↧
BRAND NEW MUSIC: JHIKOMAN - SET ME FREE (OFFCIAL MUSIC VIDEO)
↧
DC STAKI APONGEZA JAMII YA KIMASAI KUACHANA NA MILA POTOFU NA KUANZA KUMWABUDU MUNGU
Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule akisikiliza kwa makini maelezo ya mmoja ya wazee wa kabila la Kimasai kuhusu umuhimu wa elimu katika maeneo hayo
Dc Staki akisalimiana na viongozi wa dini walioendesha misa hiyo mara baada ya kuwasili katika viwanja hivyo
Dc Staki akishuhudia vijana wakipandisha Mori
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule akiwa kwenye sala wakati wa Misa
Dc Staki akifatilia kwa makini zoezi la kuingia hatua ya Uzee kwa waliokuwa vijana wa Kimasai
Na Mathias Canal, Kilimanjaro
Mkuu wa Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro Rosemary Staki Senyamule amewapongeza baadhi ya vijana wa kimasai kwa kuachana na imani potofu na hatimaye kuanza kumwabudu Mungu kwa kuhudhuria Misa mbalimbali katika makanisa.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu huyo wa Wilaya hiyo wakati wa sherehe maalumu kwa waliokuwa vijana wa Kimasai (Morani) kuingia hatua kubwa ya uzeeni na ya heshima katika kabila hilo.
Sherehe hiyo ilifanyika katika uwanja wa Kitongoji cha Endevisi, Kijiji cha Emuguru na ibada hiyo kuongozwa na Mchungaji Joshua Laiser kutoka kanisa la Kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) Wilaya ya Hai Dayosisi ya Moshi na Mchungaji Andrea Sangolo wa Usharika wa Bonde la Ruvu Same na baadaye kufuatiwa na shughuli za kutoa Baraka kwa vijana hao zoezi lililofanywa na viongozi wa dini, Serikali na Wazee wa Mila.
Sherehe hizo zimefanyika zikiwa na lengo la kufanya mageuzi kwa jamii ya kimasai na hatimaye kuachana na mila potofu kama vile kuabudu waganga wa jadi na kuanza kumuabudu Mungu wa kweli.
Pamoja na pongezi hizo za mkuu wa Wilaya ya Same kwa jamii ya kimasai kufanya mapinduzi hayo ya kuachana na mila potofu pia aliwataka kuwekeza zaidi kwenye swala la elimu na kuwataka kuwaruhusu watoto wote wa kiume na watoto wa kike kusoma kwa usawa.
Katika Jamii ya kimasai kumekuwepo na kadhia mbalimbali za mila Potofu za kuozesha watoto wadogo na kufanyiwa tohara kwa watoto wa kike, matukio ya ubabe ikiwemo wizi wa mifugo na mauaji kwa imani potofu jambo ambalo limezuiwa na Mkuu huyo wa Wilaya hiyo.
Dc Staki ametumia nafasi hiyo pia kuwataka wananchi wote wa jamii hiyo ya Kimasai kutumia rasilimali walizo nazo kwa kuuza kiasi ikiwemo Ng’ombe ili kujenga Hospitali zitakazo wasaidia kuimarisha afya zao na kujenga shule ambazo zitawaimarisha watoto wao kielimu.
Tukio hilo la Ibada kwa vijana hao ni kubwa katika historia ya kabila la Kimasai na limejumuisha jamii ya Kimasai kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo Tanzania na nchi jirani ya Kenya.
↧
↧
MASHINDANO YA MGIMWA CUP YAMEZINDULIWA RASMI NA DC WA MUFINDI JUMHURI WILIAMU

Mkuu wa Wilaya ya mufindi Jumhuri Wiliamu akipiga mpira katika eneo la penati kuashiria kuwa mashindano ya mgimwa cup yamezinduliwa rasmi

Mkuu wa Wilaya mufindi Jumhuri Wiliamu aliyeshika mpira kulia sambamba na mwenyekiti wa ccm mufindi yohanis kaguo aliyeshika mpira kushoto wakiwa na baadhi ya wachezaji
Na Fredy Mgunda,Iringa.
MASHINDANO ya kombe Mgimwa Cup yamezinduliwa rasmi katika kijiji cha Ikwea kata ya Ikwea wilayani mufindi mkoani Iringa kwa kushirikisha timu za vijiji vyote vya jimbo la mfundi kaskazini kwa lengo la kuinua vipaji wa wachezaji wa jimbo hilo.
Akizindua mashindano hayo yaliyofanyika Kiwanja cha Ikwea katika kijiji cha Ikwea mkuu wa wilaya Jumhuri Wiliamu kwa niaba ya Mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini alisema ni wakati mzuri kwa sasa kuyageukia mashindano ya mchangani kwani yamesheheni vipaji vingi vitakavyosaidia kuendeleza mpira wa Tanzania wakati ambapo taifa likiendelea kupata matokeo yasiyoridhishwa kwenye soka kwa sasa,
"Mashindano haya ni muhimu sana kwa wakati huu kwani yatasaidia kuinua vipaji vya vijana wetu na kuweza kupata timu bora ya taifa hivyo nidhamu ni muhimu wakati wa michezo hiyo" alisema Wiliamu
Aidha Wiliamu aliongeza kwa kusema kuwa mpira wa miguu umekuwa na faida kwa wachezaji kwani wanaweza kujitengezea vyanzo vya ajira kama mbwana samatta na wachezaji wengine walipwa vizuri saizi hapa nchini hata nje ya nchi.
“ Soka imewapa ajira mamilioni ya wachezaji na viongozi ulimwenguni na wameweza kuishi maisha ya kifahari kutokana na mishahara wanayopata”, alisema Wiliamu
Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano hayo Felix nyimbo aliwataka washiriki wa mashindano hayo kujituma ili ipatikane timu ya kata ambayo itakuwa ikiwakilisha kata hiyo katika mashindano ya wilaya, kanda hadi taifa.
“Mwaka huu tumekuja na wataalamu wanachagua vipaji maalumu kwaajili ya kujiunga na timu yetu ya kurugenzi ya mafinga na lengo likiwa ni kuhakikisha vipaji vyote vya jimbo la mufindi kaskazini vinaonekana na vinafika mbali kwa kuwa sasa mpira ni ajira si mnamuana mchezaji Mbwana Samatta”.alisema nyimbo
Kwa upande wake mlezi wa mashindano hayo mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (ccm) wilaya mufindi Yohanes Kaguo alisema ataendelea kwaunganisha vijana kupitia michezo na kusaidia kukuza mpira wa wilaya ya mufindi.
“Ilani ya chama cha mapinduzi inatutaka mwenyeviti kote nchini kuhakikisha michezo inafanyika mara kwa mara na kuleta tija kwa taifa ili tuondokane kuwa kuwa vichwa vya wendawazimu”alisema kaguo.
Mashindano ya mgimwa Cup ni miongoni mwa mashindano yanayolenga kuibua vipaji vya vijana vijijini ili kuwawezesha kupata nafasi ya kucheza katika vilabu vikubwa nchini.
![]()
Mkuu wa Wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza.
![]()
![]()
Mkuu wa Wilaya mufind Jumhuri Wiliamu akikagua timu kabla mtanange kuanza huku akiwapa neno wachezaji wa timu husika katika kiwanja cha Ikwea.

