Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

WASHINDI WA MBIO ZA BAISKELI ZA KANDA YA ZIWA ,WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

$
0
0
  Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi pamoja na waendesha Baiskeli.
  Mgeni rasmi katika Mashindano hayo,Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akiwa meza kuu kwa ajili ya zoezi la utoaji wa zawadi kwa washindi wa mashindano hayo.kulia kwake ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi ,Asa Mwaipopo. 
Mshindi wa kwanza katika Mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Kanda ya ziwa yajulikanayo kama Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 ,Seni Konda akifurahia zawadi ya kikombe mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura.
Mshindi wa pili katika Mashindano ya Mbio za Baiskeli ya Kanda ya ziwa yajulikanayo kama Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle Challange 2016 ,Makoja Hamis akionesha zawadi ya kikombe mara baada ya kukabidhiwa na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo,Anastazia Wambura.


Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akikabidhi kikombe kwa mshindi wa tatu wa Mashindano hayo ya baiskeli, Hamis Clement.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akimvisha medali mshindi wa kwanza kwa upande wanawake wa mbio za baiskeli za Acacia tufanikiwe pamoja cycle Challange 2016,Martha  Anthony. 

 Mshindi wa kwanza kwa upande wanawake wa mbio za baiskeli za Acacia tufanikiwe pamoja cycle Challange 2016,Martha  Anthony akiwa amenyanyua juu kikombe mara baada ya kukabidhiwa na mgeni rasmi.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akikabidhi kitita cha fedha kwa mshindi wa pili wa mashindano ya baiskeli ,Salma William .
  Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Anastazia Wambura akikabidhi zawadi ya kikombe na fedha kwa mshindi wa tatu wa mbio za baiskeli,Elizabeth Clement.
Washindi wa Mbio za Baiskeli kwa upande wa wanawake na wanaume katika mashindano ya Acacia tufanikiwe pamoja Cycle Challange 2016 wakifurahi mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao.
Washindi kwa upande wa wanawake wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Washindi kwa upande wa wananume wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi.
Bingwa mara mbili wa mashindano ya Mbio hizo, Masunga Duba akipeana mkono na mgeni rasmi mara baada ya kuhitimisha mbio hizo akishika nafasi ya nne.
Mkuu wa kitengo cha biashara katika Mgodi wa Buzwagi,Jackson Kanumba akikabidhi zawadi kwa mshiriki wa mbio hizo Ashiraf.
Mshiriki Ashraf ambaye amekua akishiriki mashindano mbalimbali ya baiskeli ,akipongezwa na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi,Asa Mwaipopo.
Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa umma wa kampuni ya Madini ya Acacia,Necta Foya akikabidhi zawadi kwa mmoja wa washindi waliofanikiwa kuwa kati ya washiriki 30 bora.
Meneja wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa umma wa kampuni ya Madini ya Acacia,Necta Foya (katikati) pamoja na Afisa Mawasiliano wa Mgodi wa Buzwagi,Magesa Magesa wakitoa maelekzo kwa mshereheshaji wa shughuli hiyo,Mc Kalinga.
Wasanii wa kikundi cha Ngoma wakitumbuiza katika hafla ya utoaji wa zawadi kwa washindi wa mbio za baiskeli.
Msanii Marry Banyukwa akitumbuiza katika hafla hiyo.
Viongozi wa mgodi wa Buzwagi wakisakata Rhumba pamoja na Washiriki wa mbio za baiskeli .

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog. 
FAINALI ya mashindano ya mbio za baiskeli zijulikanazo kama “Acacia Tufanikiwe Pamoja Cycle challange 2016 zinazoandaliwa na chama cha mchezo wa mbio za baiskeli (CHABATA) na kudhaminiwa na kampuni ya kuchimba Madini ya Acacia zimemalizika mjini Kahama huku mwendesha baiskeli Seni Konda akiweka rekodi ya kushinda mbio hizo kwa kutumia saa 4:15:07 .

Konda mkazi wa mkoa wa Shinyanga amefanikiwa kushika nafasi hiyo baada ya kuwashinda wapinzani wake Makoja Hamis aliyemaliza nafasi ya pili na Hamis Clement aliyemaliza nafasi ya tatu huku wakifuatiwa na waendesha baiskeli zaidi ya 150 walioshiriki mbio hizo kutoka mikoa sita ya kanda ya ziwa.

Kwa upande wa wanawake ,mwendesha baiskeli,Martha Anthony kutoka mkoani Mwanza amefanikiwa kutetea ubingwa wake akimaliza wa kwanza huku akiwashinda washindani wake,Salma William aliyeshika nafasi ya pili na Elizabeth Clement aliyeshika nafasi ya tatu.
Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume ,Seni Konda amejinyakulia kitita cha sh Mil 1.5 ,mshindi wa pili Makoja Hamis akijinyakulia kiasi cha sh Mil moja huku mshindi wa tatu ,Hamis Clement akiambulia kiasi cha sh 700,000.

Upande wan wanawake mshindi wa kwanza Martha Anhtony amejinyakulia kiasi cha sh Mil 1.2,mshindi wa pili Salma William akipata sh 800,000 huku mshindi wa tatu ,Elizabeth Clement akipata sh 600,000.

Akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi wa mbio hizo mgeni rasmi naibu waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na michezo Anastazia Wambura amesema michezo ni ajira na afya ambapo pia amewataka wachezaji kutotumia madawa ya kusisimua misuri kwa kuwa kitendo hicho ni kinyume cha taratibu za michezo na atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Baiskeli cha Tanzania (CHABATA) Jacx Mhagama alisema  CHABATA na kampuni ya madini ya ACACIA wamesaini mkataba wa udhamini wa mashindano hayo  kwa muda wa miaka mitatu kuanzia 2014 mpaka 2016.

“Kipindi hiki cha miaka mitatu kimekuwa na mengi kiutendaji na kimahusiano kwetu sote CHABATA na ACACIA. lakini kwetu imekuwa ni kipindi chenye chenye changamoto zenye kutukomaza na kutujenga.  Hivyo tumevuna tuliyoyategemea na ziada pia.”alisema Mhagama.

 “ACACIA ni kampuni yenye machimbo ya madini kwenye eneo hili la kanda ya Ziwa, lakini wameonyesha upendo na uzalendo mkubwa hata kwa Taifa. Pamoja na kujishughulisha na michezo kwenye eneo hili la kanda ya ziwa, wameenda juu Zaidi kufikia taifa kwa kuifadhili timu yetu ya Taifa ya Baiskeli kwenye mashindano ya Ubingwa wa Afrika mwaka jana 2015, yaliyofanyika huko Petermarizburg nchini Afrika ya Kusinu.”aliongeza Mhagama.

Mwisho.

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA SAMAKI WATAKA KUHAMIA SOKO LA MICHUNGWANI TANGA

$
0
0

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akizungumza na wafanyabiashara wa samaki katika soko la kuuzia samaki wabichi na wakavu ambalo limevunjwa na kutakiwa kuhamia kwenye soko la michungwani ambalo limejengwa kwa ubora kwa ajili ya kufanya shughuli zao

Mfanyabiashara wa soko la samaki la kulia akimuonyesha mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat, Mhandisi Mwanasha Tumbo kitu wakati alipotembelea soko la kuuzia samaki wabichi na wakavu ambapo aliwataka wafanyabiashara hao kuondoka eneo hilo kuhamia eneo la michungwani.

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akisisitiza jambo kwa wafanyabiashara wa soko la samaki wabichi na wakavu kuhusu kuondoka eneo hilo na kuhamia soko la michungwani ambalo limejengwa kwa ubora mzuri kwa ajili ya kufanyia biashara zao

Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo kulia akimsikiliza mmoja wa wafanyabiashara ya samaki katika soko la kuuzia samaki wilayani humo ambao waliamuriwa kuhamia kwenye soko la Michungwani ambalo limejengwa kwa ubora kwa ajili ya shughuli zao.


Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

DK. KIGWANGALLA ASIMIKWA UCHIFU WA WANYAMWEZI WA TANZANIA, AAHIDI MAKUBWA

$
0
0

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amepewa heshima ya Uchifu wa Watanzania wa Kabila la Wanyamwezi na Wazee wa Kijiji cha Isalalo katika Kata ya Utwigu iliyopo katika Jimbo hilo la Nzega Vijijini Mkoani Tabora.

