Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

KIONGOZI WA WAYAHUDI AWAITA WATU WEUSI “NYANI” KATIKA IBADA

$
0
0

Na Mwandishi Wa Kimataifa
Immamatukio

Kiongozi wa dini Israel (chief rabbi) amezua mzozo kwa kuwaita watu weusi “nyani’ wakati akiendesha ibada ya wiki. katika ibada hiyo, Rabbi Yitzhaj Yosef alitoa matamshi ya dharau kwa lugha ya kiyahudi na kuwaita watu weusi kuwa ni “nyani”

Matamshi hayo yalitafsiriwa kuwa yanaamsha “hisia za ubaguzi wa rangi” jambo ambalo halikubaliki kwa wanaharakati kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Hata hivyo ofisi ya Rabbi Yosef ilijibu madai hayo kwa kudai alinukuu maandishi kutoka katika kitabu cha Talmud ambacho ni kitabu cha sharia ya Wayahudi. Yosef aliwahi kuleta mzozo baada ya kusema wanawake wa kidunia wanatabia za kinyama sababu wanavaa nguo za kuaibisha.


Rabbi ni kiongozi wa jamii ya Wayahudi wa Sephardic waliloko Mashariki ya Kati pamoja na wale wa kaskazini mwa bara la Afrika.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

Trending Articles