
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akikata utepe kuzindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo wa pili (kushoto) ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Uratibu na Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenister Mhagama, (kushoto)wa pili kutoka kushoto ni Meya wa jiji la Arusha, Calist Lazaro (wa kwanza kutoka kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya PPF, Ramadhan Kijjah, Mkurugenzi Mkuu wa PPF, William Erio na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango.

Hapa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akihutubia wakazi wa Arusha na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PPF(hawapo pichani)wakati alipozindua rasmi, Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo (PPF) lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akimpongeza Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, baada ya kuweka Jiwe la Msingi la uzinduai wa Jengo la Kitegauchumi la Mfuko huo lililopo Mtaa wa Korido Jijini Arusha leo Mei 9, 2006.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi PPF, Ramadhan Kijja, wakati alipowasili kwenye Viwanja vya Jengo la Kitegauchumi la Mfuko wa Pensheni PPF lililopo Mtaa wa Korido jijini Arusha kwa ajili ya uzinduzi wa jengo hilo.

Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya uzinduzi.(Picha na Sufian Mafoto).