Dk. Kigwangalla ambaye yupo ziarani katika maeneo mbalimbali ya Jimbo hilo kwa lengo la kushukuru Wananchi hao kwa kumpigia kura nyingi za zilizomwezesha kuingia Bungeni, ambapo katika tukio hilo lililoshuhudiwa na umati mkubwa wa wanakijiji wa Kijiji hicho, 


Wazee hao wa Mila walieleza kuwa, hatua hiyo ya kusimikwa Uchifu wa heshima wa kabila la Wanyamwezi ni ishara kubwa kuwa Kijana mashuhuri na kijana mpiganaji sawasawa hivyo kwa ushindi wake kuchaguliwa nahata kupewa Uwaziri (Naibu Waziri), ni ishara kubwa ya kufikia malengo yake aliyokusudia katika Taifa hili.

Wazee hao wa Mila waliweza kumkabidhi mishale, Mkuki, upinde na kumtakia kila lakheri katika safari yake hiyo ya kiutawala.

Akitoa shukrani zake katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla amesema kuwa, Wananchi wake wategemee neema kubwa kwani kwa sasa yupo katika hatua ya utendaji kazi Zaidi na kuwataka wawe na Imani naye pamoja Serikali iliyopo madarakani kwani imejipanga kuleta maendeleo makubwa.

“Nawashukuru nyie kwa kuniwezesha kunipigia kura nyingi sana ambazo zimeniwezesha mimi kupata nafasi ya kuingia Buangeni. Nawaahidi kuwatumikia kwa nguvu zangu zote. Nguvu nilizozianza tokea awali na kwa sasa zitakuwa kubwa Zaidi, muendelee kuniombea.

Nafahamu kuna kero nyingi sana, shida za barabara za kuingia na kutoka huku Vijijini, Suala la Umeme na mengine mengi haya yote yanafanyiwa kazi na taratibu zote zinaenda vizuri.” Alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho cha Isalalo.

Ziara hiyo iliyoanza tokea Julai 13 mwaka huu, Mbunge huyo ambaye Jimbo lake hilo lenye jumla ya Kata 19, zikiwemo Kata ya Puge, Ndala, Nata,, Sanzu, Lusu, Milambo Itobo, Magengati, Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi, Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe.

Ambapo katika Vijiji vya Kata hizo amewafikia wananchi na kuwashukuru kwa hatua yao ya kumchagua ambapo pia ameweza kutekeleza ahadi aliyoitoa yeye mwenyewe ikiwemo vifaa vya michezo kwa timu za vijana, pamoja na kutimiza ahadi za michango mbalimbali ikiwemo ya kuchangia ujenzi wa shule, makanisa, misikiti, Zahanati na mambo mbalimbali huku pia akipokea maoni na uashahuri kutoka kwa wapiga kura wake hao.
DSC_2015DSC_2023DSC_2030Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Wanakijiji cha Isalalo
DSC_2032
Wazee wa Mila
DSC_2037
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni
DSC_2038
Wazee wa Mila wakiwa upande wa wageni maalum
DSC_2043
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akivishwa shuka katika hatua ya kusimikwa uchifu huo
DSC_2044DSC_2047
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akikabidhiwa mkoba wa mishale
DSC_2050DSC_2051DSC_2054DSC_2059
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipewa baraka na wazee hao
DSC_2083DSC_2062DSC_2066DSC_2073DSC_2073DSC_2083DSC_2084DSC_2088
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akirejea kukaa baada ya kukabidhiwa Uchifu wa Wanyamwezi
DSC_2089
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akinyanyua juu mkuki ishara ya Kijana shujaa wa Wanyamwezi..
DSC_2095
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akisalimiana na Diwani wa Kata Utwigu
DSC_2104DSC_2123
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa shukrani zake kwa wananchi
DSC_2174
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha ya pamoja na viongozi wa Kijiji
DSC_2186
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea salamu kutoka kwa watoto
DSC_2201DSC_2212DSC_2217
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipata picha ya pamoja na wazee wa mila pamoja na wanakijiji
DSC_2219
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiwaaga wazee wa mila
DSC_2224
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akipiga picha pamoja na vijana wa kijiji hicho. (Picha zote na Andrew Chale,Nzega-Tabora).

WANAHABARI WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA GOMBE

$
0
0

Baadhi ya wanahabari wakiwa katika Boti wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe,hifadhi maarufu kwa kuwa na mnyama aina ya Sokwe mtu.

Watalii wakielekea Hifadhi ya Taifa ya Gombe .
Eneo mojawapo linalotumiwa na wavuvi katika mwambao mwa ziwa Tanganyika jirani na Hifadhi ya taifa ya Gombe.
Baadhi ya wanahabari muda mfupi baada ya kufika hifadhi ya taifa ya Gombe.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) ,Pascal Shelutete akiwatamburisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini  walipotembelea hifadhi ya taifa ya Gombe.
Kaimu Mhifadhi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe,Goodluck Tarimo akizungumza na wanahabari waliotembelea hifadhi hiyo.
Baadhi ya Wahifadhi waongoza wataalii katika Hifadhi ya taifa ya Gombe.
Daktari wa Mifugo katika Hifdhi ya Taifa ya Gombe,Dkt Jane Raphael akizngumza mbele ya wanahabari (hawapo pichani) kabla ya kuaza safari ya kutembelea hifadhi hiyo.
Mhifadhi Hussein 
Mhifadhi Isaya Mkude akitoa maelezo kwa wanahabari wakati wa kuanza safari ya kwenda kuwatizama Sokwe.
Safari ya kwenda kuwatizama Sokwe ikaanza.
Maeneo mengine Mhifadhi Isaya Mkude aalikua akitoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali na majibu ya maswali yaliyoulizwa na wanahabari.
Nyani ni miongoni mwa wanyama wanaoonekana kwa urahisi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe.
Safari ya kuwatafuta Sokwe ili kua ni ya vipando pia.
Wakati mwingine wanahabari walilazimika kupumzika kwa ajili ya kupata pumzi mpya ya kuendelea na safari 
 Baadhi ya Sokwe mtu walioonekana kwa mbaali sana wakiwa katika miti.
Hatimaye safari ya kurudi katika makazi ikaanza kwa kupita katika fukwe ya ziwa Tanganyika inayopakana na hifadhi ya taifa ya Gombe. 

Na Dixon Busagaga wa Michzui Blog.

MADIWANI WA KYERWA NA BIHARAMULO MKOANI KAGERA WAPEWA SOMO LA USIMAMIZI NA UDHIBITI WA FEDHA ZA SERIKALI ZA MITAA

$
0
0
Mwezeshaji kutoka Mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3), Magdalena Katunzi akiwasilisha mada ya uzimamizina Udhibiti wa fedha katika Mamlaka za serikali za mitaa. Mada hiyo ilitolewa kwa madiwani wa Halmashauri za Wilaya za Kyerwa na Biharamuo Mkoani Kagera leo.
Lengo kuu la mada hiyo kwa Madiwani ahao ambao halmashauri zao zimechaguiwa kuanza utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za umma ni pamoja na kumuwezesha Diwani kupata taarifa na uweewa juu ya taratibu za usimamizi na udhibitiwa fedha katika Mamlaka za Serikali za mitaa.

Aidha Katunzi alianisha mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyanzo vya mapato vya Mamlaka za serikali za Mitaa, ikiwa ni mapato ya ndani, ruzuku kutoka serikali kuu na Mikopo.

Madiwani walifundishwa mbinu za kuongeza mapato ya Hamashauri ambapo walifundishwa namna ya kubuni na kuanzisha vyanzo vipya vya mapato, kuboresha viwango vya tozo, kuboresha mbinu za ukusanyaji mapato, kusimamia matumizi ya fedha za serikali ya mitaa na udhibiti wa fedha za Halmashauri. Source:Father Kidevu Blog,Kagera
Madiwani kutoka Hamashauri za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo wakifuatilia mada hiyo ya Usimamizi na Udhibiti wa fedha za Mamlaka ya Serikali za mitaa.
Wakuu wa Wiaya za Kyerwa na Biharamulo mkoani Kagera, Kanali Mstaafu, Shaabn Lissu (kushoto) wa Kyerwa na Saada Malunde wa Biharamulo wakiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Wende Ng'ahala (kulia) wakifuatilia mada hiyo.
Madiwani kutoka Hamashauri za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo wakifuatilia mada hiyo ya Usimamizi na Udhibiti wa fedha za Mamlaka ya Serikali za mitaa.

