↧
KOFFI OLOMIDE AKIWA NA ALIYEMPIGA, AELEZA KILICHOTOKEA KWA WANAHABARI
↧
MWENYEKITI CCM MARA ATUHUMIWA KWA USALITI
Na Mwandishi Wetu, MWANZA
BAADHI ya wenyeviti wa Kata,Matawi pamoja na mabalozi wa nyumba kumi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya za Mkoa wa Mara wamemtuhumu Mwenyekiti wa chama hicho mkoani humo Christopher Sanya kuwa alikihujumu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana na kusababisha kipoteze majimbo manne kati ya tisa na kumtaka ajiuluzu kabla ya kutimuliwa.
Pia walidai kuwa anaongoza kwa majungu akiongozwa na mmoja wa wabunge wa majimbo ya mkoa wa Mara huku wakimtuhumu kujihusisha na kundi linalopinga Rais John Magufuli asikabidhiwe Uenyekiti wa CCM Taifa na amekuwa akiwashawishi wajumbe wasimpigie kura.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili jijini Mwanza jana kwa sharti la hifadhi ya majina wenyeviti hao kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana alikisaliti chama pamoja na kuwachonganisha wanachama na kusababisha majimbo manne kunyakuliwa na wagombea wa UKAWA.
Walieleza kuwa Sanya kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka jana alitafuna posho za mabalozi wa CCM akishirikiana na Katibu msaidizi wa CCM wakashindwa kufanya kampeni kisha katibu huyo akahamishiwa wilayani Rorya.
Kutokana na tuhuma hizo wanachama wa Wilaya za Rorya,Serengeti, Tarime na Bunda wamemwomba mwenyekiti mpya wa CCM Taifa atakapobidhiwa rungu atumbue jipu hilo linalokwamisha maendeleo ya chama na wananchi.
“ Tunafahamu mwenyekiti wetu wa CCM mkoa wa Mara ni jipu na msaliti mkubwa kwenye kampeni alishiriki kuwaangusha wagombea wetu Bunda (Wassira) na Serengeti (Kebwe) kwa kuwasaidia wapinzani.Matokeo baada ya kutangazwa alifanya sherehe” alisema mmoja wa wenyeviti hao wa matawi na kata kwa sharti la hifadhi ya jina.
Wenyeviti hao walionya kuwa endapo mwenyekiti mpya akipuuuza kumfukuza kwenye chama kwa usaliti pamoja na washirika wake basi CCM Mara itaparaganyika kama si kufutika na majimbo yaliyopotea hayatarudi na hata waliyoshinda watayapoteza.
Naye Sanya akizungumza kwa simu na gazeti hili kuhusiana na tuhuma hizo alikana na kumtuhumu Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Rorya Samwel Kiboye “ Namba 3” kuwa ndiye anatengeza habari hizo kwani hakuna mwenyekiti anayeweza kumtuhumu.
“ Usipoteze muda kwa mambo kama hayo,kama ni malalamiko tuna vikao vya kuyasikiliza na kutoa uamuzi,uchaguzi ulishaisha na wananchi walifanya uamuzi.Tuhuma za usaliti sina sera hiyo ya kuhujumu chama na ukweli utabaki pale pale.Mi ni Mwenyekiti, acha mambo hayo usipoteze muda,
“ Wananchi na wanachama si wajinga.Tatizo la kupoteza majimbo linafahamika maana baada ya uchaguzi tulikaa na kubaini nani alifanya nini,hivyo hakuna logic.Lakini kuna wakati tuliwaudhi wananchi na jimbo moja hilo la Bunda haliwezi kuwa na madhara kiasi hicho,” alisema Sanya.
Mwenyekiti huyo alidai kuwa yote hayo yanatengezwa na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya moja kwa sababu anataka kugombea na hivyo anatafuta nafasi ya kumchafua na kuelea kuwa binafsi anaishi vizuri na wenyeviti wake wa wilaya na watashangaa kusikia mambo hayo.