WANANCHI WANAKUBALI HATUA ZINAZOCHUKULIWA NA SERIKALI MPYA
Hususani kuhusu uondoaji wa wafanyakazi hewa,
Sera ya elimu bure na usimamishwaji wa watumishi wa serikali kutokana na makosa mbalimbali.
Lakini wananchi hawakubaliani na kuzuiwa uagizwaji wa sukari kutoka nje pamoja na bei elekezi ya sukari
15 Septemba 2016, Dar es Salaam: Uondoaji wa wafanyakazi hewa ulitajwa na asilimia 69 ya wananchi wa Tanzania, kama juhudi mojawapo ya Rais John Pombe Magufuli, wanayoifurahia sana. Elimu bure (asilimia 67) na usimamishwaji wa watumishi wa serikali (asilimia 61) navyo pia vilishika nafasi za juu. Walipoambiwa wataje vitendo ambavyo hawakubaliani navyo, asilimia 32 walitaja kuzuiliwa kwa uagizwaji wa sukari na bei elekezi ya sukari. Hatahivyo, asilimia 58 hawapingi kitendo chochote cha Rais. Kwa ujumla kiwango cha kukubalika kwa Rais Magufuli anakubalika na asilimia 96 ya wananchi. Kiwango hiki kinaendana na viwango vya kukubalika kwa marais wa Tanzania waliopita.
Pamoja na hayo, asilimia 88 ya wananchi wana imani kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi aliyoanza nayo, mpaka mwisho wa awamu yake ya uongozi.
Viwango vya kukubalika vya viongozi wengine wa serikali pia vipo juu Wananchi wanaonekana kumkubali mwenyekiti wao wa kijiji/mtaa (asilimia 78), diwani wao (asilimia 74) na mbunge wao (asilimia 68).
Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye utafiti uitwao Rais wa Watu? Tathmini na matarajio ya wananchi kwa serikali ya awamu ya tano. Muhtasari huu unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, ambao ni utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaotumia simu za mikononi. Matokeo haya yanatokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,813 kutoka maeneo yote Tanzania Bara (Zanzibar haihusiki kwenye matokeo haya) kati ya tarehe 4 Juni na tarehe 20 Juni 2016.
Wananchi wengi wanasema serikali ya awamu ya tano imeleta maboresho kwenye huduma nyingi za umma. Inayoongoza ni Mamlaka ya Mapato Tanzania ambapo asilimia 85 ya wananchi wanasema huduma zimeboreshwa chini ya serikali mpya. Wananchi pia wanasema huduma ni nzuri mashuleni (asilimia 75), vituo vya polisi (asilimia 74), mahakamani (asilimia 73), vituo vya afya (asilimia 72) na mamlaka za maji (asilimia 67). Ni vema ikafahamika kuwa takwimu hizi zinaonyesha mitazamo na maoni ya wananchi kuhusu huduma za umma na siyo lazima ikawa ndiyo hali halisi ya mabadiliko kwenye huduma hizo. Vilevile, karibu wananchi wote (asilimia 95) wanasema watumishi wa umma wanaotoa huduma, kama madaktari, walimu, pamoja na maofisa tawala wa umma wamekuwa wakiwajibika zaidi.
Hata hivyo, wananchi wenyewe wanakubali kuwa hawapati taarifa za kutosha kuhusu masuala muhimu ya kitaifa. Ni asilimia 4 tu wanaosema wanapata taarifa za kutosha kuhusu masuala ya siasa nchini na asilimia 9 tu wanasema wanapata taarifa kuhusu masuala yanayohusu afya na elimu. Hii inamaanisha kuwa maboresho yanayosemwa kuhusu huduma za umma yanatokana na uzoefu binafsi au kutoka vyanzo visivyo rasmi. Hatahivyo, wananchi wanatamani kupata taarifa kutoka katika sekta ambazo zinagusa maisha yao. Walipoulizwa masuala gani wangependa kumuuliza mwenyekiti wao wa kijiji, diwani au mbunge, masuala yanayohusu afya, elimu, maji na barabara yalijitokeza kama mambo muhimu. Kwa upande wa Rais Magufuli, wananchi wawili kati ya kumi (asilimia 18) wangependa kumuuliza kuhusu suala la mfumuko wa bei kwa bidhaa mbali mbali.
Mwenendo unaofanana umejitokeza pale wananchi walipoulizwa iwapo wanamfahamu au wameshazungumza na viongozi wao wa vijiji, wilaya na kitaifa. Karibu wananchi wote (asilimia 96) waliripoti kumfahamu Afisa Mtendaji wa Kijiji chao na karibu nusu yao (asilimia 47) walikuwa wameshawahi kuzungumza naye. Hatahivyo, asilimia 21 ya wananchi wanamfahamu Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya yao na asilimia 4 pekee wamezungumza naye.
Pamoja na kiwango kikubwa cha kukubalika kwa serikali ya awamu ya tano na Rais John Pombe Magufuli, wananchi wapo makini na kanuni za demokrasia na haki na wanataka zifuatwe. Wananchi nane kati ya kumi (au 80%) wanasema watendaji wa umma waondolewe pale tu panapokuwepo udhibitisho wa vitendo viovu. Asilimia 75 wanasema kuwa watendaji waondolewe pale wanaposhindwa kufanya kazi zao na siyo wanaposhindwa kufuata maagizo ya Rais. Pamoja na shauku yao juu ya uondoaji wa watumishi wa umma, wananchi wana maoni tofauti kuhusu matokeo ya kuwaondoa watumishi wa umma. Japokuwa asilimia 90 wanasema uondoaji wa watumishi hawa utawafanya watumishi wengine kuepuka vitendo viovu, asilimia 37 wanasema itawapunguzia morali watumishi wengine. Asilimia 48 wanasema uondoaji wa watumishi utawasababishia watumishi kutafuta njia mpya za kuficha maovu.
“Wananchi wana mitazamo chanya kuhusu utendaji wa serikali ya awamu ya tano pamoja na Rais Magufuli mwenyewe. Wanasema kuwa watumishi wa umma kwenye maeneo mbalimbali wanawajibika zaidi na kwamba wamegundua kuwa kuna maboresho kwenye huduma za umma. Hata hivyo wananchi wana mashaka kuhusu utaratibu unaotakiwa kufuatwa. Kwa mfano, wanataka udhibitisho wa vitendo viovu upatikane kwanza kabla ya watendaji kuwajibishwa, kulaumiwa ama kutiwa aibu. Vilevile wana mashaka kuhusu maamuzi ambayo yanaweza kugharimu fedha zao, kama kuzuia uingizwaji wa sukari. Hii inaonyesha kuwa wananchi hawatakuwa wakikubaliana na vitendo vyote vinavyofanywa na Rais bila kuhoji. Wananchi wanaendelea kuthamini misingi ya utawala bora unaozingatia sharia zilizopo,’ anasema Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza, Aidan Eyakuze.
“Jambo muhimu kuhusu matokeo haya”anaendelea Bwana Eyakuze, “ni kuwa matarajio ya wananchi yamebadilika. Kipindi cha nyuma kulikuwa na hali ya kutokujali miongoni mwa wananchi, uzoefu uliotokana na utendaji duni uliodidimiza matarajio yao, na matokeo yake yakichangia utendaji usioridhisha kuendelea. Lakini mabadiliko tunayoyaona hivi sasa yanaonyesha kuwa utendaji wa sekta ya umma unaweza kuimarika. Wananchi wanaweza kutarajia viwango vya juu zaidi kama utaratibu huu mpya ni wa kudumu.”
↧
JESHI LA POLISI KILIMANJARO LAWATUNUKU ZAWADI ASAKARI WAKE 34

