Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live

MEGATRADE YAVIPIGA JEKI CHUO KIKUU NA CHAMA CHA SOKA KILIMANJARO.

$
0
0

Meneja masoko wa Kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha,Edmund Rutaraka akimkabidhi hundi ya kiasi cha shilingi Milioni 1.5 ,katibu wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro ,KRFA,Mohamed Musa kwa ajili ya kusadia ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa iliyoanza hivi karibuni.







Mweka hazina wa Chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro,Kusianga Kiata,akitizama hundi iliyotolewa na kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha.







Baadhi ya wadau wa soka waliofika kushuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ofisi za chama hicho zilizopo jengo la Voda House.







Meneja Masoko kanda ya Kaskazini ,Edmund Rutaraka akimkabidhi Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ushirika na Biashara ,Moshi,( MOCU),Profesa Faustine Bee hundi ya kiasi cha shilingi Mil 2 kusaidia maeneo mbalimbali yenye changamoto chuoni hapo.







Meneja Masoko wa kampuni ya Megatrade Investment ya jijini Arusha,Edmund Rutaraka akizungumza jambo mara baada ya kukabidhi hundi kwa mkuu huyo wa chuo.







Makamu mkuu wa Chuo kikuu cha Ushirika na Bashara (MOCU) Profesa Faustine Bee akizungumza mara naada ya kukabidhiwa hundi hiyo.

Na Blobu ya Jamii




BREAKING NEWS: KADI ZA KRISMASI NA MWAKA MPYA MARUFUKU

RIPOTI YA RUSHWA BARANI AFRIKA KUZINDULIWA, TANZANIA PIA IPO

$
0
0
Transparancy International, inategemea kuchapisha utafiti unaoangalia maoni ya watu uzoefu na mtazamo wao kuhusu masuala ya rushwa katika nchi 28 barani Afrika.

Maandalizi ya ripoti hiyo iitwayo People and Corruption, Africa Survey 2015 Global Corruption Barometer Transparency International imeungana na Afrobarometer, walioongea na watu wasiopungua 43,143, katika nchi 28 katika nchi zilizoko pembezoni mwa jangwa la Sahara.

Kwa mujibu wa African Press Organisation, shirika la Transparency International litachapisha utafiti huo tarehe 1/12/2015, unafuatia ule uliopita uliojulikana kama Global Curruption Barometer, uliochapishwa mwaka 2013

WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA BANDARINI,ATOA AMRI YA KUKAMATWA KWA MAAFISA TRA

$
0
0




Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa  amewasimamisha kazi maofisa watano na watumishi watatu wa mamlaka ya mapato Tanzania(TRA)kutokana na upotevu wa makontena 349 yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni 80.
 Akizungumza na viongozi wa mamlaka ya Bandari pamoja na viongozi wa TRA,katika ziara ya kushtukiza leo,Waziri Mkuu amewataka Kamishna Mkuu wa TRA,Rished Bade na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA,Lusekelo Mwasena,wahakikishe wanashirikiana na polisi kufuatilia upotevu huo na na kwamba fesha hizo zinapatikana na zinarudi Serikalini.
 Akitangaza uamuzi huo baada ya kufanya kikao na viongozi wa Serikali bandarini hapo,Waziri Mkuu aliwataja waliosimamishwa kazi kuwa ni Kamishna wa forodha,Tiagi Masamaki na mkuu wa kituo cha huduma kwawateja, Habibu Mponezya.
 “IGP,Ninaagiza watu hawa wakamatwe na kuisaidia polisi,hati zao za kusafiria zikamatwe na mali zao zikaguliwe kama zinaendana na utumishi wa umma,”alisema Waziri Mkuu. 
 Watumishi wengine waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA,Haruni Mpande,Hamisi Ali Omari(hakutaja anatoka kitengo gani)pamoja na mkuu wa kitengo cha Bandari Kavu (ICD In –Charge),Eliachi Mrema na alitaka wawe chini ya polisi lpaka uchunguzi utakapokamilika.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amemuagiza Katibu mkuu wa hazina,Dkt.Servacius Likwelile,kuhakikisha kuwa anapeleka wataalamu kutoka mawakala wa serikali Mtandao(e-Gvt)ili kukagua mifumo ya taarifa na kubaini jinsi ambavyo wizi huo unafanyika.
“Ninataka uchunguzi uanze mara moja pia tafuteni njia mabazo zinatumika kama mianya ya wizi kutokea hapa bandarini pamoja na makontena yatafutwe na fedha zirudishwe serikalini.
 Akijibu maswali ya Waziri Mkuu,Kamishna Mkuu wa TRA,Rished Bade alikiri kuwepo kwa upotevu wa makontena na kwamba walifanya ukaguzi kwenye ICD moja na kukuta makontena 54 yamepotea kwa njia ya wizi .“Hata hivyo tulipoendelea na ukaguzi namba iliongezeka na kufikia 327.tunaendelea kufuatilia kwa kushirikiana na TAKUKURU hata hivyo mmiliki wa ICD ametakiwa kulipa faini sh.bilioni 12.6 na mpaka sasa ameshalipa sh.bilioni2.4,”alifafanua Bade.
Lakini alipoulizwa kuwa ana majina ya watumishi wanaohusika katika wizi huo hakutoa jibu la moja kwa moja na badala yake alisema anayo na ampe muda wa kuyatafuta ambapo Waziri mkuu aliyatoa na akamuonyesha orodha ya makontena yaliyopotea moaka namba za magari ambayo yalitumika kuyabebea hivyo hakuwa na jinsi na kukiri kuwa ni ya kweli.

Waziri Mkuu Majaliwa kasim Majaliwa akizungumza na viongozi wa TPA na TRA .
Hapa Waziri Mkuu akiagana na baadhi ya viongozi kutoka TRA na TPA mara baada ya mkuatano.
Waziri Mkuu Majaliwa Kassim akionyesha orodha ya makontena yaliyopotea wakati alipofanya ziara ya kushtukiza bandarini.