“Uchaguzi wa kiti ujao ndio umeanza hivyo,wana CCM sio wajinga, niko imara na chama changu na fitna ni sehemu ya siasa.Namba 3 ndiye anatengeneza story ili apate kunichafua sababu anataka kugombea uenyekiti na mimi lazima nitulize hali hiyo maana uchaguzi bado, muda ukifika wanachama wataamua nani anafaa kuwaongoza,”alisema Saa
nya kwa simu.

KOFFI OLOMIDE AKAMATWA NA POLISI KWA KUMPIGA TEKE MNENGUAJI WAKE(VIDEO)
↧
MAMBO YAMENOGA MKUTANO MKUU MAALUMU WA CCM MJINI DODOMA
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kulia), akiwa pamoja na Diwani wa Kata ya Igoma Jijini Mwanza, wakiwa katika Viunga vya Ukumbi mpya wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Dodoma wa Dodoma Convetional Centre ambapo Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unafanyika.
Ni Mkutano Maalumu kwa ajili ya Wajumbe hao kumchagua Mwenyekiti Mpya wa CCM Taifa, ambapo jana Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM walipitisha kwa kura zote jina la Rais Dkt.John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa chama hicho. Dkt.Magufuli anapokea kijiti cha uongozi wa chama kutoka kwa Rais Mstaaf wa awamu ya nne Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Mji wa Dodoma umegubikwa na shamra shamra mitaa yote na tayari wajumbe wa Mkutano Mkuu wameanza kuingia Ukumbini kwa ajili ya Mkutano huo huku hali ya usalama ikiwa imeimarishwa vyema kila kona.Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula akisalimiana na mjumbe mwenzake wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma hii leoMbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (kushoto) akiwa na Katibu wake, Heri James, Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma hii leoHeri James (kushoto) akiwa na mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM, wakisalimiana ukumbini.Mbunge wa Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza, Angelina Mabula (kushoto), akiwa ukumbini na mmoja wa wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM.Kaimu Katibu wa CCM mkoani Mwanza Elias Mpanda (kulia) akisalimiana na aliekuwa Mkuu wa Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, Manju Msambya (kushoto).Baadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka mkoani MwanzaBaadhi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM akiwemo Le Mutuz (kulia) wakiperuzi taarifa mbalimbali kuhusiana na Mkutano huo.Mbunge wa Jimbo la Mtama ambae pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akitoa burudani na Bendi ya TOT PusNi burudani kutoka kwa bendi ya TOT Pus UkumbiniMbunge wa Jimbo la Mtama ambae pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nhauye, akitoa mwongozo wa kuanza kwa Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaofanyika Mjini Dodoma.Taswira Ukumbini

Wanafunzi watarajiwa chuo cha UDSM wafundwa juu ya maisha ya chuo

↧
↧
KIJANA GOZBERT BWELE ALIVYOMPAGAWISHA MAKAMU WA RAIS WA HISPANIA MJINI NANSIO
WAKATI wasanii wa kundi la ngoma za utamaduni la Utandawazi wanajipanga kutumbuiza, watu wengi waliokusanyika kwenye viwanja wa shule ya msingi Bukongo mjini Nansio walikuwa wanajiuliza mtoto Gozbert Bwele (8) aliyekuwa amekumbatia ngoma alikwenda kufanya nini pale.
Lakini mara tu ngoma zilipoanza kupigwa, uwanja mzima ukalipuka kwa furaha na haikushangaza wakati makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandez de la Vega, aliposhindwa kuvumilia na kutoka kwenda kucheza na mtoto huyo aliyeonyesha ufundi mkubwa katika upigaji wa ngoma.
Mama Maria Teresa, ambaye ni rais wa taasisi ya Mfuko wa kusaidia Wanawake Afrika, alijitoma uwanjani kucheza na kumtunza mtoto huyo anayesoma darasa la kwanza kwenye shule ya msingi Nansole katika halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.
Makamu huyo wa rais mstaafu wa Hispania alizuru kisiwani Ukerewe akiwa ameongozana na ujumbe wake kwa lengo la kujionea kilimo cha viazi lishe na usindikaji wa mazao mbalimbali yatokanayo na viazi hivyo.