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.
↧
↧
WAZIRI MWIGULU AFANYA ZIARA MWANZA NA KUAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA ASKARI NCHINI
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, alipofanya ziara kwenye makazi ya askari ya kigoto yalipopo Kata ya kirumba Manispaa ya Ilemela Jijini Mwanza hii leo.
Na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Wizara ya Mambo ya Ndani nchini imeahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazovikabili vyombo vya ulinzi na usalama ikiwemo uhaba wa makazi na sale za askari ili kufanikisha vyombo hivyo kufanya kazi kwa weledi na ufanisi mkubwa.
Waziri anayeshughulikia wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, ametoa agizo hilo hii leo kwenye kikao baina yake na viongozi mbalimbali wa vikosi vya Ulinzi na Usalama mkoani Mwanza, kilichofanyika kwenye gereza kuu la Butimba Jijini Mwanza.

Amesema jitihada za ujenzi wa nyumba za ghorofa kwa ajili ya makazi ya askari katika miji mikuu ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Dar es salaam zitaenda sambamba na ujenzi wa nyumba za kawaida katika wilaya mbalimbali nchini ili kutatua kero hiyo.
Katika hatua nyingine, Waziri Nchemba ametoa onyo la kukamatwa wale wote wanaotoa kejeli kwenye mitandao ya kijamii juu ya utendaji kazi wa vyombo vya ulinzi na usalama nchini pamoja na askari wanaopata madhara wakipambana na uhalifu, kama ilivyotokea katika tukio la mauaji ya askari lililotokea hivi karibuni Jijini Dar es salaam.
Awali Kamanda wa jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, amebainisha baadhi ya changamoto zinazolikabili jeshi hilo kuwa ni pamoja na ukosefu wa makazi ya askari, uhaba wa fedha pamoja na madeni ya askari, ambazo zikifanyiwa kazi zitaboboresha zaidi utendaji wa jeshi hilo.
Waziri Nchemba amefanya ziara ya siku moja mkoani Mwanza, akitokea mkoani Kagera alikoenda kujionea uhalibifu uliotokana na tetemeko la ardhi lililotokea mwanzoni mwa mwezi huu na kuzungumza na watendani mbalimbali wa taasisi za wizara yake, ambapo ametembelea makazi ya askari ya Kigoto na gereza kuu la Butimba Jijini Mwanza, kabla ya kuendelea na ziara yake hapo kesho mkoani Mara.

Mkuu wa Kituo cha Polisi Kirumba Ilemela Jijini Mwanza (kushoto) akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba (kulia) kwenye makazi ya askari Kigoto Jijini Mwanza. Katikati ni Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi.
Maofisa mbalimbali wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kwenye makazi ya skari Kigoto Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akiwa amembeba mmoja wa watoto kwenye makazi ya askari Kigoto Jijini Mwanza.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) akisalimiana na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, alipowasili kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.

Afisa wa polisi akitoa taarifa fupi kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, kushoto) alipowasili kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Ahmad Msangi, akizungumza kwenye kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba, akizungumza kwenye kikao baina yake na maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.

Baadhi ya Maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, wakiwa kwenye kikao baina yao na Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe.Mwigulu Nchemba kwenye Gereza la Butimba Jijini Mwanza hii leo.

NEW RELEASE: DIAMOND PLATNUMZ Ft. RYAVANNY - SALOME (TRADITIONAL OFFICIAL MUSIC VIDEO)
↧
MKUU WA MAJESHI GEN MWAMUNYANGE APOKEA UJUMBE TOKA CHINA

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (Kulia) akipokea zawadi ya nembo ya Jeshi la China kutoka kwa Mkuu wa Tawi la Ugavi wa China, Luteni Jenerali Liu Shengjie alipomtembelea ofisini kwake jana makao makuu ya jeshi jijini Dar es Salaam (Picha na Luteni Selemani Semunyu)

Mkuu wa Tawi la Ugavi wa Jeshi la China Luteni Jenerali Liu Shengjie akipokea zawdi ya nembo ya JWTZ kutoka kwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange (kulia) alipomtembelea ofisini kwake jana, Makao Makuu ya Jeshi jijini Dar es Salaam (Picha na Luteni Selemani Semunyu)

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunnyange akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa maofisa wa jeshi toka China ukiongozwa na Mkuu w Ugavi wa Jeshi hilo Luteni Liu Shengjie mara baada ya kumtembelea ofisini kwake Makao Makuu ya Jeshi jana jijini Dar Es Salaam. (Picha na Luteni Selemani Semunyu)
↧
DC MUHEZA APIGA MARUFUKU BODABODA KUENDESHWA ZAIDI YA SAA SITA
Mkuu wa wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo akizungumza na bodaboda wa wilaya hiyo ambapo alikutana nao na kuzungumza nao kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo ambapo alipiga marufuku kuendeshwa usiku zaidi ya saa sita.

Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza (Das) akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa wilaya hiyo,Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo aliyekaa kushoto na anayefuata ni Mwenyekiti wa Waendesha Boda Boda wilayani Muheza
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Muheza ambaye pia ni Afisa Biashara wa wilaya hiyo,Ally Mokiwa akielezea namna walivyojipanga kuhakikisha waendesha bodaboda hao wanakata leseni za kuendesha shughuli zao katikati ni Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo
wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Muheza, Hajat,Mhandisi Mwanasha Tumbo akimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Usalama Barabarani wilayani Muheza(DTO) Herbert Kazonde wakati wa mkutano huo na waendesha bodaboda uliofanyika kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani humo kulia ni Katibu Tawala wa wilaya ya Muheza.
Katibu wa Chama cha Waendesha Boda Boda wilayani Muheza,Francis Gerald akizungumza katika mkutano huo kuhusu changamoto ambazo zinawakabili
Baadhi ya waendesha bodaboda wilayani Muheza wakimsikiliza Mkuu wa wilaya ya Muheza,Hajat Mhandisi Mwanasha Tumbo alipokuwa akizungumza nao kusisitiza umuhimu wa wao kutii sheria za usalama barabarani ikiwemo kuacha kufanya vitendo vya uhalifu
Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimepaki kwenye uwanja wa Jitegemee wilayani Muheza huku madereva wakiwa kwenye kikao chao na Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi,Hajat Mwanasha Tumbo
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
↧
↧
MBUNGE PETTER MSIGWA AKABIDHI MADAWATI 537 YA JIMBO LA IRINGA MJINI
MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati 537 akiwa na meya wa manispaa ya iringa Alex Kimbe
NA FREDY MGUNDA,IRINGA
MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa amekabidhi madawati hayo 537 ambayo ameyatoa katika jimbo lake yataweza kuwa mkombozi mkubwa kutokana na kuweza kuwasaidia wanafunzi waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya kusoma katika mlundikano mkubwa na baadhi yao walikuwa wanakaa chini ya sakafu.
Aidha Msigwa katika hotuba yake ya kukabidhi madawati hayo amewataka viongozi wa manispaa ya iringa na tabia ya kuhujumu na kuiharibu miundombinu ya shule na badala yake wahakikishe wanatunza mali zote za serikali kwa lengo la kuweza kuwasaidia watoto wengine wa vizazi vijavyo waweze kusoma katika mazingira mazuri.

“Sipendi kuona wanafunzi wanaosoma katika shule za jimbo langu wanakaa chini,kitendo hicho huwa kinaniumiza sana ndio maana nimeamua kupambana kutafuta madawati ili kufanikisha adhima yangu ya kukuza elimu kwa wanafunzi wa jimbo la iringa mjini”alisema Msigwa
Naye meya wa halmashauri ya manispaa ya iringa Alex Kimbe amesema kwamba kwa sasa hawana mapungufu yoyote ya madawati hivyo hakutakuwa na changamoto ya mwanafunzi wake kujisomea wakiwa wamekaa chini ya sakafu.
MADAWATI hayo 537 ambayo yametolewa na ofisi ya Mbunge wa Iringa Mjini yamegharimu kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 60 yatasambazwa katika kata zote ambapo pia yataweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuwaondolea adha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto hiyo kwa kipindi cha muda mrefu na hatimaye kuongeza kiwango cha ufaulu.

