkoani humo.

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA WA MWEZI JULAI 2016 UMEPUNGUA HADI ASILIMIA 5.1.

$
0
0

  Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraimu Kwesigabo (kulia) akitangaza Mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Julai, 2016 ambao umefikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.5 za mwezi Juni 2016.Kushoto ni Kaimu Meneja wa wa Idara ya Takwimu za Ajira na Bei wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bi. Ruth Minja.
Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia taarifa ya Mfumuko wa Bei wa Mwezi Julai, 2016 iliyokuwa ikitolewa na Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ephraimu Kwesigabo leo jijini Dar es salaam. 


Na. Aron Msigwa – Dar es salaam.

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU (NBS) imetangaza mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Julai 2016 na kueleza kuwa umepungua hadi kufikia asilimia 5.1 kutoka asilimia 5.5 iliyokuwepo mwezi Juni mwaka huu.

Akitangaza taarifa ya mfumuko wa Bei wa Taifa wa mwezi Julai, 2016 leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Bw. Ephraimu Kwesigabo amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2016.

Ameeleza kuwa kupungua kwa mfumuko wa Bei wa mwezi Julai 2016 kumechangiwa na kupungua kwa kasi ya bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula na zile zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Julai 2016 zikiwemo bidhaa za samaki kwa asilimia 6.6, mafuta ya kupikia asilimia 4.9 na maharage kwa asilimia 1.9 huku bei zisizo za vyakula zikihusisha  ni gesi kwa asilimia 21.5, mafuta ya taa 9.4 na dizeli kwa asilimia 10.3.

Kwa upande wa bidhaa zisizo za vyakula zilizoonesha kupungua bei ni pamoja na bidhaa za gesi kwa asilimia 21.5, mafuta ya taa kwa asilimia 9.4 na dizeli kwa asilimia 10.3.

Aidha, ameeleza kuwa pamoja kupungua huko, kasi ya upandaji wa bei ya bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2016 kwenye baadhi ya bidhaa umeonesha kuongezeka katika kipindi hicho hasa kwenye kama  mchele, mahindi, unga wa mahindi, vyakula kwenye migahawa na mkaa.

Bw. Kwesigabo amesema kuwa Fahirisi za Bei nazo zimeongezeka hadi kufikia 103.50 mwezi Julai, 2016 kutoka 103.47 za mwezi Juni 2016, ongezeko  ambalo limechangiwa na kuongezeka kwa bei ya baadhi ya bidhaa za vyakula zile  zisizokuwa  za vyakula.

Amesema ongezeko hilo la Fahirisi linahusisha kundi la bidhaa na huduma za vyakula na vinywaji baridi, Vinywaji vyenye kilevi na bidhaa za Tumbaku, Mavazi ya nguo na viatu, nishati, maji na Makazi pamoja na Samani, vifaa vya nyumbani na ukarabati wa nyumba.

Kundi lingine linahusisha gharama za Afya, usafirishaji, Mawasiliano, Utamaduni na Burudani, Elimu, hoteli na migahawa pamoja na bidhaa na huduma nyinginezo ambazo jumla ya Fahirisi za Bidhaa hizo kwa mwezi huo zimefikia 103.50.

“Baadhi ya bidhaa zilizo sababisha kuongezeka kwa Fahirisi ni pamoja na mafuta ya kupikia asilimia 1.1, samaki wabichi asilimia 6.0, matunda asilimia 4.9, maharage makavu kwa asilimia 2.7, ndizi za kupika asilimia 1.9 na mahindi kwa asilimia 1.5” Amesisitiza Kwesigabo.

Mbali na hilo ameeleza kuwa Mfumuko wa Bei wa Bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi Julai 2016 umepungua hadi kufikia asilimia 7.6 kutoka asilimia 8.1 ya mwezi Juni 2016.

Kwa upande wa uwezo wa shilingi ya 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 96 na senti 62 mwezi Julai 2016 ikilinganishwa na shilingi 96 na senti 65 ya mwezi Juni, 2016.

Aidha, hali ya Mfumuko wa Bei kwa baadhi ya nchi za Afrika Mashariki imeonesha kuwa nchi ya Kenya Mfumuko wa Bei wa mwezi Julai umeongezeka hadi kufikia asilimia 6.39 kutoka asilimia 5.80 za mwezi Juni, 2016, Uganda ikiwa na Mfumuko wa Bei uliopungua wa asilimia 5.1 kwa mwezi Julai kutoka asilimia 5.9 za mwezi Juni, 2016.


RC MONGELLA AZUNGUMZIA ZIARA YA RAIS MAGUFULI MKOANI MWANZA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia) akitoa taarifa ya ujio wa Rais Magufuli mkoani Mwanza. Kushoto ni Katibu Tawala mkoani Mwanza, CP.Clodwig Mtweve.

