Quantcast
Channel: Matukio
Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

MASHINDANO YA CHESS KUANZA 23 APRIL MWAKA HUU.

$
0
0
PICHA:Katibu wa Chama cha Mchezo wa Chess Tanzania (TCA) Bw. Nurdin Hassuji ambaye pia ni Bingwa wa Taifa wa mchezo huo akiongea na waandishi wa Habari hawapo pichani kuhusu mashindano ya mtu mmoja mmoja ya ukanda wa Afrika 4.2 yajulikanayo kama (2016 Africa Zone 4.2 Individual Chess Championship), kulia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Geofrey Mwanyika. Picha na BMT 


Na BMT

Mashindano ya mchezo wa chessi yanayojulikana kama mashindano ya mtu mmoja mmoja ya ukanda wa Afrika 4.2 (2016 Africa Zone 4.2 Individual Chess Championship) yanatarajiwa kuanza tarehe 23 mwezi huu mpaka tarehe 30 April
 
Akizungumza hayo mbele ya waandishi wa habari Mwenyekiti wa chama cha mchezo huo nchini (TCA) Bw. Geofrey Mwanyika amesema kuwa michuano hiyo iyafanyika katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es salaam Tanzania ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Aidha Bw. Mwanyika ameinisha nchi ambazo zimeleta washiriki wake ni Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi, Djibout, Eritrea,Somalia,Ethiopia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania

“Jumla ya washiriki 32 watachuana katika mashindano hayo ambayo yamegawanyika katika makundi mawili ya Wanaume na Wanawake na kati ya nchi hizo ambazo zinashiriki Sudan na Seychells hazijathibitisha kushiriki”. Aliongeza Bw. Mwanyika.

Kwa upande wa Katibu wa TCA Bw. Nurdin Hassuji ambaye pia ni Bingwa wa Taifa wa mchezo huo amesema kuwa zawadi za washindi ni Dola 4500 za Kimarekani ambazo zitagawanywa kwa watakaoshinda.

Aidha Bw. Hassuji amewataka wadau wa Michezo na waandishi wa habari kujitokeza siku hiyo ili kuipa sapoti timu yao na kuutangaza mchezo ujulikane na kupendwa zaidi nchini.

Mbali na hayo Bw. Hassuji amesema kuwa mchezo huo wameupa kipaumbele na kwenda kuufundisha mashuleni kwa sababu inawasaidia wanafunzi kuweza kufikiri kwa haraka zaidi na kufanya mwanafunzi awe mwepesi kwenye kupambanua mambo.





Viewing all articles
Browse latest Browse all 3497

Trending Articles