Ofisa Mipango wa Wilaya ya Biharamulo, Andambike Kyomo akifafanua jambo kuhusu namna ya ugawaji wa fedha za Halmashauri kwa makundi ya Vijana, Wanawake na matumizi mengine.
Mratibu wa Mradi wa PS3 kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bertha Swai akifafanua jambo kuhusu mada hiyo na maswali yaliyoulizwa na washiriki.
Madiwani kutoka Hamashauri za Wilaya ya Kyerwa na Biharamulo wakifuatilia mada hiyo ya Usimamizi na Udhibiti wa fedha za Mamlaka ya Serikali za mitaa.
Ili kuondoa uchovu kwa washiriki kunakosababisha kusinzia wakati wa mafunzo, washiriki walifanya mazoezi kuchangamsha mwili na kuimarisha usikuvu.
Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde (kulia) akifurahia kuonana na Mkurugenzi Mpya wa Hlamashauri ya Wilaya ya Biharamulo, Wende Israel Ng'ahala. Watendaji hao ndio walioonana kwa mara ya kwanza na wote ni wapya katika Wilaya hiyo.

SBL YAZINDUA BOMBA LA 470M/- KUDHIBITI MAJITAKA

$
0
0

Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina (katikati) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie wakiongozana kuelekea kwenye bomba la kudhibiti wa majitaka ambalo linalenga kuhakikisha kiwango cha juu kiafya kwa kampuni, mazingira na wakazi wa maeneo yaliyo karibu.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa kampuni ya bia ya Serengeti, John Wanyancha akifafanua jambo kwa wageni waalikwa katika hafla ya uzinduzi wa bomba la majitaka ambalo lilizinduliwa na Mhe. Luhaga Mpina Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira mapema leo katika kiwandani hapo mapema leo.

Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina , Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie na waandishi wa habari wakifuatilia kwa makini jinsi mtambo wa kusafirisha majitaka unavyofanya kazi kutoka kwa mmoja wa wasimamizi wa mradi huo.

Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina (katikati) akifurahi jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie mara baada ya kukata utepe katika mtambo kusafirisha majitaka katika hafla iliyofanyika mapema leo kiwandani hapo,

Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina akiwasha mtambo wa kusafirisha majitaka kiwandani hapo mara baada ya kuzindua rasmi katika hafla iliyofanyika katika kiwanda hicho Temeke Jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa bomba la kudhibiti majitaka katika kiwanda cha bia cha serengeti wakifuatilia kwa makini

Naibu Waziri ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Mheshimiwa Luhaga Mpina akiongea na wafanyakazi wa kiwanda cha bia ya serengeti mara baada ya uzinduzi wa bomba la kudhibiti majitaka katika kiwanda hicho Jijini Dar es salaam.




Dar es Salaam, Julai 19, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti leo imezindua bomba la kudhibiti wa majitaka ambalo linalenga kuhakikisha kiwango cha juu kiafya kwa kampuni, mazingira na wakazi wa maeneo yaliyo karibu.

Bomba hilo limejengwa chini ya usimamizi wa Kampuni ya Maji Safi na Taka ya Dar es Salaam (Dawasco), Mamlaka ya Barabara (Tanroads) na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke likihusisha takribani kilometa mbili kuanzia katika kiwanda cha bia cha Serengeti kilichpo Temeke hadi Kurasini ambako ndip ulipo mfumo wa majitaka wa Dawasco.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, huo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Helene Weesie, alisema kwamba mradi huo wa aina yake na wa kwanza nchini unadhihirisha juhudi zisizo na ukomo za kampuni hiyo katika kuhifadhi mazingira.

“Ubora wa maji ni jambo lililo mstari wa mbele katika utengenezaji wa bia lakini suala la usafi kutokana na kuzalishwa kwa majitaka ni sehemu kubwa inayotujengea hisia za kimazingira katika shughuli za kutengeneza bia. Kwa hiyo uzinduzi wa bomba hili ni moja ya hatua ya kusonga mbele katika kuhakikisha yanakuwepo mazingira safi kiafya,” alisema Weesie.

Mkurugenzi Mtendaji huyo alibainisha kwamba majitaka yanayotolewa na bomba hilo yatakuwa yanafanyiwa tiba kwanza ili kuondoa aina yoyote ya sumu kabla ya kuachiwa ili kuingia katika mfumo wa majitaka wa Dawasco.

Alisema kuwa uzinduzi huyo uko katika mkondo mmoja na sera ya Kampuni ya Serengeti ya kujikita katika ustawi wa jamii ambayo imeainishwa katika maeneo manne ya vipaumbele ambavyo vinajumuisha, Utoaji wa Stadi za Maisha, Uendelevu wa Mazingira na Kuboresha Unywaji wa Kistaarabu.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Masuala ya Muungano na Mazingira, Mh. Luhanga Mpina aliipongeza Serengeti kwa kuzindua bomba hilo akibainisha kwamba ujenzi unaendana na ajenda ya serikali ya uhifadhi wa mazingira.

Mpina alibainisha kwamba uchafuzi wa mazingira katika miji na maeneo ya pembezoni unaathiri afya za watu wengi na kupunguza tija inayotokana na mazingira na kutoa wito kwa makampuni mengine kuiga kazi nzuri ya Kampuni ya Bia ya Serengeti katika kuhifadhi mazingira.

RAIS MSTAAFU MWAI KIBAKI ATEMBELEA DARAJA LA MWALIMU NYERERE

$
0
0
Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Maonesho ya Wiki ya Maji Afrika (Sylivester Matemu) wakati wa maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika yanayoendelea jijini Dar es salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo.


Na Mwandishi Wetu

Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki ametembelea mabanda ya maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika yanayoendelea jijini Dar es salaam.

Katika tukio hilo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo amimweleza Mwakilishi huyo kuwa Tanzania imejipanga kuhakikisha kuwa hadi ifikapo 2020 iweze kufikisha maji kwa wananchi wote kwa maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Mhandisi Kalobelo aliongeza kuwa hatua hiyo itaifanya Tanzania kufikisha maji kwa wakazi wa mijini kwa asilimia 95 na kwa wakazi wa vijijini kw asilimia 85.

Aidha, katika hatua nyingine, Mwakilishi huyo alitembelea barabara iliyopewa jina la Mwai Kibaki inayoanzia eneo la Morocco hadi njia panda ya Kawe jijini Dar es salaam pia alitembelea na daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam.
Maonesho ya sita katika ya wiki ya maji Afrika mwaka huu yanayoendelea jijini Dar es salaam yanaongozwa na kaulimbiu inayosema “Kufikia lengo la Mendeleo Endelevu (SDGs) juu ya Usalama wa Maji na Usafi wa Mazingira”.          
Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki akisalimia na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo leo jiji Da es salaam.
Katibu wa Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (katikati), Profesa Nick Wanjohi akifafanua jambo kwa mwakilishi huyo alipotembelea na daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam.

Mwakilishi Maalumu wa masuala ya maji kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa Kenya Mwai Kibaki (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi walioandamana kutembelea daraja la Mwalimu Nyerere linalounganisha eneo la Kigamboni kupitia bahari ya Hindi na eneo la katikati ya jiji la Dar es salaam.

(Picha na Eleuteri Mangi-MAELEZO)

RATIBA YA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA 2016/2017

$
0
0
Ratiba rasmi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/2017, imetoka. Ratiba hiyo imezingatia michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa ngazi ya klabu na timu za taifa ili kukwepa dhana yoyote ya upangaji wa matokeo na kurundikana kwa michezo. Hii ni ratiba rasmi ukiachana na ile ambayo ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii.

Ile ya mitandao ya kijamii imekosewa anwani ya Posta ya TFF kadhalika kuonesha kuwa mchezo kati ya Azam FC na African Lyon ungefanyika Agosti 21, 2016 ilihali hii rasmi ina anwani sahihi na mchezo huo wa raundi ya kwanza ukionesha utachezwa Agosti 20, 2016. Tunaomba familia ya soka kuegemea kwenye hii ya sasa rasmi inayotolewa na TFF.












IBADA NA MAZISHI YA MWANAHABARI CHARLES SOKORO YAFANYIKA JIJINI MWANZA.

$
0
0
Ibada ya Mazishi ya aliekuwa Mkuu wa Vipindi na Afisa Mahusiano katika kituo cha runinga cha Barmedas Tv cha Jijini Mwanza, Mwalimu Charles Sokoro, imefanyika jana katika Kanisa la AICT Makongoro na kufuatiwa na mazishi yaliyofanyika katika Makaburi ya Kitangiri.

Mwalimu Sokoro ambae pia alikuwa mwalimu wa muziki wa Injili na Mwenyekiti wa Kwaya ya AICT Makongoro, alifariki jumamosi Julai 16,2016 majira ya saa mbili usiku katika Hospitali ya Rufaa Bugando baada ya kuugua kwa miezi kadhaa.