Lakini tatizo la kupanda na kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika baadhi ya shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya manispaa ya iringa lilikuwa linasababishwa na wanafunzi wengine kujisomea wakiwa wamekaa chini ya sakafu sambamba na kuwepo katika mazingira ya miundombinu ambayo sio rafiki kwao hivyo kujikuta wanashindwa kutimiza malengo yao.
Hayo yamebainishwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari na shule za msingi katika manispaa ya iringa.
Wanafunzi hao akiwemo Ayoub Joseph,Paul Kisige pamoja na Riziki Ismail walisema kwamba kitendo cha baadhi yao kujisomea wakiwa sakafuni kimepelekea kupunguza uwezo wa kifikiri na kujikuta wanafanya vibaya katika masamo yao na kushindwa kufaulu, hivyo wamempongeza mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji Petter Msingwa kwa juhudi wanazozifanya za kupambana na adha ya madawati.
“Hapo mwanzoni kwa kweli hali ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu wanafunzi wengine walikuwa wanasoma wakiwa wanakaa chini ya sakafu na hii kiukweli unamwondolea kabisa uwezo wa kufanya vizuri mwanafunzi, lakini kutokana na agizo hili la Rais tumepata nafuu kubwa na wanafunzi tuna imani tutaweza kufanya vizuri katika masomo yetu, na pia tunampongeza mbunge wetu kwa juhudi zake za kutuletea madawati,”walisema wanafunzi hao.
Pia walisema kwamba pamoja na changamoto ya kuwepo kwa upungufu wa madawati lakini serikali inatakiwa kuhakikisha inatilia mkazo suala linguine la nyumba za walimu pamoja na kuimarisha mambo mengine ya msingi, kama kuongeza madarasa mwengine ili kuweza kuepukana na mlundikano kwa wanafunzi.
MBUNGE wa Jimbo la Iringa mjini mchungaji Petter Msigwa akikabidhi madawati 537 akiwa na meya wa manispaa ya iringa Alex KimbeHayo yamebainishwa na baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari na shule za msingi katika manispaa ya iringa.
Wanafunzi hao akiwemo Ayoub Joseph,Paul Kisige pamoja na Riziki Ismail walisema kwamba kitendo cha baadhi yao kujisomea wakiwa sakafuni kimepelekea kupunguza uwezo wa kifikiri na kujikuta wanafanya vibaya katika masamo yao na kushindwa kufaulu, hivyo wamempongeza mbunge wa jimbo la iringa mjini mchungaji Petter Msingwa kwa juhudi wanazozifanya za kupambana na adha ya madawati.
“Hapo mwanzoni kwa kweli hali ilikuwa ni ngumu sana kwa sababu wanafunzi wengine walikuwa wanasoma wakiwa wanakaa chini ya sakafu na hii kiukweli unamwondolea kabisa uwezo wa kufanya vizuri mwanafunzi, lakini kutokana na agizo hili la Rais tumepata nafuu kubwa na wanafunzi tuna imani tutaweza kufanya vizuri katika masomo yetu, na pia tunampongeza mbunge wetu kwa juhudi zake za kutuletea madawati,”walisema wanafunzi hao.
Pia walisema kwamba pamoja na changamoto ya kuwepo kwa upungufu wa madawati lakini serikali inatakiwa kuhakikisha inatilia mkazo suala linguine la nyumba za walimu pamoja na kuimarisha mambo mengine ya msingi, kama kuongeza madarasa mwengine ili kuweza kuepukana na mlundikano kwa wanafunzi.
↧
BRAND NEW MUSIC VIDEO: MORGAN HERITAGE - SELAH (WACTH HERE)
↧
RC KILIMANJARO SAIDI MECK SADICK ATEMBELEA KIWANDA CHA TANGAWIZI
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadick akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wake wa kazi alipozuru wilaya ya Same
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadick akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wilaya ya Same kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki akitoa salamu kwa wajumbe wa kamati ya ulizni na usalama na salamu za kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadick alipotembelea Wilayani hapo
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadic kakikagua mashine katika kiwanda cha Tangawizi kilichopo kata ya Miyamba Wilayani Same
Na Mathias Canal, Kilimanjaro
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick amezuru katika kiwanda cha Tangawizi kilichopo kata ya Miyamba Wilayani Same.
Sadick ametembelea kiwandani hapo akiwa ba dhamira ya kukifufua kiwanda hicho ili kianze kufanya kazi ya izalishaji katika kiwango cha juu ili kwenda sawia na kasi ya Maendeleo inayohitaji kwa wananchi wa eneo hilo sambamba na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara alisema kuwa uongozi wa kiwanda hicho pia unapaswa kutunza vyanzo vya maji lakini pia kuchemsha maji ya kunywa ili kuepukana na Maradhi mbalimbali yatokanayo na unywaji wa maji yasiyo safi na salama.
Katika sekta ya elimu amesema kuwa ni dhahiri kuwa miundombinu ya shule inapaswa kuboreshwa ili waalimu wakae kwenye vituo wanavyopangiwa na kuachana na tabia ya kuhamahama.
Rc Sadick amezungumzia pia mimba za utotoni ambapo amewataka wananchi kuwaacha watoto wa kike waweze kusoma ili baadae wasiwe tegemezi tofauti na ilivyo sasa anbapo wazazi wengi wanawaozesha wabinti wakiwa na umri mdogo jambo ambalo ni kinyume kabisa na utaratibu wa ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa.
Kabla ya mkutano huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick, Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same walifanya mazungumzo na Bodi ya uongozi wa Ushirika wa kiwanda hicho na kuwataka waongeze juhudi kuhakikisha wakulima wa Tangawizi hawapati hasara tena.
Rc Sadick ameutaka uongozi wa viwanda vidogo vidogo SIDO ambao ndio wenye mitambo iliyofungwa kiwandani hapo kuboresha mashine hizo ambazo kwa sasa zinatumia OIL chafu kuhamia kwenye umeme ili kiwanda kiwe rafiki kwa mazingira pia.
Zao la Tangawizi linalimwa sana katika Kata hiyo ya Miyamba hivyo kufufuliwa kwa kiwanda hicho kutaleta mapinduzi makubwa katika uchumi wa mwananchi mmoja mmoja pamoja na kuongeza ajira kwa wakazi wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadick akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Wilaya ya Same kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki
Wananchi wakisikiliza kwa makini mkutano wa mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
Mkuu wa Wilaya ya Same Mhe Rosemary Staki akitoa salamu kwa wajumbe wa kamati ya ulizni na usalama na salamu za kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadick alipotembelea Wilayani hapo
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadic kakikagua mashine katika kiwanda cha Tangawizi kilichopo kata ya Miyamba Wilayani Same
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadick akipokea maelezo kuhusu mashine hizo
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Meck Sadickalipokagua mfereji wa Mshana
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick amezuru katika kiwanda cha Tangawizi kilichopo kata ya Miyamba Wilayani Same.
Sadick ametembelea kiwandani hapo akiwa ba dhamira ya kukifufua kiwanda hicho ili kianze kufanya kazi ya izalishaji katika kiwango cha juu ili kwenda sawia na kasi ya Maendeleo inayohitaji kwa wananchi wa eneo hilo sambamba na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza na wananchi kwenye Mkutano wa hadhara alisema kuwa uongozi wa kiwanda hicho pia unapaswa kutunza vyanzo vya maji lakini pia kuchemsha maji ya kunywa ili kuepukana na Maradhi mbalimbali yatokanayo na unywaji wa maji yasiyo safi na salama.
Katika sekta ya elimu amesema kuwa ni dhahiri kuwa miundombinu ya shule inapaswa kuboreshwa ili waalimu wakae kwenye vituo wanavyopangiwa na kuachana na tabia ya kuhamahama.
Rc Sadick amezungumzia pia mimba za utotoni ambapo amewataka wananchi kuwaacha watoto wa kike waweze kusoma ili baadae wasiwe tegemezi tofauti na ilivyo sasa anbapo wazazi wengi wanawaozesha wabinti wakiwa na umri mdogo jambo ambalo ni kinyume kabisa na utaratibu wa ndoa kwa mujibu wa sheria ya ndoa.
Kabla ya mkutano huo Mkuu huyo wa Mkoa wa Kilimanjaro Said Mecky Sadick, Mkuu wa Wilaya ya Same Rosemary Staki Senyamule na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Same walifanya mazungumzo na Bodi ya uongozi wa Ushirika wa kiwanda hicho na kuwataka waongeze juhudi kuhakikisha wakulima wa Tangawizi hawapati hasara tena.
Rc Sadick ameutaka uongozi wa viwanda vidogo vidogo SIDO ambao ndio wenye mitambo iliyofungwa kiwandani hapo kuboresha mashine hizo ambazo kwa sasa zinatumia OIL chafu kuhamia kwenye umeme ili kiwanda kiwe rafiki kwa mazingira pia.
Zao la Tangawizi linalimwa sana katika Kata hiyo ya Miyamba hivyo kufufuliwa kwa kiwanda hicho kutaleta mapinduzi makubwa katika uchumi wa mwananchi mmoja mmoja pamoja na kuongeza ajira kwa wakazi wa maeneo hayo na Taifa kwa ujumla.
↧
DC HANDENI.MH GONDWE AFANIKIWA KUTATUA MGOGORO WA MPAKA WILAYANI HANDENI
Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Gdwin GOndwe akisalimiana na mkazi wa kijiji cha nyasa.
Mkuu waa Wilaya ya Handeni,Mh Godwin Gondwe Jana alifanikiwa kusuluhisha mgogoro wa mpaka uliokuwa ukivihusisha vijiji viwili vya kata ya kang'ata wilayani Handeni .Vijiji hivyo ni Madebe na Nyasa ambao walikua hawafahamu mpaka wao unaishia wapi,suluhu hiyo ilifanikiwa kumalizwa na mkuu wa wilaya na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Handeni ,Bwa.William Makufwe.
DC Gondwe pia aliwataka wananchi na viongozi wajikite katika shughuli za kimaendeleo badala ya kujikita kwenye suala la mipaka ,Kwa madai wapate maeneo ya kulima wakati wakigombania maeneo ili wauze. Amewaonya wasiuze ardhi kiholela na kufanya vizazi vijavyo kuwa watumwa kwenye ardhi yao.Mkuu wa wilaya Mh.Godwin Gondwe akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Handeni,Ndugu William Makufwe (pichani kushoto) akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa vijiji vya nyasa na madebe.Mwenyekiti wa kijiji cha nyasa na madebe wakipeana pongezi baada ya kujua mipaka yao huku wakisistizwa kujikita zaidi katika masuala ya maendeleo.Mkuu wa wilaya ya Handeni Mh. Gondwe akipeana mkono wa pongezi na Mwenyekiti wa kijiji cha Nyasa baada ya kupata mpaka wa maeneo yao.Mkuu wa wilaya ya handeni Mh.Gondwe akizungumza na wananchi wa vijiji vya nyasa na madebe akiwakataza wasiuze ardhi kiholela na wasigombanie maeneo ili wayauze.

