
Si jambo la kawaida kihistoria, Alicia Keys na aliyekuwa mke wa Swizz Beatz, Mashonda…mwanamke ambaye aliwahi kumlaumu na kumtukana Alicia Keys hadharani kuwa alisababisha ndoa yake kuvunjika.
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ uliofanikiwa kupiga picha unayoiona hapo juu, ilipigwa wikiendi hii huko St.Barts, Marekani ikimuonesha Swizz, Alicia na Mashonda wote wakiwa katika mapumziko ya pamoja na watoto ( Swizz amekuwa akiwalea watoto hao akishirikiana na wanawake hao wawili).
ENDELEA. . .
Ni Karibu miaka 5 iliyopita, Mashonda alimuandikia Alicia barua chafu ya wazi kufuatia talaka yake na Swizz Beat, akimlaumu Alicia kuhusu mahusiano yaliyosababisha kuvunjika kwa ndoa na familia yake.
Kutokana na barua hiyo, ungefikiri Mashonda na Alicia wangekuwa maadui wa maisha – lakini picha zinaonesha mambo tofauti kabisa.