Wafanyakazi wa zoo (eneo la kuhifadhi wanyama) huko China wamefanikiwa kuokoa maisha ya mtu ambaye anadaiwa kuwa na matatizo ya akili baada ya kutangaza kuwa anataka kuwaongeza afya ya chui waliofungiwa katika zoo hiyo kwa kujitolea mwili wake kama kitoweo.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, Yang Jinhai, 27, aliandika kwenye mitandao ya kijamii jinsi anavyojiandaa kuanza maisha mapya baada ya kupata kazi ya ulinzi Chengdu, kusini magharibi mwa China katika jimbo la Sichuan.

Baada ya kutembelea zoo, aliandika jinsi ambavyo “chui wenye hadhi ya juu” wanavyoishi kwa unyonge wakiwa wamezungukwa na mazingira ambayo wamefungiwa na kushindwa kuishi kama asili yao ya uwindaji na kuua.
Na ndipo alipotangaza nia yake ya kujitoa sadaka ili awasaidie chui hao wanaojulikana kama Bengal Tiger.

“Akaendelea kuwasumbua chui hao kwa kuwatishia, na ndipo chui dume akamrukia na kumrarua kwa makucha na kung’atwa kabla hajaokolewa na mhifadhi ambaye alimpiga risasi ya usingizi chui huyo.”
Familia ya Yang waliviambia vyombo vya habari kuwa Bw. Jinhai amekuwa na msongo wa mawazo kwa muda mrefu na kudai amepelekwa nyumbani ambapo anatibiwa na wanasaikolojia jinsi ya kupambana na matatizo yake.