Lindi
Waandisi wa Halmashauri za Wilaya katika Mkoa wa Lindi wamelalamikiwa kwa
vitendo vya kutoa kazi kwa upendeleo pamoja na kupokea rushwa kwa
wakandasi vitendo ambavyo vimeelezwa kuwa vinachangia kazi za barabara
kutekelezwa chini ya kiwango na si kwa wakati hali ambayo husababisha
kero kwa jamii.
bodi ya barabara kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Lindi Jana.
Mamalaniko hayo yametolewa na wajumbe wa bodi ya barabara kwenye kikao cha
Akizungumzia suala hilo mkuu wa wilaya Nachingwea Ragnal Chonjo alisema
kuwa kitendo cha waandisi wa wilaya kugawa zabuni zaidi ya 5 kwa
mkandarasi moja kuchangia kucheleweshaji wa kazi na kusababisha kero kwa
jamiii.
Chonjo alisema katika halmashauri ya wilaya Nachingwea kuna kampuni ya
ujenzi ya inayotambulika kwa jina la Yakwetu kwa kipindi cha mwaka wa
fedha 2013/14 imeshinda zabuni ya kutengeneza barabara zaidi ya 5 zenye
urefu wa kilomita 55 zenye thamani ya zaidi ya shs milioni 702 lakini
utendaji wake uko chini ya kiwango.
Chonjo alizitaja barabara hizo kuwa ni Kiegei ,Mbwemkuru umbali wa kilomita
6.5 , kilimarondo -Kiegei,kilomita 20,Mbondo, Nahimba kilomita 12.5 Nafico-
Nangorola,kilomita 5.1 Naipanga Litama, 7.5 Stesheni Naipanga kilomita1.7
na Naipanga Nangondo km2.0.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Lindi amewataka madiwani na wakurugenzi
pamoja na watendaji wa Halmashauri zote Mkoani humo kusimamia na
kufuatilia kwa ukaribu miradi na fedha za maendeleo zinazotolewa na
serikali ili ziweze kutumika kama zilivyokusudiwa.
Mwananzila alisema iwapo madiwani hawatasimamia vyema fedha za miradi ya
maendeleo iliyopo kwenye maeneo yao huduma za kijamii zinaendelea kuwa duni
kutokana na fedha hizo kuliwa na wajanja wachache wa wasiokuwa waadilifu.
Alisema ili kupata maendeleo kunahitaji uadilifu wa hali ya juu baina ya
viongozi pamoja na jamii lakini kama viongozi watakuwa si waadilifu katika
kusimamia miradi ya maendeleo iliyopo katika maeneo yao bado upatikanaji wa
maendeleo utakuwa mgumu.
↧
HAPA NAPO PAKOJE: RUASHWA KWENYE UGAWAJI WA ZABUNI
↧