Alizaliwa mwaka julai mosi mwaka 1965 katika Kijiji cha Kahunda Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza na hadi mauti yanamkuta alikuwa na umri wa 51 ambapo ameacha watoto wanne, alikuwa mgane.

Na BMG
Kwaya ya AICT Makongoro ikiimba katika ibada ya mazishi ya Sokoro
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la AICT Makongoro akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya mazishi ya marehemu Sokoro.
Baba Askofu Mkuu Mstaafu wa Kanisa la AICT Makongoro, akitoa salamu za rambirambi katika ibada ya mazishi ya marehemu Sokoro.
Mmoja wawanafamilia wa marehemu Sokoro akisoma wasifu wa marehemu Sokoro.
Mchungaji Mika Ngusa kutoka TCRA akihubiri katika ibada ya mazishi ya marehemu Sokoro.
Jackson Manji Songo akiongoza ibada ya mazishi ya marehemu Sokoro
Mkurugenzi wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania, Abubakar Karsan, akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Wanahabari
Maganga James Gwensaga ambae ni Meneja wa HHC ALive Radio ya Jijini Mwanza, akitoa salamu za rambirambi kutoka kwa wanahabari wa kundi la mtandao wa Whatsupp la BMG Tanzania, ambalo pia marehemu Mwl.Sokoro alikuwa mwanachama.
Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi akitoa salamu za rambirambi
Mkurugenzi wa Barmedas Tv, alikokuwa akifanya kazi Mwl.Sokoro
Viongozi mbalimbali wa dini mkoani Mwanza, pamoja na waombolezaji wakiwa katika ibada ya marehemu Sokoro.
Viongozi mbalimbali wa dini mkoani Mwanza, pamoja na waombolezaji wakiwa katika ibada ya marehemu Sokoro.
Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mwanza, na mwanachama wa BMG Tanzania, Edwin Soko, pamoja na waombolezaji wakitoa wakiuaga mwili wa marehemu Sokoro
Mhariri wa Lake Fm Radio ya Jijini Mwanza, na mwanachama wa BMG Tanzania, Amos Gomba, pamoja na waombolezaji wengine wakiuaga mwili wa marehemu Sokoro
Haleluya Benjamin kutoka Mtandao wa Wanahabari Watoto mkoani Mwanza pamoja na waombolezaji wengine wakiuaga mwili wa marehemu Sokoro
Meneja wa Metro Fm ya Jijini Mwanza, na mwanachama wa BMG Tanzania, Alphonce Tonny Kapela, pamoja na waombolezaji wengine wakitoa wakiuaga mwili wa marehemu Sokoro
Baadhi ya wafanyakazi wa Barmedas Tv pamoja na waombolezaji wengine wakiwa katika mazishi ya mwalimu Sokoro
Mmoja wa watoto wa marehemu Sokoro (mwenye shati jeupe) akiwa na waombolezaji wengine katika mazishi ya Mwalimu Sokoro
Ibada ya Mazishi katika makaburi ya Kitangiri
Shangazi wa marehemu akimwaga udongo ishara ya kuuaga mwili wa marehemu Sokoro
Viongozi wa Barmedas Tv wakimwaga udongo ishara ya kuuaga mwili wa marehemu Sokoro
Mkurugenzi wa Barmedas Tv akimwaga udongo ishara ya kuuaga mwili wa marehemu Sokoro
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa kundi la Whatsupp la BMG Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Barmedas Tv
Baadhi ya Waandishi wa Habari wa kundi la Whatsupp la BMG Tanzania, wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Barmedas Tv

MSUBI BINAGI KUIBUKA NA KIPINDI KIPYA CHA RUNINGA

$
0
0
Inyake hii kutoka kwa coming up Star Actor/ Video King na Presenter Msubi Binagi. Usikose kumfuatilia kupitia akaunti yake ya Instagram @msubi_binagi ili upate updates kuhusu kipindi chake kipya cha Tv cha "Jua la Utosi" kitakachoanza kuonekana online na baadae katika runinga ambayo utatangaziwa. Pia utafahamu kuhusu filamu yake mpya itakayotoka hivi karibuni akiwa na timu yake.

NAVY KENZO KUMSINDIKIZA MISS TANGA 2016

$
0
0

                      

NA, MWANDISHI WETU TANGA
MSANII wa Mziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania Navy Kenzo anatarajiwa kutumbuiza kwenye shindano la kumtafuta malkia wa Mkoa wa Tanga Miss Tanga 2016 litakalofanyika Julai 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort.

Licha ya Navy Kenzo wasanii wengine ambao watasindikiza onyesho hilo kwa kutoa burudani ni kundi la mziki wa kizazi kipya mkoani Tanga,Wazenji Classic pamoja na Dances. Akizungumza jana,Mratibu wa Onyesho hilo, alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri ambapo tayari warembo watakaoshiriki wameanza kuingia kambini .


Shindano hilo ambalo limeandaliwa na kituo cha Radio cha TK FM 88.5 kilichopo mjini Tanga kwa kushirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort wameelezea namna walivyo jipanga kuhakikisha onyesho hilo linakuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya warembo waliopo .

“Nisema tu tumejiandaa vizuri kuhakikisha shindano hilo linafanyika kwa umakini mkubwa ili kuwawezesha wadau wa tasnia ya urembo mkoani hapa kuweza kupata ladha halisi ya onyesho hilo kwani licha ya kuwaona warembo wakali wakini pia mzee wa kamatia chini atakuwepo kuwapagawisha “Alisema.

Hata hivyo alisema kuwa mazoezi ya warembo watanaoshiriki onyesho hilo yanaendelea kwenye ukumbi wa New Hotel uliopo mjini hapa kuanzia saa kumi jioni.

Aidha alisema kuwa kabla ya kufanyika shindano hilo warembo hao watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii mkoani hapa ikiwemo Mapango ya Amboni na Hifadhi ya Taifa ya Saadani.

Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha

KUELEKEA MKUTANO MKUU MAALUMU WA CCM, WAJUMBE MWANZA WAELEZEA IMANI YAO.

$
0
0
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Mwanza, Simon Mangelepa, akizungumzia maandalizi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho kutoka mkoani Mwanza, ambao tayari wameanza kuwasili mkoani Dodoma kwa ajili ya Mkutano huo ambao unatarajiwa kufanyika Jumamosi Julai 23,2016 ambapo pamoja na mambo mengine pia Mkutano huo ni maalumu kwa ajili ya uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Katika Mkutano huo, Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM wanatarajiwa kumpitisha kwa kura za ndiyo Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, akipokea Uongozi kutoka kwa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka mkoani Mwanza, wamesema wana imani kubwa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli ambaye anatarajiwa kukabidhiwa uenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Taifa.

Katibu Mwenezi wa CCM mkoani Mwanza, Simon Mangelepa, ameyasema hayo hii leo, wakati akizungumzia maandalizi ya wajumbe hao ambao baadhi yao tayari wamewasili mkoani Dodoma kwa ajili ya Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM unaotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Julai 23 mwaka huu.

“Sisi wajumbe tunaotoka Mkoa wa Mwanza tunaamini kwamba anatosha (JPM) na yuko makini na chama chetu kitaendelea kuimarika zaidi akikabidhiwa uongozi. Amesema Mangelepa na kuwasihi viongozi wengine wa CCM kuanzia ngazi ya Mashina, Matawi, Kata, Wilaya na Mkoa, kuendelea kukiimarisha chama, ikiwemo kusimamia vizuri Ilani ya uchaguzi katika kuwaletea maendeleo wananchi hususani wanyonge kama Rais Magufuli anavyosisitiza.

Ametanabaisha kwamba wananchi wakiwemo wanaccm, wanayo matumaini makubwa kwa Rais Magufuli katika utendaji wake wa kazi, na kwamba wapenda amani na maendeleo wanaochukia rushwa pamoja na ubadhirifu wanampenda sana.

Katika hatua nyingine Mangelepa amepuuzilia mbali madai yanayotolewa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wanaobeza utendaji kazi wa Rais Magufuli na kwamba hiyo inaashiria hofu waliyo nayo baada ya kukabidhiwa uongozi wa CCM kwa kuwa watakosa hoja za kuzungumza kisiasa.


Bonyeza HAPA Kusikiliza. Au Bonyeza Play Hapo Chini.

