Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

WANANCHI WAHAMASISHWA KUNUNUA DHAMANA ZA SERIKALI

$
0
0
Frank Mvungi-Maelezo

Benki Kuu ya Tanzania imewataka wananchi kununua dhamana za Serikali ili kuchangia katika kukuza uchumi wa Taifa.

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha Bw. Alexander Ngwinamila toka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) wakati wa mkutano na vyombo vya Habari.

Akifafanua, Ngwinamila amesema kuwa Dhamana za Serikali hutolewa kama uthibitisho wa Serikali kukopa kwa wananchi (Exchange for money borrowed from Public) na baadae kulipa fedha hizo kwa riba kulingana na kiwango kilichowekezwa kwa kuzingatia sheria na taratibu za uwekezaji kwenye dhamana za Serikali.

“Dhamana za Serikali zina kiwango cha faida inayoridhisha hivyo wananchi wanaweza kutumia utaratibu huu kujiwekea akiba kwa ajili ya watoto wao” alisisitiza Ngwinamila.

Utaratibu wa kuwekeza kwenye dhamana za Serikali ni salama kwani Serikali haitarajiwi kukiuka mategemeo ya wadai wake wakati wa malipo.

Faida nyingine ni kuwa amana za Serikali zinahamishika hivyo mwekezaji anaweza kuziuza kabla ya muda wake wa kuiva na pia zinaweza kutumika kama dhamana kwa ajili ya mkopo.

Dhamana za Serikali zimekuwa zikiuzwa kwenye soko la awali (Primary market) kwa njia ya mnada wenye ushindani kwa kila wiki.

Wakati kwenye Soko la upili dhamana za muda mrefu huuzwa na kununuliwa wakati wowote ambapo mnada wa dhamana za Serikali unaendana na Kalenda ya Serikali inayotengenezwa kila mwaka.

Akizungumzia watu wanaoruhusiwa kushiriki kwenye mnada huo, Ngwinamila amesema kuwa Watanzania pamoja na wananchi wote wa Afrika mashariki wanaruhusiwa kushiriki kununua dhamana za Serikali.

Viwango vya ushiriki katika ununuzi wa dhamana za Serikali unaanzia laki tano kwa dhamna za muda mfupi. Na shilingi 1,000,000/ kwa dhamana za muda mrefu (hati funguni).

Benki Kuu ya Tanzania kama wakala wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imepewa wajibu wa kuuza dhamana za Serikali za muda mfupi na muda mrefu. (Treasury bills and bonds).







Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

Latest Images

Trending Articles