↧
RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZA LA MAPINDUZI, DK.SHEIN AFUNGUA BUNGE LA JUMUIYA YA AFIKA MASHARIKI (EALA
↧
WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI WATAKIWA KUWA MABALOZI WA ELIMU YA MPIGA KURA

Afisa Uchaguzi wa NEC Bw. Stephen Elisante akiwaonyesha wanafunzi wa shule ya Sekondari Kidinda fomu maalumu zinazotumika kujaza matokeo ya uchaguzi katika vituo vya kupigia kura wakati akitoa elimu ya Mpiga Kurra kwa wanafunzi wa shule hiyo, Bariadi mkoani Simiyu.

Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Bi. Fausta Mahenge akitoa elimu ya mpiga kura kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria yanayosimamia chaguzi za Tanzania kwa wanafunzi 743 wa Shule ya Sekondari Kidinda wilayani Bariadi mkoani Simiyu.
Na.Aron Msigwa – NEC, Bariadi-SIMIYU.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa wito kwa wanafunzi wa shule za Sekondari waliopatiwa elimu ya Mpiga Kura katika maeneo mbalimbali nchini kuwa mabalozi wazuri wa kuifikisha elimu waliyoipata kwa jamii inayowazunguka.
Wito huo umetolewa na Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Bi. Fausta Mahenge wakati akitoa elimu ya mpiga Kura na kuhusu masuala ya kisheria na utendaji wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kidinda Bariadi mkoani Simiyu.
Amewaeleza wanafunzi hao kuwa NEC imezindua programu ya kuwafikia wanafunzi wa Shule za Sekondari na vyuo Vikuu ambayo haikuwepo hapo awali ili kuwafikia vijana wengi zaidi kwa kuzingatia nafasi ya vijana katika kufikisha elimu hiyo katika ngazi ya familia, mitaa na vijiji.

“ Baada ya elimu hii nawaomba muwe mabalozi wa elimu ya mpiga kura katika maeneo yenu, ninajua ninyi mmetoka katika mitaa na vijiji mbalimbali, mkawe mabalozi wa kuelezea kazi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika ngazi za familia zenu ili tusaidiane kufikisha ujumbe na kuiwezesha Tanzania kusonga mbele” Amesisitiza Bi. Fausta.
Amesema tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu mwezi Oktoba mwaka 2015, NEC imekuwa ikitekeleza programu endelevu za kutoa elimu ya mpiga kura katika maeneo mbalimbali ili kuongeza uelewa kwa wananchi ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kufanikisha chaguzi mbalimbali zinazofanyika na Uchaguzi Mkuu utakaofanyika mwaka 2020.
Ili kufanikisha lengo hilo Tume itashirikiana na Asasi mbalimbali za Kiraia ambazo zitapewa vibali maalumu ili kutoa elimu ya mpiga kura katika maeneo mbalimbali nchini.
Akitoa ufafanuzi wa kuhusu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo kuhusu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), mipaka yake na maamuzi ya kisheria yanayochukuliwa na baadhi ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi amesema kuwa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaweka wazi mamlaka ya Tume katika kusimamia na kuratibu shughuli za chaguzi nchini za kidemokrasia hapa nchini.
Amesema kwa mujibu wa sheria NEC inaratibu na kusimamia Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani pamoja na kutangaza matokeo ya ngazi hizo kwa upande wa Tanzania Bara na kufafanua kuwa chaguzi za viongozi wa Serikali za mitaa zimeachwa chini ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
“Kwa upande wa Serikali za Mitaa, Sheria haiipi mamlaka Tume ya kusimamia chaguzi hizo badala yake uchaguzi wa Serikali za Mitaa uko chini ya Wizara inayohusika na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imeachiwa jukumu hilo” Amesema.
Kuhusu kubatilishwa kwa matokeo ya uchaguzi amefafanua kuwa Mahakama inaweza kubatilisha matokeo ya mgombea yoyote pale taratibu za uchaguzi zinapokiukwa pia mgombea aliyepitishwa kwa nafasi husika kugundulika kuwa amekosa sifa hali inayosababisha matokeo yake kubatilishwa na Mahakama.
Kwa upande wake Afisa Uchaguzi wa NEC Bw. Stephen Elisante akielezea historia ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) amesema kuwa ilianzishwa mara baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini mwaka 1993 na kuongeza kuwa kuwa Ibara ya 74 kifungu cha 6 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza majukumu ya NEC ikiwemo kusimamia na kuratibu uandikishaji wa wapigakura na kusimamia uendeshaji wa uchaguzi Tanzania Bara.

Amewaeleza wanafunzi hao kuwa NEC ina mamlaka ya kuchunguza mipaka na kuigawa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya uchaguzi wa wabunge kwa kuzingatia vigezo mbalimbali vikiwemo vya idadi ya watu, hali ya kiuchumi ya eneo na ukubwa wa eneo husika.
Naye Afisa Habari wa NEC Bi. Margareth Chambiri akitoa ufafanuzi kuhusu programu ya NEC ya kutoa elimu ya mpiga kura amesema kuwa NEC itaendelea kuwafikishia elimu ya Mpiga kura wananchi ili kuongeza uelewa wa wananchi na kuondoa baadhi ya dosari zilizojitokeza kwenye chaguzi zilizopita kabla ya uchaguzi Mkuu ujao mwaka 2020.
“Licha ya changamoto mbalimbali za Kijiografia katika kuwafikia wananchi tungependa kuona idadi kubwa ya vijana na wananchi wanajiandikisha na kujitokeza kupiga kura, naomba vijana mshiriki kikamilifu katika kuwaelimisha wananchi kwa kuwa hii ndio Demokrasia tunayoitaka Tanzania vijana mliopata elimu leo muwe chachu kwa wenzenu ili tuongeze idadi ya wapiga kura na wagombea katika miaka ijayo” Amesisitiza.
Kwa upande wao walimu na wanafunzi wa shule hiyo wakizungumza kwa nyakati tofauti mara baada ya kumalizika kwa program ya utoaji wa elimu ya mpiga kura katika shule hiyo wameishukuru NEC kwa kuwapatia elimu wanafunzi hao.
Wamesema hatua ya NEC kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule hiyo inaongeza uelewa kwa wanafunzi wa shule hiyo katika somo la Siasa na kuwafanya wanafunzi hao kuwa raia na wapiga kura wema.
Wameiomba Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuendelea kutoa elimu hiyo kwa vijana wengi zaidi ili kuwawezesha kuwa mabalozi wazuri wa kutoa elimu sahihi ya Mpiga Kura katika maeneo mbalimbali nchini.

Afisa Uchaguzi wa NEC Bw. Stephen Elisante akisisitiza jambo kwa wanafunzi wa shule ya Sekondari Kidinda wakati akitoa elimu ya Mpiga Kurra kwa wanafunzi wa shule hiyo, Bariadi mkoani Simiyu.

Makamu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kidinda Mwalimu Paul Susu akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo mara baada ya kuwakaribisha Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi waliofika shuleni hapo kutoa Elimu ya Mpiga Kura kwa wanafunzi wapatao 743 wa shule hiyo.