MKUU WA WILAYA YA MPWAPWA AMSIMAMISHA KAZI MKUU WA CHUO CHA MAENDELEO YA WANANCHI (FDC)-CHISALU
Na Mathias Canal, Dodoma
Mkuu wa Chuo cha Maendeleo ya wananchi (FDC)-CHISALU amekalia kuti kavu mara baada ya kubainika kuwa ameruhusu udahili wa wanafunzi wanaosoma fani ya utaalamu wa Kilimo na Mifugo ilihali chuo hicho ni maalumu kwa ajili ya mafunzo ya utaalamu wa Maendeleo ya jamii (Community Development).
Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa Mhe Jabir Shekimweri amemsimamisha kazi Mkuu huyo kutokana na kupokea malalamiko ya baadhi ya wanafunzi chuoni hapo ambapo malalaniko yao yamekuwa na hoja za msingi zilizopelekea kuibuka kwa kadhia mbalimbali zinazofanywa na chuo hicho.
Katika kutaka kubaini udhaifu unaohusu utendaji wa uongozi wa chuo hicho Dc Shekimweri alisikiliza hoja za wanafunzi chuoni hapo ambapo walitaka kujua sababu zinazopelekea wao kufanya mtihani unaoandaliwa na Chuo cha Ufundi VETA ilihali mtaala wao sio wa VETA.
Mbali na kadhia hiyo wanafunzi hao wamehoji pia fani ya kilimo wanafunzi hao wanayosoma ya Kilimo na Mifugo ambayo haitakiwi kwa mujibu wa taratibu pia haina namba ya mtihani (Exam Code) hivyo ni kwa kiasi gani wanafunzi hao watahakikishiwa ajira kama maafisa Mifugo pindi wamalizapo masomo yao.
Dc Shekimweri alizuru Chuoni hapo kwa lengo la kutaka kujua hatma ya wanafunzi wa chuo hicho kufungwa pasina sababu ndipo alipobaini uongo uliotumiwa na Mkuu wa Chuo hicho kwa kudai kuwa chuo kimefungwa kwa sababu ya kujiandaa na mitihani ambapo hata hivyo mtihani huo unataraji kufanyika Oktoba 10, 2016.
Mkuu wa chuo hicho alieleza kuwa chuo hicho kitafungwa hadi Tarehe 9/10/2016 siku moja kabla ya kufanyika kwa mitihani ambapo janja hiyo ilibainiwa na Mkuu wa Chuo kwa kudanganywa ratiba ya mtihani huo ambayo inaonyesha kuwa tarehe 26/09/2016 ndipo ambapo mtihani huo unataraji kuanza.
Hata hivyo Mkuu huyo wa chuo hicho amefunga chuo hicho pasina kushirikisha Bodi ya Chuo ambapo pia alihoji sababu za kudanganywa kufungwa chuo hicho bila maamuzi ya kusitisha kufanyika kwa mitihani ambapo ratiba yake imekwisha tolewa jambo ambalo lilimuacha mdomo wazi Mkuu huyo wa Chuo hicho.
Kutokana na kadhia hizo Dc Shekimweri amemsimamisha kazi Mkuu wa chuo hicho kwa kutumia uongo wakati wa kujitetea na kushindwa kitekeleza majukumu yake kikamilifu ikiwemo kutoitisha vikao vya Bodi, Kutosikiliza kero za wanafunzi hata alipojulishwa kwa maandishi na wanafunzi hao, kufunga chuo kwa dharula ilihali tatiba ya mtihani inaendelea na kuwashauri vibaya wanafunzi kuhusu hatima yao kutokana na mkanganyiko wa mtaala.
Dc Shekimweri alisema kuwa serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli inahubiri zaidi uwajibikaji hivyo maamuzi hayo yanatuma salamu ili mamlaka ya uteuzi ifuatilie na kushughulikia tuhuma dhidi yake na kuchukua stahiki za kisheria.
Mkuu huyo wa Wilaya amesitisha Bodi ya chuo na kumtaka mwenye mamlaka nanuteuzi wa Bodi aivunje Bodi hiyo kwa kushindwa kukutana hata mara moja tangu bodi hiyo ilipoanzishwa Mwaka 2013hivyo kushindwa kitafsiri na kusimamia Dira kwenye mpango mkakati (Strategic Plan) pia kutokuwa na kalenda ya mwaka wa taaluma.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya pia alihoji pasina kupatiwa majibu kuhusu uidhinishwaji wa mpango wa bajeti wa chuo kuhusu anayeufanya ilihali Bodi haikutani kwa ajili ya vikao.
Dc Shekimweri alienda mbali zaidi kwa kutaka kujua vipi vipaombele vya chuo, mabadilko na mitaala, mafanikio na changamoto za chuo vinajadiliwa na kufikiwa maamuzi na watu gani iwapo Bodi haikutani kujadili.
Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya ya Mpwapwa alisema Changamoto za mitaala, Udahili na mtihani pamoja na vyeti vya kuhitimu litafanyiwa kazi kwenye Mamlaka husika (VETA) na Wizara ya Maendeleo ya Jamii.

TANESCO YAWAOMBA RADHI WATEJA WA KINONDONI KASIKAZINI
SHIRIKA la Umeme Tanzania ( TANESCO) linapenda kuwataarifu wateja wake wa
Mkoa wa Dar es Salaam kuwa leo Jumamosi tarehe 24/09/2016 kumetokea hitilafu katika Kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza Umeme cha Ubungo 220kV/ 132kV na kusababisha kukosekana Umeme kwenye maeneo ya jiji la Dar es Salaam yanayotegemea Vituo vya Kumduchi na Makumbusho.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu jijini mapema leo, tayari hatua za kurekebisha hitilafu hiyo zinaendelea kuchukuliwa ambapo mafundi wa TANESCO wanaendelea na kazi ya kurekebisha hitilafu hiyo na umeme utarejea masaa machache yajayo.
Taarifa hiyo inawaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu wowote utakaojitokeza.