Judith Ferdinand, Mwanza
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli, anatarajia kufanya ziara fupi ya kikazi mkoani Mwanza.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, leo amesema, Rais Magufuli atafanya ziara ya siku mbili kuanzia kesho agost 10 na 11, ambapo atapokelewa hiyo kesho wilayani Sengerema akitokea Chato mkoani Geita alikokuwa na mapumziko mafupi.

"Rais Magufuli atawasili kesho asubuhi katika mkoa wetu akitokea Chato mkoani Geita na ataanza ziara katika wilaya ya sengerema kwa ajili ya kuwasalimia wananchi, kuwapa taarifa za mikakati na maendeleo awamu ya tano pamoja na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi". Amesema Mongella.

Pia amesema hiyo kesho Rais Magufuli atasimama maeneo mbalimbali kwa ajili ya kuwasalimu wananchi kabla ya kuwasili wilayani Nyamagana.

Ametanabaisha kwamba Rais Magufuli ataitimisha ziara yake kesho kutwa agost 11, kwa kukagua ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu la Furahisha Jijini Mwanza, pamoja na upanuzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi ambapo ataweka jiwe la msingi katika ujenzi wa miundombinu hiyo.

Mongella amewasihi wananchi kujitokeza kwa wingi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika kuanzia majira ya saa nanne mchana katika uwanja wa Furahisha ambapo Rais Magufuli atahutubia wananchi baada ya kukagua miradi hiyo ya ujenzi.


Mwanahabari akiuliza swali

Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.

BUZWAGI YAKABIDHI SHULE MPYA NA NYUMBA ZA WALIMU KWA SERIKALI WILAYANI KAHAMA

$
0
0
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo akifafanua jambo kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Kahama wakati wa ziara ya kupokea miradi ya maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (aliyeweka mkono kwenye mfuko wa suruali) akiwa na wajumbe wengine wa kamati ya ulinzi na Usalama wa wilaya ya Kahama walipofanya ziara katika mgodi wa Buzwagi wa kukabidhiwa miradi ya maendeleo.

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog kanda ya Kaskazini.

Kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi uliyoko wilayani Kahama, katika mkoa wa Shinyanga, umekabidhi kwa uongozi wa katika Halmashauri ya mji wa Kahama majengo ya shule mpya ya msingi Budushi yenye madarasa sita, ofisi ya walimu na nyumba moja ya walimu yenye uwezo wa kuishi familia mbili.

Akikabidhi madarasa hayo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi mhandisi Asa Mwaipopo amesema ujenzi huo umefadhiliwa na Mgodi wa Buzwagi kwa zaidi ya shilingi milioni mia nne na themani kupitia mfuko wa Acacia Maendeleo Fund, ambao umelenga kuwapunguzia adha wanafunzi wa eneo hilo la Budushi na maeneo yanayozunguka eneo hilo kuondokana na adha ya kutembea mwendo mrefu kwenda shule.

Aidha, Meneja mkuu huyo wa Mgodi wa Buzwagi alikabidhi pia nyumba mbili za kisasa za walimu zenye uwezo wa kuishi familia nne kwa shule ya msingi Mwime hatua ambayo amesema kuwa itasaidia katika kupunguza tatizo la nyumba kwa walimu kwa shule hiyo. Nyumba hizo ambazo zimejengwa kwa kutumia teknolojia ya Tofali za kufungamana zimegharimu shilingi milioni mia mbili arobaini na nane (248,126,000/=)

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Mh. Fadhili Nkurlu aliyepokea miradi hiyo ameupongeza uongozi wa Mgodi wa Buzwagi kwa jitihada ambazo wamekuwa wakizifanya katika kuhakikisha wanashirikiana na jamii katika kutekeleza miradi ya Maendeleo”

Akizungumza kwa niaba ya halmashauri ya mji wa Kahama Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Abel Shija ameupongeza uongozi wa Mgodi na kuahidi kuendelea kushirikiana nao katika kuiletea Jamii Maendeleo.

