
Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi na Madawa ya kulevya, Mhe. Matter Salum akiongoza uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo katika kikao kilichofanyika jana katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.

Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge wakifuatilia uchaguzi wa kumteua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo uliofanyika jana katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.

Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. Eng. Ramo Makani akiongoza uchaguzi wa kumchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo katika kikao kilichofanyika jana katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Mhe. Dkt. Christine Ishengoma (aliesimama) akiwashukuru Wajumbe baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo katika uchaguzi uliofanyika jana katika kumbi za Bunge Mjini Dodoma. kushoto kwake (aliekaa) ni Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mhe. Emmanuel Mwakilasa