MIRADI 45 KUZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU MKOANI TABORA
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri (Kulia)
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe akisoma Risala wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru
Baadhi ya wakuu wa Wilaya za mkoa wa Tabora wakiulaki mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Mkoani humo
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri akisoma Risala wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru
Kutoka Kushoto ni Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Ikungi Bw Dandala Mzunguor, Katibu wa Mkuu wa Mkoa wa Singida Fute Martin, Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe, na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu wakijadili jambo muda mchache kabla ya makabidhiano ya Mwenge wa uhuru
Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanriakimkabidhi Mwenge wa Uhuru mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe john Mwaipopo kwa ajili ya kushirikiana na wakimbiza Mwenge Kitaifa kuukimbiza Wilayani humo
Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji jumanne Mtaturu, Mkuu wa Wilaya ya Manyoni Geofrey Mwambe,Mkuu wa wilaya ya Iramba Emmanuel Uhahula, Mkuu wa wilaya ya Iramba, Injinia Masaka John Masaka, Mkuu wa wilaya ya Singida Elias Choro Tarimo
Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew J. Mtigumwe, kulia ni Mkimbiza Mwenge Kitaifa George J. Mbijima
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew J. Mtigumwe akimuaga Mkimbiza Mwenge Kitaifa lucia Vitalis kutoka Manyara mara baada ya kumaliza ziara ya Mwenge katika Mkoa wa Singida na kuanza ziara Mkoani Tabora
Na Mathias Canal, Tabora
Mwenge wa Uhuru umewasili Mkoani Tabora ambapo unatarajiwa kuzindua miradi 45 yenye thamani ya shilingi Bilioni ishirini na tatu, Milioni nne, laki nne elfu na arobaini na saba mia tano sitini na sita 23,004,447,566/= ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 40% ukulinganisha na miradi ya mwaka 2015 iliyokuwa na thamani ya shilingi 9,207,720,213.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru katika Kijiji cha Mgongolo, Kata ya Igunga, Wilayani Igunga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri amesema kuwa sera ya Vijana Tanzania ya Mwaka 2007 inatambua kuwa vijana ni watu wote wenye umri wa miaka 15-35 ambapo kulingana na sensa ya Mwaka 2012 inaonyesha kuwa Mkoa huo una jumla ya vijana 439,455 hivyo hekari 681 zimetengwa kwa ajili ya shughuli za vijana ili kukidhi kauli mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2016.
Mwanri alisema kuwa Mwaka 2015 Mwenge wa Uhuru mkoani Tabora ulikimbizwa katika Halmashauri 7 zilizokuwepo ambapo Mwaka huu utakimbizwa katika Halmashauri 8 ambazo ni Igunga, Nzega Mji, Tabora Vijijini (Uyui), Sikonge, Urambo, Kaliua, Tabora Manispaa na Nzega Vijijini.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe Aggrey Mwanri mara baada ya kukabidhiwa Mwenge huo naye amemkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga Mhe John Mwaipopo ili aukimbize katika Miradi iliyopangwa ukiwemo wa kuzindua Mradi wa maji Vijijini, Kufungua vyumba viwili vya madarasa na choo cha matundu 10 katika Shule ya Sekondari Mwayunge, Kuweka Jiwe la msingi katika Hoteli ya Mjasiriamali Zengo T. Kija, Kuzindua mradi wa Kilimo cha bustani na Ufugaji wa samaki wa kikundi cha Vijana cha Msongela, na Kuzindua zahanati ya Kijiji cha Igogo.
Miradi mingine ambayo Mwenge wa Uhuru utazuru ni pamoja na kugawa kadi za CHF kwa wanachama wapya, Kugawa vyandarua kwa wananchi na baadaye utazuru katika Shule ya Sekondari Nanga.
Akizungumza wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru kwa uongozi wa Mkoa wa Tabora, Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Mathew J. Mtigumwe amewashukuru wananchi wa Mkoa wa Singida kwa kujitokeza kwa wingi kutokana na juhudi na ushiriki wao kwenye kuibua, Kutekeleza na Kusimamia miradi mbalimbali ambapo pia amewataka wananchi hao kwa umoja wao kuitunza miradi hiyo.
Mtigumwe alisema kuwa tangu Mwenge wa Uhuru ulipokabidhiwa Mkoani Singida ukitokea Mkoani Dodoma Septemba 17, 2016 umepita kwenye miradi 61yenye thamani ya Shilingi 14,266,628,518 iliyopo katika Halmashauri saba ambayo ni pamoja na Mradi wa elimu, Afya, Maji, Barabara, Biashara, Mazingira, Kilimo, Mifugo, Ushirika na programu mbalimbali za mapambano dhidi ya Rushwa, Dawa za Kulevya, Ukimwi na Malaria.
Mtigumwe alisema kuwa mbali na Mwenge wa Uhuru kupita kwenye Miradi mbalimbali Mkoani Singida Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa amewaongoza wakimbiza Mwenge wenzake kitoa ujumbe wa Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2016 ambao ni "Vijana ni nguvu kazi ya Taifa, Washirikishwe na kuwezeshwa" Vile vile, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa amesisitiza umuhimu wa vijana na wananchi wote kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya Rushwa, Dawa za kulevya, Kuchukua hatua dhidi ya tabia hatarishi zinazoweza kuchochea maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi na kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria.