MAKAKAMA TANZANIA BEGA KWA BEGA NA WAANDISHI WA HABARI

$
0
0




Jaji kiongozi wa Mahakama kuu ya Tanzania Shaaban Lila amesema kuwa majaji wa Tanzania wanabusara katika kufanya maamuzi yao na ndio maana hata vyombo vya habari nchini hata vinapowachafua hawaangaiki kufikisha kwenye vyombo vya dola.

 Jaji kiongozi huyo amesema hayo leo wakati wa kufunga mafunzo ya siku mbili  kwa waandishi wanao ripoti habari za mahakamani yaliyokuwa na lengo la kuwajengea uwezo zaidi wa kuripoti habari za mahakama.
"Si uoga bali ni busara zinazotumika kwa majaji kutosumbuana na vyombo vya habari pale waandishi wanapotoa taarifa za maamuzi ya hukumu katika kesi zenye mvuto wa jamii ambazo zinaashiria kama majaji wanapendelea upande mmoja."alisema
Aliongeza kuwa majaji wana mioyo ambayo inasikia uchungu kama binadamu wengine pale wanapoandikwa ndivyo sivo wakati wanapokuwa wakisikiliza na kutoa maamuzi ya kesi mbalimbali.
Alisema kuwa majaji kama wasingekuwa na busara wangefungua kesi nyingi mahakamani dhidi ya vyombo vya habari kutokana na vichwa vya habri vya magazeti kwa namna vinavyoandikwa ndivyo sivyo.
"Tungefungua kesi nyingi dhidi ya vyombo vya habari kwa kutuandika habari ambazo si sahihi huku wakishambulia majaji jambo ambalo halileti picha nzuri kwa jamii na kupelekea jamii kutoaiamini mahakama."alisema
Alisema kuwa mahakama haikwepi kuambiwa kasoro za kiutendaji wa kazi zake na kwamba wapo tayari kupokea changamoto lakini changamoto hizo ziripotiwe vizuri.
Jaji alisema kuwa wao wapo tayari kushirikiana na vyombo vya habari na kwamba wataboresha utoaji habari na kuwataka waandishi kama hawajaelewa kitu kwenye kesi wawafuate ili wapewe ufafanuzi wa kilichoamriwa na si kuandika kinyume na kilichoelezwa.
Aidha alitoa wito kwa waandishi kuwa na utaratibu wa kushirikiana na mahakam pale wanapoona kuna habari inayotakiwa lakini haipatikani.
Pia alisisitiza waandishi kuandika habari za mahama kwa usahihi ili jamii iweze kurudisha imani kwa mahakama zao kwa kuwa mahama haifanyi siasa na hakuna siasa kwani wao wanadiri na sheria.
Hata hivyo katika mafunzo hayo ya siku mbili waandishi wa habari kupitia Baraza la habari Tanzania MCT walitoa maadhimio kwa Mahakama ambapo katika maadhimio hayo waliomba mahakam kwa ushirikiano na MCT kujenga utaratibu wa kuandaa mafunzo ya mara kwa mara.

Aidha waliwaomba Majaji pindi wakishasoma hukumu watoa nakala za hukumu hizo ili ziweze kuwasaidia waandishi wahabari ili kuweza kuandika habari sahihi.

TANZIA:ALIYEKUWA MKURUGENZI MSAIDIZI WA SHUGHULI ZA BUNGE BI.HELLEN MBEBA AFARIKI DUNIA

$
0
0
Katibu wa Bunge Dkt. Thomas Kashililah, anasikitika kutangaza kifo cha mtumishi wa Bunge, Bi. Hellen Stephen Mbeba (36), aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi-Shughuli za Bunge, kilichotokea ghafla leo Ijumaa tarehe 27/11/2015 wakati akipelekwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu.

Msiba upo nyumbani kwake eneo la Kisasa, Mjini Dodoma. Taarifa zaidi na taratibu nyingine ikiwa ni pamoja na ratiba kamili ya maziko zitaendelea kutolewa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu pindi mipango itakapokamilika.

MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI AMEN.
Imetolewa na:

Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano
Ofisi ya Bunge
Dar es Salaam
27.11.2015

KAMANDA MPINGA AZINDUA OPARESHENI YA PAZA SAUTI DAR

$
0
0
 Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,DCP  Mohamed Mpinga, akisalimiana na Mabalozi wa Usalama Barabarani, muda mfupi kabla ya kuzindua Operesheni ijulikanayo kwa jina la “Paza Sauti” yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona kuna viashiria vya uvunjifu wa sheria za barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.

 Kamanda  wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Mohammed Mpinga, akitoa maelekezo ndani ya moja ya basi linalofanya safari  zake mkoani wakati wa  kuzindua  wa Operesheni Paza Sauti yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa mara wanapoona  viashiria vya uvunjifu wa sheria za  barabarani. Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
 Wadau wanaotumia  usafiri wa barabara, wakiwemo madereva na abiria wakimsikiliza Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohammed Mpinga(hayupo pichani) alipozindua  Operesheni Paza Sauti, yenye lengo la kuwaelimisha abiria ili waweze kutoa taarifa  wanapoona kuna viashiria vya  uvunjifu wa sheria za barabarani,Operesheni hii ilizinduliwa jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo na Matukio wa Mabalozi wa Usalama Barabarani,Jackson Kalikumtima(kulia), akitoa elimu kuhusiana naOperesheni ya Paza Sauti kwa mmoja wa wadau wanaotumia  usafiri wa barabara, Operesheni hii ilizinduliwa Stendi ya Mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, jijini Dar es Salaam leo.(Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

PICHA: RAIS MAGUFULI AAZIMISHA UHURU DAY KWA KUFANYA KAZI

$
0
0
Rais John Magufuli ameungana na watanzania wote kushiriki katika Siku ya Uhuru kwa kufanya usafi katika eneo la Ikulu Magogoni jijini Dar es salaam.