Meneja Mkuu wa Mgodo wa Buzwagi Asa Mwaipopo akieleza jambo kwa wajumbe wa kamati ya ulinzi na Usalama wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu.
Kifaa maalumu cha kupoza umeme ambacho kitatumika kupeleka umeme katika mji wa Kahama na kungunguza tatizo la kukosekana kwa umeme kikiwa kimefungwa katika kituo cha Umeme cha mgodi wa Buzwagi.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (Mwenye kofia ya blue) akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu (mwenye kofia ya kaki) wakati wa makabidhiano ya madarasa ya shule mpya ya msingi ya Budushi, wengine katika picha ni mbunge wa kahama mjini Mhe.Jumanne Kishimba na Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Kahama Mhe.Abel Shija.
Mkuu wa wilaya Kahama Fadhili Nkurlu na Mbunge wa Kahama Mhe.Jumanne Kishimba wakizindua majengo ya shule mpya ya Budushi iliyojengwa kwa ufadhili wa mgodi wa Buzwagi.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu na Mwenyekiti wa kijiji cha Budushi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa majengo na nyumba moja ya walimu katika shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu (mwenye kofia ya kaki) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Mgodi wa Buzwagi na Watendaji wa Kata ya Mwendakulima
Moja ya majengo ya madarasa yaliyojengwa katika Shule ya Msingi Budushi chini ya ufadhili wa Mgodi wa Buzwagi.
Mkuu wa wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu akiteta jambo na baadhi ya viongozi wa kata ya Mwendakulima.

GAZETI LA MSETO LATAKIWA KUMWOMBA RADHI NAIBU WAZIRI WA UJENZI

$
0
0
Na: Abushehe Nondo, MAELEZO
Dar es salaam.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi. Edwin A. Ngonyani (Pichani Kulia) amelitaka gazeti la Mseto kumuomba radhi na kumlipa fidia ya shilingi bilioni moja kutokana na kuandika habari ya kumchafua.

Akizungumza na waandishi wa habari Ofisi kwake Waziri Ngonyani amesema kuwa Gazeti hilo la tarehe 4 Agosti 2016 liliandika habari yenye kichwa cha Habari “Waziri amchafua JPM” ikimuhusisha na upokeaji wa fedha kutoka moja ya Kampuni ya Madini wakati akiwa Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Madini la Taifa (Stamico).
“Nimewaandikia notisi ya siku saba ikiwataka waombe radhi na kunilipa fidia, na wasipofanya hivyo hatua stahiki kuwapeleka mahakamani akiwemo Mwandishi Josephat Isango, Mwanahalishi Publisher na Mchapaji wa gazeti hilo”. Alisema Mhandisi Ngonyani.

Mhandisi Ngonyani amesema kuwa habari hiyo siyo ya kweli na mwandishi ametumia nyaraka za kughushi ikiwemo barua iliyoandikwa tarehe 24 Julai na kutiwa saini yake akiwa Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO wakati ukweli ni kwamba tarehe hiyo yeye alikuwa ni Mkurugenzi kamili na siyo Kaimu kama barua hiyo inavyosomeka.
Ameongeza kuwa habari hiyo imewachafua watu wengi ikiwemo familia yake, wapiga kura wake wa jimbo la Namtumbo ambao walijitoa katika kumsaidia wakati wa kampeni na hali kadhalika zimemchafua Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumhusisha na fedha kutoka kwa wawekezaji wa nje kwa kuwaahidi kuwa mitaji yao nchini itakuwa salama.

“Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli alishasema kama kuna mfanyabiashara yeyote aliyechangia kuingia kwake ikulu ajitokeze na hakuna aliyefanya hivyo, Iweje leo mtu tu anaibuka na kuandika habari za kugushi? ”. Aliongeza.

Aidha Naibu Waziri huyo ametumia fursa hiyo kuwataka waandishi wa habari nchini kuwa waangalifu pindi wanapoandika habari za kutunga kwa kutotumia majina halisi kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na kanuni za uandishi wa hadithi (Habari za kutunga).
“Waandishi wa habari mnatakiwa kufuata maadili ya kazi yenu kwa kuandika habari zenye ukweli ili kuliepusha taifa kuingia katika machafuko na migogoro isiyo ya lazima” Alisema Naibu waziri huyo.

TANZANIA NI MIONGONI MWA NCHI ZINAZOFANYA VIZURI UWEZESHAJI WANAWAKE.

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na wageni mbalimbali waliohudhuria hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani. Kwa mujibu wa Hanns Seidel Foundation, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa wanawake.
Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller akitoa uzoefu wa nchi ya Bavaria katika kushughulikia masuala ya wanawake kupitia Sera zilizopo nchini humo wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani jijini Dar es salaam.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula (kushoto) ambaye ni miongoni mwa wanawake viongozi wa Tanzania walionufaika na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation akizungumza jambo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati wa hafla fupi ya Tathmini ya Mafanikio ya Mfuko wa Hanns Seidel Foundation nchini Tanzania, jana usiku jijini Dar es salaam.


Na.Aron Msigwa – Dar es salaam.

Mfuko wa Hanns Seidel Foundation (HSF) unaojihusisha na uwezeshaji wa wanawake katika nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali umeitaja Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa wanawake duniani.

Mwenyekiti wa Mfuko huo ambao makao yake yako nchini Ujerumani Prof. Prof.Ursula Mannle ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati hafla fupi iliyoandaliwa na mfuko huo kwa lengo la kufanya tathmini ya mchango wa HSF nchini Tanzania katika kuwajengea uwezo wanawake vijana katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa.

