Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akizungumza na wakufunzi watarajiwa Kambi ya JKT Makutupora, alipowatembelea kuona maendeleo ya darasa hilo.
![]()
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama wa pili kutoka kulia, akifuatilia mada ya ‘mbinu za ufundishaji’, ilikuwa ikifundishwa na Mkufunzi Joseph Migunda. Kutoka kushoto wa pili ni Katibu Mtendaji wa NEEC, Bi. Beng'i Issa na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkuu wa Kambi ya JKT Makutupora, Meja Andrew Lwanda. Kaimu Mkuu wa Kambi ya JKT Makutupora, Meja Andrewa Lwanda, akimkaribishwa WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, alipotembelea kuona maendeleo ya mafunzo yanayotolewa na NEEC kwa wakufunzi watarajiwa wa JKT. (Picha zote na Hemed Athuman).

Na Mwandishi Wetu,
Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, juzi alifanya ziara Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Makutupora, kujionea jinsi darasa la wanafunzi linavyoendelea.
Alipoingia darasani, aliungana na washiriki wa mafunzo ya Ujasiliamali, Biashara na Ushirika kumsikiliza Mkufunzi Joseph Migunda, aliyekuwa akifundisha mbinu za ufundishaji.
Akizungumza katika darasa hilo, aliwasisitiza washiriki wa mafunzo hayo, kuzingatia elimu inayotolewa, ili baadaye waweze kuwafundisha vijana wanaojiunga na JKT kwa kujitolea yatakayowasaidia kujiajiri wenyewe, badala ya kutegemea sekta za umma na binafsi.
Alisema kuwa, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, iliamua kuwapatia mafunzo hayo, ili yawe chachu kwa vijana wa JKT kuwasaidia kuunda vikundi vya ujasiliamali, baada ya kumaliza mkataba wa miaka miwili jeshini.
Mhe. Mhagama, aliwaambia kuwa, Serikali inatambua changamoto za ajira kwa vijana nchini, hivyo ililiagiza Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), ishirikiane na JKT kufundisha wakufunzi watakaofikisha elimu ya ujasiliamali, biashara na ushirika kwa vijana, ili kuleta mabadiliko chanya kiuchumi.
Alilitaka JKT liungane kwa dhati na Serikali kuondoa changamoto zilizopo na kuwasaidia vijana kujiajiri kupitia mafunzo yanayotolewa na NEEC kwa nadharia na vitendo.
Alisema kuwa, vijana wakifundishwa na kutambua umuhimu wao kwa taifa, wataweza kuunganisha nguvu zao na kuanzisha shughuli za ujasiliamli, miradi ya biashara na kampuni mbalimbali, ambazo zitasaidia kuajiri wenzao.
Waziri Muhagama aliridhishwa na mafunzo yanayotolewa na NEEC chini ya wakufunzi toka Taasisi ya Washauri wa Biashara (TAPBDS), Joseph Migunda na Nyakainja Migunda.