Mwanasheria wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),Bi. Fausta Mahenge akiwaonesha mfano wa karatasi inayotumika kupigia kura yenye majina ya wagombea wa vyama mbalimbali wakati akitoa elimu ya Mpiga Kura katika Shule ya Sekondari Kidinda wilayani Bariadi mkoani Simiyu.

Mwanafunzi wa Kidato cha tatu wa shule ya Sekondari Kidinda, Filipo Madeni akiwauliza swali Maofisa wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhusu mfumo unaotumika kuwapata wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kidinda wakifuatilia kwa makini darasa la Elimu ya Mpiga kura kutoka kwa maofisa wa NEC walioitembelea shule hiyo.
↧
↧
MHE ANASTAZIA WAMBURA AFANYA MAZUNGUMZO NA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA
↧
TIMU YA GOLF YA JESHI YATAMBA KUREJEA NA USHINDI ARUSHA OPEN
Naibu Katibu Mkuu wa klabu ya gofu ya Lugalo ya Jijini Dar es Salaam Kanali Rajabu Mwenyumbu akiangalia Mazoezi ya mwisho ya timu ya klabu hiyo ambayo inatarajia kushiriki katika mashindano ya wazi yanayotarajia kufanyika Mwishoni mwa Wiki Hii Jijini Arusha.
Naibu katibu mkuu wa Klabu ya Gofu ya Jeshi ya Lugalo Kanali Rajabu Mwenyumbu akisalimiana na wachezaji wa gofu wa timu hiyo wanao tarajiwa kushiriki katika mashindano ya wazi Jijini Arusha mwisho wa Wiki hii.

Na Luteni Selemani Semunyu, JWTZ
TIMU ya Golf ya Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania ya Lugalo imetamba kuendeleza ushindi katika mashindano ya wazi ya Mchezo wa golf yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi Oktoba 15 na 16 Jijini Arusha kwa kurejea na Ushindi.
Hayo yamesemwa na Naibu katibu mkuu wa Klabu hiyo Kanali Rajabu Mwenyumbu wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kwa Niaba ya mwenyekiti wa Klabu hiyo Brigedia Jenerali Michael Luwongo wakati akiaga Timu hiyo katika Uwanja wa Golf wa Lugalo Jijini Dar es Salaam.
Kanali Mwenyembu alisema maandalizi mazuri yamefanyika kwa Timu zote ambazo zitashiriki mashindano hayo ambazo ni Daraja Senior ,A,B,C na Wanawake na watoto na kila daraja liko Vizuri na matumaini ni makubwa.
“Nataka muendeleze nidhamu ya Kijeshi katika Michezo lakini weledi katika mashindano ili kuhakikisha wanarejea na ushindi badala ya kuwa washiriki katika mashindano hayo ambayo ni muhimu kwa viwango vya Wachezaji” Alisema kanali Mwenyumbu.
Kwa Upande wake Mmoja wa Wachezaji hao Sara Damas Alisema ni matumaini yake kuwa licha ya kuibuka na ushindi lakini pia wanatarajia kupanda viwango vya uchezaji ukilinganisha na wakati uliopita.
Naye Mchezaji Juma Likuli alisema mazoezi yaliyofanyika ni tofauti zaidi yaliyowajenga ipasavyo hali inayowapa matumaini makubwa ya kuibuka ushindi.
Kwa upande wake Nahodha wa Klabu hiyo Kapteni Japhet Masai alisema Jumla ya wachezaji 10 wanatarajiwa kwenda kushiriki michuano hiyo wakiwemo wanawake watatu na wanaume Saba.
Aliongeza kuwa kikosi cha wachezaji hao Kitaongozwa na Kapteni Amanzi Mangengule, Kapteni Japhet Masai, Kapteni Kibuna Shabani, Juma Likuli,Noel Mheni,Nicolous Chitanda ,Michael Obare, Amina Hamisi,Sara Denis na Sophia Mathias.
Kapten Masai aliongeza kuwa maandalizi yote yamekamilika na kinachosubiriwa ni kurejea na Ushindi kama ilivyokuwa katika mashindano yaliyopita ya Tanzania Open,Moshi Open na CDF Trophy ambayo klabu ya Lugalo iliibuka washindi.
Naibu katibu mkuu wa Klabu ya gofu ya jeshi ya Lugalo Kanali Rajabu Mwenyumbu akizungumza na wachezaji wa gofu wa klabu hiyo ya jijini Dar es salaam wanao tarajiwa kushiriki katika mashindano ya wazi yanayotarajia kufanyika mwisho wa Wiki hii Jijini Arusha .(PICHA ZOTE NA LUTENI SELEMANI SEMUNYU)
↧
PROF. MBARAWA AKAGUA UJENZI WA BARABARA YA KIBONDO-NYAKANAZI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa tatu kulia) akimsikiliza Mkandarasi wa Kampuni ya Ujenzi ya Nyanza (kulia), inayojenga barabara ya Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 50 mkoani Kigoma. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ameipa miezi minne Kampuni ya ujenzi ya Nyanza Road Works kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara ya Kibondo-Nyakanazi yenye urefu wa KM 50 kukamilika kwa wakati na wananchi wa Kibondo na maeneo ya jirani kuweza kuitumia.
Waziri Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo wilayani Kakonko mkoani Kigoma mara baada ya kukagua barabara hiyo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wake. "Mwezi wa pili mwakani nitarudi hapa kukagua tena maendeleo ya ujenzi wa barabara hii sababu bado kasi mnayokwenda nayo hainiridhishi na kampuni hii ni ya kizalendo ambayo ilitakiwa kuwa ya mfano", amesema Prof. Mbarawa.
Waziri Mbarawa amemsisitiza mkandarasi huyo kuzingatia viwango bora vya ujenzi wa barabara kama ilivyosainiwa kwenye mkataba na kumtaka kuzingatia thamani ya fedha katika ujenzi anaoufanya. "Rafiki yangu ni yule anayefanya kazi vizuri hata kama awe mwanangu kama hafanyi kazi vizuri nitamfukuza", amesisitiza Waziri Mbarawa.
Naye, Mkandarasi wa kampuni hiyo Bw. Atul Ramji ameahidi kutii na kulifanyia kazi agizo la waziri huyo na kusema kuwa ifikapo mwezi wa pili mwakani ujenzi utakuwa umepiga hatua kubwa.
Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS),mkoa wa Kigoma Eng. Narcis Choma amesema ujenzi wa barabara hiyo kwa sasa umefika asilimia 18 kutoka asilimia tano zilizokuwepo awali ambapo kwa sasa kazi zinazofanyika ni ujenzi wa makalvati katika barabara hiyo.
Katika hatua nyingine Waziri Mbarawa amemuagiza mkandarasi wa kampuni hiyo kuanza mara moja kuipatia huduma ya maji Shule ya Sekondari ya Kanyonza angalau mara moja kwa wiki kutoka kwenye kambi ya ujenzi wa barabara wakati Serikali ikiendelea kutafuta suluhisho la kudumu.
Prof. Mbarawa amechukua hatua hiyo baada ya wananchi wa kijiji cha Kanyonza kumsimamisha na kumueleza changamoto ya Shule ya Sekondari hiyo iliyopo katika kijiji hicho wilayani Kakonko kukabiliwa na uhaba wa maji hali inayowalazimu wanafunzi kutembea umbali wa zaidi ya kilometa nne kufuata huduma hiyo.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini,Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
↧
↧
WAZIRI LUKUVI. HAKUNA MAKAZI HOLELA YATAKAYOBOMOLEWA JIJINI MWANZA
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, alipofanya ziara Jijini Mwanza hii leo.
Waziri ameziagiza halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, kuhakikisha zinakamilisha zoezi la upimaji na urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela hadi ifikapo june 30 mwakani.
Na BMG
Na George Binagi-GB Pazzo
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willium Lukuvi, ameziagiza halmashauri za Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza, kuhakikisha zinakamilisha zoezi la upimaji na urasimishaji makazi yaliyojengwa kiholela hadi ifikapo june 30 mwakani.
Waziri Lukuvi ametoa agizo hilo hii leo Jijini Mwanza alikofanya ziara ya kujionea utekelezaji wa urasimishaji makazi yaliyoendelezwa kiholela Jijini Mwanza ambapo amebainisha kwamba Serikali haina mpango wa kuwavunjia wananchi makazi yaliyojengwa kiholela na badala yake imeandaa mpango huo ili kutambua makazi hayo na kuwapatia wananchi hati miliki ya makazi yao
Aidha amewatahadharisha wananchi kwamba, mpango wa kurasimisha makazi yaliyojengwa kiholela hautayahusisha makazi yaliyojengwa kwenye maeneo hatarishi ikiwemo kwenye mabonde, miinuko, mafuriko pamoja na hifadhi za barabara.
Baadhi ya wananchi Jijini Mwanza ambao makazi yao yamerasimishwa na kupewa hati ya umiliki, wameipongeza serikali kwa hatua hiyo ambapo wameomba kasi ya zoezi hilo kuongezeka ili wananchi zaidi ya elfu 35 ambao makazi yao hayajapimwa, yaweze kupimwa na kupatia hati za umiliki kwa wakati kama Waziri Lukuvi alivyoagiza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella, amemuhakikishia Waziri Lukuvi kwamba hadi kufikia mwezi Januari mwaka ujao, zoezi la kupima makazi yaliyojengwa kiholela na kuyarasimisha katika Jiji la Mwanza na Maspaa ya Ilemela, litakuwa limekamilika.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akizungumza na wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, alipofanya ziara Jijini Mwanza hii leo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akimkabidhi hati ya umiliki wa ardhi na makazi mmoja wa wakazi wa Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza ambaye makazi yake yamerasimishwa kutoka makazi holela baada ya zoezi la upimaji kufanyika.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Willium Lukuvi, akizungumza na watendaji mbalimbali Jijini Mwanza (Ilemela na Nyamagana).
Baadhi ya Watendaji na Madiwani wa Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza
Baadhi ya Watendaji na Madiwani Jijini Mwanza
Pia Waziri Lukuzi amempandisha cheo aliyekuwa Afisa Mipango na Maendeleo ya Jiji la Mwanza, Deogratius Kalimerize, kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mipango Miji na Vijijini Kanda ya Ziwa.
Ni baada ya kuridhishwa na kazi yake ya usimamiaji na uandaaji wa Mpango Kabambe wa Jiji la Mwanza wa mwaka 2015-3015 ambao umelenga kulifanya Jiji la Mwanza kuwa kitovu cha kiuchumi na biashara katika nchi za maziwa makuu.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza kwenye mkutano huo baina ya waziri Lukuvi na watendaji mbalimbali wa Jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela.
Watendaji na wananchi wa Kata ya Buhongwa wakimsikiliza waziri Lukuvi (hayupo pichani).
**********************
↧
CHUMI AENDELEA KUTAFUTA WADAU WA KUISAIDIA SHULE YA MSINGI MAKALALA

