Msanii wa filamu nchini Rose Ndauka akifanya usafi mtaa wa Rumumba eneo la Mnazimmoja huku akishirikiana na baadhi ya wasanii wenzake, ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha jamii kutambua umuhimu wa kufanya usafi.
Rose ameamua kujitolea kwa jamii kwa ajili ya kufanya usafi ili jamii itambue kuwa kufanya usafi ni jukumu la kila mmoja na siyo kusubili halmashauri au serikali, ambapo zoezi hilo ni endelevu na atalifanya nchi nzima.