Lady Jaydee akiongozana na mumewe, Gadner Habash leo asubuhi wakiingia katika Mahakama ya Kinondoni
Kwa mujibu wa wakili wa Jaydee, Bw. Mabere Nyaucho Marando, kesi hiyo imeahirishwa kwasababu upande uliofungua mashtaka haukutokea mahakamani, na wala kutoa taarifa yoyote.
'Kesi haiwezi kusikilizwa kama hawakutokea' alisema Marando.
Kesi ya madai iliyofunguliwa na uongozi wa Clouds Media Group, ilikuwa isikilizwe leo kutokana na maombi ya kuwa iharakishwe lakini upande wa Clouds Media hawakutokea.
Jaydee kama kawaida yake aliwasili katika Mahakama ya Kinondoni saa tano kasoro kumi akifuatana na mumewe Gadner G Habash na kuelekea moja kwa moja chumba cha mahakamani. lakini katika hali isiyo ya kawaida waandishi hawakuruhusiwa kuingia ndani.
Jaydee anashtakiwa kwa madai ya kuwachafua viongozi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba.
Kesho Jaydee anatarajiwa kufanya show yake ya miaka 13 ya Jaydee, na siku ya tarehe 15 (keshokutwa) msanii huyo atasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Clik here to view.