Mkurugenzi wa TEA Joel Laurent katikati akiangalia darasa la Tehama Computer ambazo baadhi zilitolewa kama msaada na TEA kwa shule hiyo.
na fredy mgunda,Iringa.
MBUNGE wa jimbo la mafinga mjini cosato chumi amewataka wananchi kuendelea kujituma kufanya kazi wakati akitafuta ufumbumzi wa kero na changamoto mbalimbali za jimbo hilo jimpya.
Aliyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania Bw Joel Laurent katika Shule ya makalala yenye mahitaji maalumu huku lengo likiwa ni kumuonyesha mkurugenzi huyo jinsi hali ilivyombaya ya kitaalum na mazingira yalivyo magumu kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu.
“Ninajitahidi kufanya kila kinachowezekana ili mradi kutatua changamoto za wananchi wa jimbo la mafinga na kuleta maendeleo kadili ninavyoweza” alisema chumi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elim Tanzania Bw Joel Laurent alisema kuwa atatuma timu yake ya wataalam kwa ajili ya kufanya tathimini ya mahitaji ya miundombinu katika Shule ya Msingi Mchanganyiko ya Makalala iliyopo Mafinga.
Bw Laurent aliyasema hayo siku Alhamis alipoitembelea Shule hiyo kufuatia ombi la Mbunge wa Mafinga Mjini.
Mkurugenzi huyo alisema kwamba TEA pamoja na mambo mengine Ina wajibu wa kusaidia miundombinu na vifaa saidizi vya kufundishia na kujifunzia na kwamba Mwaka huu wataelekeza nguvu katika Shule za mahitaji maalum kama Makalala na kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum katika Shule za kawaida.
Shule hiyo yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 48 wa bweni wenye ulemavu wa akili, wenye ualbno na wenye uono hafifu inakaribiwa na uhaba wa Bweni ambapo kwa Sasa wanafunzi wanalazimika kulala mpaka watoto Sita katika baadhi ya vyumba.
Naye mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri Williamu alisema kuwa anaishukuru TEA kwa kuitikia wito wa kuitembele shule hiyo yenye mahitaji maalumu na kuomba serikali kuwapa ushirikiano kutatua changamoto za shule ya makalala sambamba na kuwaomba wada wengine kuendelea kuisadia shule hiyo.
Wiki iliyopita TEA ilitoa msaada wa vifaa visaidizi vya kusomea katika shule ya Ilboru sambamba na kukabidhi fimbo nyeupe mkoani Mbeya.
↧
HATIMAYE ULIOKUWA MGOGORO MKUBWA WA UMEYA TANGA WAMALIZIKA
Na Mwandishi Wetu, Tanga.
Hatma ya mgogoro wa kiti cha umeya katika Halmashauri ya Jiji la Tanga yamalizika leo baada ya madiwani wa chama cha wananchi CUF kuingia kwa mara ya kwanza katika kikao cha baraza la madiwani na kukiri kumaliza tofauti iliyokuwepo sanjari na kufanya uchaguzi wa kuunda kamati za Halmashauri hiyo.
Hatimaye madiwani hao wameamua kumaliza tofauti zao zilizodumu kwa takribani mwaka mmoja kufuatia sakata la uchaguzi wa umeya uliosababisha kusimama kwa shughuli za kimaendeleo katika Halmashauri hiyo.
Kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika leo ni muendelezo wa vikao vingine vya baraza la madiwani vilivyokaliwa ambapo madiwani wa chama cha wananchi CUF hawakushiriki kutokana na kikao hicho kuvunjika.
Kikao cha leo ni muendelezo wa kikao cha tarehe 19 desemba mwaka jana ambapo waliingia katika tofauti baada ya Mkurugenzi wa jiji kutangaza nafasi ya umeya kuchukuliwa na chama cha mapinduzi ccm ambapo chama cha wananchi CUF hakikuridhika na matokeo hayo.
Awali akifungua rasmi kikao cha kwanza cha baraza la madiwani Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Mustafa Selebosi alisema wameamua kuondoa tofauti zao na kuungana kwa pamoja ili waweze kuwatumikia na kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua sambamba na kufanya kazi za Halmashauri kwa pamoja ili kuliletea Jiji la Tanga maendeleo.
Selebos alisema wameamua kuangalia maslahi ya Tanga kwa kuondoa tofauti zao kwani kuanzia hivi sasa wanakwenda kutekeleza majukumu ya halmashauri ipasavyo kwa kufuata misingi kanuni na taratibu ili kuhakikisha wanafidia muda wote waliosimama katika kuwaletea wananchi maendeleo kutokana na mgogoro huo.
Aliwataka madiwani hao kufanya kazi kwa uadilifu na kusimamia kanuni ili kufikia malengo na kuepuka majipu madogomadogo huku akitaka ruzuku za serikali na fursa zilizotaka kuletwa Tanga zipelekwe kwa kuwa hivi sasa hakuna mgogoro tena wameamua kumaliza tofauti zao.
"Muda wa uchaguzi umepita ni wakati wa kuungana kwa pamoja na kushirikiana kwa kila hali ili tuweze kufanya mabadiliko makubwa katika jiji letu kwani Nchi nzima sasa imekuwa ikisubiri muafaka wa jambo hili upatikane naamini leo hii tumekuwa kitu kimoja tumeivisha nguo serikali wananchi mjivunie sasa kufanya kazi na Halmashauri yenu,"alisisitiza Selebos.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Tanga Daudi Mayeji aliwashukuru madiwani hao kwa kuamua kwa moyo mmoja kufanya kazi ya kuungana kwa pamoja ili waweze kuwaletea maendeleo wananchi waliowachagua katika maeneo yao.
Mayeji alisema kwa muda mrefu swala hilo limekuwa likiwapa wakati mgumu kutokana na vikao vya baraza kutokaliwa na kueleza kuwa viongozi wa serikali na vyama wamefanya kazi kubwa na nzuri ya kuwaunganisha madiwani hao sanjari na kumaliza tofauti hiyo.
Naye Mbunge wa jiji la Tanga kupitia chama cha wananchi CUF Mussa Mbaruku alisema madiwani ni jicho la serikali katika Halmashauri hivyo wanapaswa kutambua wajibu wao ili penye hitilafu warekebishane na kuwataka kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa nafasi aliyonayo ili Halmashauri iweze kupiga hatua.
"Tujue Halmashauri ni wananchi watendaji na madiwani bila umoja upendo na ushirikiano basi hakuna chochote kitakachofanyika hivi sasa maendeleo ya Tanga yatapatikana kutokana na fursa nyingi zinazokuja ikiwemo uwekezaji viwanda pamoja na bomba la mafuta tunapaswa kuelewa kidole kimoja hakivunjo chawa," alisisitiza Mbunge.
Alisema kufikia muafaka wa jambo hilo ni sahihi kwani maisha yanaendelea na kuwataka madiwani hao kufanya kazi kwa kujutuma bila kujali itikadi za vyama vyao ili kuhakikisha Halmashauri ya jiji la Tanga hairudi nyuma katika utendaji wake kwani ufanyaji kazi kwa bidii ndio utapelekea Halmashauri kutorudi nyuma.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga Thobias Milapwa alisema amefurahishwa na kumalizika kwa mgogoro kwani hakuridhishwa na kazi za serikali kufanyika bila vikao vya madiwani kutokana na wao kutoa kauli nzito za shughuli zinazofanywa na Halmashauri na kuamini kuwa shughuli za maendeleo kwa wananchi ni kutokana na sauti za madiwani.
Katika kikao hicho waliteua kamati mbalimbali za Halmashauri ya jiji la Tanga kwa kuzingatia jinsia na itikadi za vyama ikiwemo kamati ya fedha na uongozi Alat, Maadili ya madiwani, Kamati ya kugawa viwanja, kamati ya ajira, kamati ya ukimwi, kamati ya mipango miji na mazingira, pamoja kamati ya uchumi afya na elimu.