Kilimo hicho kinafanywa na akinamama 25 chini ya Mradi wa Green Voices unaofadhiliwa na taasisi ya Mfuko wa kusaidia Wanawake Afrika, ambao kwa hapa nchini umewawezesha wanawake wa Tanzania kubuni miradi endelevu inayoendana na utunzaji wa mazingira pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Lakini mara tu ngoma zilipoanza kupigwa, uwanja mzima ukalipuka kwa furaha na haikushangaza wakati makamu wa rais mstaafu wa Hispania, Mama Maria Teresa Fernandez de la Vega, aliposhindwa kuvumilia na kutoka kwenda kucheza na mtoto huyo aliyeonyesha ufundi mkubwa katika upigaji wa ngoma.
Mama Maria Teresa, ambaye ni rais wa taasisi ya Mfuko wa kusaidia Wanawake Afrika, alijitoma uwanjani kucheza na kumtunza mtoto huyo anayesoma darasa la kwanza kwenye shule ya msingi Nansole katika halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza.
Kilimo hicho kinafanywa na akinamama 25 chini ya Mradi wa Green Voices unaofadhiliwa na taasisi ya Mfuko wa kusaidia Wanawake Afrika, ambao kwa hapa nchini umewawezesha wanawake wa Tanzania kubuni miradi endelevu inayoendana na utunzaji wa mazingira pamoja na kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
↧
TAARIFA ZA KUPOTEA KWA MTOTO GERALD DAVID BWANAMGANGA
Mtoto GERALD DAVID BWANAMGANGA anayetafutwa na wazazi wake.
Tunaomba Watu, Mtu yeyote atakayeweza kumuona, basi anaweza kumfikisha Kituo Cha Polisi kilicho karibu nae. Au unaweza kuwasiliana na wazazi wa mtoto kwa namba 0713 040 615 ama 0712 185 226. Pia unaweza kupiga simu namba 0675 306 990.
Lakini Endapo mtu atamuona basi anaweza kutoa taarifa Polisi au hata Pia Kutoa taarifa kupitia makundi mbalimbali ya Whatsapp ambayo tunaamini pia taarifa itawafikia haraka wazazi au hata ndugu kama ambavyo taarifa ya kupotea kwake ilivyoweza kutufikia sisi na kuamua kutoa msaada wa kutangaza kupitia hapa.
Tunajua ni jinsi gani Maumivu wanayoyapata wazazi wake lakini Tunamuombea kwa Mungu amlinde huko aliko na Malaika wake wamrudishe mtoto wetu GERALD DAVID BWANAMGANGA Salama Salimini kwenye himaya ya wazazi wake.
Tunatoa pole kwa Wazazi kwa kupotelewa na Mtoto wao Kipenzi lakini tunapenda kuwaambia kuwa Wamwamini Mungu kwa maana Kila hatua wazikabidhizo kwake na kuamini basi Mungu atawatendea.
TUNAOMBA MSAADA KUSAMBAZA TAARIFA HIZI.
↧
TANAPA YAIONGEZEA NGUVU TIMU YA TAIFA YA RIADHA INAYOJIANDAA NA MASHINDANO YA OLIMIPIKI

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
SHIRIKA la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza kutumia fursa ya mashindano ya Olyimpiki yanayotarajia kuanza mwezi ujao katika jiji la Rio de Janeiro nchini Brazili kutangaza vivutio vya utalii kupitia wanariadha wa Tanzania.
Hadi sasa ni wanariadha wanne ,wakiume watatu na wa kike mmoja ndio waliofuzu kushiriki mashindano hayo na tayari wako kambini katika hosteli za Chuo cha Misitu cha FITI zilizoko West Kilimanjaro wilayani Siha.
Akiongea mjini Arusha wakati akikabidhi msaada wa fedha na vifaa kwa ajili ya wanariadha hao Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA,Allan Kijazi amesema wameamua kutumia fursa hiyo pia kusaidia wanariadha hao wanaoiwakilisha nchi katika mashindano hayo ili waweze kurejea na medali.
Akishukuru kwa msaada huo Rais wa Shirikisho la Riadha nchini ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu AnthonY Mtaka amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuwakatia bima ya Afya mwaka mmoja wanariadha hao pamoja na familia zao ili wanapokua nchini Brazili wasiwe na mawazo mengi kuhusiana na familia zao walizoziacha hapa nchini.