MOTISHA YA NUNUA, UZA, SHINDA NA KONYAJI YAZINDULIWA KANDA YA ZIWA

$
0
0
Meneja Masoko na Udhaamini wa Kampuni ya TBL, George Kavishe (wa pili kulia), akizungumza katika Uzinduzi wa Motisha Mpya ya Nunua, Uza, Shinda na Konyagi kwa Wasambazaji wa kinywaji cha Konyagi Kanda ya Ziwa ambao ulifanyika jana Jijini Mwanza.

Wengine ni Joseph Mwaigombe ambae ni Meneja Mauzo na Usambaji wa Kampuni ya TDL Kanda ya Ziwa (wa kwanza kushoto), Deogratius Nabigambo ambae ni msambazaji wa vinywai vikali eneo la Ngara na Biharamulo mkoani Kagera (wa pili kushoto), na Martha Bangu ambae ni Meneja wa chapa yaa Konyagi (wa kwanza kulia).

Katika Motisha (Promotion) hiyo, wasambazaji wa kinywaji cha Konyagi wataingia katika droo ya kushindania magari mawili ambapo kila moja lina thamani ya Shilingi Milioni 46 pamoja na zawadi mbalimbali ikiwemo kitita cha fedha.

Zawadi za Motisha hiyo zitatolewa kwa Wasambazaji na Wauzaji wote nchini watakaouza katoni za Konyaji kuanzia 400 hadi 30,000 kwa mwezi.

Na BMG
Meneja Masoko na Udhaamini wa Kampuni ya TBL, George Kavishe (kushoto), akizungumza katika Uzinduzi wa Motisha Mpya Nunua, Uza, Shinda na Konyagi kwa Wasambazaji wa kinywaji cha Konyagi Kanda ya Ziwa ambao ulifanyika jana Jijini Mwanza. Kushoto ni Martha Bangu ambae ni Meneja wa chapa yaa Konyagi
Deogratius Nabigambo ambae ni msambazaji wa vinywai vikali eneo la Ngara na Biharamulo mkoani Kagera (kushoto) akizungumza katika uzinduzi huo ambapo alisema akibahatika kushinda zawadi ya gari itamsaidia katika shughuli zake za usambazaji wa Kinywaji cha Konyagi ambapo aliwasihi wasambazaji wengine kuitumia fursa hiyo kwa kuongeza mauzo yao ili kuingia katika droo hiyo ya Nunua, Uza, Shinda na Konyagi. Kulia ni Meneja Masoko na Udhaamini wa Kampuni ya TBL, George Kavishe
Wasambazaji na wauzaji wa vinywaji vikali Kanda ya Ziwa wakiwa katika Uzinduzi wa Motisha (Promotion) ya Nunua, Uza, Shinda na Konyagi uliofanyika jana Jijini Mwanza.
Ufafanuzi ukitolewa kwa Wasambazaji na Wauzaji wa Vinywaji Vikali Kanda ya Ziwa, katika Uzinduzi wa Motisha Mpya ya Nunua, Uza, Shinda na Konyaji uliofanyika jana Jijini Mwanza
Meneja Masoko na Udhaamini wa Kampuni ya TBL, George Kavishe, akizungumza na Wanahabari katika Uzinduzi wa Motisha Mpya Nunua, Uza, Shinda na Konyagi kwa Wasambazaji wa kinywaji cha Konyagi Kanda ya Ziwa ambao ulifanyika jana Jijini Mwanza.

WASIFU WA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, MGOMBEA NAFASI YA MWENYEKITI WA CCM

$
0
0
1.0. MAISHA YAKE

Ndugu John Pombe Joseph Magufuli alizaliwa Oktoba 29, mwaka 1959 katika kijiji cha Chato, Wilayani Biharamulo katika Mkoa wa Kagera. Hivi sasa Chato ni Wilaya katika Mkoa wa Geita. Ndugu Magufuli ni Daktari wa Falsafa (PhD) ya Kemia. Ana mke na watoto saba. Alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Oktoba, 2015 kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (C.C.M). Aliapishwa na kuanza rasmi majukumu yake ya kuiongoza Tanzania tarehe 5 Novemba, 2015.

Tangu ameingia madarakani, Rais Dkt. Magufuli, ameonesha kuwa ana sifa zote muhimu za uongozi. Ana dira, maono na malengo kuhusu anakotaka Taifa liende. Ana mikakati ya kutekeleza dira na maono yake. Haogopi kufanya maamuzi makini. Ana kiu ya kuona Taifa linapata maendeleo. Amejipambanua kuwa yeye ni mtetezi wa wanyonge na dhamira yake kubwa ni kuona wananchi wanapata huduma bora za jamii na kero zao zinaondoka.

2.0. ELIMU NA MAFUNZO

Rais Dkt. Magufuli alianza elimu ya msingi katika Shule ya msingi Chato mwaka 1967 na kumaliza mwaka 1974. Mwaka 1975 alianza masomo ya sekondari katika Shule ya Seminari ya Katoke Mkoani Kagera. Mwaka 1977 alihamia shule ya sekondari ya Lake iliyopo Mkoani Mwanza na kuhitimu kidato cha Nne mwaka 1978. Kuanzia mwaka 1979 hadi 1981 alifanya masomo ya kidato cha Tano na Sita katika shule ya Sekondari ya Mkwawa Mkoa wa Iringa .

Mwaka 1981 hadi 1982 alisoma Chuo cha Ualimu Mkwawa na kuhitimu Stashahada ya Ualimu ya Masomo ya Kemia na Hisabati. Mwezi Julai hadi Disemba mwaka 1983, Dkt. Magufuli alipata mafunzo ya kijeshi katika Jeshi la kujenga Taifa kikosi cha Makutupora mkoa wa Dodoma. Mwezi Januari hadi Machi 1984 alihamishiwa kikosi cha mafunzo Jeshi la Kujenga Taifa Makuyuni, Arusha. Mwezi huo wa Machi alihamia kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa Mpwapwa Dodoma na kumaliza mafunzo mwezi Juni 1984.


Mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kusoma Shahada ya kwanza ya Sayansi na Ualimu akijikita katika masomo ya Kemia na Hisabati. Alitunukiwa Shahada hiyo mwaka 1988. Mwaka 1991 hadi 1994 alisoma na kutunukiwa Shahada ya Uzamili katika fani ya Kemia iliyotolewa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu cha Salford cha Uingereza. Mwaka 2006 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa ajili ya Shahada ya Uzamivu katika Fani ya Kemia na kufanikiwa kuhitimu mwaka 2009.

3.0. UZOEFU WA NDANI YA SERIKALI

Baada ya kuhitimu masomo yake ya Stashahada ya Ualimu, mwaka 1982 hadi 1983 Dkt. Magufuli alikuwa Mwalimu katika shule ya Sekondari ya Sengerema iliyopo Mkoani Mwanza akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati. Mwaka 1989 alijiunga na Chama Cha Ushirika cha Nyanza Mkoani Mwanza, ambapo alifanya kazi kama Mkemia Mkuu hadi mwaka 1995.

Mwaka 1995 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki Mkoa wa Kagera. Baada ya Uchaguzi, Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2000. Mwaka 2000 alichaguliwa kwa mara ya pili kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mashariki lakini mara hii akipita bila kupingwa. Mwaka huo huo aliteuliwa kuwa Waziri kamili wa Wizara ya Ujenzi hadi mwaka 2005.

Mwaka 2005 Rais Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya tatu kuwa mbunge wa jimbo la Biharamulo Mashariki, kwa mara nyingine akipita bila kupingwa. Baada ya uchaguzi, Rais wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alimteua kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuanzia mwaka 2005 hadi mwaka 2008 ambapo alihamishiwa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi hadi hadi mwaka 2010.

Mwaka 2010 Dkt. Magufuli alichaguliwa kwa mara ya nne kuwa Mbunge lakini, kufuatia mgawanyo wa majimbo uliofanyika, mara hii katika Jimbo jipya la Chato. Baada ya uchaguzi, aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi kuanzia mwaka 2010 hadi mwaka 2015.

Wakati akiwa Mbunge na Waziri, Dkt. Magufuli amefanya shughuli na kushika nyadhifa kadhaa ndani na nje ya nchi. Mwaka 2014, Dkt. Magufuli alishiriki katika Bunge Maalum la Kutunga Katiba Mpya akiwa ni Mjumbe wa Bunge hilo. Aidha, wakati akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi aliweza kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti Mwenza (Co-Chair) wa Mkutano wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Makazi (UN-Habitat).

Tarehe 25 Oktoba, 2015 Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na tarehe 5 Novemba, 2015 aliapishwa kushika rasmi wadhifa huo.

