Kampuni ya Apple imeripoti anguko la mauzo ya iPhone kwa mara ya kwanza, jambo ambalo limelazimisha kurudi na kufanya tathmini na kuleta shinikizo kubwa ndani ya kampuni hiyo. Kampuni hiyo yenye thamani kubwa kuliko zote katika soko la fedha duniani, imeripoti mauzo ya iPhone milioni 51.2 katika miezi mitatu ya kwanza(robo ya kwanza ya mwaka), 2016 ambalo ni anguko tokea milioni 61 ukifananisha na kipindi kilichopita.
Kampuni ya Apple ambayo ndio inazalisha simu za mkononi za iPhone, kinyume na matarajio yao, imepata anguko la mauzo la asilimia 13 mpaka dola za Marekani bilioni 50.6. jambo hilo linamaanisha kuwa kampuni ya Apple imeripoti anguko la kwanza la mauzo katika kipindi cha robo ya mwaka toka mwaka 2003.
Simu ya iPhone kwa mara ya kwanza ilizinduliwa mwaka 2007, na kuchangia zaidi ya nusu ya mapato ya kampuni hiyo.
Kampuni hiyo inapambana vita ya kimtazamo kudhibitisha kwa watumiaji wa simu za iPhone kuwa toleo jipya la iPhone lina tofauti kiuwezo na lile la mwisho, katika soko lenye ushindani mkubwa jambo ambalo pia limechangia anguko la mauzo ikichangiwa pia na mwenendo mdogo wa kukua kwa uchumi wa dunia. Sambamba na hilo mauzo ya kompyuta za Mac na iPad pia yameshuka.
Hisa za kampuni ya Apple pia zimeshuka kwa asilimia 8 katika mauzo yake sokoni. Hiyo inawezekana pia ni kutokana na matarajio yake ya anguko la asilimia 13 au zaidi katika robo ya tatu ya mwaka. Ahadi za kulipa wanahisa wa Apple dola za Marekani bilioni 50 hazikuweza kuzuia anguko la hisa pamoja na mauzo katika soko.
Thamani ya Apple imeanguka zaidi ya mara tano katika kipindi cha mwaka mmoja na kuleta shinikizo la kuunda toleo jipya la iPhone 7 ambalo linatarajiwa kuingia sokoni baadaye mwaka huu. Mtendaji Mkuu wa Apple, Tim Cook alisema, “timu yetu imekumbwa na upepo mkali wa anguko la kiuchumi.
Hata hivyo tunafurahishwa na maendeleo ya kukua kwa kipato kutokana na huduma, nashukuru nguvu ya Apple na kuendelea kukuza msingi wake kwa zaidi ya matukio bilioni moja katika vifaa mbalimbali.” Apple imesema inatanua malengo yake katika maeneo mengine ili kuziba pengo la anguko la simu hizo.
Angelo Zino, mchambuzi wa masuala ya fedha kutoka kampuni ya S&P Global Market Intelligence, anasema: "Wanatakiwa kuja na kitu kipya. Apple inatakiwa kuanza kutawanya msingi wao wa mapato.”