Naye mmoja wa wanariadha waliofuzu kushiriki mashindano hayo Alphonce Felix pamoja na mkufunzi wa timu hiyo ya Riadha Francis John wameushukuru uongozi wa Riadha kwa kuiwezesha timu hiyo kukaa kambini kwa miezi saba na kuahidi safari hii timu hiyo haiendi kushiriki bali kupambania medali.
Wanariadha waliopo katika timu hiyo ya taifa wanaotarajiwa kwenda Brazili ni mwanamke pekee Sara Ramadhani, Fabiani Joseph, Saidi Makuka na Alfonce Felix .
↧
MAALIM SEIF KUNGURUMA TENA MAREKANI
Na Mwandishi wetu, Philladelphia
Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar na Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, anatazamiwa kunguruma tena chini Marekani wiki hii.
Maalim Seif Sharif Hamad akiwasili katika uwanja wa ndege Philladelphia
Gwiji huyo wa siasa ambaye aliwasili jijini Philladelphia hapo jana, anatarajiwa kuwakhutubia Watanzania katika Mkutano wa hadhara utakaofanyika Jumamosi hii katika jiji la Boston. Katibu huyo Mkuu wa CUF pamoja na ujumbe anaofuatana nao aliwasili nchini humu akitokea Uingereza baada ya kukamilisha ziara yake ya Ulaya iliyochukua muda wa zaidi ya wiki moja.
Akiwa Ulaya Maalim Seif alitembelea Uiengerza na kufanya mikutano na Maofisa wa ngazi za juu wa Serikali ya Uingereza, Vyama vya kisisasa na Taasisi mbalimbali. Baadaye alielekea nchini Ubelgiji ambako alifanya ziara kwenye Makao Makuu ya Umoja wa Ulaya na kufikisha madai ya Wazanzibari ya kurejeshewa haki yao ya Kidemokrasia.
Aidha alitembelea nchini Uholanzi ambako pamoja na mambo mengine, alikutana na maofisa wa Mahakama ya Ukhalifu ya Kimataifa na kufikisha kilio cha Wazanzibari dhidi ya Uvunjaji wa Haki za Binadamu unaendelea Visiwani Zanzibar.
Ziara hiyo ya Ulaya ilikuja katika kile maofisa wa CUF walichokielezea kuwa ni awamu ya pili ya ziara za nje za mwanasiasa huyo mkongwe katika juhudi za kutafuta uungwaji mkono wa Kimataifa kwa mgogoro wa Kisiasa Zanzibar.
Maalim Seif ambaye anafuatana na Mkuuwa Watumishi katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa CUF Bwana Issa Kheir Hussein, yupo nchini Marekani kuitikia mwaliko wa kuhudhuria kwenye Mkutano Mkuu wa Chama Cha Democratic ulioanza jana jijini Philladelphia, mkutano ambao unatazamiwa kumpitisha Bi Hillary Clinton kuwa mgombea wa Urais wa Marekani kwa kuoitia tiketi ya Chama hicho.
Katika mkutano wake wa hadhara na Watanzania, Maalim Seif, aliyekuwa mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha CUF katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Oktoba mwaka jana, anatazamiwa kuzungumzia zoezi zima la uchaguzi huo uliofutwa, na kusisitza madai ya Chama chake ya kurejeshewa haki yao waliyoporwa katika uchaguzi huo, na mwenendo mzima wa Demokrasia nchini Tanzania.
Itafaa kukumbusha kuwa hii ni mara ya pili kwa Maalim Seif kuzuru Marekani katika kipindi cha chini ya miezi miwili. Mwezi uliopita, Maalim Seif alikuwepo nchini humu na kufanya mazungumzo na viongozi wa Kisiasa na mashirika binafsi, na kutembelea Umoja wa Mataifa ambako alifikisha madai ya Chama chake ya ukandamizaji wa demokrasia nchini Tanzania. Aidha alizungumza na Watanzania waishio nchini Marekani katika jiji la Washington.