Prof. Ursula amesema kuwa HSF imekuwa ikitekeleza program mbalimbali za uwezeshaji kwa wanawake kisiasa, kuwaandaa na kuwajengea uwezo wa kuwa viongozi mahiri katika nchi wanazotoka.


Amesema HCF imeamua kuanzisha programu maalumu nchini Tanzania kwa ajili ya kuwaangalia wanawake wanaojitokeza kugombea katika nafasi mbalimbali za uongozi ili kuwawezesha kuwa viongozi katika nafasi mbalimbali serikalini pia kuziba pengo lililopo la uwakilishi katika nafasi za kisiasa.
Ameeleza kuwa Hanns Seidel Foundation itaendelea kuwaunga mkono wanawake wa Tanzania wanaojitokeza kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa nchini Tanzania kupitia program mbalimbali za ufadhili ili kuwawezesha kumudu gharama na kuwajengea uwezo wa kushindana katika majukwaa ya Siasa.

Waziri Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto kutoka Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa hafla hiyo amesema kuwa Serikali ya Tanzania imeendelea kutoa kipaumbele katika nafasi za uongozi kwa wanawake.

Amesema licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali zinazowakabili wanawake vijana wa Kitanzania zikiwemo za kijamii na kimila pia ndoa na mimba za utotoni zinazochangia vijana wanafunzi wa kike kuacha masomo yao, Serikali ya awamu ya Tano imeamua kuja na Sera ya Elimu bure kuwawezesha vijana wa kike wa kitanzania kupata elimu.

Amesema Tanzania imeendelea kuwathamini wanawake katika uteuzi wa ngazi mbalimbali za uongozi Serikalini kuanzia wakuu wa Wilaya, Mikoa, Wakurugenzi, Mawaziri na Naibu Mawaziri pia uwepo wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye ni alama ya hamasa na ushindi katika uongozi kwa wanawake wengine Tanzania.

Mhe. Mwalimu ameushukuru Mfuko huo kwa mchango wake katika kuwainua wanawake wa Tanzania pia program mbalimbali zilizoanzishwa na mfuko huo kwa lengo la kuwawezesha wanawake nchini.

Kwa Upande wake Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller akitoa uzoefu wa nchi ya Bavaria katika kushughulikia masuala ya wanawake amesema kuwa kupitia Sera zinazosimamia masuala ya wanawake mambo mengi yameweza kufanyika.
Ametoa wito kwa Tanzania kuendelea kuzishughulikia changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa kikwazo kwa wanawake wa Tanzania kufika mbali na kuwazuia wasiweze kusimama wenyewe katika masuala ya Siasa.

Naye Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe. Angelina Mabula ambaye ni miongoni mwa wanawake wa Tanzania walionufaika kutokana na HSF amesema kuwa alianza harakati za siasa mwaka 2004 licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali.

Amesema kuwa ipo haja ya wagombea wanawake vijana wanaoingia katika ulingo wa siasa kusaidiwa kifedha na mfuko huo pamoja na vyama vyao vya siasa wanavyoviwakilisha pindi wanapogombea nafasi mbalimbali za uongozi na kuongeza kuwa wakati umefika kwa wanawake wanaoingia katika siasa kusimama wenyewe kwenye majimbo ya uchaguzi.

Ametoa wito kwa HSF kuendelea kuwasaidia wanawake vijana wanaoingia kwa mara ya kwanza katika masuala ya siasa kwenye chaguzi zinazokuja ili kuwawekea mazingira mazuri ya kukabiliana na changamoto zinazowakabili.

Prof.Ursula Mannle, Mwenyekiti wa Mfuko wa Hanns Seidel Foundation wenye makao yake nchini Ujerumani unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani akizungumza wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko huo jijini Dar es salaam. Kwa mujibu wa Hanns Seidel Foundation, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika uwezeshaji wa wanawake.
Waziri wa Nchi, Kazi na Mambo ya Jamii kutoka nchini Bavaria Emilie Müller (kulia) akifurahia picha ya kuchorwa aliyokabidhiwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (katikati) jana jijini Dar es salaam wakati wa hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani. Kushoto ni Prof.Ursula Mannle, Mwenyekiti wa Mfuko wa Hanns Seidel Foundation wenye makao yake nchini Ujerumani.
Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla fupi iliyoandaliwa na Mfuko wa Hanns Seidel Foundation unaojihusisha na masuala ya uwezeshaji wa wanawake katika Nyanja za uongozi, usawa kijinsia na masuala ya siasa katika nchi mbalimbali duniani, jana jijini Dar es salaam.





Viewing all 3497 articles
Browse latest View live