Aidha, Rais Magufuli ameibadilisha siku ya maadhimisho ya Uhuru wa Tanzania a mbapo miaka ya nyuma watu huelekea viwanja vya Uhuru kuungana na wengine kuadhimisha siku hii ambapo mwaka huu imetumika katika kufanya usafi wa Mazingira ili kukabiliana na ugonjwa wa Kipindu pindu.

Mwaka huu Tanzania ina adhimisha miaka 54 ya Uhuru ambapo ilijipatia uhuru wake mwaka 1961.





BUSINESS TIMES LIMITED (BTL) WAUNGA MKONO AGIZO LA RAIS MAGUFULI(PICHA)

LUKUVI AAHIDI KUKOMBOA MASIKINI BAADA YA KUKABIDHIWA OFISI RASMI

$
0
0


Waziri wa maendeleo ya nyumba na makazi,William Lukuvi amesema atahakikisha wananchi maskini wanapata haki zao za kumiliki ardhi pamoja na kuwawezesha  kuwa na  makazi bora ya kuishi  na kuwashughulikia wale wote wanaotumika kama mawakala na kudhulumu maeneo yao.

 Aidha ametoa siku saba kwa Mkurugenzi wa Wizara hiyo kuainisha utaratibu wa namna ya kuwawezesha wananchi hao kujenga nyumba bora za kuishi la sivyo atambadilisha kazi na kumuweka mtu mwingine ili aweze kutekeleza suala hilo ambalo ni agizo toka kwa Rais.John Magufuli na lipo kwenye ilani yao ya Chama.

 Ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Alphayo Kidata,na kusema kuwa sasa yeye ni mtu mpya ,katika awamu mpya na mambo yake ni mapya hivyo wajipange katika kwenda na kasi yake mpya.
 “Ninataka kumwambia Mkurugenzi wa nyumba na makazi kuwa ilani yetu inataka ujenzi nyumba bora za wananchi na KUWA suala hili haliwezi kufanywa na shirika la nyumba (NHC)pekee,sera yetu inataka kila mwananchi awe na nyumba bora ya kuishi hivyo ifikapo Jumatatu asubuhi nataka kusikia mikakati ya kumuwezesha hata kama ni kwa kupunguzia bei ya vifaa kutokana na kuwa hawawezi kufanya hivyo bila mchago wa Serikali kwani hatuwezi kuvumilia kuona wakiendelea kuishi kwenye nyumba za nyasi,”alisema Lukuvi.
 Pia amesema atahakikisha kuwa kila mwananchi anamilikishwa kipande chake cha ardhi kihalali na kuwa uwezeshaji wao hautawezekana bila kuwa na hati ya umiliki ya ardhi sambamba na kuchunguza ardhi walizopewa wawekezaji kama zimetumika kihalali na kwa matumizi yaliyodhamiriwa au kinyume chake na kuwanyang’anya na pia kuwatayamilikisha maeneo ambayo hayajaendelezwa. “Tutakwenda kuangalia maeneo ya wawekezaji ili kujua kama ardhi walizopewa wamezitumia kwa matumizi waliyoombea au wamezitumia kupata fedha benki na kuzifanyia shughuli nyingine,ninataka kupata taarifa za mashamba na meneo makubwa yaliyofutwa ili tuweze kudhibiti hili,”alisema.
Lukuvi amesema anataka kuwa na chombo katika Wizara yake ambacho kitasaidia katika kudhibiti na kusimamia ujenzi wa nyumba za kibiashara (real estate)kutokana na kumekuwa na watu wengi ambao wamekuwa wakijenga nyumba na kuzipangisha bila kulipia kodi .

Pia amesema kuwa atakutana na watumishi wa Wizara hiyo kutoka idara zote nchini ili kupata taarifa za fedha zilizokusanywa tangu tarehe 1mwezi wa saba tangu pale bajeti ilipoanza na kuwa kwa lengo la kujua jinsi zilivyotumika.  
“Kutakuwa na kikao cha wakuu wa idara wote waliopo hapa na mikoani pamoja na makamishna wa kanda watakuwepo na ninataka nipate taarifa za fedha kuanzia tarehe 1/07mpaka leo yaani fedha mlizopata, mlizokusanya na matumizi yake na pia kazi zilizofanywa na serikali kipindi hicho baada ya bajeti kuanza ,kazi zilizofanywa na wizar hii pamoja na vitengo vyake kote nchini lakini pia nipate taarifa za kila mkuu wa idara malengo yake ya mwaka huu wa fedha yalikuwa yapi na mangapi ameshayatekeleza,”alisema Lukuvi.

“Lakini pia ninataka nipewe utaratibu tuliouweka kuhusu kendeleza fukwe za oysterbay ili wale waliovamia na kujenga maghorofa tujue wanaondoka lini nataka Murugenzi wa mipango miji pamija na manispaa ya kinondoni kunipa taarifa hizo mapema kwani hizo ni fukwe kwa ajili ya wananchi na Rais.Magufuli alishtoa tamko,”alisisitiza.
  Naye Naibu  Waziri wa wizara hiyo ambaye pia ni Mbunge wa Ilemela,Angela Mabula ,amemshukuru Rais.Magufuli kwa kuwaamini na kuwa watafanya kazi kwa kushirikiana katika kutetea haki za wanyonge na kuhakikisha wanapata haki zao za ardhi na kuwashgulikia watakaohusika na kuwadhulumu bila kujali nafasi zao.
Waziri wa Maendeleo ya Nyumba na Makazi,William Lukuvi akizungumza na wakuu wa Idara mbalimbali leo mara baada ya kukabidhiwa rasmi ofisi na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Alphayo Kidata(kulia) na kushoto ni Naibu Waziri Angela Mabulla.