GGM YAFANIKISHA ZOEZI LA KUKUSANYA PESA KWA AJILI YA MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI

Makamu wa Rais wa Kampuni ya Mgodi wa Geita Gold Mining (GGM) Simon Shayo akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya mapokezi ya washiriki wa changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi.
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
↧
DC MUHEZA AFANYA ZIARA HOSPITALI YA MUHEZA, AWATAKA WATUMISHI KUACHA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA
MKUU wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto akipofanya ziara ya kuitembelea hospitali ya Teule kuangalia changamoto zinazoikabili kulia ni Mganga Mfawizi wa Hospitali hiyo,Malahiyo Rajabu katikati ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza
Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyekaa kulia kuzungumza na watumishi wa Hospitali Teule ya Muheza
Mganga Mfawizi wa Hospitali Teule ya Muheza Malahiyo Rajabu akizungumza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo ambaye hayupo pichani wakati alipofanya ziara ya kuitembelea hospitali hiyo
Mganga Mfawizi wa Hospitali Teule ya Muheza Malahiyo Rajabu kulia akitoa ufafunuzi kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo kushoto katikati ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza wakati mkuu huyo wa wilaya alipofanya ziara kwenye hospitali hiyo
kulia ni Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo akisisitiza jambo kwa DMO wa wilaya ya Muheza wa pili kutoka kushoto Dkt Elias Mayala wakati alipofanya ziara ya kuitembelea hospitali Teule ya Muheza
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo wa pili kutoka kulia aliyevaa hijabu akipata maelezo kutoka kwa mhudumu wa zama katika hospitali Teule ya Muheza kushoto mara baada ya kufanya ziara ya kuitembelea anayefuatia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Teule Muheza Mkoani Tanga,Malahiyo Rajabu kushoto akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kabla ya kuingia kwenye chumba cha maabara wakati alipofanya ziara ya kuitembelea hospitali hiyo
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo katikati akitembea hospitali ya Teule wilayani humo kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo,Malahiyo Rajabu kushoto ni DMO wa wilaya ya Muheza,Daktari Elius Mayala
Kulia ni Mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule ya Muheza,Malahiyo Rajabu akimueleza jambo Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kuhusua namna wanavyofanya kazi kwenye maeneo mbalimbali ambaye alifanya ziara ya kushtukiza ya kuitembelea hospitali hiyo Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
↧
BRAND NEW MUSIC: KALA JEREMIAH ft. MIRIAM CHIRWA - WANANDOTO (OFFICIAL VIDEO)
↧
VODACOM FOUNDATION YATUMIA BILIONI 15 KATIKA MIRADI YA JAMII NCHINI
Vodacom Tanzania imekuwa na kauli mbiu ya “Kufana maisha ya watanzania kuwa bora,sio kupitia huduma za mawasiliano pekee bali pia kusaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii kupitia taasisi yake ya kusaidia masuala ya kijamii ya Vodacom Tanzania Foundation.
Katika kipindi cha miaka 10 taasisi ya Vodacom Tanzania imekuwa ikifanya kazi na taasisi za serikali na wadau wengine kukabiliana na changamoto zinazowakabili wananchi wengi hususani katika sekta za elimu , afya na uwezeshaji wa kuinua makundi mbalimbali kiuchumi.
Kwa mujibu wa ripoti ya Vodacom Tanzania Foundation imebainishwa kuwa kuanzia mwaka 2006 hadi imetumia shilingi bilioni 15 kwa kufadhili miradi ipatayo 130 ya kijamii lengo kubwa likiwa ni kuleta mabadiliko kwa kuboresha maisha ya wananchi kwenye jamii.
Uboreshaji wa maisha ya wananchi umefanika kwa kutumia teknolojia ya mtandao wake kuboresha huduma mbalimbali na kuokoa maisha ya wananchi kupitia miradi mbalimbali.
Vodacom Tanzania Foundation imekuwa ikitumia teknolojia katika miradi ya kuboresha huduma za uzazi na kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga kupitia huduma ya kutuma na kupokea pesa ya ijulikanao kama M-Pesa.