WAZIRI MHAGAMA AZINDUA KIWANDA CHA MAZIWA MEATU SIMIYU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akikata utepe kabla ya kuzindua kiwanda cha kusindika maziwa wilayani Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akiweka jiwe la uzinduzi katika kiwanda cha kusindika Maziwa wilaya ya Meatu, Mkoani Simiyu.
Na Stella Kalinga
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amefungua kiwanda cha kusindika maziwa kinachoendeshwa na kikundi cha Vijana wa Meatu kilichopo wilayani humo Mkoa wa Simiyu.
Akizungumza na Vijana hao wanaosindika maziwa ya Meatu (MEATU MILK), Waziri Mhagama amewataka kuutunza mradi huo ili uwe mradi mkubwa wa kuwaingizia mapato wao na Serikali kwa ujumla.
Mhagama amesema kwa kadri mradi huo utakavyokuwa mkubwa ndivyo wafugaji wa Wilaya ya Meatu na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla watakavyonufaika kwa kupata soko la uhakika la maziwa.
Aidha, Waziri huyo amewataka Viongozi wote wa wilaya kuunga mkono juhudi zilizofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka za kuwatengenezea vijana mazingira mazuri ya kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo yao, ikiwa ni pamoja na kushughulikia upatikanaji wa mitaji na mafunzo ya kuwajengea uwezo.
Wakati huo huo Waziri Mhagama ameahidi kuwa Ofisi yake itatoa mkopo wa shilingi 30,000,000 kwa lengo la kuwasaidia vijana hao kuongeza uzalishaji ili kupanua soko la maziwa yao ndani na nje ya Mkoa.
“Mhe. Mkuu wa Mkoa Ofisi ya Waziri Mkuu itawapa mkopo vijana wa “Meatu Milk”ili wapanue uzalishaji; Wizara yangu itatoa mikopo kwa vijana walio tayari kutekeleza ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitakavyowasaidia kuwapa ajira na kujikwamua kwenye umaskini” alisema Mhagama.
Akizungumza na wananchi wa wilaya ya Meatu kabla ya kumkaribisha Waziri Mhagama Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka amesema Mkoa huo umejipanga kuzalisha bidhaa mbalimbali kwa kutumia malighafi zinazopatikana hapa nchini.
“Tumejichagua kuwa pacha wa Mhe. Rais katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa Vitendo na tumedhamiria kuwa miongoni mwa mikoa mitano inayofanya vizuri katika uchumi”, alisema Mtaka.
Akiwasilisha taarifa ya mradi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu kwa Mhe. Waziri, kiongozi wa kikundi cha Meatu Milk Lightness Benedicto amesema Halmashauri imewapa mtaji na kuwajengea uwezo kwenye teknolojia za usindikaji, ufungishaji wa bidhaa za maziwa pamoja na elimu ya ujasiriamali.
Naye Mbunge wa Jimbo la Meatu, Mhe. Salum Mbuzi ameahidi kuwaongezea mtaji wa shilingi 5,000,000 vijana hao pamoja na kuwasaidia kukutafuta soko la uhakika kwa maziwa watakayosindika.
Mradi wa kiwanda cha kusindika maziwa Meatu wenye vijna 18 hadi sasa umegharimu jumla ya shilingi 34,903,000 kati ya hizo shilingi 10,000,000 ni michango ya wanachama kutoka kwenye gawio la fedha za mkopo uliotolewa na Wizara yenye dhamana na vijana,shilingi 24,903,000 ni mkopo kutoka kwenye 5% ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, akipewa maelezo na vijana wa kikundi cha Meatu Milk wanaojishughulisha na usindikaji wa maziwa kabla ya kuweka jiwe la uzinduzi katika kiwanda cha kusindika Maziwa Meatu.
Naibu Waziri wa kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde akizungumza na Vijana na wananchi wa Meatu baada ya Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama kufungua kiwanda cha maziwa Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na Vijana na wananchi wa Meatu wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha maziwa Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi zawadi ya maziwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua kiwanda cha maziwa Meatu.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu Mhe. Pius Machungwa akipokea zawadi ya maziwa kutoka kwa Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama mara baada ya kufungua kiwanda cha maziwa Meatu.
Baadhi ya viongozi wa Wilaya Meatu, mkoa wa Simiyu na viongozi wa kitaifa wakicheza muziki ishara ya kufurahia uzinduzi wa Kiwanda cha Maziwa wilayani Meatu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (waliokaa) wa nne) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa wilaya ya Maswa, Mkoa wa Simiyu, na Vijana wa Meatu Milk.
↧
↧
UVCCM MUFINDI WATAKA MWALIMU NYERERE AENZIWE KWA VITENDO

