![]() |
Dar Es Salaam, 14 Juni 2016, Kufuatia tamko la serikali la kuzima simu zote bandia ifikapo tarehe 16 Juni 2016, Airtel Tanzania imeanzisha ofa kabambe ya “simu za bure na halisi" zinazopatikana katika maduka yote ya Airtel.
PICHANI: Mkuu wa kitengo cha Internet Airtel Gaurav Dhingra akionyesha simu zinazopatikana kwenye maduka yote ya Airtel katika ofa iliyozinduliwa hivi karibuni kufuatia tamko la serekali la kuzima simu zote bandia ifikapo tarehe 16 Juni 2016. Simu hizo zinauzwa kwa gharama nafuu kabisa.
Tangazo hilo limesema kwamba simu za Bure na halisi zinapataikana kwa wateja wote wenye simu bandia na ambazo sio za viwango vinavyokubalika katika soko la Tanzania , kwa kununua kifurushi chenye dhamani ya sh. 22,000 / = Tshs tu.
Simu hizi za bure na halisi zinazotolewa na Airtel ikiwemo ITEL 2090 na FERO 180, zikiwa na dakika 550 kwa kupiga mitandao yote, zenye ujumbe mfupi 3000 na 250 MB kwa muda wa miezi minne.
Akitoa maoni yake juu ya ofa hii, mkuu wa kitengo cha Internet Airtel Tanzania, Gaurav Dhingra alisema "tunatambua kwamba baadhi ya wateja wetu bado wanatumia simu ambazo hazina uhalisia, hivyo wako katika hatari ya kuzimiwa simu zao hapo itakapofika siku ya Alhamisi, Juni 16.
Tunachukua fursa hii kuwahakikishi wateja wetu kuwa simu zao zitazimwa lakini laini zao hazitahadhirika na katika kuwasaidia wateja kuweza kununua simu zenye kiwango kinachokubalika, tumeamua kutoa simu zenye uhalisi bure pindi mteja atakaponunua kifurushi kitakachodumu kwa muda wa mienzi 4
Dhingra aliendelea kufafanua kuwa, ili kuwapa wateja wetu uwezo wa kuchagua simu zinazokidhi mahitaji yao , tumeongeza simu za aina mbalimbali ikiwemo Magnus Z11, Huawei Y3C na Techno W3 ambapo mteja akinunua anapata kifurushi chenye dakika zaidi ya 1000 . "Tunatoa wito kwa wateja wetu wa Airtel wenye simu bandia kufika kwenye duka letu lolote la Airtel na simu yake ili ajipatie simu yenye kiwango kinachokubalika kwa gharama nafuu zaidi kwa kununua kifurushi cha Airtel na kupata simu bure. "alinukuliwa Dhingra
Wateja wa Airtel wanaweza kuhakikisha kama simu zao ni bandia au la, kwa kupiga *#06# au kutembelea mawakala katika maduka ya Airtel lililokaribu nae.