Moja ya mradi huu wa kuokoa maisha ya akina mama wajawazito kupitia huduma ya M-Pesa unaendeshwa katika wilaya za Sengerema na mkoani Shinyanga ambao unafanika kwa kushirikiana na madereva wa teksi.Madereva waliosajiliwa katika mradi huweza kuwawahisha akina mama wajawazito katika vituo vya afya waonapo dalili za kujifungua ambapo madereva hao hupatiwa malipo yao kupitia simu zao za mkononi na umeonesha mafanikio makubwa ukiwa umeweza kuokoa maisha ya akina mama wajawazito na watoto wachanga wapatao 225 kwa mwezi.
Mradi mwingine ambao Vodacom Tanzania Foundation imeufankisha na umeleta mabadiliko makubwa ni mradi wa kutokomeza ugonjwa wa Fistula ambao imeuendesha kwa kushirikiana na taasisi ya Comprehensive Community Based Rehabilitation in Tanzania (CCBRT).
Kupitia huduma ya M-Pesa akina mama waliobainika kuwa na ugonjwa wa Fistula walikuwa wakilipiwa gharama za usafiri za kuwawezesha kufika katika hospitali ya CCRBT kupatiwa matibabu bila malipo na wakipona wanaripiwa gharama za kurejea makwao.Mradi huu umeweza kuwanufaisha akina mama wapatao 2, 482.
Kwa upande wa elimu ,Vodacom Tanzania Foundation imewezesha wanafunzi kutoka shule za msingi na sekondari kuingia katika ulimwengu wa kompyuta kwa kusaidia kuzipatia vifaa vya maabara za kompyuta ili waweze kusoma somo hilo kwa nasharia na vitendo.Kwa kushirikiana na kampuni ya Samsung imekuwa ikiendesha mradi wa Smart School ambao umekuwa na mafanikio makubwa na kuwanufaisha wanafunzi zaidi ya 8,000 kwa kupatiwa laptop ,vifaa vya kujifunzia kwa njia ya mtandao wa kidigitali na kuunganisha mtandao wa interneti mashuleni.
Afisa Mtendaji wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Rosalynn Mworia amesema kuwa matumizi ya teknolojia ameboresha mabadiliko ya wananchi kuwa bora “Tumeshirikiana na serikali na wadau wengine kuboresha huduma za elimu,afya na kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi”.Baadhi ya miradi ambayo imeleta mabadiliko makubwa kwa jamii ni mradi wa kuwawezesha wasichana wa Hakuna Wasichoweza na mradi wa kuelimisha masuala ya afya na uzazi ujulikanao kama Wazazi Nipendeni.
Katika mradi wa Hakuna Wasichoweza ambao unatekelezwa kwa ushirikiano na shirika lisilo la kiserikali la T-MARC katika mikoa ya Lindi na Mtwara umefanikiwa kupunguza utoro kwa wasichana mashuleni uliokuwa unatokana na changamoto za vipindi vya hedhi kwa kutokuwa na vifaa vya kuwakinga na shule zao kutokuwa na miundombinu ya kuwawezesha kujiweka vizuri katika kubaliana na hali hiyo.
Kupitia mradi huu wasichana wanapatiwa elimu ya afya ya uzazi na kuwapatia taulo za kujihifadhi wanapokuwa kwenye vipindi vya hedhi na hadi sasa zaidi ya wasichana 5,000 wamenufaika na mradi huu.
Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation pia imekuwa ikishirikiana na serikali kupitia Wizara ya Afya katika miradi ya kufikisha jumbe za kuelimisha masuala ya afya bure kwa wananchi kupitia mtandao wa Vodacom na zaidi ya wananchi milioni 1 wanaendelea kunufaika na huduma hii.
Kwa kutumia bilioni 15 ndani ya kipindi cha miaka 10,taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation imeboresha maisha ya watanzania wengi na inaendelea kutimiza dhamira yake ya kuunga mkono jitihada za serikali za kupambana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii na kubadilisha maisha ya watanzania kutoka hali duni kuwa bora.

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII AKUTANA NA VIONGOZI WA HIFADHI YA KISIWA CHA RUBONDO

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog,Kanda ya Kaskazini.
