Huyu mtoto anaitwa Merlyn (pichani) ametekwa na story ya mashuhuda ni kama ifuatavyo.
Merlyn likuwa nyumbani na dada yake, wakatoka wote kwenda gengeni, ndio njiani wakakutana na mbaba akauliza "Mama Merlynyupo?"akaambiwa hayupo, kisha akauliza kama na Baba Merlyn yupo akaambiwa pia hayupo. kisha jamaa akauliza wanarudi saa ngapi, akajibiwa sijui.
Binti akarudi na Merlin nyumbani, nyumbani kwao alikuwepo mama yake mdogo Merlyn, yule kaka akaja nyumbani, safari hii aliomba kutumia choo, akaelekezwa choo cha nje. Kisha dada akaaga kwenda kwa fundi na kumuacha Merlyn na watoto wengine wanacheza uani.
Inadaiwa jamaa alipotoka chooni akamwita Merlyn na kumwambia twende nikakununulie ndizi, akatoka nae huku watu wanamwona, akachukua bodaboda na kutoweka na mtoto, na mpaka tunavyoongea hajaonekana.