.
                                               

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MABALOZI NA KUKAMRIBISHA RASMI JANUARY MAKAMBA

$
0
0
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na  Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Jorge Luis Lopez, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Mhe. Jorge Luis Lopez, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam, le.
                                                                                                                    

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na  Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Mhe. Yasemin Eralp, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari Makamba, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu  kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika mazungumza na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari Makamba, wakati alipofika Ofisini kwake Ikulu leo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mhe. Januari Makamba, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Mhe Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, leo alipofika kujitambulisha baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.(Picha na OMR).

Article 1

$
0
0
Historia  inaonyesha panya walianza kufugwa nyumbanitangu karne ya 19. Wengi wakiwa ni panya wa kahawia lakini hata weusi na ‘Giant pouched rats’(wanaopatikana Jangwa laSahara) nao pia hufugwa.Panya wafugwao huwa na tabia tofauti ukilinganisha napanya wa mwituni kulingana na vizazi vingapi vimewekwa kama mifugo.
Hawa panya wafugwao,huwa hawaleti hatari sana ya magonjwa kama mifugo mingine, yaani paka na mbwa huwa marafiki na wanaweza kuzoeshwa kufanya kazi mbalimbali.
Panya wafugwao huwa watiifu na wasikivu kuliko panya wa kale, pia hupata magonjwa mara kwa mara kotokana na kuzaliana na jamii tofauti.
Panya wa kufugwa ni tofauti sana na wale wa mwituni. Ni wapole na hung’ata kwa nadra sana pia huvumilia uwepo wa watu wengi na huzaliana mapema na kwa wingi sana na ubongo, maini, mafigo, tezi ya adrenali na mioyo yao ni midogo sana. (Barnert 2002).
Tofauti na Panya wanaoishi mwituni ambao inaaminika kuwa wanaweza kubeba baadhi ya magonjwa na kuyapeleka kwenye mamalia wengine kwa mfano huko Ulaya katika miji kadhaa ugonjwa wa ‘Black Death’maarufu kama tauni uliua zaidi ya watu milioni 25 katika miaka ya 1348-1350 huku ikisemekana kuwa ulisabbishwa na vimelea vya yersinia pestis vilivyobebwa na kunguni wa panya wa tropiki waliokuwa
wanajishibisha kwa panya wengi wa huko Ulaya.
Hiyo imeendelea kwenye nchi nyingi kwani licha ya magonjwa ya binadamu pia panya wanahusishwa na
magonjwa ya mifugo kama vile homa ya ini ya nguruwe.Kwa kawaida panya huishi kwa muda wa miaka mitatu, lakini wengi huishi kwa mwaka mmoja tu kutokana na kuwindwa na wanyama wengine kama nyoka.
Kwa kawaida panya kama anavyochukuliwa na watu wengi kuwa myama mchafu, hatari na anayeweza kusababisha magonjwa bila kutambua kuwa kuna faida nyingi zinatokana na panya ambapo hutumika kama, KIUNGO CHA TAFITI:
Aina moja ya panya wa maabara inayojulikana kama panya Zucker,wao wanazalishwa wakiwa na uwezo wa kupata kifua kikuu na magonjwa mengine ya binadamu.Mfano 1895, chuo kikuu cha Clark, Worcester, Massachusetts(Marekani) kilianzisha kundi kubwa la panya weupe kwa ajili ya kujifunza madhara ya chakula na mapungufu mengine ya mwili.
Kwa miaka mingi panya wametumika kama viungo vya tafiti za magonjwa mbalimbali na kuongeza ufahamu wetu kuhusu viasilia, magonjwa na madhara ya madawa, na mada nyingine ambazo zimechangia kwa kiwango kikubwa kwenye masuala ya afya ya mwili wa binadamu.
Na hapa Nchini kwetu wamekuwa wakifundishwa kuchunguza magonjwa ya kifua kikuu na kuchunguza dalili za mapema katika mate ya binadamu Kutokana na uwezo wao wa kunusa harufu mara nane kwa
sekunde ikilinganishwa na mara mbili kwa binadamu. Panya pia ana uwezo wa kutambua harufu mbili kwa kunusa mara moja kwa mujibu wa chuo kikuu cha Sokoine Tanzania.
Na uchunguzi wa mwaka 2007 umebaini kuwa panya wana uwezo na akili ambapo hapo awali ulionekana upo kwa binadamu pekee na baadhi ya wanyama wa kale babu wa binadamu.

PANYA KAMA CHAKULA:
Imebainika kuwa nyama ya panya huwa ni chanzo kizuri cha protini kuliko nyama nyingine.Mfano huko Amerika ya Kusini baadhi ya watumwa wa kiafrika walitumia nyama hiyo kutosheleza milo yao,Australia
watu jamii ya Aborigines, wanatumia panya kwenye milo yao na huko India wanawake wa jamii ya Mishmi, hutumia panya sababu huruhusiwa kula nyama ya samaki, nguruwe na panya tu.
Aidha Shirika la chakula na kilimo la umoja wa mataifa lilikadiria kuwa zaidi ya nusu ya nyama inachotumiwa naWaghana ni panya na kwa Nchi za Magharibi huruhusu ulaji wa nyama hiyo tofauti watu wa jamii ya Shipibo (Peru) na watu wa Sirionó(Bolivia)wao ni marufuku kula panya.
Mathalani wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika Maonyesho ya Vyuo Vikuu nchini wameshauri kufuga na kula panya aina ya ndezi huku wakieleza kuwa nyama hiyo haina mafuta mengi, ikiwa pia na virutubisho muhimu na vilivyo adimu.
Pia panya hutumiwa kama chakula na nyoka, na wanyamawengine walao nyama. Ambapo jamii mbili za chatu hulapanya pekee na wengine huwafuga ili kulisha mifugo yao.