↧
NAIBU WAZIRI WA AFYA AKUTANA NA UJUMBE WA VIONGOZI WA MFUKO WA ABBOTT
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akizungumza na viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka nchini Marekani na wale wa Tanzania waliomtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam kuzungumza naye kuhusu masuala mbalimbali ya uboreshaji wa huduma za Afya na Elimu kupitia program mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo nchini. Kutoka Kulia ni Makamu Mtendaji wa Rais wa Mfuko wa Abbott, Stephen Fussell na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund Bi.Elaine Leavenworth (katikati).Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kulia) akimweleza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) juu ya namna Mfuko wa Abbott ulivyojipanga kuendelea kutekeleza Program mbalimbali nchini Tanzania zikiwemo za Matumizi ya Teknolojia ya kisasa katika utoaji wa Tiba, maabara za kisasa, dawa na vifaa vya mafunzo kwa wanafunzi wa masomo ya Sayansi.Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akifurahia jambo na Makamu wa Rais Mwandamizi wa Mfuko wa Abbott (Abbott Fund) Bi.Elaine Leavenworth (kushoto) mara baada ya ujumbe wa viongozi wa mfuko huo kutoka nchini Marekani kumtembelea Ofisini kwake jijini Dar es salaam.Ujumbe wa viongozi wa mfuko wa Abbott (Abbott Fund) kutoka Marekani ukimsikiliza Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla mara baada ya kumtembelea Ofisini kwake leo jijini Dar es salaam.Makamu wa Rais wa Mfuko wa Abbott (Abbot Fund) nchini Tanzania Andy Wilson akielezea utayari wa Mfuko huo katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazoikabili sekta ya Afya na Elimu nchini kupitia ufadhili wa Programu mbalimbali zinazofanywa na Mfuko huo kwa niaba ya Watu wa Marekani. Picha/ Aron Msigwa –MAELEZO.
↧
ELIUD NYAUHENGA ATEULIWA KUWA KAIMU MENEJA MFUKO WA BARABARA
↧
WIMBO MPYA WA INJILI KUTOKA KWA MWIMBAJI ELISHA WAUPENDO
Bonyeza HAPA Kusikiliza na Kupakua Wimbo Mpya wa Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tanzania, Elisha Waupendo. Wimbo Unaitwa Umenipa Kibali. Pia waweza kuusikiliza ama kuupakua moja kwa moja hapa chini. Tafadhali sikiliza kwa umakini wimbo huo na utakuwa wa tofauti moyoni mwako.
Na BMG
↧
↧
RATIBA YA USAILI MAISHA PLUS EAST AFRICA 2016
Baada ya Usaili kufanyika kwa kishindo katika mikoa ya Mtwara na Dar es salaam usaili wa Maisha Plus unaendelea katika mikoa mingine ndani ya Tanzania.
30/07/2016 - MBEYA - Ukumbi wa City Pub
31/07/2016 - IRINGA - Savanna Garden
02/08/2016 - DODOMA - Matei Lounge
04/08/2016 - MWANZA - Rock Garden
06/08/2016 - ARUSHA - Via Via
13/08/2016 - ZANZIBAR - Ngome Kongwe
Vijana wote wenye umri wa miaka 18 - 26 wanakaribishwa kujitokeza kwa wingi. Elimu na ujuzi ni kiwango chochote. Zawadi kwa mshindi ni Tzshs. Milioni 30. Fomu zinapatikana BURE kabisa kupitia www.maishaplus.tv na katika maeneo tajwa hapo juu.
Maisha Plus East Africa 2016 | #VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu
Bofya hapa chini kuona video 33 fupi za usaili wa Maisha Plus Dar es salaam.