4.0. UZOEFU WA UONGOZI NDANI YA CHAMA

Rais Dkt. Magufuli alijiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977. Amekuwa Mwanachama mwaminifu na ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama. Nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wilaya, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Mkoa, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Mkoa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa.

Sambamba na kushika nafasi mbalimbali za uongozi, Dkt. Magufuli mara zote alijitoa kukitetea Chama na kuhakikisha kinapata ushindi. Alishiriki kikamilifu kuwafanyia kampeni wagombea wa CCM katika Chaguzi Ndogo zilizofayika katika majimbo ya Busanda, Biharamulo Magharibi na Igunga na kupata ushindi. Katika Mkutano Mkuu wa CCM wa tarehe 11 – 12 Novemba mwaka 2012, Dkt. Magufuli alikuwa miongoni mwa Mawaziri wachache waliopata fursa ya kuelezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama ya Mwaka 2010 – 2015. Alielezea mafanikio ya utekelezaji wa Ilani, hususan katika sekta ya miundombinu.

Tarehe 11 mwezi Julai, 2015 Mkutano Mkuu wa Taifa wa CCM ulimchagua na kumteua Dkt. Magufuli kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aliinadi vyema Ilani ya uchaguzi ya CCM (2015) na kukiwezesha Chama kupata ushindi mkubwa. Tarehe 25 Oktoba, 2015 alichaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nafasi hiyo imemwezesha kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa.

5.0. UFANISI KATIKA UONGOZI

Dkt. Magufuli ni kiongozi mnyenyekevu, aliye na hofu ya Mungu, mkweli, mtekelezaji wa ahadi, mwadilifu, shupavu, mahiri, mbunifu, mtafiti, mchapakazi na mtetezi wa wanyonge. Ni kiongozi mpenda haki na mchukia dhuluma, rushwa, ufisadi na ubaguzi wa aina yoyote ile. Ni kiongozi mwenye msimamo na mtetezi wa yale anayoyaamini.

Katika nyadhifa zote alizopata kutumikia alifanya kazi kwa uadilifu na umahiri mkubwa. Amejidhihirisha na kujipambanua kuwa ni mfuatiliaji na msimamizi wa sheria. Akiwa Mwalimu Sengerema Sekondari aliwezesha wanafunzi wote wa darasa lake kufaulu masomo ya Hesabu na Kemia aliyokuwa akiyafundisha. Akiwa Mkemia Mkuu wa Chama cha Ushirika cha Nyanza alisimamia vyema ubora wa uzalishaji wa mafuta ya Pamba na kuifanya Kampuni ya Nyanza kuwa mzalishaji mzuri wa mafuta ya Pamba.

Akiwa Waziri wa Ujenzi anakumbukwa kwa kubuni na kusanifu miradi ya ujenzi wa barabara, kusimamia vizuri matumizi ya fedha na kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango na kwa wakati uliopangwa. Uwezo wake katika kubuni na kusanifu miradi ya barabara uliigwa na nchi majirani, ikiwemo Kenya. Ameondoka Wizara ya Ujenzi akiwa amesimamia ujenzi wa zaidi ya Kilometa 17,000 za barabara za lami, madaraja makubwa zaidi ya 14 na madaraja madogo madogo zaidi ya 7,000 na vivuko. Aidha, alisimamia vizuri taasisi mbalimbali za Makandarasi, Wahandisi, Wabunifu na Wakadiriaji Majengo.

Dkt. Magufuli pia anasifika kwa uwezo wake mkubwa wa kuweka kumbukumbu ya kazi zake. Akiwa Wizara ya Ujenzi aliweza kutaja majina ya barabara zilizojengwa au zilizokuwa katika hatua za ujenzi, urefu wake, majina ya wakandarasi pamoja na gharama za ujenzi bila kusoma mahali popote. Wakati wa Rais Mstaafu Benjamini William Mkapa alimwita “Askari wa Mwavuli”.

Akiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi alisimamia upimaji wa ardhi za vijiji na viwanja vya makazi, na kushughulikia migogoro mingi ya ardhi iliyowahusu wananchi wa maisha ya chini. Wakati akiwa Waziri wa Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi alikuwa maarufu wa kutambua na kutaja idadi ya mifugo, kama vile samaki, ngómbe, mbuzi, kondoo, kuku, mbwa n.k. Kitendo cha kukamata meli ya kichina iliyokuwa ikivua samaki kwa wizi ndani ya Bahari Kuu ya Hindi eneo la Tanzania kilidhihirisha uzalendo kwa Taifa lake. Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Kikwete alimpachika jina maarufu la “Tingatinga”.

Sifa hizi nzuri ameendelea nazo hata baada ya kuchaguliwa kuwa Rais. Katika miezi michache ya uongozi wake amethibitisha anatekeleza ahadi. Aliahidi kutoa elimu bila malipo na kuanzisha Mahakama ya Mafisadi. Ameweza kusimamia nidhamu kwenye utumishi wa umma kwa kuondoa watumishi hewa na kuchukua hatua dhidi ya watumishi wa umma wasio waaminifu, wala rushwa, wazembe na wanaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo. Ameweza kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali. Kwa hakika Dkt. Magufuli anaakisi uongozi bora unaopaswa kuigwa na viongozi wengi Barani Afrika na Dunia.

6.0. DHIMA YA UONGOZI WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO 2015 – 2020) NA MALENGO YAKE MAHSUSI

Ilani ya uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 inazielekeza serikali zake kutumia nguvu zake zote kuendelea kupambana na changamoto kubwa nne;- Kwanza kuondoa umaskini, Pili, kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira hasa kwa vijana, Tatu, kuendeleza vita dhidi ya adui rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma, na Nne, kuendelea kudumisha amani, ulinzi na usalama wa maisha ya Watanzania na mali zao.

Sambamba na kutekeleza mambo hayo makubwa manne, kipindi cha Kampeni na wakati akizindua Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 20 Novemba, 2015 Rais Dkt. Magufuli alitaja malengo mahsusi ya Serikali ya Awamu ya Tano. Malengo hayo ni haya yafuatayo:

· Kudumisha Muungano, Amani na Umoja wa Tanzania. Serikali haitamwonea aibu mtu mwenye nia ya kuvunja Muungano na kuvuruga amani na mshikamano katika nchi. Hili alilidhihirisha vizuri wakati wa uchaguzi wa marudio huko Zanzibar, kwani Uchaguzi ulifanyika kwa amani na utulivu.
· Kujenga Uchumi wa Viwanda ili kufikia azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati kulingana na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025. Viwanda vinalengwa ni vyenye kutumia nguvu kazi kubwa, malighafi za ndani ya nchi, kuzalisha bidhaa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi. Nia ni kukabiliana na tatizo la ajira na umasikini;

· Kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya kiuchumi, hususan miundombinu ya usafiri na nishati;

· Kuimarisha huduma za jamii, hususan elimu, Afya na Maji. Lengo ni kuhakikisha huduma hizo zinapatakana sio tu kwa urahisi bali pia kwa ubora unaostahili ili kukabiliana na maadui ujinga, umaskini na maradhi;

· Kusimamia uwajibikaji wa utumishi wa umma na kuondoa urasimu ndani ya Serikali. Lengo ni kuhakikisha watumishi wa umma wanafanya kazi kwa ueledi, uadilifu na kujituma ili kuwawezesha wananchi kupata huduma kwa wakati;

· Kuimarisha usimamizi wa rasilimali za nchi, ikiwemo kuhifadhi mazingira na kuzidisha vita dhidi ya ujangili. Lengo ni kuhakikisha rasilimali za nchi zinawanufaisha watu wote wa kizazi cha sasa na kijacho. Aidha, ukusanyaji wa mapato ya Serikali na udhibiti wa matumizi ya Serikali nao utaimarishwa;

· Kusimamia utawala bora unaozingatia sheria na haki za binadamu. Jitihada za makusudi zitaelekezwa katika kuzidisha mapambano dhidi ya rushwa, ufisadi, dhuluma na uonevu wa aina yoyote. Aidha, maslahi ya makundi mbalimbali katika jamii, ikiwemo wanawake, wazee, watu wenye ulemavu na watoto yatalindwa. Kwa upande mwingine, wananchi watahimizwa kuheshimu na kufuata sheria za nchi;

· Kulinda usalama wa raia na mali zao kwa kupambana na uhalifu, ikiwemo wizi, ujambazi, tatizo la dawa za kulevya n.k.

