
Maafisa wakuu wa kisiasa wamefungwa jela baada ya kupatikana na makosa ya ufisadi. Kila siku, ni kama kawaida kupata habari za maafisa wa serikali waliochunguzwa au kuadhibiwa kwa sababu ya ufisadi, kutumia vibaya mamlaka au tuhuma nyingine zinazohusiana na ulaji rushwa.
Idadi ya walioadhibiwa mwaka 2015 ilitangazwa wakati wa kikao cha kila mwaka cha bunge la Uchina.
Mtathmini wa BBC anayehusika na masuala ya Uchina anasema tangazo hilo linaonekana kama onyo kwa wajumbe wa chama waliokusanyika Beijing kwamba chama hicho kitaendelea kuwaadhibu maafisa wafisadi.