Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

TANESCO YAWAOMBA RADHI WATEJA WA KINONDONI KASIKAZINI

$
0
0
SHIRIKA la Umeme Tanzania ( TANESCO) linapenda kuwataarifu wateja wake wa
Mkoa wa Dar es Salaam kuwa leo Jumamosi tarehe 24/09/2016 kumetokea hitilafu katika Kituo kikubwa cha kupooza na kusambaza Umeme cha Ubungo 220kV/ 132kV na kusababisha kukosekana Umeme kwenye maeneo ya jiji la Dar es Salaam yanayotegemea Vituo vya Kumduchi na Makumbusho.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano TANESCO Makao Makuu jijini mapema leo, tayari hatua za kurekebisha hitilafu hiyo zinaendelea kuchukuliwa ambapo mafundi wa TANESCO wanaendelea na kazi ya kurekebisha hitilafu hiyo na umeme utarejea masaa machache yajayo.

Taarifa hiyo inawaomba radhi wananchi kutokana na usumbufu wowote utakaojitokeza.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

Trending Articles