mwenyekiti wa chama cha mapinduzi wilaya ya Mufindi Yohannis Kaguo kushoto akiteta jambo na katibu mkuu wa chama cha mapinduzi mkoa wa Iringa Hassani Mtenga wakati kukagua mabanda ya maonyesho yaliyofanyika katika ofisi za CCm wilaya ya Mufindi
na fredy mgunda,iringa
VIJANA wa chama cha mapinduzi (CCM)wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa wamewataka wafanyakazi na viongozi wa serikali kufanya kazi kwa kujituma ili kumuenzi mwalimu Nyerere kwa vitendo.
Haya yalisemwa na katibu wa UVCCM Mufindi Fatuma Ngailo wakati akisoma lisala kwa mgeni rasmi wakati wa maazimisho ya siku ya vijana wa chama cha mapinduzi yaliyofanyika wilayani Mufindi.
viongozi wa vyama vya Siasa wametakiwa kuiga kwa vitendo uzalendo na moyo wa kujitoa aliokuwa nao Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere enzi za uhai wake ili kuliwezesha Taifa kupiga hatua kimaendeleo.
“nitahakikisha nazilinda mali za taifa,nasisitiza uwajibika,uzalendo,uandilifu na nidhamu katika kulitumikia taifa la Tanzania kama unakumbuka mwalimu alikuwa anapenda kutumia neno (it can be done play your part) kila mtu atimizi majukumu yake” Alisema Ngailo
Amesema kuwa kumbukumbu za Baba wa Taifa zilizohifadhiwa vizuri katika makumbusho hiyo zina mambo mengi ya kujifunza ambayo wanasiasa wanatakiwa kuyafanya kwa vitendo hasa uzalendo kwa nchi, uvumilivu, upendo na moyo wa kujitoa kwa dhati kuwatumikia wananchi.
“Kupitia kumbukumbu hizi sisi vijana tumejifunza ukomavu wa demokrasia aliokuwa nao Mwalimu Nyerere akiwa ndani na nje ya Bara la Afrika,wengi wanadhani Demokrasia ni wakati wa uchaguzi tu, kumbe demokrasia ni pamoja na kuheshimu watu wengine” Alisema Ngailo
Akiongea kwenye sherehe hizo mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi felix Lwimbo Alieleza kuwa maisha aliyoishi Baba wa Taifa ni mfano wa kuigwa na viongozi na watanzania wote hasa pale alipojitofautisha na viongozi wengi wa Bara la Afrika alipoepuka tamaa ya madaraka na mali kwa manufaa ya taifa.
“Sote ni mashahidi kupitia kumbukumbu zake tumeona mahali alipokuwa anaishi mwalimu kabla hajajengewa nyumba na Jeshi kama Rais mstaafu wengi walitegemea asingeishi katika eneo lile, kumbukumbu hii nzuri aliyoiacha inatufundisha watanzania kuwa mwalimu aliitanguliza Tanzania mbele kuliko maslahi yake binafsi” Amesisitiza Lwimbo
Lwimbo amebainisha kuwa serikali itaendelea kumuemzi Baba wa Taifa kwa yale aliyoyafanya na kuyasimamia kwa manufaa ya taifa huku akitoa wito kwa viongozi wa vyama vya Siasa wawe na kiasi na waridhike na vile walivyonavyo.
“Suala la kuridhika na kuwa na kiasi linapaswa kuzingatiwa, wanasiasa wanapaswa kuwaheshimu wananchi wanaowachagua kupitia chaguzi mbalimbali, matokeo yanapotoka kama ni sahihi basi wanasiasa wakubaliane na maamuzi yao” Ameainisha Lwimbo
Lwimbo amemalizia kwa kuwataka watendaji wote wa serikali ya wilaya ya Ileje kufanya kazi kwa uaminifu,uadilifu,kuwajibika kwenye majukumu yao na kujituma na kamwe hata kuwa tayari kuwavumilia watendaji ambao ni wazembe kazini.
Kwa upande wake katibu wa CCM mkoani Iringa Hassani Mtenga ambaye ndio alikuwa mgeni rasmi katika sherhe hizo alisema kuwa watanzania wanayo mengi ya kujifunza kupitia vitu alivyoviacha Baba wa Taifa ambavyo vimehifadhiwa katika Makumbusho hiyo.
Amesema kuwa maisha ya uadilifu aliyoishi enzi za uhai wake na mchango wake katika kuiletea maendeleo Tanzania na Bara la Afrika vinapaswa kuenziwa kwa nguvu zote na viongozi wa Tanzania.
![]()
katibu wa UVCCM Mufindi Fatuma Ngailo na mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi felix Lwimbo wakielekea kufanya usafi katika hospitali ya mafinga
![]()
hawa ni baadhi ya vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi wakiwa wamemaliza kufanya usafi katika hospital ya mji wa Mafinga wakiongozwa na katibu msaidizi wa mufindi.

