Ally Masoud maarufu kwa jina la Kipanya akiwa katika kijiji na Babu mwenyeji wa kijiji cha Maisha Plus wakijadili jambo wakati wakiwangoja washiriki wa shindano hilo hapo jana ambapo pia ilikuwa ikirushwa live na kituo cha Luninga cha AZAM TWO chaneli 102Babu mwenyeji wa kijiji cha Maisha Plus akiwa anaandaa mazingira ya kijijini hapoHaya ni Baadhi ya maeneo katika kijiji cha Maisha Plus ambapo washiriki hao kutoka Nchi Tano za Afrika Mashariki watakaa kwa wiki 8Washiriki wa shindano la Maisha Plus Msimu wa tano wakiwa wanaingia kijijini huku kila mmoja akiwa amefungwa kitambaa usoni wasijue wapo wapi.Mwenyeji wa Kijiji Babu wa Maisha Plus akiwa anawakaribisha washiriki kwa namna yakeHapa Washiriki wakiendelea kuingia katika kijiji cha Maisha Plus huku wasifahamu wapo wapi.Masoud Kipanya akiwapa maelekezo washiriki wa Shindano la Maisha Plus kabla hawajafugua rasmi vitambaa na kujua wapo wapiHivi ni Baadhi ya Vifaa na vitu ambavyo vijana wa Maisha Plus watakuwa wakivitumia kipindi wapo kijijini kwa Muda wa Wiki8Masoud Kipanya akitoa msisitizo wa Jambo kwa washiriki wa shindano la Maisha Plus Msimu wa tanoWashiriki wa wa Shindano la Maisha Plus Msimu wa tano wakiwa wanafungua vitambaa kuona rasmi kijiji ambacho wataishi kwa wiki 8Hapa ilikuwa ni kasheshe baada ya kufungua vitambaa na kukuta wapo porini sehemu wasiyo ijua huku kukiwa hakuna jengo lolote.Hapa washiriki wa shindano la Maisha Plus wakiwa wanajipanga kuanza kufanya mchakato wa kuanza kujenga nyumba zaoBado shughuli ilikuwa ni Pevu sana hawaelewi kabisa wanaanzia wapi wanaishia kujishauri kwanza huku kila mmoja akiwaza Milioni 30 atazipata vipi?Hapa bado shughuli ndio kwanza ilikuwa inaanza washiriki hawa pia walikuwa wakibadilishana mawazo wafanyaje.Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwa anatoa maelezo ya kina kwa washiriki wa shindano hilo ambao wanatoka katika Nchi 5 Afrika Mashariki jinsi gani wataishi, watakavyojenga nyumba zao na watakavyo ishi katika kijiji cha Maisha PlusWakiwa wanaleta mizigo yao ndani ya Kijiji cha Maisha PlusMmoja wa washiriki wa Shindano la Maisha Plus akinoa panga kwa ajili ya kujiandaa kwenda kukata miti kwa ajili ya kujenga nyumba zao za kuishi ambapo kila nyumba moja watakuwa wanaishi washiriki watatu.Baadhi ya Mizigo ya washiriki baada ya kuwasili katika kijiji cha Maisha PlusWashiriki wa Shindano la Maisha Plus wakiwa wameanza kuandaa makazi yaoKazi Ikiendelea ya Kuandaa sehemu ya KuishiHapa kazi tuu yani kila mtu yupo na yake alimradi tuu wapate kujenga nyumba za kuishi katika kijiji hicho cha Maisha Plus.Kulikuwa hakuna namna lazima kila mmoja afanye kazi ili wapate sehemu ya kulalaWakati wenzake wamekwenda tafuta Miti ya Kujengea nyumba yeye alikuwa anatengeneza mpiniBabu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwa anatoa maelekezo na kutoa vipimo vya jinsi watakavyokujenga nyumba zaoKila mshiriki akiwa ameshika nyenzo yake kwa ajili ya kujenga nyumba zao zakuishiKazi zinaendelea hapa na sasa ilikuwa ni mwendo wa kukata miti ili kuwahi kumaliza kujenga nyumba na kuanza kuishi.Babu wa Maisha Plus akiwa anafatilia jambo kijijini hapo.Bila kuchakalika na kazi ya kujiandaa kutafuta miti na kujenga nyumba unaweza kujikuta unalala njeBaadhi yao walikuwa wamesha anza kuweka nguzo za nyumba zaoAkionekana akikomaa kuchimba kitu kabla hajawekea mpiniUkiwa katika kijiji cha Maisha Plus lazima upate na ubunifu sana .. hawa jamaa washiriki wa Shindano la Maisha plus msimu wa 5 2016 wakiwa wanakata miti kwa ajili ya kujenga nyumba ambapo wataishi kwa wiki 8Pori kwa poriKazi kwa kwenda mbele
MAISHA PLUS EAST AFRICA 2016 itakuwa ikionyeshwa na AZAM Two Chaneli 102
#HapaKaziTuu
#VijanaNdioNgazi