↧
MAALIM SEIF KUONGEA NA WATANZANIA BOSTON
↧
MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI SHAURI LA KUPINGA MATOKEO YA UCHAGUZI JIMBO LA PANGANI
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso katika akipongezwa na wananchi wa Jimbo la Pangani mara baada ya kutangazwa na Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kuwa mshindi halali katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka jana mara baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina Mwidau
Mbunge Aweso Jumaa akiwa amebebwa juu juu na wananchi wa Jimbo la Pangani mara baada ya kesi iliyofunguliwa dhidi ya mpinzania wake wa CUF Amina Mwidau ya kupinga matokeo ya uchaguzi kutupiliwa mbali na mahakama kuu kanda ya Tanga
Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM)Jumaa Aweso wa pili kutoka kulia akiwa na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Stephen Ngonyani "Proffesa Maji Marefu " wakiwa ndani ya Mahakama Kuu Kanda ya Tanga wakisuburia kuanzwa kwa kesi hiyo hata hivyo hukumu hiyo ilimpa ushindi halali Mbunge Aweso katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Octoba mwaka jana mara baada ya kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo katika kesi ya kupinga matokeo iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CUF Amina Mwidau
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tanga jana imetupilia mbali shauri la kupinga matokeo ya Ubunge Jimbo la Pangani lililofunguliwa na aliyekuwa mgombea kupitia tiketi ya CUF Amina Mwindau dhidi ya Mbunge wa Jimbo hilo Jumaa Hamidu Aweso CCM na kuonekana hakuna vigezo vya kutengua matokeo hayo.
Akizungumza wakati akitoa huduma ya Shauri hilo,Jaji Patricia Fikirini alisema mlalamikaji Amina Mwindau CUF ameonekana kushindwa katika shauri hilo dhidi ya mlalamikiwa Jumaa Aweso katika upingaji wa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika oct 25 mwaka jana.
Alisema miongoni mwa malalamiko yalioambatanishwa kutoka kwa mlalamikaji katika zoezi zima la kupinga matokeo hayo ni pamoja na kuwa mlalamikiwa ambae ni Jumaa Aweso katika kampeni zake alikiuka taratibu za uchaguzi,ubaguzi wa mgombea wa jinsia ya kike na kutumia lugha ya siziokuwa za kiungwana jambo ambalo mlalamikaji alidai lilimgharimu kupata matokeo mazuri katika uchaguzi huo.
Alisema sambamba na vielelezo vilivyoletwa mahakamani hapo pamoja na ushahidi uliotolewa kwa upande wa mlalamikaji havikuwa na ushawishi wa kuweza kutengua matokeo ya uchaguzi huo.
Jaji Fikirini alisema amezingatia hoja zote kutoka pande mbili na kujiridhisha Jumaa Aweso ambae ni mbunge hivi sasa kuwa ni mbunge aliyepita kihalali na hakukuwa na vigezo vya upingwaji wa matokeo aliyopata katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.
Alisema haki zote za kisheria zipo wazi kwa pande zote mbili mlalamikiwa na mlalamikaji ikiwa pamoja na kukata rufaa kwa maamuzi yaliyochukuliwa na Mahakam hiyo ikiwa kama kuna upande hauta ridhika na hukumu iliyotolewa.
Kwa upande wake Wakili wa kujitegemea na mahakama kuu Warehema Kibaha alisema Jaji Patisia Fikirini amefanya maamuzi sahihi ya kutenda haki kwa mteja wake katika shauri hilo lililo dumu kwa takriban miezi 7.
Wakili Kibaha alisema katika shauri hilo walijiandaa kwa ushahidi na mashahidi wazuri ili kuweza kukabiliana na kesi hiyo jambo ambaloliliwawezesha kupata ushindi wa kihalali na kuweza kumpa nafasi mteja wake kuendelea na majukumu yake ya Kibunge.
Nae Wakili Mashaka Ngole aliyemsimamia Mlalamikaji Amina Mwindau alisema hana pingamizi lolote na atamsikiliza mteja wake ikiwa ataamua kukata rufaa wataangalia vigezo muhimu vitakavyo wasaidia katika awamu ya pili pindi watakapo kata rufaa hiyo Mbunge wa Jimbo la Pangani Jumaa Aweso ambaye alikuwa anakabiliwa katika shauri hilo alisema kipindi chote alichokuwa anakabiliana na kesi hiyo kulimpotezea umakinifu wa kufanya majukumu yake ya kibunge na kuweza kuangalia shida za wananchi wa Pangani kwa umakini zaidi.
Aweso alisema kesi imekwisha na sasa kilichombele yake ni kupambana na kero za wananchi wa Wilaya hiyo ili kuweza kuwaletea maendelo kama alivyowaahidi kipindi cha kampeni.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
↧