“kwa wale mliopata nafasi ya kuitembelea makumbusho na jua mmejifunza vitu vingi kumhusu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwamba alikuwa ni mtu wa namna gani kwa viwango vya Afrika na dunia kutokana na kumbukumbu ya uadilifu aliyoiacha ndani na nje ya mipaka ya Tanzania” alisema Mtenga
Naye mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Yohannes Kaguo aliwataka vijana kuacha kulalamika kwa kukosa ajira kutoka na mfumo wa serikali na kuwaomba wajitume na kuwa wabunifu ili waweze kujiajiri wenyewe.
“Saizi unakuta vijana wengi wanashinda mitaani na kupiga siasa tu na sio kupanga mipango ya kutatua changamoto zao za kimaendeleo ,saa moja asubuhi unawakuta vijana kwenye mabao,pooltable na draft sasa unafikiri hapo utapata maendeleo”alisema Kaguo
Naye mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mufindi Yohannes Kaguo aliwataka vijana kuacha kulalamika kwa kukosa ajira kutoka na mfumo wa serikali na kuwaomba wajitume na kuwa wabunifu ili waweze kujiajiri wenyewe.
“Saizi unakuta vijana wengi wanashinda mitaani na kupiga siasa tu na sio kupanga mipango ya kutatua changamoto zao za kimaendeleo ,saa moja asubuhi unawakuta vijana kwenye mabao,pooltable na draft sasa unafikiri hapo utapata maendeleo”alisema Kaguo

katibu wa UVCCM Mufindi Fatuma Ngailo na mwenyekiti wa vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi felix Lwimbo wakielekea kufanya usafi katika hospitali ya mafinga

hawa ni baadhi ya vijana wa chama cha mapinduzi wilayani Mufindi wakiwa wamemaliza kufanya usafi katika hospital ya mji wa Mafinga wakiongozwa na katibu msaidizi wa mufindi.
↧
MTANDAO WA WIZI WA BAJAJI NA BODABODA WANASWA MBEYA
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashali akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya kuhusiana na tukio la kuunasa mtandao wa wizi wa Bajaji na Pikipiki (BodaBoda) Mkoani Mbeya.(JamiiMojaBlog)
Mkutano wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya na Waandishi wa habari.
JESHI la Polisi Mkoani Mbeya limefanikiwa kuunasa mtandao uliokuwa ukihusika na matukio mbalimbali ya wizi wa bajaji na Pikipiki (bodaboda) katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa anayehusika na matukio hayo imefahamika kwa jina la Getruda Mwakyusa Mkazi wa Mtaa wa Manga Veta jijini hapa.
Akizungumza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari amesema jeshi la polisi limeendelea kufanya misako katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya ili kudhibiti uhalifu .
Amesema Octobar 13 katika misako hiyo jeshi hilo la polisi lilifanikiwa kuunasa mtandao wa wizi wa bajajai na pikipiki ambapo mtuhumiwa wa matukio hayo alifanikiwa kutoroka ambapo nyumba yake mara baada ya kufanyiwa upekuzi zilikutwa pikipiki 3,bajaji 3,bodi 7 za bajaji .
Amesema kati ya mali hizo pikipiki mbili tayari zimekwisha tambuliwa na wamiliki wake kuwa ziliibiwa wilayani Chunya septemba25 mwaka huu katika kijiji cha Isenyela kata ya Mbugani.
Aidha Kamanda wa Polisi Mkoani humo ametoa wito kwa jamii husasani vijana kuacha tabia ya kutaka mali kwa njia ya mkato badala yake wafanye kazi kihalali ili kijipatia kipato sanjali na kutumia fursa zilizopo ili kujitafutia ajira.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashali akionesha baadhi ya Bjajai na Pikipiki ziizokmatwa katika msako uliofanywa na jeshi hilo la POLISI Mbeya.
Askari Polisi wakiwa wamebeba moja ya bajaji iliyokamatwa mara baada ya Jeshi la Polisi Kufanya masako .
Bajaji zilizokamatwa na Jeshi la Polisi mara baada ya kufanya msako.
↧
WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI AZINDUA BODI MPYA YA WAKURUGENZI WA MUWSA

Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Mbunge wa jimbo la Moshi mjini Jafary Michael aliyekuwa mjumbe wa bodi ya MUWSA , zawadi ya Tablet.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji ,Mhandisi Gerson Lwenge akimkabidhi Meneja wa Benki ya Azania tawi la Moshi ambaye pia ni mjumbe wa bodi hiyo,Hajira Mmambe zawadi ya Tablet.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
WAJUMBE WA BODI MPYA YA MUWSA
BIBI ELIZABETH MINDE
ENG: ABDALLA MKUFUNZI
BW: BONIFACE MARIKI
BW: FILBERT KAHETA
BIBI HAJIRA MMAMBE
Mh. RAYMOND MBOYA
Eng. AISHA AMOUR
BW. MICHAEL MWANDEZI
WAJUMBE WA BODI ILIYOMALIZA MUDA WAKE
Mh. SHALLY RAYMOND (MB)
Mh. JAPHARY MICHAEL (MB)
Eng. ALFRED SHAYO
BW. JESHI LUPEMBE
↧
MBUNGE VENNANCE MWAMOTO AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA JIMBO LA KILOLO

Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo

na fredy mgunda,iringa.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto amegawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu za Jimbo hilo kwa lengo la kukuza vipaji vya wanamichezo na kuwandeleza ili wawe wachezaji bora hapo baadae.
Mwamoto ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Kilolo katika ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.
Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo vya Michezo, Mwamoto amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni kutokana na ahadi yake yeye kama Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao kuwapatia vifaa hivyo huku baadhi yao pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.
“Niliahidi kuleta vifaa vya Michezo kwa kila Kata.Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa nan leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mwamoto. Mwamoto ameongeza kwa kusema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.
“Mimi nimecheza mpira kwa mafanikio ndio maana hadi saizi,kwa hilo mimi najua kuwa michezo ni ajira rasmi hivyo mtu kama unakipaji kitumie kipaji chako vizuri”. Mwamoto
Amesema kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
Vifaa hivyo vya michezo ikiwemo seti nzima za Jezi na mipira ya kuchezea ni hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo ambao wamekuwa na shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu.
“Leo nimetoa mipira na jezi hizi kwa timu za Bomalang’ombe na vijiji vya jirani kwa timu zote za wanaume na wanawake kwa lengo la kuendeleza vipaji vyenu”alisema Mwamoto
Aidha, amewataka Vijana hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku kipaji cha mpira wa miguu kikiwa ni ajira kwao pia endapo michezo itaendelezwa zaidi hasa kwa vijana walio pembezoni.

Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya wanawake wa kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo

Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo

↧
↧
TAASISI YA ADLG YAANZA KUWANOA WANAHABARI JIJINI MWANZA KUHUSIANA NA SEKTA YA MADINI NCHINI
Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza, wakijadiliana wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari zenye tija katika jamii kuhusiana na sekta ya madini nchini.
Pia wanahabari hao walipata wasaa wa kuwasilisha tathimini yao kuhusiana na ziara mbalimbali ambao wamezifanya kwenye maeneo yenye wawekezaji wa madini Kanda ya Ziwa ikiwemo mkoani Shinyanga.
Wa kwanza kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo, Fredirick Katulanda, ambaye pia ni mhariri wa magazeti ya kampuni ya New Habari (2006) Ltd Kanda ya Ziwa. Mafunzo hayo yanaandaliwa na Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ADLG, yenye makao yake makuu Jijini Mwanza.
Na BMG
Na George Binagi-GB Pazzo
Waandishi wa Habari mkoani Mwanza, wameanza kupatiwa mafunzo yatakayowasaidia kuandaa habari, makala pamoja na vipindi vyenye tija katika jamii kuhusiana na sekta ya madini nchini.
Mkufunzi wa mafunzo hayo, Fredrick Katulanda, amesema hatua hiyo itasaidia kuibua chachu ya wananchi kutambua haki zao kuhusiana na masuala ya uwekezaji wa madini na hivyo kuondoa migogoro iliyopo baina yao na wawekezaji.
Baadhi ya waandishi wa habari wanaonufaika na mafunzo hayo wamesema yatawasaidia kuandaaji wa habari zenye tija kwa jamii ikiwemo kuondokana na madhara yanayotokana na shughuli za migodini kama vile athari za maji taka.
Mafunzo hayo yanaandaliwa na Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ambapo Mkurugenzi wa taasisi hiyo, Jimmy Luhende, amesema mafunzo yatawasaidia waandishi wa habari kuibua masuala mbalimbali yenye changamoto katika sekta ya madini ili kutafutiwa ufumbuzi.
![]()
Mkurugenzi wa Taasisi ya Demokrasia na Utawala bora nchini ADLG, Jimmy Luhende, akifuatilia majadiliano hayo.
![]()
Baadhi ya Wanahabari/Bloggers Jijini Mwanza
![]()
Baadhi ya wanahabari Jijini Mwanza wakiwa kwenye mjadala mzito kuhusu sekta ya madini nchini.

DC HAI AMALIZA MGOGORO WA ARDHI, AREJESHA SHAMBA KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA HAI

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MGOGORO wa ardhi uliodumu kwa zaidi ya miaka 40 wa shamba la Fofo lilipo wilayani Hai ,umemalizika baada ya Mkuu wa wilaya hiyo ,Gelasius Byakanwa kutangaza kurejesha shamba hilo chini ya usimamizi wa Halmashauri ya wilaya ya Hai.
Hatua ya Mkuu huyo wa wilaya inatokana na mgogoro baina ya Wananchi wa vijiji vinne vya Urori,Tella ,Mula na Usali vilivyoko kata ya Machame Narumu lilipo Shamba hilo dhidi ya aliyekuwa mtendaji mkuu wa Chama cha Ushirika cha Narumu Manushi,Peter Karanti anayedaiwa kujimilikisha shamba hilo .
Akitoa historia ya mgogoro huo Byakanwa alisema shamba hilo lililopewa namba 240 na 242 Ex .C.T No.NP 405 EP.LOT.661 (FOFO ESTATE) lilikuwa linamilikiwa na raia wa kigeni Dkt A Phones ambaye aliweka rehani shamba hilo mwaka 1966 kwa ajili ya mkopo wa kiasi cha Sh 100,000 kutoka benki ya CRDB .
“Baadae Dkt ,Phoneas alitoroka nchini kabla ya kulipa mkopo huo ,Benki baada ya kugundua hilo ilichukua hatua ya kuliza shamba ili kurudisha mkopo aliokuwa akidaiwa Dkt Phoneas”alisema Byakanwa.
Alisema Chama cha Ushirika cha Narumu Manushi ambacho wanachaa wake ni wananchi wa vijiji vine lilipo shamba hilo kilifanikiwa kununua shamba hilo kwa kulipia deni la sh 100,000 ambapo kilitoa kiasi cha Sh 20,000 huku kikibaki na deni la sh 80,000.
“Taarifa ambazo ofisi yangu ilizipata ni kuwa chama kilipewa miaka 10 kiwe kimemaliza kulipia deni hilo ,lakini ndani ya miaka miwili zikatokea taarifa za kuwa Chama cha Ushirika cha Narumu kilishindwa kumaliza deni lake”alisema Byakanwa.
“Bahati mbaya zaidi ,shahidi wa taarifa hizi ni Peter Karanti aliyekuwa mtendaji mkuu wa chama cha Ushirika na haikujulikana yeye kama mtendaji mkuu alichukua hatua gani za kuhakikisha chama kinamaliza deni lake”aliongeza Byakanwa.
Alisema hakuna ushahidi unaoonesha kuwa benki ya CRDB ilikususdia kuliuza shmaba hilo kwa kigezo cha kuwa Chama cha Ushieika cha Narumu kimeshindwa kulipa deni ndani ya muda husika zaidi ya kuwepo kwa taarifa kuwa Mtendaji mkuu wa Chama cha Ushirika alitafuta baadhi ya wanachama na wasio wanachama wachange pesa ya kulikomboa na kulimiliki.
“Baadae chama cha ushirika kilipitisha maamuzi ya kuwapa jukumu la kulipa deni la chama,Karanti na wenzake walilipa deni na kukabidhiwa Shamba hata hivyo walishindwa kupata hati miliki ya Shamba hilo kwa kuwa ilikua bado inashikiliwa na benki kutokana na mkataba uliokuwepo ulikuwa ni Chama cha Ushirika na si Karanti na wenzake.
Akitoa maamuzi juu ya mgogoro huo wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi wa vijiji hivyo uliofanyika katika uwanja wa michezo wa shule ya sekondari Tunoma ,Byakanwa alitangaza kuzuia kufanyika kwa shughuli za maendeleo katika shamba la Fofo zinazofanywa na mtu binafsi.
“Kwa kuwa hati ya Dkt Phoneas aliyekuwa mmiliki wa shamba hilo ilikwisha batilishwa na kuamuliwa shamba hilo limilikishwe kwa kijiji na vijiji ndivyo vinalipa kodi ya ardhi,wakulima wote waliolima katika shmba hilo wavune mazao yao ndani ya kipindi cha miezi mitatu” alisema Byakanwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya ufuatiliaji wa shamba hilo John Kweka alisema awali Wenyeviti wa vijiji hivyo ndio walikuwa wakifuatilia mgogoro huo kabla ya kubaini kuwa wenyeviti hao kuwa na maslahi katika mgogoro na kulazimika kuunda kamati nyingine.
“Tumefuatilia hili suala hadi kwa Waziri wa Ardhi,tumepokea kwa furaha maamuzi ya mkuu wetu wa wilaya kwa sababu sisi kama kamati tulipendekeza maeneo katika hili shamba yatumike kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati,Shule ,Taasisi,Soko na Mahali pa kuzikia hili ndio lilikuwa lengo letu”alisema Kweka.