PANYA KAMA TAMADUNI:

Vilevile baadhi ya jamii katika nchi mbalimbali huwatumia panya kama kielelezo au sehemu ya utamaduni wao,kwa mfano Panya wa asili huruhusiwa kutembea huru kwenye Hekalu la Karni Mata(India)wanawawekwa kama wanaume watakatifu. Wahudumu huwalisha panya hao kwa nafaka na
maziwa na mtu akila chakula kilichoguswa na panya hao huonekana kama baraka toka kwa Mungu. .
Katika Nchi ya China, panya ni mmoja kati ya wanyama wa walio kwenye kalenda ya Zodiac ya wachina.Na wanaamini kuwa watu waliozaliwa kwenye mwaka wa panya huwa wana tabia za panya zikiwemo: ukweli, ukarimu, kiu ya kufanya mambo, hasira ya haraka na ufujaji.
Faida nyingine ya panya kutokana na utafiti uliofanywa na raia wa Ubelgiji,Bart Weetgen mwaka 1998 ambayo pia ni adimu kupatikana kwa wanyama wengine ukiacha mbwa ni kuwa panya ana uwezo mkubwa wa kunusa na kutegua mabomu yaliyotegwa ardini kwa umbali mrefu wa kipimo cha mita.Hiyo inatokana na udogo wa umbile lake pamoja na uzito humfanya asiweze kulipua mabomu ardhini pale anapoyabaini
na ili aweze kufanya kazi hiyo ni lazima apate mafunzo ambayo humpitisha katika hatua 9 mojawapo ikiwa kumfanya rafiki na kumjengea mazingira ya kumzoea mwanadamu.
Kiongozi Mkuu wa Mafunzo ya panya Nchini(SUA),Abdullah Mchovu,anaeleza sifa na tabia ya kipekee ya panya ni uwezo wa kuhifadhi na kufukua ."Kwa uasilia panya hukusanya mazao wakati wa mavuno,kisha kuyaficha katika mashimo shambani na baadaye wakati wa ukame hutumia njia ya kunusa ili kuyapata mazao waliyoyaficha,"Anaongeza kuwa "Sifa za kunusa ndizo zilizofanya wahakiki kumteua panya kuwa mteguaji bingwa wa mabomu kuliko binadamu au vifaa vya kiteknolojia.Ni nafuu zaidi kumtunza panya kuliko mbwa kwani wao wanafuata zaidi vitendo kuliko kufuata kinachofanywa na muongozaji,".
Hata hivyo itambulike kuwa pamoja na faida zote hizo lakini panya anatajwa kuwa ni chanzo kikubwa cha ongezeko la umasikini katika Nchi zinazoendelea hususani Tanzania.
Ni ukweli usiopingika kuwa kilimo ndio uti wa mgongo kwa nyingi za kiafrika na panya ni tatizo kubwa kwenye kilimo katika Bara la Afrika.Ambapo milipuko husababisha uharibifu mkubwa wa mazao
ya nafaka, Kituo cha kutafiti udhibiti wa viumbe hai waharibifu (SUA) kimeeleza kuwa uharibifu huo wa nafaka unakaribia asilimia 48, ambayo ni haraka kubwa kwa wakulima masikini.
Tanzania pekee hupoteza zaidi ya tani 400,000za mahindi kila mwaka,chakula hicho kinngeweza kutosha kulisha zaidi ya watanzania milioni 2 kwa mwaka mzima. Milipuko ya panya kulingana na utafiti wa kituo hicho ,huweza kusababisha hasara inayofikia asilimia 100 na husababisha matukio ya njaa kuongezeka kwa kiwango kikubwa katika jamii.
Kutokana na hali hiyo, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kupitia Kituo hicho, kilianzisha mradi wa utafiti wa kudhibiti milipuko ya panya kwa kutumia vizuia uzazi.
Hatua ambayo pengine ni hatari kubwa kwa maisha ya binadamu na wanyama wengine kutokana na udhibiti wa panya hao kutegemea matumizi ya sumu ukiachilia mbali ya kuwa za gharama na hazimfikii mkulima wakati anapohitaji. Lakini pia utafiti uliofanywa na Shirika la Utafiti wa Sayansi na Viwanda la Australia (CSIRO), duniani kote panya kumi huzaliwa sawa na mtoto mmoja wa binadamu anayezaliwa.
Kila siku watoto 360,000 waliozaliwa karibuni wanahitaji kulishwa, wakati huohuo panya 3,600,000 waliozaliwa karibuni pia wanataka chakula.Kwa mfano, nchi ya Indonesia ina wakazi milioni 230 na asilimia 60 kati yao hula wali kila siku.
Hata hivyo, katika nchi hiyo panya hula asilimia 15 ya mazao ya mpunga kila mwaka. Mwanasayansi Dkt. GrantSingleton, mfanyakazi wa shirika la CSIRO anasema kuwa:“Jambo hilo linamaanisha kwamba panya hula kiasi cha mchele ambacho kingeweza kuwalisha Waindonesia zaidi ya milioni 20 kwa mwaka mmoja.”
Zipo njia mbalimbali zinazoweza kutumika ili kupambana na wanyama hao waharibifu.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kitengo cha kuthibiti wanyama waharibifu,Profesa Loth Mulungu,njia kubwa na ya haraka ambayo pia haina gharama ni mkojo wa paka(jike) ambao umebainika kuwa na harufu kali inayowafanya panya wakimbie mara tu wanapoinusa kwa kudhani panya yupo eneo hilo tofauti na kutumia sumu.

WAHITIMU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI YALIYOFANYIKA CHUO CHA UONGOZI JKT KIMBIJI WAONYESHA UMAHIRI WA MAFUNZO WALIYOYAPATA

$
0
0

Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakionyesha jinsi ya kuzima moto wakati wa maonyesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi hilo,yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.