MUHIMBILI YAPOKEA MSAADA WA RUNINGA
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kibosho (UVIKI) Bw. Sevelin Mushi wa kwanza kulia akimkabidhi ungo wa king’amuzi cha azam Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha kushoto kwa ajili ya wodi ya wazazi wakati wa hafla fupi ya kuchangia damu katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kibosho (UVIKI) Bw. Sevelin Mushi wa kwanza kulia akimkabidhi luninga Afisa Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano MNH, Aminiel Aligaesha kushoto kwa ajili ya wodi ya wazazi wakati wa hafla fupi ya kuchangia damu katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kibosho (UVIKI) Bw. Marceli mushi akichangia damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakati wa hafla fupi ya kuchangia damu katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Kibosho (UVIKI) Bw. Sevelin Mushi akichangia damu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) wakati wa hafla fupi ya kuchangia damu katika hospitali hiyo leo jijini Dar es salaam.
↧
↧
VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA ZILIZOPO KUJIAJIRI
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Dk Leornad Akwilapo amewataka vijana kutafuta ajira sehemu mbalimbali kwa kutumia fursa zilizopo badala ya kutegemea fursa za serikali.
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, iliyolenga kuweka mkakati wa pamoja kati ya wadau wa elimu, serikali katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu lengo la nne.
Alisema kwamba ni imani yake kwamba elimu waliyonayo vijana inawaruhusu kufanya shughuli mbalimbali ambazo si lazima kuajiriwa na serikali. Alisema hakuna nchi duniani ambayo inaweza kuajiri kila mmoja lakini elimu zinazotolewa pamoja na ya Tanzania zinawaandaa vijana kujiajiri wenyewe.
Akizungumzia warsha hiyo alisema kwamba wadau wanakutana kutengeneza mkakati wa pamoja wa kutoa elimu bora kwa wananchi wa Tanzania na namna ambavyo malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) yanavyoshirikishwa katika utoaji elimu.
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, Makuru Petro akiwasilisha mada wakati wa kongamano lililoshirikisha Serikali pamoja na wadau mbalimbali kujadili ni kwa jinsi gani wanatengeneza mkakati bora ili kuweza kuisaidia serikali kutoa elimu bora na bila ubaguzi wa aina yoyote.![]()
Afisa Elimu Mkuu Hilda K. Mkandawire kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia akiwasilisha mada wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa sekta ya elimu wakifuatilia kwa makini mkutano uliokuwa unaendelea.![]()
![]()
![]()
Criana Connal kutoka UNESCO akizungumza jambo wakati wa warsha iliyowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu ili kujadili mpango mkakati utakaosaidia kuinua kiwango cha elimu nchini Tanzania.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Wanawake (UNWOMEN), Maria Karadenizli (kushoto) akizungumza jambo na Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues wakati wa kongamano lililowakutanisha wadau mbalimbali wa elimu.
Mkutano ukiendelea.
Baadhi ya makundi ya wadau wa sekta ya elimu wakijadiliana ili kutengeneza mpango mkakati wa pamoja kati ya serikali na wadau mbalimbali wa elimu utakaosaidia serikali kutoa elimu bila ubaguzi wa aina yoyote na kwa makundi yote ili kufanikisha lengo namba nne la Mpango wa maendeleo endelevu (SDG’s) linalohusu elimu bora kwa wote.![]()
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua warsha iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni UNESCO, iliyolenga kuweka mkakati wa pamoja kati ya wadau wa elimu, serikali katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu lengo la nne.
Alisema kwamba ni imani yake kwamba elimu waliyonayo vijana inawaruhusu kufanya shughuli mbalimbali ambazo si lazima kuajiriwa na serikali. Alisema hakuna nchi duniani ambayo inaweza kuajiri kila mmoja lakini elimu zinazotolewa pamoja na ya Tanzania zinawaandaa vijana kujiajiri wenyewe.
Akizungumzia warsha hiyo alisema kwamba wadau wanakutana kutengeneza mkakati wa pamoja wa kutoa elimu bora kwa wananchi wa Tanzania na namna ambavyo malengo ya maendeleo endelevu (SDG’s) yanavyoshirikishwa katika utoaji elimu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leornad Akwilapo akifungua warsha ya kutengeneza mkakati mmoja kati ya serikali na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu uliondaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) unaofanyika kwa siku mbili katika ukumbi wa NACTE jijini Dar es Saalam.
Alisema lengo la nne la Maendeleo endelevu la Umoja wa Mataifa linasisitiza elimu bora isyokuwa ya kibaguzi kwa watu wote na hivyo mkutano wao ni kuangalia namna wanavyoweza kushirikiana kutoa elimu bora inayowezesha watu wake kujiajiri.
Alisema kwamba mtazamo huo ambao tayari Tanzania ilikuwa nao miaka ya mwanzo ya uhuru ambapo kulikuwa na kisoma cha watu wazima kitu ambacho kilillenga kuwafanya watu kuwa na elimu ya kutosha kuhusu mazingira yao na maisha yao. Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa UNESCO nchini Tanzania, Zulmira Rodrigues alisema kwamba wameandaa warsha hiyo kwa lengo la kuelezana utoaji bora wa elimu ambao utaendana na matakwa ya sasa ya kumwezesha anayepata elimu hiyo kujiajiri mwenyewe. Aidha amesema lengo la kushirikisha wadau wa elimu ni kuhakikisha kwamba lengo la maendeleo endelevu la nne la Umoja wa Mataifa linashirikishwa katika utoaji elimu kwani lengo hilo ni kuhakikisha elimu kwa wananchi wote bila ubaguzi huku hatua zikichukuliwa katika kuwezesha wanawake kusonga mbele.
↧
WASHIRIKI KUTOKA BURUNDI NA RWANDA WAZICHAPA LIVE KATIKA MAISHA PLUS
Katika hali isiyotarajiwa katika kijiji cha Maisha Plus, jana washiriki wawili, KAREKEZI Jean kutoka Rwanda na BASWARI Nibigira kutoka Burundi walipigana hadharani huku wakirekodiwa na camera zilizofungwa kijijini hapo.
Ilikua hivi;
SOLANGE kawakuta KAREKEZI na PATRICK wamekaa wanapiga stori akawaambia kwamba BASWARI alikua anamsema KAREKEZI kwa watu.
KAREKEZI hakuonyesha kufurahishwa na ile hali, akapata hasira, PATRICK akachochea, akamwambia asikubali kudharauliwa, lazima akapigane. "Muacheni, kwani nyie hamjui BASWARI anavyojifanya anajua kila kitu?" SOLANGE akahoji.
PATRICK akaendelea kushauri kwamba KAREKEZI asikubali kuliacha liishie hapo.. Akampige BASWARI. Baada ya kuona KAREKEZI anashawishika kwenda kupigana
SOLANGE akamzuia asiende ili isijulikane kwamba yeye ndio ameleta hizo taarifa.
KAREKEZI akiwa amekasirika akasema, "Mimi sipendi dharau... awe anawadharau nyie wanawake sio sisi wanaume."
PATRICK akazidi kuchochea.. 'Nenda kampige asituchukulie hivyo... Kwanini atuseme vibaya?'
SOLANGE: "Usimdanganye mwenzio aende kupigana... Be gentle, men can't act like that... be gentle..''
Baada ya kuona mambo hayataishia pale, SOLANGE akaomba wasiseme kama yeye ndio ameleta hayo maneno.
KAREKEZI akamfuata BASWARI. Akamshika. BASWARI naye akamshika. Wakavutana. KAREKEZI akamwambia BASWARI, "Usiwe unaingilia maisha yangu, haunijui, wala sipendi unavyonisema kwa watu..."
KAREKEZI akamtukana BASWARI kwa kifaransa.
Ugomvi ukaendelea kwa muda.
SOLANGE akakasirika akatoka eneo la tukio akaona kama amesalitiwa... "Kwanini umenifanyia hivi, watu wakijua mimi ndio nimesema hayo maneno nitakua na bad image kwenye society.."
"Unaharibu reputation yetu kwa kugombana kijijni."
BABU hapendagi Ujinga. Kuna kikao cha kijiji asubuhi hii. Mjadala mkali unaendelea juu ya hatima ya hawa washiriki. Tukutane Azam Two saa 3.30 usiku kujua kitakachojiri.![]()
#VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu
PATRICK akazidi kuchochea.. 'Nenda kampige asituchukulie hivyo... Kwanini atuseme vibaya?'
SOLANGE: "Usimdanganye mwenzio aende kupigana... Be gentle, men can't act like that... be gentle..''
Baada ya kuona mambo hayataishia pale, SOLANGE akaomba wasiseme kama yeye ndio ameleta hayo maneno.
KAREKEZI akamfuata BASWARI. Akamshika. BASWARI naye akamshika. Wakavutana. KAREKEZI akamwambia BASWARI, "Usiwe unaingilia maisha yangu, haunijui, wala sipendi unavyonisema kwa watu..."
KAREKEZI akamtukana BASWARI kwa kifaransa.
Ugomvi ukaendelea kwa muda.
SOLANGE akakasirika akatoka eneo la tukio akaona kama amesalitiwa... "Kwanini umenifanyia hivi, watu wakijua mimi ndio nimesema hayo maneno nitakua na bad image kwenye society.."
"Unaharibu reputation yetu kwa kugombana kijijni."
BABU hapendagi Ujinga. Kuna kikao cha kijiji asubuhi hii. Mjadala mkali unaendelea juu ya hatima ya hawa washiriki. Tukutane Azam Two saa 3.30 usiku kujua kitakachojiri.

#VijanaNdioNgazi #HapaKaziTu
↧
ISRAEL EMBASSY-PRESS RELEASE-DEATH OF SHIMON PERES (FORMER PRESIDENT)
↧