Kijana wa miaka 22 amepoteza maisha baada ya kutandikwa risasi 20 na polisi wakifikiri ameshikilia bunduki kumbe ni simu yake ya iphone.
Stephen Clarke (Pichani) alipoteza maisha akiwa uwani kwa bibi yake Sacramento, Marekani usiku wa jumapili machi 18. Polisi wanasema waliona Clarke ameshikilia kitu kama bunduki kabla ya kumfatulia risasi 20 na kupoteza maisha.
Polisi hao wawili walifika eneo la tukio kufuatia wito wa simu ya 911 kuhusiana na tuhuma za uvunjaji dirisha la gari. Ndipo walipokutana na Clarke na kuamini kuwa ndiye aliyekuwa anavunja dirisha hilo. Pia walimuona ameshika kitu mkononi ndipo kila mmoja alimfyatulia risasi mara kadhaa ili kumdhibiti.
“niliwaambia Polisi kuwa nyinyi ni wauaji” kilimuonesha kipande cha video bibi huyo akibubujikwa machozi, ‘mmemtenganisha na watoto wake” alisema
kwa mujibu wa shirka la Associated Press (AP), familia ya Clarke imeeleza kuwa marehemu ameacha watoto wawili wakiume Cairo na Aiden pamoja na mke mtarajiwa Salena Manni. Askari waliofanya tukio hilo wamesimamishwa kazi wakati uchunguzi unaendelea