Wahitimu wakionyesha mafunzo ya karate waliyopata mara baada ya kuhitimu kozi ya awali ya Sajini na Askari wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.








Wahitimu wakionyesha mafunzo ya sarakasi waliyopata mara baada ya kuhitimu kozi ya awali ya Sajini na Askari wakati wa kufunga mafunzo hayo katika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam,yaliyofanyika mwishoni mwa wiki.







Mhitimu wa Mafunzo ya Kozi ya Awali ya Sajini na Askari,Joel Daniel(kulia),akimpiga teke mhitimu mwenzake Sylvestre Mandawa, wakati wa maonyesho ya karate ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi hilo,yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam,mwishoni mwa wiki.




Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,wakiwadhibiti vijana ambao ni mfano wa wezi ambao walikamatwa wakiiba vitu wakati wa janga la moto,maonyesho hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki,Chuo Cha Uongozi JKT Kimbiji, jijini Dar es Salaam.








Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Chuo Cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam.








Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, wakiwa wamebeba mfano wa majeruhi wa ajali, mara baada ya kumuokoa kutoka eneo la tukio wakati wa maonyesho ya kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi hilo,yaliyofanyika Chuo cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki.







Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Pius Nyambacha, akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya kozi ya awali ya Sajini na Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji,yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Chuo Cha Uongozi JKT Kimbiji,jijini Dar es Salaam.(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)

WARAGHBISHI WA KIJIJI CHA NYANDEKWA KUMKOMBOA MWANAMKE

$
0
0










Baadhi ya waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa Wilayani Kahama wakiongea na waandishi wa habari waliofika kijijini hapo kwa ajili ya kujionea matokeo mbali mbali baada ya waraghabishi kuwasaidia wananchi hao kuchukua hatua katika kila jambo kwa maendeleo ya kijiji chao



Pichani nikihoji maswali kwa Dada Miriam Stefano (Aliyejishika tama ) ambaye amekuwa mchango mkubwa kwa kutoa elimu ya uzazi na mabadilko ya mwili kwa vijana wa kike katika baadhi ya shule za sekondari na msingi katika kijiji hicho




Picha ya pamoja nikiwa na waraghabishi wa kijiji cha Nyandekwa Wilayani na waandishi wa habari tuliopata bahati ya kutembelea kijiji hicho na kujifunza namna gani wameweza kuwa chachu ya maendeleo katika kijiji hicho


Na Krantz Mwantepele ,KAHAMA

Mkutano mkuu wa Kijiji cha Nyandekwa wilayani Kahama mkoani Shinyanga uliofanyika mwishoni wa mwezi wa tisa umeazimia kuwashikinikiza wazazi wa kijiji hicho kuwapeleka watoto wao shule Azimio hilo Pia limeelekezwa kwa vijana wanaokaa vijiweni kuwataka kushirki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na sio kukaa vijiweni pia kushiriki katika mikutano mbali mbali ya kijiji kujua maendeleo ya kijiji Iikihusisha mapato na matumizi.

Mkutano huo umepitisha maazimio matano yanayolenga kurejesha nidhamu Na heshima kijijini Nyandekwa hatua hiyo imefikiwa Kutokana Na wananchi wa kijiji hiki kutoona umuhimu wao kuchukua hatua za kujikwamua kiuchumi na pia Kuwa na ujasiri wa kuhoji mapato na matumizi kwa ajili ya kijiji chao .

Hali hiyo inatokana na juhudi za dhati bila kukata tamaa zilizofanywa waraghabishi na watetezi wa haki za binadamu wa kijiji hicho akiwemo Miriam Stefano, Boniface Izengo , Matilda Peter ,Na Mwenyekiti Wa kitongoji cha Busolwa Bi Ana Alphonce kuwapa ujasiri na elimu ya uraia wananchi wenzao ili wawe chachu ya maendeleo.

Kwa mujibu wa bi Anna Alphonce ambaye pia ni mwenyekiti wa kitongoji cha Busolwe aliweza kuongea na mtandao wa Mwanaharakati Mzalendo Blog alisema kupitia mikutano mbalimbali ya kijiji aliweza kutoa hamasa kwa wanawake na wanaume wa kijiji hicho kushiriki katika uchaguzi mkuu uliopita katika kusikiliza sera za viongozi na mwishowe kushiriki kupiga kura.Na kwa muda mfupi aliweza kufanikisha wanawake wengi kushiriki katika maamuzi ya kijiji pia kuwa na ujasiri wa kuhoji katika mikutano ya kijiji.

Wengi wa wanakijji ambao wamekuwa waraghabishi katika kijiji hiki waliweza kupata mafunzo haya ya uraghabishi ambapo waliweza kujua baadhi ya haki zao na kuwa na uajasiri wa kuhoji mapato na matumizi ya kijiji hicho ambapo mwanzoni walikuwa hawapati fursa hiyo kwa wakati .Waraghabishi hawa wamekuwa chachu ya maendeleo ya kijiji cha Nyandekwa katika sekta za kiuchumi ,kisiasa na kijamii kwa kuwaelimisha wanakijiji wenzao haki na wajibu wao kwa nafasi kubwa .

“Viongozi wa kijiji hiki hawakuweza kutupa mrejesho wa kila jambo linalofanyika kwa kijiji hcetu hasa katika mikutano ya kijiji na sisi tulipoanza kuhoji tulikosa ushirikiano kwao lakini mwishowe wananchi wengi waliona umuhimu wa kushirikishwa” alinukuliwa bw. Boniface Izengo mmoja wa waraghabishi wa kijiji hiki alipokuwa akiongea na mwandishi wa habari hii.

