Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

MWANAMUZIKI MKONGWE PRINCE AMEFARIKI

$
0
0
Vyanzo mbalimbali vimedhibitisha kifo cha mwanamuziki mkongwe na aliyewahi kuwa maarufu duniani Prince(PICHANI JUU) akiwa na miaka 57 aliyefia nyumbani kwake. Polisi bado wanachunguza mazingira ya kifo cha mwanamuziki huyo.

Na Mwandishi Wetu

Mwanamuziki mashuhuri na aliyewahi kuwa maarufu duniani, Prince amefariki dunia.  Alikutwa leo asubuhi katika nyumba yake Minnesota, nchini Marekani, alikokuwa akiishi, kurekodi miziki yake, alipofanyia tafrija mbalimbali, pamoja na matamasha ya muziki

Ni miaka michache tu Prince alifanya tamasha katika eneo lake hilo na kuonekana kwake.

Kituo cha televisheni cha Fox 9, kimemripoti Mkuu wa Polisi wa Kautni ya Carver Jason Kamerud kudhibitisha kupokea simu kutoka nyumbani kwa Prince ikidhibitisha kifo cha mkongwe hiyo.


“Inasikitisha kwamba nadhibitisha kifo cha mkongwe mtumbuizaji wa kuigwa, Prince Rogers Nelson, amefariki akiwa katika eneo lake la Paisley ambapo ni nyumbani kwake asubuhi leo akiwa na umri wa miaka 57”

msanii huyo alijipatia umaarufu mkubwa katika muziki na kuzoa tuzo 7 za Grammy, na alitajwa na kushirikishwa (Nominations) katika tuzo za muziki zaidi ya mara 30. Pia alishinda tuzo kubwa kuliko zote duniani za Oscar katika kibao chake kilichotumika katika filamu ya Purple Rain.

Pince atakumbukwa sana. Ameacha alama kubwa sana katika ulimwengu wa muziki pamoja na utamaduni wa POP, na hatosahaulika. Mungu amlaze mahali pema peponi.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

Trending Articles