SBL YATOA ELIMU KUHUSU UNYWAJI POMBE KISTAARABU

Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha akitoa maelezo katizo kuhusu kampeni ya unywaji kistaarabu katika mkutano na wadau mbali mbali wakiwepo toka vyombo vya usalama na wafanyabiashara wanaofanya kazi na SBL na wafanyakazi wa kiwanda cha SBL moshi katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika mapema jana katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro
Moshi, Oktoba 18, 2016. Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni inayohamasisha matumizi sahihi ya pombe au unywaji pombe kistaarabu. Kampeni hii ni hatua muhimu katika sekta ya biashara ya pombe kwa kutambua changamoto inazokabiliana nazo hususan katika masuala ya uwajibikaji kwa jamii.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkaguzi wa polisi Mkoa wa Kilimanjario, Peter Mizambwa , amesema kulishirikisha jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa matokeo ya ulevi na uendeshaji vyombo vya moto. Uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi hujisahau na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia bila kuzingati vyombo vya moto wanavyoendesha.
“Ni jambo lilisilopingika kuwa uzembe na unywaji wa pombe kupita kiasi vina athari kubwa kwa jamii. Madhara hayo hayamuathiri mtumiaji wa pombe peke yake, bali uhatarisha maisha na kuathiri mustakabali wa watu wengi” aliongeza Mizambwa .
“Kwa matinki hiyo, ni janga la jamii nzima – huduma zetu za afya zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini”, alisema Bi Zauda.
Akielezea jinsi kampeni hii itakavyosaidia Mizambwa anasema “ma kwa hakika, sote kwa ujumla wetu tunaathirika – na sote tunalo jukumu la kuchangia namna bora ya kukabiliana na tatizo la ulevi. Nafurahi kuona kwamba wazalishaji wenyewe wa vinywaji vya pombe wametambua kuwa biashara wanayofanya kwa wateja wao inahitaji uwajibikaji na umakini wakati wa kutumia”.
Kampeni hii ya unywaji wa kistaarabu inakusudia kuwafikia vijana wengi pamoja na watu wa rika la juu kwa kuwataka kuelewa hatari ya matumizi ya pombe na kufanya maamuzi kwa faida zao – maamuzi ambayo yatanusuru mustakabali wao wa baadaye.
Naye Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, amesema kampeni ya unywaji pombe kistaarabu inalenga kuwapa walengwa elimu kwamba mtumiaji wa pombe hahitaji kutawaliwa na pombe na kuipa nafasi ibadili mustakabali wa maisha wake na kuongeza kwamba vifo na ajali nyingi hutokana na uzembe au ulevi wa watu ambao si waathirika wakubwa wa pombe – ambao wangeweza kuwa waangalifu kama wangechukua tahadhari na kujifikiria marambili au kama marafiki zao wasingewahamasisha ku-“ongeza moja …au mbili”, alisema.

Meneja wa mauzo wa Sbl Mkoani Kilimanjaro Godwin Seleliii akizungumza katika mkutano na wadau kuhusu kampeni ya unywaji kistaarabu iliyofanyika katika mji wa Moshi mkoani kilimanjaro mapema jana.

Mkaguzi wa polisi Mkoa wa kilimanjaro Peter Mizambwa akitoa hotuba kwa wageni waliohudhuria uzinduzi wa keampeni ya unywaji kistarabu iliyozinduliwa mapema jana na Sbl katika mji wa Moshi

Wadau mbalimbali wakifuatilia kwa makini elimu juu ya unywaji wa kistaarabu katika uzinduzi wa kampeni hiyo mapema jana

Waendesha bodaboda wakipata elimu ya unywaji kistaarabu kutoka kwa mfanyakazi wa SBL aliyekuwa anapita mitaani

Mdau akiwa na zawadi ya kava la gari mara baada ya kujibu vizuri maswali yaliyoulizwa kuhusu unywaji wa pombe kistaarabu
↧
SHINDANO LA MISS TANZANIA 2016 JIJINI MWANZA KUWA BORA ZAIDI
Leo Oktoba 19, 2016 Kamati ya Shindano la Maandalizi ya Miss Tanzania 2016 imesema Shindano hilo linalotarajiwa kufanyika Oktoba 29,10, 2016 katika viunga vya Rock City Jijini Mwanza, litakuwa bora zaidi kutokana na maandalizi yaliyofanyika na yanayoendelea kufanyika.
Na BMG
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Hashim Lundenga (kulia) ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Rhino Agency inayoandaa Miss Tanzania, amesema baada ya mashindano hayo kufanyika Jijini Dar es salaam miaka yote, kamati hiyo imeamua yafanyike Jijini Mwanza na kwamba yatafanyika kwa miaka mitano mfululizo.
Amesema washiriki wote 30 katika shindano hilo ni bora hivyo yeyote atakayeibuka mshindi ataliwakilisha vyema taifa kwenye mashindano ya Miss World yanayotarajiwa kufanyika Disemba 18, 2016 Jijini Washingtone DC nchini Marekani.
Viingilio katika shindano hilo ni shilingi 20,000, 50,000 na 100,000 ambapo inategemewa kwamba wasanii Ali Kiba pamoja na Christian Bella ikiwa wataafiki makubaliano watadondosha burudani katika shindano hilo huku washiriki wakijipatia fursa mbalimbali ikiwemo mshindi wa kwanza kujishindia gari.
Washiriki wa shindano hilo wamesema wamejiandaa vyema na bado wanaendelea kujinoa zaidi ili kuhakikisha atakayeibuka mshindi anaiwakilisha vyema Tanzania kwenye mashindano ya dunia huku wakielezea furaha yao kubwa kwa mashindano hayo kufanyika Jijini Mwanza kwa mara ya kwanza.
![]()
Kamati ya Miss Tanzania 2016 ambapo kutoka kulia ni Hashim Lundenga, Pamela Irengo, Flora Lauwo.
![]()
Mkutano baina ya Kamati ya Miss Tanzania 2016 na Wanahabari Jijini Mwanza
![]()
Washiriki wa Miss Tanzania 2016 katika ubora wao

WILAYA YA HAI WAZINDUA KAMPENI YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA UJENZI WA MADARSA

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
↧
LAKE FM MWANZA KUTAMBULISHWA KWENYE USIKU WA MSHIKE MSHIKE NA KHADIJA KOPA

Usisahau kuhusu Show ya Usiku wa Mshike Mshike na Mfalme wa taarabu Afrka Mashariki na Kati iliyoandaliwa na 102.5 Lake Fm Mwanza.
Ni alhamisi wiki hii tarehe 27.10.2016 ndani ya kiwanja cha nyumbani, Villa Park Resort, kwa kiingilio cha shilingi 7,000 kabla ya saa tano usiku na shilingi 10,000 baada ya saa tano usiku.
Pia watatambulishwa watangazaji wa Lake Fm wakiongozwa na Aisha BBM anayetangaza kipindi cha Mshike Mshike jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa nne asubuhi hadi saa saba mchana, Ma'Djz wa Lake Fm pamoja na wananzengo wengine wanaoendelea kuhakikisha redio hiyo inazidi kupenya Jijini Mwanza.
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi
↧
MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA ASHIKILIA MSIMAMO WAKE DHIDI YA WATENDAJI WA SERIKALI ZA MITAA.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba, akihojiwa na Waandishi wa Habari Jijini Mwanza, kuhusiana na sakata la Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza kugoma kukabidhi mihuri yao ya utendaji kazi.
Na George Binagi-GB Pazzo
"Hii mihuri ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa ni dili, hivyo haitambuliki kwa sasa, kwanza imesababisha migogoro mingi kwa wananchi ikiwemo uuzaji wa viwanja kiholela". Amesisitiza Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba.
Ameshikilia msimamo wake kwamba mihuri ya Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza haitambuliki kama awali alivyosema kwamba waikabidhi ofisini kwake. Leo Wenyeviti wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza wameendelea kushikilia msimamo wao wa kutorudisha mihuri hiyo huku wakitishia kutoshirikiana na Watendaji Jijini Mwanza.
Juzi jumamosi Wenyeviti 174 wa Serikali za Mitaa Jijini Mwanza, walivunja kikao na Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, baada ya Mkurugenzi huyo kuwataka kukabidhi mihuri yao.
#Lakefm #BinagiBlog #BMG #Mwanza
↧