Mwanamuziki maarufu duniani wa miondoko ya Hip Hop nchini Marekani, Snoop Dogg (Pichani kulia) na kampuni yake ya Casa Verde Capital wanapanga kuwekeza katika sekta ya bangi nchini Marekani. Wakati Snoop hatowekeza moja kwa moja katika kliniki na biashara yoyote inayolenga kutengeneza au kulima bangi, ameshawekeza katika zaidi ya makampuni 8 yanayosaidia kuendesha biashara ya kuzalisha bangi.
Dola milioni 45 za Marekani (sawa na shilingi za Tanzania Bilioni 101.5 ), ni moja ya uwekezaji mkubwa kuwahi kufanywa na kampuni ya Casa Verde Capital kwa mwaka jana pekee. Snoop ameripotiwa kutokuwa tayari kuwekeza chini ya dola za Marekani milioni 1 (sawa na shilingi Bilioni 2.25 za Tanzania) kwa kila kampuni kwa madai kuwa sekta hiyo ni kati ya sekta muhimu kwa kizazi kijacho.
Karan Wadhera, Mkurugenzi Mtendaji wa Casa Verde Capital, ameeleza lengo lao la baadae, “ Tunalenga makampuni yanayojenga uwezo wa muda mrefu sababu malengo ya muda mfupi hayawezi kutusaidia katika mazingira ya kisheria”
Snoop Dogg amekuwa mmoja wa watu wachache walioihalalisha wazi bangi na kufahamika kama ‘mkongwe’ wa bangi. Uwekezaji huo ni mkubwa haswa kutegenewa kutoka kwa mtu ambaye analipenda zao la bangi kutokea moyoni.