Katika hatua nyingine mmoja wa waraghabishi wa kijiji hiki bi Matilda Peter amekuwa ni mmoja wa vijana wanaotoa elimu ya uzazi wa mpango kwa makundi rika ambapo hukutana na vijana hasa wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari na kuwajuza kuhusu mabadiliko ya mwili yao na pia kuwashauri jinsi ya kuepuka maambukizi magonjwa ya ngono na mimba zisizotarajiwa.

Maazimio yaliyopitishwa kuwa ni vijana wanaokaa au kusimama ovyo barabarani na maeneo mengine bila shughuli maalum kuwajibishwa na pia kuweza kuwawezesha kuwashirikisha katika shughuli za kijiji hicho ikiwemo kushiriki katika shughuli mbalimbali za uzalishaji kijijini hapo

Pia mkutano wa kijiji hiki uliazimia kuwa mapato na matumizi kuweza kujadiliwa kwa uwazi na pia kubandikwa katika mbao za matangazo hapo kijijini kuwezesha wananchi hao kuweza kusoma na kuelewa kila kinachoendelea kijijini kwao katika swala la maendeleo ya uchumi .

MWILI DOTTO WA JAMII FORUMS WASAFIRISHWA KWENDA SAME

$
0
0

Jeneza lenye Mwili wa Marehemu Dotto Mzava likishushwa Kwenye gari maalum mara baada ya kuwasili katika kanisa la Wasabato Manzese uzuri kwaajili ya sala ya kuombea kabla ya Mwili kusafirishwa kuelekea Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.



Mchungaji wa kanisa la Adventist wasabato akiendelea na ibada wakati wa ibada ya kumuombea marehemu kabla ya kusafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jamii Media Maxence Mello akitoa historia fupi ya Marehemu Dotto Mzava ambae pia alikua mmoja wa watumishi katika kampuni hiyo.


Baba Mkubwa wa marehemu Dotto Mzava akitoa maneno ya shukrani katika kanisa la Kisabato la Manzese Uzuri mara baada ya zoezi la misa kumalizika.




Heshima za Mwisho zikiendelea kutolewa




Majonzi na simanzi kwa ndugu wa marehemu




Mmiliki wa Fullshangwe Blog,John Bukuku akitoa heshima za mwisho




Heshima za mwisho zikiendelea kutolewa kwa mwili wa marehemu Dotto Mzava kabla haujasafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro kwaajili ya mazishi




Mbunge wa Jimbo la Kibamba, John Mnyika akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa marehemu Dotto Mzava kabla ya Kusafirishwa kuelekea Same Kilimanjaro kwa mazishi yanayotarjiwa kufanyika kesho




Mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media akitoa heshima za mwisho kabla ya mwili wa marehemu kusafirishwa Same Mkoani Kilimanjaro mapema leo




Ibada ikiendelea








Jeneza lenye mwili wa marehemu Dotto Mzava likipandishwa ndani ya gari tayari kwa safari ya kuelekea Same Mkoa wa Kilimanjaro leo kwaajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho




Ndugu, jamaa na marafiki wakiwa kanisani




Kwaya ya Angaza ikitoa huduma wakati wa ibada ya kumuombea marehemu Dotto Mzava




Baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu Dotto Mzava wakiwa kanisani kwenye ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika katika kanisa la Wasabato la Manzese Uzuri kabla ya Mwili kusafirishwa kwaajili ya kwenda kupumzishwa katika nyumba yake ya milele huko Kwao Same Mkoa wa Kilimanjaro.Picha na Pamoja Blog

WATOTO WENYE ULEMAVU WA NGOZI SHINYANGA WAPIGWA "TAFU "

$
0
0

Sehemu ya chakula mchele,unga na maharage tani 3.9,mafuta ya kupikia lita 100 na sabuni katoni 5,kilichotolewa na kampuni ya mtandao wa simu za mkononi wa Tigo kwa kituo cha kulelea watoto yatima na wenye albinism cha Buhangija mkoani Shinyanga




Wafanyakazi wa kampuni ya mtandao wa simu za mkononi wa Tigo wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto yatima na wenye albinism katika kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga,baada ya kuwapa msaada,ambapo walitoa mchele,unga na maharage tani 3.9,mafuta ya kupikia lita 100 na sabuni katoni 5



Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya akiwakabidhi sehemu ya msaada kwa watoto yatima na wenye albinism katika kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga,ambapo walitoa mchele,unga na maharage tani 3.9,mafuta ya kupikia lita 100 na sabuni katoni 5



Watoto yatima na wenye albinism cha Buhangija mkoani Shinyanga,wakicheza kwenye tufe la tigo,baada ya kupokea msaada wa chakula,ambapo wafanyakazi wa tigo walitoa
mchele,unga na maharage tani 3.9,mafuta ya kupikia lita 100 na sabuni katoni 5




Watoto yatima na wenye albinism cha Buhangija mkoani Shinyanga,wakiwa wamevaa fulana za tigo,baada ya kupokea msaada wa chakula,ambapo wafanyakazi wa tigo walitoa mchele,unga na maharage tani 3.9,mafuta ya kupikia lita 100 na sabuni katoni 5



Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Ziwa Ali Maswanya akizungumza na watoto yatima na wenye albinism katika kituo cha Buhangija mkoani Shinyanga wakati wa kutoa msaada kwenye kituo cha kulelea ,ambapo mchele,unga na maharage tani 3.9,mafuta ya kupikia lita 100 na sabuni katoni 5,kushoto ni Meneja wa Tigo mikoa ya Shinyanga,Tabora na Kigoma Kamara Kalembo na Meneja Huduma kwa wateja kanda ya ziwa Beatrice Kinabo(kulia)



SKENDO MISS UNIVERSE: MTANGAZAJI AMVISHA TAJI NA KUMVUA MISS, AMVISHA ALIYESHINDA(PICHA NA VIDEO)

$
0
0

Katika tukio lisilokuwa la kawaida na la kushangaza pengine laweza kuwa funga mwaka 2015, likiwa linarushwa moja kwa moja katika runinga ulimwenguni, mwanavichekesho maarufu duniani, Steve Harvey kw bahati mbaya alimvisha kimakosa taji la urembo wa ulimwengu (Miss Universe) Miss Columbia, Ariadna Gutierrez-Arévalo, mshindi wa mwaka 2015.