· Kudumisha na kuendeleza ujirani mwema, mahusiano mema na Mataifa mengine duniani pamoja na Mashirika ya Kimataifa na Kikanda;

· Kuendeleza na kusimamia vizuri shughuli za michezo, sanaa, burudani na utamaduni, ikiwemo kukuza lugha ya Kiswahili.

HITIMISHO
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imedhamiria kuongeza kasi ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi na kuwataka watanzania washiriki kufanya kazi kwa bidii na maarifa ndani ya falsafa ya HAPA KAZI TU. Dhamira hii inakusudia kuwezesha Taifa letu kufikia Uchumi wa Kati uaoongozwa na Viwanda ili kutimiza malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.

AMANA BANK TANZANIA WAZINDUA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA

$
0
0



Juma Msabaha ambaye ni senior costomer service manager wa Bank Ya AMANA nchini Tanzania akifafanua jambo kwa wanahabari wakati Bank Hiyo ikizindua Rasmi Kituo cha Huduma kwa wateja ambacho ni mahsusi kwa kuwasaidia wateja wake kuzifikia na kuzipata Huduma Zao kiurahisi zaidi

Benki ya kwanza ya Kiislam nchini Tanzania Amana benki leo imezindua kituo chake cha huduma kwa wateja ambacho kitakuwa kikiwasaidia wateja wake kuweza kupata taarifa mbalimbali kuhusu huduma zao kama maulizo kuhusu bidhaa za amana, Atms,huduma za mitandao (simu banking) na amana banki mtaani n.k.

Kituo hicho kitakuwa kikifanya kazi kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 4 na watakuwa wanapatikana kwa nambari 0657980000 ambapo amana Bank ni miongoni mwa benki zinazofanya vizuri kwa sasa wana matawi saba matano yakiwa Dar es salaam,Arusha,Mwanza na wanatarajia kufungua matawi mengine mikoa mingi zaidi ila waliyoipa kipaumbele zaidi ni Zanzibar na Tanga
Akizungumza na waadishi wa habari meneja mfawidhi na huduma kwa wateja Juma Msabaha Amesema kuwa utaratibu wanaotumia kuweza kuwapata mawakala ni kwamba wakala lazima awe na leseni ya biashara pia awe na tin namba ya biashara kuonyesha kuwa ni mlipa kodi pia awe amefanya kazi zaidi ya miaka miwili na pia anaweza kuomba uwakala kwa namba zao ambazo ni 0657980000 au info@ amanabank.co.tz na maombi yake yatapelekwa BOT kuweza kujadiliwa na kama amekidhi vigezo atapewa uwakala ambapo amesema kuwa kwa sasa wana mawakala kwa mikoa kama tabora ,bukoba,na mtwara na bado wanaendelea kupokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali.

Munir Rajab – mkuu wa idarara ya biashara amana benki amisema kuanzishwa kituo hicho kuna lengo la kuhitaji kuwa karibu na na wateja wao huku akitanabaisha kuwa huduma za kibenki huwa zinafanana lakini kinachoweza kuwatofautisha ni ubora wa huduma kwa wateja na kwamba wao wamejipanga vizuri kuingia kwenye ushindani huo ambapo wameamua kuwa mwaka huu ni mwaka wa mawakala kwa sababu wanahitaji kuweza kuwafikia wateja wao mpaka mahali ambapo hakuna matawi na wataweza kutumia huduma za kibenki kupitia mawakala wao .


Mkuu wa biashara wa Bank ya AMANA nchini Tanzania Munir rajab akieleza mambo mbalimbali kwa wanahabari kuhusu huduma hiyo mpya kutoka kwao

Bw. Juma Msabaha akijibu swali wa muandishi wa habari Alisema kuwa utaratibu wanaotumia kuweza kuwapata mawakala ni kwamba wakala lazima awe na leseni ya biashara pia awena tin namba ya biashara kuonyesha kuwa ni mlipa kodi pia aweamefanya kazi zaidi ya miaka miwili na pia anaweza kuomba uwakala kwa namba zao ambazo ni 0657980000 au info@ amanabank.co.tz na maombi yake yatapelekwa BOT kuweza kujadiliwa na kana amekidhi vigezo atapewa uwakala . na kwa sasa wana mawakala kwa mikoa kama Tabora ,Bukoba,na Mtwara na bado wanaendelea kupokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali.

MKUU WA WILAYA ATANGAZA KATA ZA WILAYA MPYA YA UBUNGO

$
0
0
TANGAZO MUHIMU

Kwa Wakazi wa Kata za Makurumla, Mburahati, Manzese, Mabibo Sinza, Ubungo, Makuburi, Kimara, Mbezi, Msigani, Saranga, Goba, Kibamba na Kwembe. Ninyi ni wakaazi wa Wilaya Mpya ya Ubungo.

Kwa kila aliye na kero, ninapendekeza tuanze na zile kero sugu na kubwa kubwa na kama hakuna basi hata zile za kawaida. Kwa miezi miwili kutoka sasa Mimi na watumishi wenzangu wa Wilaya yetu, tutasikiliza na kuharakisha utatuzi au ushauri stahili.

Utolewaji wa Huduma kwa wananchi Wilayani Ubungo unazingatia Sera ya "Mlango Wazi". Serikali Ubungo inasema "Tuambie Ukweli ili tutende haki na wewe upate Haki yako"

Tafadhali na shime wana Ubungo, tujulishane ujumbe huu, ili ndani ya muda mfupi Ubungo iwe Wilaya ya Tofauti, itakuwa ngumu mwanzo ila itakuwa uhalisia mapema zaidi tukishirikiana.

Unaweza wasiliana nami moja kwa moja kupitia 0786146700 (nisipopokea tuma ujumbe mfupi-SMS) au kwa Mwezi huu wa Julai fika Ofisi za Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Tutakuwepo kuwasikiliza na kuwahudumia.

Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano amenituma niwatumikie na kuwahudumia kama Mtumishi na Kiongozi wenu.

Humphrey Polepole
Mkuu wa Wilaya UBUNGO

MHE. UMMY MWALIMU AAGIZA KUTENGWA FEDHA YA MFUKO WA MAENDELEO YA WANAWAKE

$
0
0
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) akikagua shughuli za maendeleo za vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Kata ya Magoweko Wilayani Gairo, Mkoa wa Morogoro
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) akiendelea kukagua shughuli za maendeleo za vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Kata ya Magoweko Wilayani Gairo, Mkoa wa Morogoro akiwa na Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ahmed Shabiby (kulia)Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) akiendelea akiangalia moja ya mashine ya kufyatua matofali wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo za vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Kata ya Magoweko Wilayani Gairo, Morogoro.Kulia ni Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. Ahmed Shabiby (kulia)


Na. Mwandishi –Wetu –Gairo Morogoro. 

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu (Mb.) leo amefanya ziara katika Wilaya ya Gairo, Mkoa wa Morogoro kwa kukagua shughuli za vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Kata ya Magoweko.

Akihutubia wanawake na wananchi walio jitokeza katika maonyesho ya shughuli hizo, Mhe Ummy alieleza kuwa Serikali imejipanga katika kumuwezesha mwanamke kiuchumi.

Alisema, uwezeshaji huo utafanyika kupitia mifuko mbalimbali ya kuwawezesha wanawake, ikiwamo Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake (WDF) uliopo katika kila Halmashauri nchini na Benki ya Wanawake Tanzania. 

Katika hadhara hiyo Mhe Ummy alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, Bibi Agness Martin Mkandya, kuhakikisha Halmashauri hiyo inatenga asilimia 5 ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya Mfuko wa Maendeleo ya Wanawake ili fedha hizo ziweze kutumika katika kukopesha wanawake wajasiliamali.

Aidha, aliwaeleza wananchi kuwa serikali itatekeleza ahadi yake ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-20 kwa kutenga kiasi cha shilingi milioni 50 kwa kila Kijiji kama Mfuko wa Mzunguko (Revolving Fund) kwa ajili ya kukopesha vikundi vya wajasiriamali kupitia Ushirika wa Kuweka na Kukopa (SACCOS) katika vijiji husika; hivyo wanawake nao wazichangamkie fedha hizo kwa kuanza kujiandaa kujiunga katika vikundi ili fursa hiyo isiwapite.

Katika kukabiliana na changamoto ya masoko kwa bidhaa zinazotengenezwa na wanawake, Mhe Ummy alisema, Ilani ya uchaguzi ya ccm pia inaelekeza Halmashauri zote kutenga asilimia 30 ya thamani ya manunuzi yake kwa ajili ya bidhaa zinazotengenezwa na vikundi vya vijana au wanawake. Aidha, mbunge wa Jimbo la Gairo, Mhe. Ahmed Shabiby aliwaeleza wananchi kuwa wataandaa utaratibu wa kuwa na maonyesho rasmi ya kutangaza kazi za wanawake wajasiliamali wa Wilaya hiyo.

