Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

KESI YA OSCAR PESTORIUS IMEANZA LEO

$
0
0
Kesi dhidi ya bingwa wa mashindano ya Olimpiki kwa wanariadha walemavu kutoka Afrika Kusini, Oscar Pestorius, inaanza leo. Anatuhumiwa kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp mwezi FebruarI mwaka jana.

Mahakama mjini Pretoria ilimuachilia Pistorius kwa dhamana ya rand millioni moja, sawa na kiasi ya Dola laki moja. Pistorius anasema kuwa alipiga risasi Reeva kwa bahati mbaya akidhani alikuwa jambazi aliyekuwa amevamia nyumba yake. Mauaji yake yalitokea siku ya Valentine mwaka jana.

Wiki jana mashirika ya habari za michezo, yalipata idhini ya kupeperusha kesi ya Pistorius moja kwa moja kutoka mahakamani.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

Trending Articles