Kwa mujibu wa mtandao wa Yahoo, mkanganyiko huo ulitokea mwishoni katika tukio hilo la kimataifa ambapo Harvey alitakiwa kumtangaza mshindi wa pili (first runner-up, Ariadna Gutierrez-Arévalo) badala ya mshindi halali Miss Phillippines, Pia Alonzo Wurtzbach. Badala yake Hurvey akachemsha na kutaja jina tofauti.

Mara baada ya kutaja jina hilo watu wakainuka na kushangilia huku Gutierrez-Arévalo akipewa taji na rundo la maua. Lakini dakika chache baadaye watu walikumbwa na mshangao pale ambapo Miss Columbia akipunga mkono hakuchukua muda na furaha yake.


Harvey akarudi jukwaani akisema “Sikilizeni jamani wacha niwajibike kwa hili, hiki ndicho sahihi kilichoandikwa hapa. Ntawajibika kwa hili. Ni kosa langu, kosa bay asana, lakini ukweli na naweza kuwaonesha, ‘mshindi wa pili ni Miss Columbia’ ni kosa langu usiku huu”

Wakati huo Wurtzbach aliangalia bila kuamini. Kisha akamsogelea Gutierrez-Arévalo na kusimama kama mshindi wa mwaka jana, Paulina Vega, akavua taji kichwani mwa Miss Columbia na kulivaa.

Hata hivyo Harvey, aliomba radhi katika mtandao wa Twitter, kwa watazamaji wa televisheni kwa kuandika “ningependa kuomba radhi kwa watazamaji katika hilo kwa kuwaangusha. Kwa mara nyingiine tena ni kosa la kibinadamu”



RAIS MAGUFULI AKUTANA NA MAALIM SEIF IKULU DAR ES SALAAM

$
0
0



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekutana naMakamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharrif Hamad, leo tarehe 21 Desemba, 2015 Ikulu Jijini Dar es Salaam kufuatia maombi yake ya siku nyingi.

Mazungumzo ya Viongozi hao pia yamehudhuriwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Viongozi hawa kwa pamoja wamejadili hali ya kisiasa Zanzibar na wamefurahishwa na hali ya usalama na utulivu inayoendelea. Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, na viongozi wote wanaoshiriki katika mazungumzo ya kuleta hali ya uelewano Zanzibar.


Rais Magufuli pia amewapongeza na kuwashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kudumisha amani na utulivu wakati wa mazungumzo baina ya viongozi wa CUF na CCM yakiendelea huko Zanzibar.

Katika Mazungumzo hayo Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharrif Hamad amemueleza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya hali ya siasa Zanzibar kadiri anavyoielewa yeye na Rais Magufuli amemshukuru Makamu huyo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwa taarifa yake nzuri huku akimsihi waendelee na mazungumzo hadi suluhisho muafaka lipatikane.

Majadiliano yanayoendelea yanatoa fursa ya kudumishwa kwa utulivu na sifa njema ya nchi yetu. Wote kwa pamoja wamewaomba wananchi waendelee kuwa watulivu ili kutoa nafasi ya majadiliano yanayoendelea kufikia hatma njema. Wameelezea matumaini yao kuwa vyama vya CCM na CUF haviwezi kushindwa kupata suluhu ya mgogoro huo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemuhakikishia kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kuwa amani na utulivu unaendelea kudumishwa Zanzibar.

NEW MUSIC : FRANK MWANGOKA-SIRI (DOWNLOAD HAPA )

RAIS ASHIRIKI MAZISHI YA DADA WA RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE, MSOGA

$
0
0




Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji mke wa Rais Mtaafu Mama Salma Kikwete alipowasili kuhudhuria mazishi ya Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, dada wa Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015


Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Rais Mstafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi katika mazishi ya Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, dada yake kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015


Mbunge wa Chalinze Mhe Ridhiwani Kikwete akimlaki Rais Mstafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipohudhuria katika mazishi ya shangazi yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015


Mama Salma Kikwete akipewa pole na Mama Sitti Mwinyi katika mazishi ya wifi yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015


Mama Salma Kikwete akipewa pole na Mama Khadija Mwinyi katika mazishi ya wifi yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015




Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akimpokea Mama Janet Magufuli katika mazishi ya dada yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015


Mama Salma Kikwete akimpoke Mama Janet Magufuli katika mazishi ya wifi yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015




Rais John Pombe Joseph Magufuli akipokewa na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete alipowasili kuhudhuria mazishi ya dada yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015




Rais John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi alipowasili kuhudhuria mazishi ya dada yake Mhe Kikwete Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015. Kushoto ni Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Ghalib Bilal




Rais John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally alipowasili kuhudhuria mazishi ya dada yake Mhe Kikwete Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015




Mama Janet Magufuli (kulia) akiwa na wafiwa kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21, 2015




Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally akitoa hutba wakati wa mazishi




Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally akiongoza swala




Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo kaburini wakati wa mazishi ya dada yake Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, kijijini Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani Jumatatu Disemba 21




Rais Joseph Pombe Joseph Magufuli akiweka udongo kaburini




Rais Mstaafu Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiweka udongo kaburini




Ni wakati wa dua baada ya mazishi




Rais Joseph Pombe Joseph Magufuli na Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete wakiondoka makaburini baada ya mazishi. PICHA NA IKULU
Viewing all 3497 articles
Browse latest View live