Quantcast
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

MATUKIO MBALIMBALI BUNGENI LEO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akiwasilisha hoja za makadirio ya matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2016/17 katika mkutano wa Bunge tarehe 27 Aprili, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akizungumza na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge), Musa Uledi mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Ofisi hiyo Aprili 27, 2015 Mjini Dodoma.Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) Mhe Dkt. Abdallah Possi (kushoto) akizungumza na Kamshna Msaidizi Kitengo cha Wenye Ulemavu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Beatrice Fungamo mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Ofisi hiyo Aprili 27, 2015 Mjini Dodoma. Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb) akimsikiliza Mratibu wa Taifa wa Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARAF) Bw.Walter Swai nje ya Ukumbi wa Bunge mara baada ya kuhairishwa kwa shughuli za Bunge Aprili 27, 2016. Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde (kulia) akizungumza na Mkurugenzi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Prof. Godius Kahyarara (kushoto) mara baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma tarehe 27, Aprili, 2016.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (wa saba kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Watendaji wa Ofisi hiyo, kulia kwake ni Naibu Waziri (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe. Anthony Mavunde na kushoto ni Naibu Waziri (Watu wenye Ulemavu) Mhe Dkt. Abdallah Possi katika viwanja vya Bunge Dodoma. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

Trending Articles