Baadhi ya Wanawake walioshiriki katika shughuli hiyo walieleza kuwa kupitia shughuli za vikundi wameweza kushiriki katika shughuli mbalimbali za kujiongezea kipato ikiwa ni pamoja na kuhamasisha vijana kujiunga na vikundi hivyo, wakilenga pia kuwaelimisha vijana kuacha matumizi ya madawa ya kulevya. Aidha, wanawake hao waliainisha moja ya changamoto kubwa inayo wakabili kuwa ni ukosefu wa mtaji wa kutosha kuendesha biashara zao.

Kupitia hadhara hiyo Mhe Ummy aliwataka wazazi kutilia mkazo elimu kwa watoto wa kike. Alieleza kuwa Wilaya ya Gairo inakabiliwa na tatizo kubwa la mimba na ndoa za utotoni, tatizo ambalo kwa kiasi kikubwa linafifisha jitihada za serikali katika kumpatia mtoto wa kike Elimu.

KOFFI OLOMIDE AMPIGA MCHEZA SHOO WAKE BAADA YA KUTUA KENYA

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,MHANDISI RAMO MAKANI ATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA YA KISIWA CHA RUBONDO.

$
0
0
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akipokelewa na Mbunge wa Geita Vijijini Joseph Kasheku (Msukuma) mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita ,Herman Kapufi mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii katika Shirika la Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ,Missana Mwishawa muda mfupi baada ya kuwasili katika hifadhi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utaliii wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) Ibrahimu Musa akiteta jambo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani kabla ya kuanza kikao na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Mkurugenzi wa Idara ya Utaliii wa Shirika la Hifadhi za Taifa,(TANAPA) Ibrahimu Musa akizungumza wakati wa kikao cha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo.
Baadhi ya Madiwani wa mkoa wa Geita wakiwa katika kikao hicho.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo ,Missana Mwishawa akisoma taarifa ya hifadhi hiyo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani.
Mkuuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo,Missana Mwishawa akimkabidhi Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani taarifa ya Hifadhi hiyo.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Geita ,Herman Kapufi akizungumza katika mkutano wa Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani (kulia kwake) alipotembelea Hifadhi ya Taifa ya kisiwa cha Rubondo.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Shirika a Hifadhi za Taifa (TANAPA) Ibrahim Musa.
Baadhi ya watumishi katika Hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Rubondo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo alipofanya ziara ya siku moja katika Hifadhi hiyo.
  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo pamoja na viongozi wengine wa serikali wa mkoa wa Geita mara baada ya kumalizika kwa kikao na watumishi wa hifadhi hiyo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mhandisi Ramo Makani akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Geita mara baada ya kumaliza kikao na watumishi wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo. 

Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog kanda ya Kaskazini.

JK AONGOZA KIKAO CHA NEC LEO MJINI DODOMA, NI KIKAO CHAKE CHA MWISHO, WAJUMBE WAPITISHA JINA LA RAIS DK. MAGUFULI

$
0
0

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimuongoza Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kuingia ukumbini, kwa ajili ya kuendesha kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) leo katika ukumbi wa Sekretarieti uliopo katika Jengola White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, leo. Wanaofuata ni Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa , Rais Dk. John Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa ,Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein. Kikao hicho kilikuwa na ajenda moja, ya kupokea jina la Rais Dk. Magufuli ili kuliafiki au kulikataa kuwa Mwenyekiti wa CCM wa awamu ya tano kufuatia Mwenyekiti wa sasa atakapostaafu na kumwachia kijiti cha uongozi huo wa Chama katika mkutano mkuu maalum wa CCM utakaofanyika kesho katika Ukumbi wa Dodoma Convetion.
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan (kuashoto) akiingia ukumbini kushiriki katika kikao hicho
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akiongoza shamra shamra baada ya yeye na viongozi wenzake kuwasili ukumbini kwa ajili ya kikao hicho
Wajume wakiwa wamesimama kumlaki Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete baada yeye na viongozi wenzake kuwasili ukumbini kwa ajili ya kikao hicho cha NEC
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na viongozi wenzake wakiwa tayari meza kuu kuendesha kikao hicho. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM, mtarajiwa Rais Dk John Magufuli, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein na kulia niMakamu Mwenyekiti wa CCM-Bara Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
 
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM, kilichofanyika leo. Kulis ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mweyekiti wa CCM mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein wakati wa kikao hicho cha NEC kilichofanyika leo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein akijadili jambo na Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa, Rais Dk. John Magufuli wakati wa kikao hicho cha NEC kilichofanyika leo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajab Luhwavi akitoa taarifa ya maandalizi ya mkutano mkuu maalum wa CCM utakaofanyika kesho, Julai 23, 2016, wakati wa kikao hicho cha NEC.
Wajumbe wa NEC na Wajume waalikwa wa NEC, wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka kulia ni Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Raijab Luhwavi, Katibu wa NEC Oganaizesheni Mohammed Seif Khatib na Katibu wa NEC Uchumi na Fedha Zakia Hamdan Meghji
Katibu wa NEC Itikasi na Uenezi na Msemaji Mkuu wa CCM, Christopher Ole Sendeka wakijadiliana jambo wakati wa kikao hicho cha NEC
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akimsikiliza kwa makini Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana wakati wakijadili jambo wakati wa kikao hicho cha NEC kilichofayika leo
Kiti alichokuwa amekalia Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli (kushoto), kikiwa wazi baada ya Dk. Magufuli kutoka ukumbi kutoa nafasi ya jina lake kutajwa na Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Kikwete (wapili kushoto), kwa wajumbe wa NEC leo, Kama lilivyopendekezwa na Kikao Cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika jana kwa kumpendekeza Dk. Magufuli kuwa Mweneyekiti wa CCM wa awamu ya tano. Kulia ni Makamu Kwenyekiti wa CCM Bara na Katibu Mkuu wa CCM Abduulrahman Kinana
Wajumbe wa NEC wakiwa wamenyoosha mikono kushirikia kulipitisha jina la Rais Dk. Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM, kufuatia kulipitisha, jina hilo kesho litapelekwa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ili kupigiwa kura ya ndiyo au hapana.
Wajumbe wa NEC wakiwa wamenyoosha mikono kushirikia kulipitisha jina la Rais Dk. Magufuli kuwa Mwenyekiti wa CCM, kufuatia kulipitisha, jina hilo kesho litapelekwa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM ili kupigiwa kura ya ndiyo au hapana.
Viongozi wa Meza Kuu wakiwa wamesimama kuwaunga mkono wajumbe waliosimama na kuamsha shamrashamra baada ya jina la Rais Dk John Magufuli kupitishwa na wajumbe katika kikao hicho cha NEC
Wajumbe wakiwa wamesimama kwa shamrashamra hizo


 Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli akitoa neno la shukurani baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe wa NEC wakati wa kikao hicho cha NEC
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akimpongeza, Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli baada ya maelezo yake mazuri wakati akitoa neno la shukurani baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe wa NEC
Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein,akimpongeza, Mwenyekiti wa CCM mtarajiwa Rais Dk. John Magufuli baada ya maelezo yake mazuri wakati akitoa neno la shukurani baada ya jina lake kupitishwa na wajumbe wa NEC 
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akionyesha katarasi itakayotumiwa na wajumbe wa mkutano Mkuu Maalum wa CCM kupiga kura 
 Juma Borafya kutoka Zanzibar akisimama baada ya kuteuliwa kukubali au kukataa jina la Dk. Magufuli litakapowasilishwa kwenye Mkutano Mkuu Maalum wa CCM
 Mjumbe wa NEC, Waziri Kiongozi Mstaafu, Shamsi Vuai Nahodha akitoa neno la shukrani mwishoni mwa kikao hicho.
 Makatibu wa NEC wakiwa kazini kuhakikisha kila jambo la muhimu  la kwenye kikao hicho linanukuliwa vema.
 Wajumbe wakiwa amejaa ukumbini
 Mweneyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Dk. Jakaya Kikwete akimpongeza Nahodha kwa neno lake la shukurani
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akionyesha furaha yake kabla ya kufunga kikao hicho baada ya ajenda kumalizika hatua kwa hatua.
Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akikifunga kikao hicho cha NEC ambacho ni cha mwisho kwake kama Mwenyekiti, PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO, KWA PICHA NYINGINE KEM-KEM ZA KIKAO HICHO 
GONGA HAPA
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live